Monday, October 10, 2011

HALI YA KIAFYA YA MZEE KIPARA SI YA KURIDHISHA SANA...

Nilipata nafasi ya kumtembelea kama mara mbili hivi kwenye wiki hizo zilizopita na kiukweli kabisa ukiangalia hali yake kiafya kwasasa naweza kusema ni kama hairidhishi.. Hii ilikuwa mara ya kwanza nilivyokwenda kumuona ambapo alikuwa akiweza hata kuinuka na kutembea kidogo
Lakini nilivyorudi mara ya pili hali ilikuwa kama tete hivi sababu hata uwezo wa kutembea mwenyewe vizuri kwasasa hana, akitaka kusimama lazima ashikilie ukuta na hata akitaka kutembea anakuwa anatambalia ukuta ambao nao naweza kusema si kwamba unamsaidia, haumsaidii chochote sababu hujikuta anaanguka pia..
Hivyo muda mwingi kwasasa huutumia kulala tu, na amekuwa hajiwezi kwa chochote kwasasa, na hata kujisaidia pia saa nyingine hujikuta anamalizia sehemu aliyokuwa saabu nguvu za kuinuka hana...
Kwasasa mzee Kipara anakaa Kigogo kwenye nyumba ya Kaole chini ya Uangalizi wa kaole ambapo kuna kijana waliemuweka ambae ndio anamsaidia bega kwa bega katika kumuuguza na kumtunza, hivyo kwa mtu yoyote ambae atatamani kwenda kumuona anaweza akafika kigogo pale na kwenda kumuona...
Kikubwa tumuombee tu aweze kurudi katika hali yake ya zamani, ambapo nakumbuka zamani ulikuwa ukienda kumtembelea alikuwa akipata hadi nguvu za kukusindikiza tofauti na sasa ambapo hata kutoka nje ya chumba chake tu ni tabu na kikubwa anacholalamikia ni miguu pamoja na kwamba kuna maradhi mengine yanayomsumbua pia...

8 comments:

Anonymous said...

pole sana mzee kipara Mungu akujalie na upone iyo miguu na vingine vyote unavyoumwa,,pole sana.No Name

Anonymous said...

NAOMBA KUULIZA IVI HUYU MZEE HANA NDUGU DASLAMU NZIMA????? HAKUWAI KUZAA AU KUOA????

Anonymous said...

Hivi kwanini hapelekwi Hospital au ndio mkwanja hamna? kila siku dvd za movie zinauzwa ebu ongezeni 500 tu ktk kila dvd hizo pesa zitaweza kumtunza huyo mzee hadi mwisho wa maisha yake.
wako
James

JIGAMBE TECHNOLOGIES LIMITED said...

POLE SANA MZEE KIPARA, MWENYEZI MUNGU ATAKUPONYA. AMEN.

Anonymous said...

Naomba kuuliza: Zamaradi, naomba kuuliza si ujinga. Mzee Kipara ni nani? Bahati mbaya mimi nilikuwa ughaibuni miaka mingi na lazima nikiri kuwa sijawahi kumsikia Mzee Kipara. Ahsante.

Anonymous said...

Jamani kwani matibabu ya tatizo lake hakuna, ebu mpelekeni hospital achene kwenye kujishow tu na kumuweka kwenye mablog mpeni matibabu jamani. vipesa mnavyompelekea havisaidii kitu.

BEATRICE said...

zama unaboa, nilikuwa napenda sana blog yako lakini siku hizi inanikeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,umekuwa mvivu sana hata kama umebanwa hizi zote ni kazi zako jifunze kujigawa kotekote bwana. Kila kitu ni kujipanga tu Zama.

Anonymous said...

hivi nyie wasanii mmeshidwa kabisa kumpeleka hospital huyo mzee? hizo pesa anazopelekwa zinamsaidia nini bila kupata matibabu? na hiyo tabia ya kujionyesha kwenye mablog mkiwa mnapeleka hivyo visent vyenu kwake hatuitaki, changishaneni mumpeleke hosp. haraka