JICHO LA TATU - TUTAFIKA KWELI?
Nimeona nirudie tu kitu ambacho niliwahi kukiandika nyuma lakini kwa kuongezea baadhi ya mambo pia
Katika Entertainment Industry hapa Tanzania kuna fani tofautitofauti, lakini zile ambazo zinaonekana ziko juu zaidi na zinachukua attention ya watu wengi ni MUZIKI, MITINDO na FILAMU.
Nikianza kuzungumzia Industry ya Filamu ni kitu ambacho kimekua juu ghafla tu miaka ya hivi karibuni, tofauti na Muziki ambayo ni Tasnia kongwe zaidi, Na Industry ya Filamu imeshatoa watu wengi sana ambao mpaka sasa ni MA-STAR WAKUBWA MNO hapa Tanzania na wanaendelea kufanya vizuri.
Kuna Usemi Usemao HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA ambapo maranyingi huwa tunatumia msemo huu kujifariji na kujipa moyo pale ambapo tunaona mambo yanaenda ‘Slow’ ama tofauti na matarajio yetu. Lakini tukumbuke vilevile kwamba NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI na DALILI YA MVUA NI MAWINGU, kwa upande wa wasanii wa Filamu wanaonesha hakuna kabisa dalili ya mabadiliko kati yao, wanaridhika haraka na kusahau walipotoka. Ili kuweza kufanikiwa katika vitu tunavyovifanya siku zote ni Vizuri kuangalia ‘NEGATIVES’ zetu zaidi kuliko ‘POSITIVES’ sababu kwa kuangalia mabaya na udhaifu wetu itatusaidia kuendelea mbele zaidi kwa kurekebisha tunapokosea kuliko mazuri yanayotufanya tubweteke na kuamini kwamba kilakitu kiko sawa wakati huenda ikawa tofauti.
Ili fani zote hizo ziweze kuendelea mbele kuna kitu kimoja kikubwa kinachohitajika sikuzote ambacho ni MEDIA kwa maana ya Vyombo vya habari kama Television, Radio, Magazeti, Mitandao n.k. Kupitia Vyombo vya habari watu ndio wanatambua uwepo wa watu ama kazi Fulani.
Business without advertising ni kama kumkonyeza mtu gizani. Hata kitu chako kiwe kizuri namna gani lakini kama watu hawakifahamu hakitakuwa na faida yoyote, It’s useless. Hivyo kazi kubwa ya Media ni kuripoti habari na mambo mbalimbali yahusuyo tasnia tofautitofauti ikiwemo na WAHUSIKA WENYEWE.
Ikumbukwe kwamba si kuripotiwa kwa MAZURI TU MNAYOYAFANYA bali hata pale MNAPOKOSEA media haitakuwa nyuma kwa hilo. Na hio ni kwasababu tu unapokuwa mtu maarufu wewe ni kioo cha jamii na kama kioo cha jamii watu watataka kujua mengi sana kuhusu wewe sababu kuna wanaotamani pia siku moja wawe kama wewe. Hivyo kama umeamua kuwa Star SAHAU kuhusu PRIVACY.
Lakini kwa upande wa BAADHI ya wasanii wa filamu ambao wao ndio wangeweza kuwa muongozo kwa wenzao hali inasikitisha kidogo, Inaonekana kabisa kwamba wanasahau WALIPOTOKA, Wanasahau kwamba VYOMBO VYA HABARI ndio vimewafikisha hapo walipo, wanasahau pia kwamba wao ni vioo vya jamii hivyo kila wanalolifanya jamii inataka kujua nini kinaendelea katika maisha yao.
Ombi langu tu kwa YEYOTE anaehusika msiifanye hii fani ikaonekana kama ni ya watu waliokosa muelekeo wa maisha wakaona njia pekee ni kukimbilia huku hapana. Baadhi yenu Reaction zenu zinaonesha udogo wa IQ zenu na hiyo inatukanisha moja kwa moja tasnia yetu hii nzima ya Filamu tukichukua kauli ya Samaki mmoja akioza ni wote wakati kuna wengi ambao wanajua nini wanakifanya. Kwenye hiyo ni kama inawaharibia. Filamu ni Ulimbukeni na Ujuaji mtupu uliojaa huku.
Hebu jiulizeni kuna Mastar wangapi wakubwa hapa Tanzania wame-struggle mpaka kufikia walipofika si kijina tu bali hata Kiuwezo na bado wanaheshima na kuheshimika katika jamii, hawajisahau. Mfano mzuri ni lady Jaydee ambae ni mwanamuziki, This is a real Diva na mfano mzuri wa kuigwa na watu wa tasnia zote kwa sasa, mafanikio yake yanaonekana waziwazi na hiyo ni kutokana na msingi mzuri aliojiwekea , lakini mbona hana majigambo na hizo Showing off za kienyeji!!! I RESPECT THIS WOMAN. Sidhani kama angekuwa na hizo mbwembwe mlizonazo angefika hapo alipo.
Mnachotakiwa kujua ni NO ONE IS PERFECT, kila mtu hukosea si wewe wala mimi, hata wakubwa wa nchi hukosea pia maranyingine na ndiomana kukawekwa washauri, Ubinadamu ulizingatiwa.
Sasa wewe unapokosolewa DON’T TAKE IT PERSONAL sababu hakuna mwenye Chuki na wewe, lengo ni kujenga na si kubomoa, WEWE NI NANI mpaka upambwe kila siku!? Mbona mnapenda SIFA tena zile za kijinga?? Badilikeni jamani ni aibu, nafikiri mngekuwa mnajua mastar wenzenu wa ulaya wanaishi vipi sidhani kama mngelalamika eti kwa KUKOSOLEWA FILAMU.
AMKENI JAMANI, nafikiri wengi wenu HAMJITAMBUI!!, hamjijui nyinyi ni wakubwa kiasi gani, mngelifahamu hilo msingekuwa na hoja za kitoto kama ambazo wengi wenu mnazo, nyinyi ni VIOO VYA JAMII, mtu yoyote ambae ni kioo cha jamii hawezi kufanya madudu hadharani na watu wakakosa kuongelea (media) sababu hauko kwa ajili ya familia yako, ila uko kwa ajili ya jamii nzima, na unapoongelewa HUKO SIO KUINGILIA UHURU WAKO na wala hakuna mwenye chuki na wewe, mtu akuchukie kwa kipi!!??? ama Mnakutana wapi!!?? anakuongelea kwasababu wewe unastahili kuwa mfano kwa wengine wengi ambao wanakuangalia,wewe ni Public figure..
Kumbukeni kwamba hapahapa TANZANIA tu kuna aina fulani ya watu(a certain class of people) ambao bado hatujafanikiwa kuwateka kuangalia hizi filamu zetu, mkatae mkubali hili liko wazi, na kazi kubwa inayotakiwa kufanywa ni kuangalia jinsi gani tutawavuta hawa ili wote tuwe kwenye boti moja, HATULAUMIANI kwenye hili kwani industry yetu bado changa sana, lakini pamoja na uchanga wa industry yetu, tusioneshe basi kwamba hata akili zetu ni changa pia katika kuchanganua mambo jamani, nyinyi ni wakubwa MNO na mnaangaliwa na watu wengi sana hivyo acheni utotoutoto na KUJI-HISIHISI kusikokuwa na sababu.
Mara nyingi huwa tunajipa moyo tunavyoona filamu zetu zinakubaliwa sana nchi jirani kama RWANDA, BURUNDI na CONGO.. labda niwape siri moja kwamba sababu kubwa ya kufurahiwa hivyo ambavyo tunafurahiwa ni kwasababu ya LUGHA YA KISWAHILI ambayo tunaitumia na wao wanaielewa kirahisi na si kwamba filamu zetu ni nzuri saana kupita wengine, na ndiomana nchi kama UGANDA ambao ndio tuko karibu nao zaidi Hatupokelewi kihivyo kama ilivyo nchi hizo nyingine(language barring)...
Pamoja na kwamba hiko ni kitu cha kujivunia (kupokelewa kwetu vizuri) tusibweteke basi badala yake tuongeze juhudi ambazo hata mtu ambae haelewi lugha yetu akae chini na kuangalia na kusema hii ninayoangalia ni filamu, sababu itafika muda watazoea wataona kawaida na watachoka kwani hata kama kitu ni kizuri kiasi gani lakini kama ni kilekile kilasiku KINACHOSHA na ndiomana hata sisi tumezichoka za NIGERIA kwasasa lakini miaka kadhaa nyuma ilikuwa huambiwi kitu kwa filamu hizo za Kinigeria.. Tujaribu kuwa flexible na tukubali mabadiliko.
Lack of exposure ndio tatizo kubwa linalowakibili wengi wenu, Exposure ni kitu kizuri sana jamani, tusiishie NIGERIA tu, hebu tujaribu kuangalia mbali zaidi, siku zote siri ya mafanikio ni kuangalia wenzenu walioendelea kwenye kitu Fulani wanafanya nini juu ya jambo husika, Hakuna ubaya kuiga kitu kizuri. Tanzania ukishapita mitaa miwili mitatu watu wanakugeuzia shingo na kukuita jina basi unaona umeshamaliza kila kitu na unaridhika kabisa.
Kwa wenzetu mastar wakubwa kila wanachokifanya ni habari na wanaelewa kwamba ile ndio Price of being a superstar, sasa nyinyi kuongelewa filamu tena mara nyingine hata hujaskiliza wewe umefanya tu kuletewa tu habari “INDIRECT SPEECH” ambayo maranyingi kama sio zote haifiki kama ilivyokuwa ndio mnajipanikisha hivyo na mishipa inawasimama. Tutafika kweli? hakuna kitu kibaya kama umasikini wa mawazo/akili, ni bora umasikini wa mali.
Kiukweli mnasikitisha sana na mko kwenye hali mbaya mno bila nyinyi wenyewe kujijua. Acha wanaoendelea kuwasifia ujinga wawasifie na endeleeni kujazana ujinga ila mkikutana na WENZENU wa nchi nyingine ndio mtajiona MKO NYUMA kiasi gani, mara nyingi huwa tunapwaya.
Kibongobongo mtapeta lakini kama lengo ni kufika Hollywood kama mnavyokuwa mnajibu kwenye interview zenu kwa hali hiyo ya kutotaka mabadiliko MNAJIDANGANYA.
Katika maisha yangu mimi ni mtu ambae huwa napenda sana ukweli hata kama utaniuma na sipendi kuukimbia ukweli hata siku moja, acha uniume lakini nijifunze kutokana na huohuo ukweli, tuepuke kuwa wapumbavu, bora tuwe wajinga kwasababu tutajifunza na tutaerevuka, hakuna aliezaliwa anajua, yote tumeyakuta duniani na tunaendelea kujifunza kadri siku zinavyokwenda mbele.
Mwenye masikio na asikie mwenye macho na aone, ni mawazo yangu tu si lazima ukubaliane nayo na hayahusiani na mtu yoyote.
Asante
Zamaradi Mketema.