Wednesday, March 30, 2011

KUTANA NA JOTI a.k.a ANDUNJE..katika process za kupiga picha!!!

hapa ilikuwa ni mjengoni (Clouds) nikiwa na joti a.k.a Andunje.. mmoja kati ya wachekeshaji ninaowakubali hapa BONGO.

Naona ukikutana na muumini na wewe unajikuta taratibu unakuwa muumini ndio kilichotokea hapo kama unavyowaona VIJANA ghafla tu nao waligeuka macomedian kwenye hiyo picha.. mi kazi yangu ilikuwa kucheka tu!!!

Kutoka kushoto ni BONGE wa powerbreakfast, ARNOLD KAYANDA, mimi ZAMARADI, MILLARD AYO pamoja na JOTI ambae ndie kawasababishia wenzake wawe makatuni kwa muda...
Hapo JOTI akionesha hairstyle yake ya sikuhizi..
Vinywele juu...
pamoja na kwamba nimemzoea lakini saa nyingine huwa nashindwa kujizuia kucheka...
Hahaa haaa.. pozi la picha lilianza hivi..
Mara akanitolea ulimi nje
Ghafla akabadilisha hali ikawa kama hivyo


Mara hee...
Ukatuni unaendelea...
Mwisho wa siku ikabidi tupozi tu serious kwa picha.. huyo ndio joti ambae anapatikana kupitia 'ORIJINO' COMEDY on TBC

ILIVYOKUWA KWENYE PARTY YA KUMPONGEZA TWENTY PERCENT (20%)

Hii ilikuwa jana pale maeneo ya TABATA ambapo mkurugenzi wa GIBS media pro ambao ndio watengenezaji wa filamu ya 20% furaha iko wapi Mr. GIDO LEWANGA aliamua kumfanyia PARTY ya kumpongeza twenty percent kwa kufanikiwa kwake kunyakua TUZO TANO za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Hapo juu twenty akiwa na mkewe pamoja na mtoto wao (aliepakatwa na mkewe) kwa taarifa tu ni kwamba hapo mkewe alikuwa akitoa burudani kwani nae ni muimbaji na aliwahi kushirikiana na mumewe kuimba wimbo wa NINGEKUSAMEHE.. na ndio huo aliokuwa akiuimba hapo
Man water Man maji producer wa twenty akitoa machache kwa twenty...
Hilda hapo kushoto, Zamaradi katikati pamoja na Mrs. Lewanga hapo kulia
nikiwa na makaka.. huyo wa kushoto sikufanikiwa kupata jina lake ila huyo wa kulia ndio Editor wa Take one anaitwa junior ambapo hapo ilikuwa jana hapohapo tabata kwenye eneo la tukio..


Burudani ikiendelea.... ambapo baadae twenty alimsaidia mkewe na burudani ikaendelea...
With a friend hapo pembeni..

Saturday, March 26, 2011

WEEKEND NJEMA JAMANI...

Nawatakia weekend njema wadau na wapenzi wote wa Blog hii..
MUNGU AWABARIKI SANA!!!

Thursday, March 24, 2011

MTOTO WA MIAKA 3 (mitatu) MWENYE KILO 60 (sitini)...

Mtoto Lu Hao mwenye umri wa miaka mitatu akiwa na uzito wa kilo 60.


MTOTO Lu Hao wa nchini China ana umri wa miaka mitatu lakini ana uzito wa kilo 60.

Ana karibu mara tano ya uzito wa kawaida wa mtoto wa umri wake na anakula mabakuli matatu ya wali wakati wa chakula cha usiku.

Alipozaliwa alikuwa na uzito wa kilo 2.6, lakini baada ya miezi mitatu alianza kupata uzito wa ghafla.
Hao ni mzito sana kiasi kwamba mama yake mzazi, Chen Yuan, kwa sasa anashindwa kumbeba.

Analazimika kumpakiza katika pikipiki wakati wa kumpeleka shule ya awali badala ya kutembea kwa miguu.

Familia ya Hao imejaribu kumfanyisha mazoezi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumnunulia vifaa vya mchezo wa kikapu nyumbani na kumpeleka mtoni ili aogelee lakini imeshindikana.

Hata akifanya mazoezi ya aina gani anazidi kuongezeka uzito na wazazi wake wanadai kuwa mazoezi yanamfanya ajihisi njaa sana.

Lu Yuncheng, baba mzazi wa Lu ana wasiwasi na afya ya mwanae na anasema: "Akiendelea kukua kwa staili hii moyo wake utashindwa kufanya kazi vizuri."

PICHA NA HABARI kwa hisani ya Global publishers!!!

COMING SOON...

Filamu mpya kabisa ambayo imeendana na mazingira halisi ya watanzania wengi.. HEKIMA..!!
COMING SOON!!!

Wednesday, March 23, 2011

HAPPY BIRTHDAY BRO.. REUBEN NDEGE a.k.a NCHA KALI...

Leo siku ya tarehe 23 March 2011 mmoja kati ya watu muhimu sana hapa mjengoni anatimiza miaka kadhaa.. The creative person Anaitwa REUBEN NDEGE a.k.a Ncha kali na huyu ndio mtu ambae yuko nyuma ya maujanja yote ya hapa mjengoni (Clouds FM radio & Clouds TV)...
Happy Birthday brother though nimekawia kidogo kukuwish but i hope sijachelewa sana.. MUNGU akubariki katika kila unalolifanya na aendelee kukuweka ili na sisi wengine tuendelee kufaidika kupitia maujanja yako!!! MUCH RESPECT TO YOU!!!

Happy birthday to you.. Happy birthday to you.. Happy birthday dear Reuben.. happy birthday to YOU!!!
Hii ni moja kati ya picha tuliyopiga pamoja.. this was last year kama sikosei.. mbali na u-creative alionao, jamaa pia ana vipaji vingi sana.. GET HIM on SO SO FRESH kila Ijumaa kuanzia saa TATU NA NUSU mpaka SABA za Usiku..
ukiachana na utangazaji ambao ni kipaji pia unaweza kumpata kupitia wimbo wa SHIMO LIMETEMA ambapo ametupia mistari yake pia kwa kushirikiana na Fid Q lakini pia JIRAMBE aliofanya na watoto wa maghorofani enzi hizo kwasasa mjengoni.. na piiaaaaaaa he is a good model & actor as well though hajaamua kujikita humo zaidi but i'll give him a DEAL this year ha haaaa.. get him through a new video ya NAKAAYA inayoitwa SHUKRANI YA PUNDA then utajua nini namaanisha.. I respect you sana brother...
HAPPY BIRTHDAY!!!!

Tuesday, March 22, 2011

BEHIND THE SCENE.. UPIGAJI PICHA WA COVER....

Filamu inaitwa WHY DID I LOVE? na ni filamu ya rose ndauka ambapo wahusika ni hao kama unavyowaona kwenye cover... na huo ni muonekano wa Poster baada ya upigwaji picha kukamilika.
Hii ndio cover ya filamu kama inavyoonekana kwa mbele na nyuma... Hii ni filamu ya rose ndauka na inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu!!!
Wanaume kazini....
Anaitwa Bonitha.. A new face kwenye movie industry!!
Yusuph Mlela akiwa na Bonitha...
Patcho mwamba nae yumo kwenye hii filamu.. hapa akiwa na Jamila!!!
Kijana akiendelea ku-show love!!
Hapa Yusuph mlela akiwa na Winnie!!!
Rose Ndauka akiwa na Jamila.. hapa ni kabla ya kuanza photoshoot.... hii kitu ilifanyika I-view media pale kwa Raqey!!!
Filamu inaitwa WHY DID I LOVE... COMING SOON!!!!

Monday, March 21, 2011

MASTAR WETU WA MOVIE.........

Jackline Pentzel (jacky wa chuzi) pamoja na Miriam jolwa (Jini kabula)
Guess what was going on!!!

Wednesday, March 16, 2011

NIMEIPENDA TU HII PICHA YAKE.. MSENEGAL ANAEFANYA VIZURI MAREKANI....

Kuna waafrika wengi wanaofanya vizuri marekani kupitia tasnia tofautitofauti na katika hao huyu pia ni mmojawapo..
Anafahamika kwa jina la GABOUREY "Gabby" SIDIBE alizaliwa tarehe 6 May, 1983 na ni muigizaji mwenye asili ya AFRICA kutoka SENEGAL ambae anafanya vizuri sana Marekani... na nyota yake ilionekana zaidi mwaka 2009 alipocheza filamu ya PRECIOUS na kwa hiyo filamu moja alijikuta akiingia kwenye nomination na iliweza kumpatia tuzo..
SIDIBE alizaliwa Bedford-stuyvesant, Brooklyn New York na alikulia Harlem, mama yake alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya kiafrika ambae ni muimbaji wa R&B na Gospel na aliweza ku-appear kwenye season ya TANO ya AMERICA's GOT TALENT tarehe 15 june 2010 wakati baba yake ni MSENEGALI anaeitwa IBNOU SIDIBE ambae alikuwa ni Dereva wa Tax..

Kikubwa kilichonivutia mpaka nikaweka yanayomuhusu kwa uchache ni hiyo Picha yake hapo juu.. imenivutia sana nikaona si vibaya kuitupia pamoja na machache yanayomhusu!!!

LEO TULIPATA UGENI KUTOKA DAYSTAR COLLEGE....

hawa ni vijana kutoka chuo cha uandishi wa habari cha DAYSTAR ambapo siku ya leo walifanya ziara ya kuja kutembelea hapa mjengoni na kuona jinsi vitu tofautitofauti vinavyoendelea hasahasa kupitia CLOUDS FM RADIO pamoja na CLOUDS TV.
Hapo nikiwa nao kwenye moja kati ya vyumba vya editing vya clouds TV ambapo ndio nilikuwa mwenyeji wao kwa siku ya leo..

Ziara ikiendelea katika sehemu tofautitofauti za CLOUDS TV.. hapo nilikuwa nikijibu baadhi ya vile nilivyoulizwa kuhusiana na Clouds TV na CLOUDS FM radio.
Kulikuwa na maswali tofautitofauti ambayo walikuwa wakiuliza ili kuweza kujifunza zaidi ukizingatia kwa kitu wanachosomea kinahusika zaidi na sehemu waliyotembelea leo..
Tukiwa katika moja ya vyumba vya Clouds TV ambapo huwa na watu tofautitofauti na ndio hapo walipokutana nao na mijadala ikawa inaendelea.
Joram Nyaumba ambae ni EDITOR wa Siz kitaa pamoja na 20 za town (aliekaa) akishangaa shangaa wageni..
zamaradi (mimi) akiendelea na maelekezo...
Hiyo ilikuwa ni leo majira ya saa sita mpaka saba katika ofisi za CLOUDS media group mikocheni ambapo wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari kutoka DAYSTAR COLLEGE walitutembelea kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na tasnia ya habari...

Tuesday, March 15, 2011

USIKOSE KUANGALIA TAKE ONE LEO USIKU...

kuna mengi ndani ya take one leo usiku lakini baadhi tu... unataka kujua yaliyojiri kwenye party ya kaole!!?? wasanii waliowika zamani kwa sasa wako wapi na wanafanya nini!!??? Unamfahamu AKI na UKWA wa Tanzania!!?? yaliyojiri kwenye kikao cha macomedians (wachekeshaji).. Unamfahamu vizuri SHAROBARO(kamata mwiiz men) kupitia mtu kati utapata kujua mengi kuhusiana na yeye, vitu kama JICHO LA TATU, BEHIND THE SCENE na mengineyo..

Pamoja na mengi mengine ambayo yatakuwa kama suprise USIKOSE TAKE ONE LEO SAA TATU KAMILI USIKU kupitia CLOUDS TV!!!!

UNAWAKUMBUKA HAWA..!!!!?????

Waliwahi kuwika sana kipindi fulani kupitia tamthilia kwenye kundi la kaole.. unawakumbuka hawa!!!???
nakumbuka enzi hizo niko shule mdogodogo naangalia michezo yao na ikifika tu jumamosi nilikuwa sikosi kwenye TV...

Enzi hizo tamthilia zetu zilikuwa na msisimko wa hali ya juu sijui kwakuwa vilikuwa ni vitu vigeni ama labda kwasasa hakuna wakali sielewi, lakini zamani tamthilia zilikuwa juu sana na ziliweza kuteka watu wengi sana tofauti na sasa...

alikuwa na character ya peke yake.. unamkmkumbuka!!!???

Katika watu waliokuwa wananifurahisha na kunichekesha kwa kipindi hiko, huyu pia alikuwa ni mmojawapo na kikubwa ni maneno yake ya papo kwa papo na majibu yake ya ajabu (mashushu) akiwa na mumewe ambae nae alikuwa na misemo iliyopitiliza.. Unamkumbuka huyu!!!???? Hao ni baadhi ya watu ambao ambao waliwahi kushika sana kupitia vipindi vya kwenye LUNINGA(tamthilia) na kwa enzi hizo walikuwa juu sana kupitia michezo yao.. mimi nawakumbuka.. vipi wewe unawakumbuka!!??? kama ndio Unaweza kunitajia majina yao kuanzia huyo wa kwanza mpaka wa mwisho na nini kilikuwa kinakufurahisha kwa kila mmoja...
UNAWAKUMBUKA HAO!!!???