Monday, January 17, 2011

UKIZUNGUMZIA PICHA WITH GOOD QUALITY HAPA BONGO UNAMZUNGUMZIA RAQEY with I-view media..

Hizi ni baadhi ya zile zilizonivutia zaidi kutoka kwa Raqey... Angalia Flaviana Matata na AY wanavyoonekana bila hao watu huko nyuma
Auto-focus ya hatari.. alikuwa anahitaji hao watatu tu na ndio aliodeal nao.. Flaviana Matata, AY pamoja na Martin Aloyce!!!
Angalia hii picha ndio utaelewa namaanisha nini ninaposema Raqey ni mkali
Mi ningempiga picha Pipi sehemu hiyohiyo ambayo amepiga raqey kwa angle hiyohiyo nina uhakika isingetoka hivyo ilivyotoka.. aidha ningeiunguza yakatokea matakataka au ingetoka picha tu ilimradi picha... Kweli kila mtu na mahala pake.. RESPECT!!!
Haya sasa...
Kwa yeyote anaejua picha sidhani kama tutabishana nikisema hii picha ni kali.. Ni kama wamepanga for a photoshoot kumbe kila mtu alikuwa akiendelea na mambo yake...

UNATISHA brother... you are the BEST!!

Saturday, January 15, 2011

NATAFUTA MWENZA - Mzee Magali


Mzee magali ameamua kufunguka na kuweka wazi kwamba AMECHOKA KUISHI PEKE YAKE na kwasasa anatafuta MPENZI (mwenza) wa kuishi nae milele...

Hiyo ni baada ya kuishi takribani miaka SABA akiwa peke yake baada ya MKE wake kufariki mwezi wa NANE mwaka 2004 ambapo alimwachia WATOTO WANNE wavulana wakiwa wawili na wasichana wakiwa wawili ambapo wa kwanza anaitwa JOSHUA, wa pili HAPPINESS, wa tatu anaitwa ELIZABETH ambae yuko Form one kwa sasa na wa mwisho anaitwa FRANCIS ambae yuko darasa la saba
Mbali na watoto hao ambao amezaa akiwa na mkewe ambae ni marehemu kwasasa Mzee magali ANA WATOTO WENGINE WAWILI WA NJE ambapo mmoja alimzaa kabla ya Ndoa ambae ni MWANAMUZIKI anaeitwa SISTA FAY na mwingine amezaa baada ya wengine wote ambae ndie kitindamimba wake anaeitwa MAIMATHA hivyo kwa ujumla ana WATOTO SITA...

MZEE MAGALI ameongea hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha TAKE ONE kinachorushwa na CLOUDS TV kila jumanne saa TATU kamili Usiku ambapo aliongea mambo mengi sana kuhusiana na maisha yake na hayo ni machache tu kati ya yale aliyoyaongea...
kwa mengine mengi usikose JUMANNE hii saa TATU kamili USIKU Clouds TV!!!!

Haya kwa yeyote anaetamani kuwa MPENZI wa Mzee Magali basi MILANGO IKO WAZI cha kufanya TUMA MAOMBI YAKO tu na kama utakuwa na sifa anazozitaka basi Freeeeshiiiiii, tutakuita MRS MAGALI soon..

Friday, January 14, 2011

HII KITU ILINISHINDA KABISAA...




Katika vitu vilivyowahi kunipitia pembeni hiki ni kimojawapo...

Nikiwaangalia wasichana wanaofanya hivi naona wanapendeza sana kiukweli, na binafsi NAPENDA KUONA MSICHANA anafanya hivi lakini SIO MIMI...


Naamini kwamba kila mtu ana FASHION ama STYLE ambayo imemshinda kabisa kuifanya haijalishi ni nzuri au mbaya...

Kwa wewe unaesoma hapa uwe MSICHANA ama MVULANA ni STYLE ama FASHION gani ambayo imekushinda kabisa kuifanya..!!!????

Thursday, January 13, 2011

COUPLE OF THE DAY....

My long time friend HUSNA akiwa na husband to be wake..
asietaka na aache lakini habari ndio hiyo.. haibadiliki!!
wish u guys all the best!!!
MUNGU awatangulie

HAPA NA PALE....


With my friend Salome kiganga..

That was tuesday ambapo sikuwa na mood ya kutoka kabisa but I HAD TO kutokana na some reasons.. na safari moja ikabidi ianzishe nyingine so hapo ilikuwa ni mzalendo pub ambapo Twanga walikuwa na celebrities night hivyo baada ya kutoka Mlimani city kwenye miaka mitano ya THT nikaona si vibaya nipite kuchungulia kidogo na hivyo ndivyo ilivyokuwa....

KILA LA KHERI RUGE MUTAHABA.. KILA LA KHERI THT!!!

RUGE MUTAHABA

Hapa akiwa na muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Usiku wa jumanne ilikuwa ni Siku kubwa sana kwa Tanzania House of Talents THT ambapo waliweza kuadhimisha miaka mitano tangu ianzishwe pamoja na utambulisho wa ALBUMS za wanamuziki wake...

Ni kazi kubwa sana imefanyika mpaka THT kufika hapo walipo na hatimae kujivunia mafanikio waliyonayo mpaka kufikisha miaka mitano kwani matunda yake yameonekana na yanaonekana dhahiri..

Na kinapofanyika kitu kizuri ni lazima mtu apongezwe na kwa kazi iliyofanyika sina budi kumpongeza Mr. Ruge Mutahaba pamoja na wanamuziki na wafanyakazi wote wa THT kwani mpaka hapo ilipofika si kazi ndogo.. kinachotakiwa ni kusonga mbele na kutokukata tamaa kwa maneno yoyote yanayotaka kuwarudisha nyuma kwani kazi yenu inaonekana...
Siku ya event.. Kemi pamoja na Ruge Mutahaba wakiongoza msafara wa wageni rasmi kuingia ukumbini
Products za THT siku ya utambulisho wa Album zao kutoka kushoto ni AMINI, MWASITI, DITTO, MATALUMA, BARNABA pamoja na LINA...

Naamini kwa kuanzisha THT haujasaidia tu kwenye nyanja ya Burudani bali hata katika UCHUMI WA NCHI kupitia Ajira ambazo vijana wanapata kupitia vipaji vyao unavyoviinua..

I believe SO many people are PROUD OF YOU... and Am among them!!!
Kila la kheri THT, Kila la kheri Ruge Mutahaba...

Sunday, January 9, 2011

SI NZURI KWA IMAGE YANGU LAKINI NAPENDA KUOGELEA NIKIWA MTUPU - KELLY ROWLAND

Anafahamika kama Kelly Rowland ila jina halisi ni Kelendria Trene Rowland ambae amezaliwa 11 february 1981 huko Atlanta Georgia na mama yake anafahamika kwa jina la Doris Rowland Garrison wakati baba yake ni Christopher Lovett ambapo WALIOANA baada ya KELLY kuzaliwa..
Akiwa na miaka saba mama yake alimchukua na kuondoka nae na kumuacha baba yake yake ambae alikuwa ni CHAPOMBE.
Usichokijua kuhusu Kelly Rowland ni kwamba aliwahi kurekebisha maziwa yake kama ambavyo unaweza kuona kwenye hiyo picha hapo juu.... Ambapo mwanzo alikuwa na maziwa madogo sana kama picha ya upande wa kushoto inavyoonesha na kuyaongeza kama picha hiyo nyingine inavyoonesha.

Katika Interview moja Kelly aliwahi kudhihirisha kwamba anapenda sana kuogelea Baharini akiwa NAKED kabisa na angependa kufanya hivyo MIAMI ila kinachomkwamisha ni mapaparazzi anaowahofia otherwise angeweza kufanya hivyo ingawa anajua kabisa kwa image yake si kitu kizuri.

Mbali na hayo kuna mengi ambayo unaweza ukawa huyafahamu kuhusiana na Kelly rowland na yafuatayo ni machache tu usiyoyajua kuhusu Kelly

1. Amekiri kama angeweza kubadilisha chochote kwenye mwili wake basi angeweza kufanya MIGUU YAKE IWE MIDOGO sababu anavaa NAMBA SABA NA NUSU.

2. Ingawa watu wengi hawajagundua lakini YEYE ni mzuri sana katika kufanya MAKE-UP na mara nyingi amekuwa akijifanyia make-up mwenyewe.

3. Anapokuwa na BAD HAIR DAY huwa inamlazimu avae WIG

4. Unaweza ukawa hujui lakini KELLY ni MBOVU sana kwenye kucheza TENNIS kitu ambacho kinamfanya aone aibu kidogo sababu mmoja kati ya BEST FRIENDS ZAKE ni SERENA WILLIAMS

5. Kitu cha mwisho ambacho huwa anafanya usiku ni KUSALI

6. Anapokuwa DOWN kitu ambacho kinamfanya arudi kawaida ni kufikiria kiasi gani AMEBARIKIWA na hilo tu humfanya arudi sawa.

7. Duka ambalo hawezi kupita bila kununua kitu ni Ralph Lauren pamoja na Roberto Cavalli

8. Udhaifu wake mkubwa ni PIPI na KEKI

9. Alivyokuwa MDOGO alitaka kuwa kama WHITNEY HOUSTON na alitaka sauti kama yake which was great na anaamini bado ni mkali.

10. Wimbo ambao hauwezi kutoka kichwani mwake ni wimbo wake mwenyewe unaoitwa WHEN LOVE TAKES OVER.. anaamini ni wimbo unaogusa.

11. Hana chochote anachojutia kwenye maisha yake kwasababu anaamini kupitia makosa anajifunza mambo mengi so hajutii chochote alichowahi kufanya.

12. Her proudest moment was a perfect concert perfomance alioifanya SOUTH AFRICA.

13. The best day of her life ni pale aliporealise ana UMUHIMU kiasi gani, and that was only a few years ago..

14. Kitabu anachokisoma currently ni THE MILLIONAIRE NEXT DOOR - Its about how people get rich.

15. Kinachompa furaha ni kuwa mmoja kati ya wanamuziki.

Mbali na muziki Kelly pia ni muandishi wa nyimbo, muigizaji mwanamitindo na television host.
Na kimuziki ameshafanya kazi na labels kama COLUMBIA (1997-2009) pamoja na UNIVERSAL MOTOWN (2010 mpaka sasa)
Huyo ndio Kelly Rowland ambae personally ni mmoja kati ya watu ninaowapenda sana hata bila muziki wake.. I JUST LOVE HER kama yeye....

Saturday, January 8, 2011

UKWELI KUHUSU MIMI NA LULU.....

Hii ilikuwa ni siku ya mkesha wa mwaka mpya...

Kuna mtu kupitia FACEBOOK anajiita LULU MICHAEL akijifanya yeye ni ELIZABETH MICHAEL (LULU).. na anachofanya ni kama kuvamia mambo asiyoyajua na kujifanya yeye ni LULU wakati si kweli na kuandika maneno ya ajabu anayoyajua yeye mwenyewe ili kuonesha kama kuna BEEF kati yangu mimi na Lulu which is NOT true.. ninachotaka kuweka wazi ni kwamba huyo SI LULU wa ukweli ila huyo ni mtu anaejifanya LULU ambae ndie aliweka hata zile picha za LULU za UTUPU zilizotengenezwa ambapo alijifanya kama yeye ni LULU wa ukweli na hatimae LULU alitumia kipindi changu kuweka wazi hilo swala kwamba hakuwa yeye... sasa naona this time amekuja na style nyingine.


Kwa habari tu ni kwamba jana tu LULU ametoka kunipigia akionesha kukwazika na kitendo hiko cha huyo mtu kujifanya ni yeye na kuonesha kama kuna BEEF kati yetu wakati hakuna kitu kama hiko na hilo limenifanya niamue kuliongelea ili kuliweka wazi kwa watu ambao hawaelewi kinachoendelea..


Ukweli ni kwamba MIMI na LULU hatuna beef yoyote na wala HATUJAWAHI kuwa na BEEF yoyote, tunaheshimiana sana na ni mdogo wangu ambae tunashirikiana vizuri tu kwenye kazi na mambo mengi ya karibu, hivyo huyo ni MPUMBAVU mmoja tu ambae hana kazi ya kufanya na ana sababu zake binafsi ambazo sizielewi mpaka sasa.


Kiukweli sikutaka kabisa kuliongelea hili lakini kutokana na watu wengi Kuni-INBOX kupitia facebook, kunipigia simu na wengine kuniambia kwa kudhani ni kweli ndio hiko kimenisukuma niliweke hili swala wazi otherwise halikuwahi kunisumbua ni maneno tu ambayo mtu yoyote anaweza kuongea akijiskia kuongea ambayo ni ya kawaida sana kwangu mimi na hayanisumbui akili.... na ndiomana nimekaa kimya muda wote huo lakini kutokana na wengi kutokuelewa ukweli imebidi niliweke wazi..


NINACHOTAKA KUWEKA WAZI LEO kwa watu wengi ambao hawajaelewa ukweli uko wapi ni kwamba MIMI na LULU hatuko kwenye hiyo situation na wala huyo alieandika hivyo SI YEYE ila ni LULU FEKI na LULU mwenyewe kwenye facebook hatumii jina la LULU MICHAEL kama huyo chizi anavyojiita ila anatumia jina la ELIZABETH MICHAEL...


So kwa fans wote na wale wote ambao hawakuelewa kinachoendelea huo ndio Ukweli... YULE alieandika pale kwenye facebook SI LULU.

HAPPY BIRTHDAY to you DITTO..


Leo ni siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki kutoka THT Lameck Dotto Benard maarufu kama DITTO, kiukweli kabisa mi ni mmoja kati ya washabiki wa ukweli wa Ditto na ni wimbo mmoja tu ulionivuta kwake unaofahamika kwa jina la WAPO... mbali na wimbo naweza nikamzungumzia Ditto kama mmoja kati ya vijana wenye Discipline na heshima kwa watu wote kitu ambacho kitamfanya afike mbali zaidi....

mbali na wimbo wa WAPO kuna nyimbo nyingi ambazo ameshafanya na JUMANNE ni siku nzuri ya kujua ngoma zake zote ambazo ziko ndani ya ALBUM yake pale MLIMANI CITY kwa kiingilio cha shilingi 30,000 tu ambapo ALBUM za wanamuziki SITA kutoka Tanzania House of Talent (THT) zatazinduliwa siku hiyo... Mbali na Ditto utaweza kusikia album ya wanamuziki wanaong'ara kwa sasa kama LINA, BARNABA, AMINI, MWASITI, MATALUMA pamoja na DITTO mwenyewe.. Hii si ya kukosa!!!

Hapa Ditto akiwa na muheshimiwa Rais

Kama hufahamu kijana huyu leo hasherehekei peke yake ila ni siku ya kuzaliwa ya pacha wake pia ambapo kwa pamoja wanatimiza miaka 24...

MUNGU akubariki sana kwenye kazi ya mikono yako na kila la heri ufike mbali zaidi na zaidi.

HAPPY BIRTHDAY TO YOU BROTHER!!!!

WEEKEND NJEMA JAMANI....

Si vibaya kupita kuwasalimu tu na kuwatakia weekend njema..
Nice weekend people!!!

Thursday, January 6, 2011

WATOTO NA STYLE.. MOHAWK (KIJOGOO)

Sikuhizi hata watoto nao wamo.. Cheki katoto hako nako kameweka style ya mohawk ama kijogoo kama unavyokiona... pembeni kanyolewa katikati wameacha vinywele kidogo.. mwisho wa siku nae kama kawa anaenda na fashion.. he is looking good by the way!!!

SIJAWAHI KUVUTA UNGA ila BANGI..........- TWENTY PERCENT (20%)

Katika mahojiano niliyofanya na TWENTY PERCENT AMEKIRI kwamba yeye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa BHANGI enzi hizo ingawa kwasasa AMEACHA na hatumii tena mmea huo haramu..
lakini kuna swala lingine ambalo watu wengi walikuwa wakilisema kwamba anatumia madawa ya kulevya (UNGA)..Alipoulizwa Twenty AMEKANA na kukataa katakata swala hilo la utumiaji wa madawa hayo na amesema hakuwahi hata KUJARIBU kitu kama hiko

Katika mahojiano hayo Twenty amekiri kwamba amewahi kuishi maisha ya Ghetto kabisa na ameweza kushuhudia watu wake karibu aliokuwa akiishi nao pamoja wakichomwa moto, kukamatwa kutokana na wizi, kuvuta unga na uchafu mwingine lakini yeye kama yeye hakutaka kujihusisha kwenye njia hiyo pamoja na kukaa nao pamoja ila alichoamua kufanya ni Kufocus kwenye Muziki kwa kuamini kuwa hiyo ndio njia pekee ambayo ingemtoa....


Kwasasa twenty anatamba na nyimbo zake kama TAMAA MBAYA, YA NINI MALUMBANO na nyinginezo nyingi ingawa amekiri katika nyimbo zote alizoimba WIMBO ambao unagusa maisha yake moja kwa moja ni Wimbo wa MAISHA YA BONGO ambapo vingi vinavyoonekana na kuimbwa kwenye huo wimbo ni aina ya maisha aliyopitia..


Mbali na Muziki pia kwasasa TWENTY anatamba na FILAMU yake inayofahamika kwa jina la 20% - FURAHA IKO WAPI ambapo kwa upande wangu ndani ya 2010 hiyo ndio THE BEST FILM though kuna kasoro fulani fulani kwenye upande wa quality lakini Kistory na Script IT IS THE BEST.. trust me!!!!


KWA KUIANGALIA TU HII PICHA UNAHISI INAONGEA NINI!!!!!???????

Kwa kuiangalia tu hii picha ya GENEVIEVE ambae ameshikilia tuzo na watu walio around yeye.... unahisi inaongea nini???
Tazama huyo dada wa TATU kutoka kwa Genevieve kwenda kushoto........

GENEVIEVE MAG PHOTOSHOOT

Inni Edo.. i luv this gal

So fly.. Beautiful Girls na photoshoot ya ukweli!!!!
Kate Henshaw, Rita Dominic, Genevieve Nnaji, Inni Edo.

Wednesday, January 5, 2011

MIMI SIO SHOGA - mtoto wa mama....

Anaitwa DANIEL CLAUD maarufu kama DANNY ambae kwasasa amekuwa kama gumzo fulani kutokana na COMEDY aliyoigiza inayoitwa MTOTO WA MAMA ambapo ndani humo amecheza kama SHOGA na ameonekana kuupatia sana ushoga kiasi cha mtu kuweza kumfikiria huko.. Lakini yeye mwenyewe katika mahojiano yake na mimi amekana kabisa swala la Ushoga ila AMEKIRI kwamba yeye hupenda Kampani za watoto wa kike zaidi kuliko wa kiume na marafiki zake wengi ni WASICHANA ila yeye SI SHOGA kama inavyoonekana....
Tukiwa katika mahojiano kwa ajili ya REDIO.. usikose kusikiliza siku ya kesho saa 10:45 asubuhi kwani aliniimbia hadi TAARAB na amekiri kwamba huo ni aina ya muziki anaoupenda na ukimsikiliza Mashaallah kajaaliwa sauti lakini jamani YEYE SI SHOGA....

DANNY akiwa katika pozi....


Jamani hivi ni vitu gani vinavyoweza kumtambulisha mtu kama ni SHOGA ama si SHOGA!!!??????............. je mbali na kuigiza ambako ni sanaa kuna kitu chochote ambacho anacho ama amekifanya kinachofanya watu wamjudge hivyo wanavyomjudge.... !?
usikose kusikiliza MOVIE LEO siku ya kesho saa 10:45 asubuhi...

THANKS FOR THE NEW YEAR PARTY....

Mwaka mpya huu kila mtu aliusherehekea kivyake, ila kwa watu wengi wa Mjengoni hapa tulialikwa kwenye party moja ya kuukaribisha mwaka maeneo ya Mikocheni, it was really FUN kukutana na watu wengi ninaowajua pale and i enjoyed alot.. So special thanks kwa Omar ambae ndie alieandaa party ile na asante kwa mwaliko pia....
si mbaya nikiwaletea baadhi ya matukio kwenye picha jinsi ilivyokuwa....

Regina Mwalekwa mwenye yellow shirt, Barbara Hassan kwa nyuma hapo pamoja na mimi Zamaradi Mketema Barbara, Regina, Zamaradi...

Wana wa JAHAZI.. Regina Mwalekwa pamoja na Asma Makau...

Barbara Hassan kushoto pamoja na Dina Marios kulia

HAPPY PEOPLE

sijui umbea gani hapo ulikuwa unaendelea
Nikiwa na mdogo wangu Young dee
Fetty, Mariam, Regina Mwalekwa, Zamaradi Mketema, Irene Paul..
Timu ileile na pembeni akiwa ameongezeka Asmah Makau kulia
With a brother hapo pembeni....

Hivyo ndivyo mwaka mpya wetu ulivyokuwa... It was Fun!!!

Monday, January 3, 2011

MY BEST PHOTOS 2010 (nilizozipenda).....

Picha ni ukumbusho mzuri sana na kwangu mimi ni kitu muhimu sana kwasababu naamini binadamu tunaenda tunabadilika kadri siku zinavyokwenda na hata siku moja hauwezi kurudisha wakati nyuma na hapo ndipo UMUHIMU wa picha unapojitokeza kwangu mimi, sababu utakavyokuwa leo sivyo utakavyokuwa kesho, na ulivyokuwa jana sivyo ulivyo leo na kitu pekee kinachotusaidia kutunza kumbukumbu ya jana juzi na majuzi isipotee ni PICHA and that is the reason NAPENDA SANA PICHA..

Kwa mwaka uliopita(2010) kuna picha nyingi nimepiga, baadhi nikiwa na watu na nyingine nikiwa mwenyewe, lakini katika hizo zote kuna zile ambazo nazipenda zaidi ingawa haina maana kwamba picha hizi ndio nzuri kuliko zote kwangu mimi na huenda hata wewe zisikuvutie kabisa lakini mi nazipenda tu na nina sababu tofautitofauti za kuzipenda....

Hizi ni baadhi tu katika zile ninazozipenda na nitaendelea kukuletea nyingine kwa awamu...
I can call it photo of the year kwangu mimi, it was during my Birthday 4th October 2010, mimi na Ephraim Kibonde.. Always nikikaa na huyu mtu karibu huwa nafurahi, na hapo mbavu zangu zilikuwa kwenye hali mbaya sana.. he makes me happy kiukweli.. na hii ni moja kati ya picha zangu ninazozipenda sana...

Hii ni picha nyingine ninayoipenda, hapo nikiwa na Mohammed Dewji kwenye Birthday ya muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.. October 2010.
Ni kama anaambiwa ATEEEN-SHEN... anaitwa Baghdad anapatikana Clouds FM ukitaka kumsikia utampata kupitia CLUB 10 kila Jumamosi... Amekaa kama yuko kwenye gwaride kwenye hiyo picha.. mguu pande.. mguu sawa.. naipenda hii pia!!!
Hizo ni chache tu katika nyingi.. awamu ya kwanza ndio hiyo.. awamu ya pili inakuja SOON...

NIMERUDI RASMI

Tangu niwe kimya kwenye Blog hii nimepokea maoni mengi sana tofauti tofauti kuhusiana na ukimya wangu wengine WAKINIPAKA SANA, wengine wakiniomba nifunge Blog, wengine wakiongea kwa ukali wengine kwa upole na maoni mengi sana ambayo kiukweli yote nimeyapokea kwa mikono miwili na hayajanikwaza katika njia yoyote ile badala yake yamenifurahisha sana kuona kwamba kuna watu wanafatilia blog hii...
nilikuwa kimya kutokana na sababu ambazo siwezi kuzitaja ila naahidi kwamba nimerudi rasmi though katika kurudi kwangu nitaanza kutoa matukio tofauti tofauti ambayo yalijiri kipindi cha ukimya wangu..
Otherwise nawapenda sana wote mnaonipenda na kunichukia.....
ONE LOVE!!!!