Monday, January 31, 2011

BIFU LINA FAIDA AMA HASARA!!??? LINAMPANDISHA MSANII AMA LINAMSHUSHA!!!????

Kwasasa kwenye Entertainment industry tofauti na zamani kumeibuka system ya wasanii kugombana wenyewe kwa wenyewe na hii imekuwa kama kitu cha kawaida HASAHASA kwenye industry ya FILAMU tofauti kabisa na muziki..

Ukiangalia kwasasa kila kukicha utaskia huyu amegombana na huyu, mara huyu kamtukana huyu mpaka wengine kufikia KUPIGANA KABISA na vitu vingine kama hivyo.... ninachojiuliza MABIFU YANAMPANDISHA MSANII ama YANAMSHUSHA!!!!??????

Mifano hai ya mabifu yaliyowahi kutokea
1. AUNT EZEKIEL Vs WEMA SEPETU ambapo sababu ilikuwa Hartman ambae alisemekana kutembea na wema sepetu baada ya aunt.

2. WEMA SEPETU vs KANUMBA huu ulikuwa ni ugomvi mkubwa kabisa mpaka ilifikia kupelekana polisi baada ya Wema kuvunja kioo cha gari cha kanumba.. hili lilikuwa bifu la kimapenzi zaidi.

3. AUNT EZEKIEL Vs SHUMILETA sababu haikueleweka vizuri lakini nafkiri mpaka leo hawana maelewano mazuri

4. RAY Vs KANUMBA kabla hawajawa maswahiba waliwahi kuwa mafahari wawili wasiopikika chungu kimoja enzi hizo.

5. MAYA Vs SHAMSA FORD hawa walidundana kabisa kwenye sherehe moja (ilikuwa kwenye Baby Shower ya Emelda) kabla ya kugombana walikuwa mtu na dada yake lakini mambo yakabadilika.

6. JACKY CHUZI Vs JINI KABULA sababu ilikuwa MR. CHUZI ambae alikuwa mwanaume wao

7. JACKY CHUZI Vs WEMA SEPETU Urafiki uligeuka uadui kwasasa sielewi wako vipi

8. HEMED vs MLELA Hili ni bifu ambalo lilizungumziwa sana na nafkiri ni moja kati ya mabifu maarufu hapa Tanzania.

9. HEMED Vs RICHIE limejitokeza juzi na hili ndio limenifanya nijiulize bifu lina faida ama Hasara

10. JACKY WOLPER Vs SHILOLE ambao walidundana kabisa Leaders Club lakini naskia kwasasa ni mashosti tena.

11. THEA Vs MONALISA ambao walikuwa maswahiba hasa wa kufa na kuzikana lakini kwasasa mambo sio mambo tena

Hayo ni baadhi tu ya mabifu ambayo yaliowahi kutokea kwenye Industry ya Filamu, lakini ninachojiuliza ni kwamba MABIFU YANA FAIDA ama HASARA???? na BIFU KAMA BIFU LINAMPANDISHA MSANII AMA LINAMSHUSHA!!!???? msaada tafadhali..

4 comments:

  1. Dada huo ni ujinga, upofu, uelewa mdogo wa wasanii(elimu), sifa yaani kujiona bora zaidi, sioni kama bifu inajenga kihivyo ni ulimbukeni tuu wote mtu ana akili zako timamu msanii unaweza usiwe na bifu na mtu na sanaa inaendelea kama kawaida mbona sijasikia Mzee magari ana bifu na Mzee Chilo ?? unaona tofauti wale ni watu wazima iko mifano mingi ukiwaangalia kina Mzee majuto, Bambo, Kingendu, hawa wa vichekesho nao ni wasanii wa filamu pia just a comedy film hawa hawana neno kabisa, wana act kwa umoja bila kugombana na wanachekeana sijasikia bifu la kingwendu kapigana na mtu sasa hawa wengine inakuwaje hasa wanaojiona "hot cake" mimi naona ni ujinga tuu maana hawana kikubwa zaidi na hawajafika popote pale ingawa wakihojiwa wanasema kuwa actor/actress hollywood hakuna atakae fika huko na ujinga wao, film zenyewe wana act kwa buku 50 wanadaia mil 2 huku bado umepanga kigogo unasema nalipwa mil 2 kwa mwezi na matumizi m1 kwa mwezi.

    Kikubwa waende shule huku wana act wawe na ufahamu mzuri kichwani na utaona mpaka wanapo act wanaongea kiingereza kibaya wana mix ovyovoyo nani ataelewa film zao? maana waangaliaji ni hapa Tz na vijijini huko.
    wameniudhi sanaaaa .




    mdau wako Ben.

    ReplyDelete
  2. kwa fikra zangu mimi naona bifu halina faida hata kidogo zaidi linampunguzia sifa mtu,nikitolea mfano wa hemed na mlela naona kama wanajiharibia umaarufu wao hasa hasa hemed kwani kila siku anaibua bifu jipya,kwa upande wangu bifu halijengi linabomoa,

    ReplyDelete
  3. Mi nadhan kwa wanao jua bifu linaweza kuwaletea faida kama watakuwa wamejipanga couz litawaongezea umaarufu na wakitoa kazi zao wanaweza kuuza! tumesikia hata kwa wasanii wakubwa huko mbele mtu kabla ya kuto albam anweza kuzua tu kituko ili mradi tu kufufua jina na wakati huo anachia albam wakati bado mwatu wana jina lake mdomoni sikuji kwa hapa kwetu wao wako vipi@zama

    ReplyDelete
  4. Mh! Bifu! Mi naona hakuna bifu ila kuna ujinga2. Hayo mambo wanafanyaga watoto wadogo tena wakiwa wanagombania vikopo.
    Wa2 wazima wanaitanaga kiu2 uzima bwana, wanayamaliza kikubwa.

    Holiness

    ReplyDelete