Thursday, May 20, 2010
Wednesday, May 19, 2010
UNAKUMBUKA ENZI HIZO - PICHA BLACK N WHITE...


Hapo ni BUGGY MASTER kushoto, MWASITI akiwa kati na MIMI hapo pembeni kulia...
Tuesday, May 18, 2010
SHUKRANI KWA WOOTE TULIOKUWA PAMOJA KATIKA 40 YA MZEE WANGU
















Friday, May 14, 2010
NAWASALIMU TU.........
Wednesday, May 12, 2010
UNATAKA KUJUA KUHUSU NANI????
Nakupa hiyo nafasi unataka kujua kuhusu STAR gani hapa Bongo...
Na si vibaya ukiniambia unataka kujua nini kuhusu yeye ili nikupe kitu roho inapenda...
I will do that for you ili tuweze kwenda sawa...
Hope tuko pamoja!!!
Tuesday, May 11, 2010
VIPI HAMNA STORY...!!???
Thursday, May 6, 2010
KANUMBA AIBUKA NA WEMA TENA
Tumeshawaona kwenye A POINT OF NO RETURN, FAMILY TEARS na RED VALENTINES ambazo zote zilikuwa gumzo kubwa na ziliweza kufanya vizuri sana lakini baadae ikawa kimya kidogo kwa wao kuonekana pamoja...
Hatimae kimya kimevunjika na kwa 2010 huu ni ujio mpya kabisa wakiwa pamoja... WHITE MARIA!!!
Picha kwa hisani ya ABDALLAH MRISHO.
WANTED.....!!! WANATAFUTWA...
Awali alionekana na mtu aliekuwa akimtambulisha kama MJOMBA WAKE lakini wazazi hawamtambui kabisa mjomba huyo.
Hatimae siku ya siku alitoroka alfajiri ya saa kumi na moja, na alipofika huko akampigia simu mzazi wake na kumwambia asimtafute yuko salama na hawezi kurudi lakini mbaya zaidi katoroka na MDOGO WAKE ambae yuko kidato cha pili (FORM TWO)
Mbaya zaidi inasemekana wanaonekana mtaani wakirandaranda usiku bila muelekeo wowote.
TAFADHALI KWA YEYOTE ATAKAEWAONA WATOTO HAWA ATOE TAARIFA KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA POLISI.
Wednesday, May 5, 2010
MZEE ANAENG'ARA KWENYE FILAMU - MZEE CHILO
Jina lake halisi ni AHMED ULOTU.. amezaliwa huko Moshi Kilimanjaro siku ya tarehe 9 December 1950 akiwa ni mtoto wa pili kati ya saba, watano wakiwa wa kike na wa kiume wawili.
Elimu yake ya sekondari alianzia pale AZANIA secondary school mwaka 1966 na kumalizia hapo wakati elimu ya chuo kikuu aliipatia ISLAMIC UNIVERSITY OF MADINA huko SAUDI ARABIA ambapo alisomea Theology...
Mbali na Uigizaji Mzee Chilo ni mfanyabiashara na mwalimu by proffesional ambapo alishawahi kufundisha shule za sekondari WERUWERU, KIBOSHO, UMBWE na OLDMOSHI huko Kilimanjaro..
Kabla ya kuingia kwenye fani alikuwa anatamani sana kuwa muigizaji na siku moja alisikia tangazo la kutafuta waigizaji na ndio hapo kipaji chake kikaanza kuonekana na kiligunduliwa na mtu anaitwa Aunt Chaiba, na baada ya hapo alijiunga na DUNIA INC kama promoter kisha akajikuta ameingia kwenye fani rasmi.
Mzee Chilo ana mke na MTOTO MMOJA anaeitwa Fatma(24), na mbali na muonekano wake wa filamu kiuhalisia ni mtu wa swala tano na anamjua MUNGU vizuri sana. ila ikija kwenye kazi anafanya vizuri sana kwenye filamu.
Anamzungumzia mkewe kama mtu muelewa na anajua kwamba lengo lake ni Kuelimisha jamii hivyo hawezi kuchagua sehemu ya kucheza kwasababu pale inakuwa si yeye (tabia yake) ila ni filamu, hivyo maranyingi anapoigiza tofauti humpa taarifa mkewe kabla hata hajafanya hiko kitu.
Kitu ambacho kiliwahi kumpa ugumu katika filamu zote alizofanya ni ile sehemu aliyotakiwa kuigiza kama MZEE ANAELAWITI WATOTO WADOGO ambapo ilikuwa ni filamu ya MARIA SARUNGI inayoitwa DOGODOGO ila mwisho wa siku alifanikiwa kuifanya na ni filamu ambayo ilipata tuzo kutoka UNICEF.
Kwasasa yuko pale pilipili entertainment akiendeleza fani yake lakini Lengo lake kubwa ni kuwa Director by proffesional na si uzoefu kama madirector wengi wanavyofanya hapa Tanzania, na zaidi anataka kufika aidha Hollywood ama Bollywood hapo ndipo atakuwa amekamilisha ndoto yake ya mda mrefu.
Binafsi nampa Big up sana kwa kazi zake nzuri kwani mara zote ambazo namuona kwenye filamu anauvaa uhusika inavyotakiwa.
UNAWAJUA HAWA??? UPCOMING MOVIE STARS.. BONGOWOOD
Tuesday, May 4, 2010
HAPPY BIRTHDAY DJ VENTURE

Kila jumamosi huwa anatusababishia pale Mzalendo Pub Millenium tower unaweza ukapitia jumamosi hii uone pana happen kiasi gani.
Wish you luck in everything you do na MUNGU akubariki sana.
HAPPY BIRTHDAY BROTHER.....