Wednesday, April 28, 2010

Tuesday, April 27, 2010

MAIL KUTOKA KWA MDAU

Habari Zamaradi,

Nimefurahishwa na uchambuzi wako na kuonesha ni jinsi gani hujafurahishwa na suala la matumizi ya lugha ya kiingereza katika filamu zetu.Mimi naomba niliongelee suala hili kwa mtazamo wangu.

Nimewahi kukaa na hawa jamaa zangu na kuongea nao juu ya matumizi ya kiingereza lakini kama ulivyo sema, ueledi umekuwa mkubwa sana kwao kiasi kwamba, kuwashauri ni kama kutwanga maji kwenye kinu.Kwanza kabisa, sielewi hii ya kuzipa filamu majina ya kiingereza imetoka wapi, mimi sioni kama kuna maana ya jina liwe la kiingereza alafu filamu inachezwa kwa kiswahili.

Umeongelea wasiwasi wako kwamba hadhira kubwa ya filamu hizi ni kina mama wa nyumbani, watoto n.k, nakubaliana na wewe ila hata kama wangekuwa na ufahamu mkubwa wa lugha hiyo, bado nisingeona maana ya matumizi ya "kiing-kiswa" kwenye hizi filamu zetu. Tuamue moja kama ni kiingereza ama kiswahili.

Umeongelea tafsiri (sub-tittle)ni kitu kizuri, ila nazo zina makosa mno ya lugha ya kiingereza hasa kwenye sarufi (grammar) kiasi kwamba wala auhitaji uelewa mkubwa wa kiingereza kutambua makosa. Mimi nashindwa kuelewa, Tanzania kuna wataalam kibao wa lugha ambao wanaweza kutafsiri kwa kiingereza fasaha. Hii ni moja ya mambo ambayo yanasababisha tasnia ya filamu ionekane kuwa haina watu makini. Ukija kwenye matamshi ndo usiseme si kiingereza tu hata kiswahili chenyewe wakati mwengine unashindwa kuelewa hapa inakuwaje? Lugha ni kitu muhimu mno katika filamu na cha kufanya ni kuonesha kwamba uko makini na kile ukifanyacho.

Kama tunataka filamu zetu zifikie katika kiwango cha kimataifa lazima tuwe makini, unapompelekea mgeni filamu na kukuta makosa kama hayo sidhani kama kazi yako ataichukulia kwa uzito.Kwenye suala la hadithi naona tunacheza hadithi za kufikirika saana. Unajua katika mazingira yetu kuna story ambazo mtu akika chini na kuzipangilia kwa kuweka matukio yenye mvuto, hakika filamu zetu zitakuwa nzuri zaidi ya hapo.

Ukiangalia nyingi ya ya filamu zetu utaona, kikubwa kioneshwacho ni maisha ya hali ya juu mno, kunavitu hapo nyumbani ukivifanyia utafiti utapata hadithi nzuri sana. Nakupa mfano, utakuta mtu akimfumania mpenzi wake anatoa bastola, kitu ambacho kwa kwetu hapo bastola ni kitu adimu kwa sisi wananchi wa kawaida kuona, mara nyingi silaha tusionazo labda upite benki, polisi n.k na kumkuta skari na SMG.

Mwisho jamaa zangu life style wanayo ishi si nzuri kwa mustakabali wa tasnia ya filamu. Haiwezekani haipiti wiki bila kuona skendo kwenye udaku inayo muhusu msanii wa filamu. Unajua kuna maarufu wengi tu Tanzania, lakini wa filamu wamekuwa warahisi mno kiasi kwamba hawana hesma tena.

Angalia jinsi wasanii wa bongo flava wanavyo shirikishwa katika masuala muhimu ya kitaifa, mfano mabalozi wa Malaria, why kusiwe na wengi wa filamu. Hata mimi siwezi kukufanya uwe balozi wangu kama jamii inakuona ni zimbukuku, bongo-lala,fisadi wa mapenzi,na hayawani!

Shule muhimu ndugu zangu, wenzenu tumepitia huo umaarufu vidole hauna maana hata kidogo.

Shukrani.

MATUMIZI YA LUGHA YA KINGEREZA KWENYE FILAMU ZETU NI SAWA?

Ikumbukwe kabisa kwamba MLENGWA mkubwa wa filamu za kitanzania ni mwananchi wa kawaida sana ambae kingereza kwake si lugha anayoitumia kabisa na huenda hata haifahamu, Walengwa wakubwa wa hizi filamu ni wamama wa nyumbani, vijana wa kawaida tu na watoto, Hao wanaojua kingereza ni WACHACHE sana wanaoangalia, wengi wao hawazifuatilii kabisa hizi filamu za kwetu.

Lakini pamoja na yote kumekuwa na wimbi kubwa la kutumia lugha ya kingereza kwenye filamu zetu za kitanzania bila hata kuangalia kama kinachoongelewa ni fasaha ama la.

Si kitu kibaya kuongea lugha hiyo kama script inasema hivyo na wanaoongea lugha hiyo wana uwezo wa kuitendea haki, lakini kwa jinsi kingereza kinavyotumika inaonekaana kabisa kwamba kimechomekewa na hakukuwa na ulazima wa kutumika kwenye sehemu husika.

Nafkiri imekuwa kama FASHION na njia ya waigizaji kuonesha kwamba WANAJUA zaidi sababu kuna fikra potofu ambayo imejengeka miongoni mwetu kwamba kuongea kingereza ndio kuonekana umesoma ama unajua zaidi.

Lakini badala yake matumizi ya kingereza yanaleta matokeo tofauti kwani HAYAMPANDISHI yule mzungumzaji bali YANAMSHUSHA zaidi kwa watazamaji.
Na hiyo ni kupitia vitu kama PRONOUNCIATION(matamshi) ambayo mara nyingi inakuwa mbovu kuliko kawaida mfano kuchanganya R na L na vitu vingine, kitu ambacho kinatia aibu unapoangalia.

Kuna filamu nyingi sana zimeigizwa katika lugha tofauti kabisa na bado zinaeleweka na kupendwa hata kwa wasiojua lugha hiyo kupitia kitu kinachoitwa SUB-TITLE, ambazo hizi humfanya mtu asieelewa lugha inayotumika kuelewa filamu ile kwakuwa imetafsiriwa kwa chini.

Nafkiri SUB-TITLES ndio kitu kikubwa cha kuangalia zaidi na kukitilia mkazo kwenye filamu zetu.

Je kuna UMUHIMU wowote wa kuongea lugha ya kingereza kwenye filamu zetu ilhali TUNAIKOSEA????

Thursday, April 22, 2010

WOLPER - NAPENDA MWANAUME ANAENUKIA

Akiwa katika pozi

On the interview with clouds TV


Alizaliwa miaka 21 iliyopita huko MOSHI Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa kwanza na msichana peke yake kati ya watoto wanne wa mzee Wolper.
Elimu yake ya msingi aliipatia katika shule ya msingi Mawenzi huko Kilimanjaro wakati Sekondari alipitia katika shule za St. Magreth, Ikenye Arusha na akaja kumalizia Masai huko Kenya.. na baadae akajishughulisha na biashara zake binafsi hatimae mtu ambae anaitwa Lucy Komba akagundua kipaji chake na ndio ikawa mwanzo wa kuingia kwenye filamu.

Mbali na mwanaume anaenukia pia kuna vingi kama vigezo vya aina ya mwanaume anaependa.. ukitaka kujua mengi kuhusiana na yeye shuka nae kwenye interview hapo chini...

QN: Kama Ingetokea nafasi ya kuzaliwa upya, ungependa kuwa nani?
ANS: Ingetokea nafasi ya kuzaliwa upya kwanza nisingeingia kwenye filamu, unajua kwanini napenda sana kazi yangu na naiheshimu lakini magazeti yanatuharibia, nachukia sana magazeti, naona kabisa kwamba usupastaa ni mzigo wa mwiba, unaweza ukawa unafanya tu kitu kwa mapenzi yako kwa ajili ya kuenjoy lakini kikakurudia tofauti, labda uko tu club unacheza ama umevaa unavyojiskia basi mtu atakupiga picha inakufanya ukose uhuru, hivyo mimi ningezaliwa upya SIDHANI KAMA NINGEINGIA KWENYE FILAMU.

QN:Kwako Furaha ya kweli ni nini?
ANS: Asikwambie mtu pesa ndio kilakitu Zamaradi, NAPENDA SANA PESA aisee, nikiwa sina hela huwa nakuwa kama naumwa yani, hivyo kwangu pesa ndio kila kitu na ndio furaha yangu.. Ujue mi mchaga eeh!! lakini ninavyosema pesa simaanishi kwamba pesa ya kupewa ama nikae tu naisubiri hapana ila napenda kila ninachokifanya kiniingizie hela, napenda kuitafuta pia na ndiomana najishughulisha na biashara zangu nyingine mbali na filamu.

QN:Unapenda mwanaume wa aina gani??/ vigezo vyako ni vipi kwa mwanaume?
ANS: Kwanza mchapakazi, awe ananielewa na aelewe nini nachokifanya, asiwe na wivu, anijali, aniamini lakini kubwa awe smart yani hapo ndio uuh.. napenda mwanaume SMART na ANUKIE.

QN: Kitu gani ambacho watu huwa wanakusifia nacho sana??
ANS: Mara nyingi kitu ambacho watu naskia wananisifia nacho sana ni MACHO.. wanasema nina macho mazuri lakini mi sijui chochote mi naona kawaida tu.. na vingine vingi under carpet.

QN: Unapendelea nguo/mavazi ya aina gani?
ANS: Zamani kabisa nilikuwa napenda sana kuvaa ki-tom boy (kiume) hata mavazi yangu mengi yalikuwa hivyo lakini watu wengi walikuwa hawapendi miniwe hivyo so baada ya watu kunisema ikabidi tu niache hivyo sasahivi navaa kike nimebadilika navaa kike ingawa siku mojamoja sana huwa navaa kitom boy kama naenda kwenye michezo ama kitu kinachofanania, napenda kuvaa mavazi yoyote yanayonipendeza,napenda kupendeza in short.

QN: Nani ni mtu muhimu sana katika maisha yako??
ANS: Mtu muhimu katika maisha yangu ni MAMA YANGU kwakweli, yani huyu ndio kila kitu kwangu.. nampenda sana mama yangu.

Huyo ndio Jaqueline Wolper mtoto wa kichaga ambae kwasasa anafanya vizuri sana kwenye sanaa ya filamu hapa BONGO na ni mmoja kati ya wale waigizaji wa kike wakali.. Hope utakuwa umejua japo kwa uchache kuhusu yeye.

Wednesday, April 21, 2010

MZEE YUSUPH AANGUKA GHAFLA LEO...

Hapa ilikuwa ni harakati za kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.

Ilikuwa mishale fulani ya sasa sita, mwanamuziki wa kundi la taarab la JAHAZI alipokuja clouds FM leo kwa shughuli zake binafsi lakini ghafla tu wakati anaingia ndani mguu ukashtuka ukawa umekaza na unashindwa kunyooka kabisa, akaomba kiti akae lakini ghafla nyonga nayo ikakaza ikabidi atandikiwe chini ajinyooshe huku utaratibu wa kumpeleka hospitali ukiwa unashughulikiwa..

mara akakimbizwa Hospital ambako yuko mpaka sasa na ripoti ya daktari inasema ni mshipa umekaza kitu ambacho kinaweza kutokea saa yoyote hivyo amechomwa sindano na baada ya nusu saa huenda akarudi kwenye hali yake ya kawaida..
Get well soon!!

Monday, April 19, 2010

FLAVIANA ANATOKA NA MMILIKI WA PHAT FARM..??

Kuna mtandao mmoja huko marekani umeandika kuhusu uhusiano wa mwanamitindo kutoka Tanzania FLAVIANA MATATA na aliekuwa mume wa Kimora Lee RUSSEL SIMONS ambae ni mmoja kati ya mafounder wa hip-hop label ya DEF JAM records na pia ni creator wa clothing fashion line yaPHAT FARM. Flaviana akiwa na Russel Simmons
Russel Simons

Huyu ndio Russel Simons mwenyewe ambae INASEMEKANA yuko na uhusiano wa kimapenzi na Flaviana kwa sasa..
Alizaliwa 4th October 1957, ni mtu anaeheshimika sana huko America na ana mchango mkubwa sana katika muziki wa hip hop.
na inasemekana anapenda sana kudate Models kwani hata aliekuwa mke wake (Kimora lee) ambae ni mmiliki wa Baby phat ni model.

KIMORA LEE (4th May 1975)
Russel Simons alikutana na model kimora lee mwaka 1992 katika New York Fashion Week ambapo waliweza kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka sita na hatimae wakafunga ndoa December 20 1998.. na March 2006 walitangaza kutengana kwao hatimae January 2009 walipeana talaka moja kwa moja

Aliyekuwa mke wa Russel Simons, anaitwa KIMORA LEEKabla ya kutengana walifanikiwa kupata watoto wawili wa kike pamoja ambao ni Ming lee aliezaliwa January 21st 2000 na mwingine aliezaliwa 2002 August anaeitwa Aoki lee.. na watoto wao wote ni mamodel wa BABY PHAT kids collection.

Flaviana Matata akiwa na Russel Simons

Bado haijajulikana kama hii habari ni kweli ama la..
Ila ntajitahidi kumtafuta Flavy atuelezee ukweli wa hii habari.

Flavy say Something baby gal...

Sunday, April 18, 2010

SIMBA OYEEEEEEEEEEE

Leo ilikuwa ni siku ya hekaheka na upinzani wa hali ya juu kati ya watani wa Jadi (Simba na Yanga) hatimae mtanange ukafikia mwisho na SIMBA wakaibuka kidedea dhidi ya wenzao kwa Goli 4-3.
Ilikuwa ni mechi kali sana na nilifanikiwa kuishuhudia live pale uwanja mpya wa taifa.. sikutaka kuhadithiwa leo.
Kiukweli kabisa mimi si mpenzi wa kihivyo wa mpira wa miguu na huwa sina timu, lakini cha kushangaza zaidi na hata mimi huwa najishangaa mwenyewe YANGA ikifungwa huwa ninajiskia vibaya sana though sina timu sasa sijui nijieleweje!!!!
Ila hiyo haitafanya niache kuwapa hongera zao SIMBA...
SIMBA OYEEEEEEEEEEE...!!!!!!!!!!!
kwa picha zaidi tukutane kesho.......

Thursday, April 15, 2010

USO KWA USO NA STEVE NYERERE



Watu wanasema kwamba kijana yuko kimya sana lakini leo nilivyokutana nae akaniambia kwamba Huu ndio muda wake wa kurekebisha mipango...... na ukiona KOBE KAINAMA ujue...
Handsomeboy Steve mwalimu.. hapa akiwa 'amejihandsamisha'

Kwa wale wapenzi wake kaeni mkao wa kula sababu sasahivi amesema HATAKI MCHEZO alikuwa kambini huko GHUBA YA SOMALIA akijifua na baada ya kukoswakoswa na silaha amekuwa na hasira sana na sasahivi ameongeza sauti nyingine ya RAIS WA SOMALIA ..


Subiri umuone live ndani ya mavazi na sura ya kisomali huku akilalamikia UGAIDI unaofanywa na wananchi wake wa SOMALIA.. hapo akikupa za KIKWERE

NIMEWABAMBA!!!!!

Nilikuwa napita tu hapa Best Bite leo nikakuta
watu wanashoot filamu inaitwa NANI ALAUMIWE
Director kushoto akiwa busy kuweka vijana
wake sawa na kitu wanachokifanya anaitwa YUSUPH EMBE maarufu kama DEOWaigizai wakiwa kwenye set, huyo mvulana kulia ndio muhusika mkuu wa hiyo filamu kijana mpya kabisa katika industry anaitwa MOHAMMED ISSA na msichana pembeni anaitwa BAHATI MBONDE. Kazi ikiendelea
Isubiri filamu hii kutoka kampuni mpya ya MCLISA PRODUCTION itakayoitwa NANI ALAUMIWE
Hizo ndio filamu zetu nyuma ya pazia



KWANINI WASANII WETU NI VIGUMU KUWA ROLE MODELS???

Niljaribu kufanya interview na wasanii tofauti tofauti wachanga wa hapa Tanzania katika tasnia ya Filamu na kila mtu nilimuuliza kuhusiana na Role model wake kwa maana ya mtu anaemu-inspire, lakini cha kushangaza katika hao niliowahoji hakuna hata mmoja ambae alinitajia msanii wa TANZANIA kama role Model wake badala yake majibu yalikuwa watu kama DENZEL WASHINGTON, NICK CANON, MICHAEL SCOFIELD, INNI EDDO, ANGELO na wengineo.. ambao wote hawatoki Tanzania..

Unafikiri ni kwanini wasanii wetu wa Tanzania hawatajwi kama role models?? ina maana hatuna ma role models hapa kwetu Tanzania!? ama?

Tuesday, April 13, 2010

NILIPATA MTOTO NIKIWA FORM FIVE - HEMED

Wiki hii nniliweza kufanya mahojiano kidogo na HEMED na nilitaka kujua machache kuhusiana na yeye si kifilamu ila maisha yake nyuma ya pazia.. Anafahamika kwa jina la HEMED SULEIMAN kijana aliezaliwa mwaka 1986 31st August na elimu yake ya Msingi alianzia pale OYESTERBAY primary School na kumalizia katika Shule ya Msingi BUNGE na baada ya hapo akajiunga na masomo ya sekondari pale ANNUUR ISLAMIC SECONDARY mkoani Tanga na baadae akaendelea na kidato cha tano na sita katika Shule za ECKENFORDE na COASTAL high school zote za huko Tanga ambako ndiko alikomalizia Elimu yake ya High School.
Majibu yake hayakuwa mabaya ila hakuweza kuendelea na chuo badala yake akajiunga kwenye TUSKER PROJECT FAME na mwaka uliofatia pia alishindwa kuingia chuo ila kwasasa ana mpango wa kujiunga na chuo kwa mwaka huu akienda kusomea MARKETING.

Kwa kujua mengi zaidi kuhusu yeye cheki na interview yake hapo chini

QN: NI KITU GANI AMBACHO UNAPENDA SANA KATIKA MAISHA YAKO?
ANS:Kiukweli kabisa napenda sana kula na kwa siku nakula mara NANE, mpaka ikifika saa sita usiku kila siku nakuwa nimeshamaliza kuku WAWILI NA NUSU ama WATATU na kitu kingine napenda sana kuwa na BABY(mpenzi) na sio kuwa na mpenzi wangu labda tutoke twende Club hapana ila napenda sana kuwa na mpenzi wangu tujifungie ndani faragha tupeane vitu.. Hivyo ndio vitu viwili ninavyovifeel zaidi.

QN: INASEMEKANA WEWE NI MTU WA WATOTO SANA KWA MAANA YA KUPENDA WASICHANA, HIYO NI KWELI?
ANS: hiyo ilikuwa zamani kiukweli kwasababu wanasema ujana maji yamoto kwasababu nakumbuka wakati naanza resi za kuwa star nilikuwa nataka kila mtu anijue kila mtu anione kwahiyo nilikuwa mtu fulani sijatulia lakini nimekuja kugundua kwamba ukiwa serious sana na kazi na uki-concetrate katika ku-build future yako upumbavu unatakiwa uache pembeni kwasababu ukiendekeza sana inaweza ikakuharibia mbele kwahiyo nina imani sasahivi nimekua na NIMEBADILIKA na niko na mchumba mmoja.

QN: KATIKA HIZO PITAPITA ZAKO HUKUFANIKIWA KUPATA MTOTO?
ANS: Niko na MTOTO MMOJA wa kiume ana miaka miwili na miezi saba anaitwa TRINIDAD huyu mtoto nilimpata nikiwa Form five nakumbuka kwenye kuingia form six wakati nasoma na nimezaa na msichana mmoja anaitwa ...... ah!! acha nimpotezee jina ntampa promo kwasababu alinimwaga ni msichana fulani hivi so.. yeah yupo nina mtoto mmoja nashkuru nimemkubali kwasababu amefanana na mimi.. Handsome boy!

QN: ANACHUKIA NINI?
ANS: Sipendi dharau na sipendi mtu ambae anasema uongo ndiomana huwa mimi najaribu sana kuwa mkweli kwa kila kitu ambacho nakifanya ama kitu ambacho niko nacho kwahiyo mtu akiwa muwazi kwangu nakuwa namuelewa zaidi.
pia sili chakula ukiweka vitunguu na ukitaka kuninyima msosi weka vitunguu mi sili na mama yangu anajua, kwahiyo hata nyumbani kwetu msosi ukipikwa unakuwa hauna vitunguu kwasababu sipendi, pia sili mboga ya majani yoyote unayoijua wewe na hata matunda pia nachagua nakula maembe, ndizi na mananasi mengine yote sili.


QN: UNAPENDA MSICHANA WA AINA GANI?
ANS: Kitu cha kwanza kabisa ninachokiangalia kwa msichana ni RANGI, ila kitu cha ajabu ni kwamba SIPENDI MSICHANA MWENYE RANGI YA AINA YANGU, napenda msichana MWEUSI.. aanzie kwenye U-brown fulani mpaka kwenye weusi ila asiwe mweusi sana na kingine awe MKALI, ila WADADA WENYE RANGI YANGU MTANISAMEHE.

QN: UNAJIVUNIA NINI MPAKA SASA KUTOKANA NA FILAMU?
ANS: mafanikio ni makubwa sana kwanza kujulikanam, nimetokea ni mtu fulani najulikana sana hasa mikoani, filamu zimenifanya mpaka huko vijijini ndanindani watu wanitambue hivyo imenifanya umaarufu umeongezeka na kunipa heshima kwa watu wazima hilo la kwanza
La pili ni MAENDELEO YANGU BINAFSI, sikufichi sasahivi NAPIGA PAMBA KALI, GHETTO KWANGU PAKO FRESH na hata kula sasahivi nakula fresh kama hivyo kuku wawili watatu kwasiku nakula wakati zamani ZEGE(chips mayai) nilikuwa nalifkiria yani.. hivyo nashkuru MUNGU niko fresh.


QN: Asante sana
ANS: Karibu.

Huyo ndio HEMED.. Natumaini utakuwa umejua machache kuhusiana na yeye kama alivyojielezea kwenye majibu yake ambayo sijapunguza wala kuongeza neno langu lolote..
UNATAKA NIKULETEE NANI MWINGINE na nini unataka kujua kutoka kwake???

Monday, April 12, 2010

MY MIND IS BLANK

Kwa sasa ndio najua kwamba si kila unaemuona anacheka usoni basi ana furaha moyoni, kiubinadamu saa nyingine inabidi tu ujisahaulishe mambo mengine ili maisha yaweze kuendelea na ndiomaana mtu huweza kujivika uso wa tabasamu lakini kuna mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.

For all this time nilikuwa nikienda kazini na kurudi maybe kutoka na marafiki sometimes tukicheka na kufurahi lakini haikuwa na maana kwamba nilikuwa HAPPY kama nilivyokuwa nikionekana, nilikuwa katika mawazo mazito ya kumfikiria baba yangu ambae alikuwa mgonjwa kwa kipindi hiko na mawazo mengi yalikuwa yakiingia na kutoka katika kipindi hiko cha kumuuguza.

Hatimae safari yake ya maisha ikafika mwisho na MUNGU akaamua kumchukua siku ya tarehe 4 april 2010..kazi ya MUNGU haina makosa.. ni siku ambayo SITAWEZA kuisahau katika maisha yangu kwani baba yangu hakuwa baba tu kwangu.. ila alikuwa zaidi ya BABA, My Dad was a big friend to me kiasi cha kuwa free kumueleza tatizo langu lolote.. so kuondoka kwake ni kitu ambacho naweza nikasema kimeni-affect kinamna moja ama nyingine na kimebadilisha mambo mengi katika maisha yangu.

Pamoja na kuondoka kwa mtu muhimu katika maisha yangu lakini bado kuna majukumu ambayo yananikabili na msema kweli mpenzi wa Mungu kichwa changu hakijawahi kuwa wazi kama kilivyo sasahivi, kila ninavyojitahidi kufikiria akili yangu inagota kabisa ni kama MIND yangu iko BLANK kabisa yani. sielewi nini cha kufanya akili yangu imelala kabisa na haitaki kufikiria mbali...

KWA WALE WADAU na wafatiliaji wa BLOG hii mnafkiri tufanye nini kama kuna mtu yoyote ana MAWAZO,MAONI ama MCHANGO wa nini kifanyike ama kizungumziwe ndani ya blog yetu... ungependa kuona nini humu ndani ama tuzungumzie kitu gani kuhusiana na tasnia yetu ama burudani kwa ujumla au chochote kile??? ...msaada tutani tafadhali.. mawazo yenu ni muhimu sana kwangu.

Sunday, April 11, 2010

SHUKRANI

MIMI pamoja na Familia nzima ya HUSSEIN MKETEMA wa Kinondoni DSM tunatoa shukrani za DHATI kabisa kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika mazishi ya BABA yetu mpendwa HUSSEIN MKETEMA aliefariki tarehe 4 April 2010..
Ni ngumu sana kumshukuru mmoja mmoja hivyo shukrani za dhati ziwaendee WOTE walioshiriki nasi katika kipindi hiki kigumu, MUNGU awabariki sana...
INNALILLAHI WAINA ILAIHI RAJIUN.
MWENYEEZI MUNGU aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.. AMEEN!

Tuesday, April 6, 2010

BURIANI BABA

PASAKA YA MWAKA HUU NIMEISHEREHEKEA KATIKA HALI YA MAJONZI MAZITO KUFUATIA KIFO CHA BABA KILICHOTOKEA JUMAPILI NA MAZISHI KUFANYIKA JUMATATU JANA KWENYE MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR. PICHANI JENEZA LENYE MWILI WA BABA LIKITOLEWA NYUMBANI NA KUANZA SAFARI YAKE YA MWISHO KUELEKEA MSIKITI WA MTAMBANI NA KISHA MAKABURINI. NALIA NASIKITIKA KUBAKI MKIWA. HATA HIVYO KAZI YA MOLA HAINA MAKOSA. MOLA IWEKE ROHO YA MAREHEMU BABA MAHALA PEMA PEPONI - AMINA

Sunday, April 4, 2010

DIANA ASTON VILLA AFARIKI DUNIA

Marehemu DIANNA ASTON VILLA enzi za uhai wake

Marehemu alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Amana ilala jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa.

Atakumbukwa sana katika sanaa ya muziki hasa katika fani ya unenguaji ambapo aliwahi kuwa mnenguaji mahiri katika bendi kubwa mbalimbali za hapa Tanzania.

kwa habari zaidi tembelea www.issamichuzi.blogspot.com

Thursday, April 1, 2010

KIZAZI KIPYA CHA MUZIKI WA BONGOFLAVOR

Kutoka kushoto anaitwa DIAMOND(nenda kamwambie), BARNABA kutoka THT, ANGIE, NIKI WA PILI, MATALUMA (mama mubaya), BABY J kutoka ZnZ, YOUNG DEE pamoja na ROMA.
BARNABA kutoka THT anaetamba na nyimbo kama Wrong number, njiapanda na nyinginezo akiwa amepozi na ANGERIS FABOR (Angie) ambae kwasasa ameachia bonge moja la Video ambayo ameifanyia pale kwa kallaghe inayokwenda kwa jina la My Boo

Kutoka kushoto BELLE9 ambae ni mmoja kati ya watu walioingia kwenye tuzo za KILI kama msanii aliechipukia kwa 2009 akiwa na BARNABA ambae yumo kwenye category hiyohiyo pamoja na DIAMOND ambae bado anendelea kubanana nao kwenye category hiyohiyo ya msanii chipukizi kupitia single kali iliyomtambulisha ya Nenda kamwambie...

Belle9, Angie,Diamond

Wakiwa wote

UNATAKA KUWA MUIGIZAJI???



kama unapenda kuwa muigizaji huenda ndoto yako ikawa imetimia, baada ya ziara ndefu ya kutafuta waigizaji wa Tamthilia mpya katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, kampuni ya Tuesday Entertainment chini ya mkurugenzi wake Tuesday Kihangala sasa inatafuta vipaji vipya kabisa vya uigizaji katika mkoa wa DAR ES SALAAM.

Usaili utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 11th April 2009 pale NEW MSASANI CLUB jirani na zantel kuanzia saa mbili asubuhi.

Hii ni kwa ajili ya tamthilia mpya kabisa ambayo inategemewa kuwa tishio itakayoitwa MILLOSIS. hii ni kampuni ambayo imeshafanya tamthilia nyingi zilizoweza kushika watu vibaya mno mojawapo ikiwa ni JUMBA LA DHAHABU.

Chukua fomu yako mapema kuanzia sasa katika vituo vifuatavyo

1. SAMAKI SAMAKI - Mlimani City

2. VIJANA SOCIAL HALL - Kinondoni

3. BAHAMA MAMA - Kimara

4. MSASANI CLUB - Drive in.

5. BIGGY RESPECT - Kariakoo

6. ZAKHEM PUB - Mbagala

7. MASHUJAA PUB - Vingunguti

Na usaili utafanyika chini ya madirector wa siku nyingi ambao ni GEORGE TYSON, CHRISSANT MHENGA na TUESDAY KIHANGALA.