Wednesday, March 23, 2011

HAPPY BIRTHDAY BRO.. REUBEN NDEGE a.k.a NCHA KALI...

Leo siku ya tarehe 23 March 2011 mmoja kati ya watu muhimu sana hapa mjengoni anatimiza miaka kadhaa.. The creative person Anaitwa REUBEN NDEGE a.k.a Ncha kali na huyu ndio mtu ambae yuko nyuma ya maujanja yote ya hapa mjengoni (Clouds FM radio & Clouds TV)...
Happy Birthday brother though nimekawia kidogo kukuwish but i hope sijachelewa sana.. MUNGU akubariki katika kila unalolifanya na aendelee kukuweka ili na sisi wengine tuendelee kufaidika kupitia maujanja yako!!! MUCH RESPECT TO YOU!!!

Happy birthday to you.. Happy birthday to you.. Happy birthday dear Reuben.. happy birthday to YOU!!!
Hii ni moja kati ya picha tuliyopiga pamoja.. this was last year kama sikosei.. mbali na u-creative alionao, jamaa pia ana vipaji vingi sana.. GET HIM on SO SO FRESH kila Ijumaa kuanzia saa TATU NA NUSU mpaka SABA za Usiku..
ukiachana na utangazaji ambao ni kipaji pia unaweza kumpata kupitia wimbo wa SHIMO LIMETEMA ambapo ametupia mistari yake pia kwa kushirikiana na Fid Q lakini pia JIRAMBE aliofanya na watoto wa maghorofani enzi hizo kwasasa mjengoni.. na piiaaaaaaa he is a good model & actor as well though hajaamua kujikita humo zaidi but i'll give him a DEAL this year ha haaaa.. get him through a new video ya NAKAAYA inayoitwa SHUKRANI YA PUNDA then utajua nini namaanisha.. I respect you sana brother...
HAPPY BIRTHDAY!!!!

Tuesday, March 22, 2011

BEHIND THE SCENE.. UPIGAJI PICHA WA COVER....

Filamu inaitwa WHY DID I LOVE? na ni filamu ya rose ndauka ambapo wahusika ni hao kama unavyowaona kwenye cover... na huo ni muonekano wa Poster baada ya upigwaji picha kukamilika.
Hii ndio cover ya filamu kama inavyoonekana kwa mbele na nyuma... Hii ni filamu ya rose ndauka na inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu!!!
Wanaume kazini....
Anaitwa Bonitha.. A new face kwenye movie industry!!
Yusuph Mlela akiwa na Bonitha...
Patcho mwamba nae yumo kwenye hii filamu.. hapa akiwa na Jamila!!!
Kijana akiendelea ku-show love!!
Hapa Yusuph mlela akiwa na Winnie!!!
Rose Ndauka akiwa na Jamila.. hapa ni kabla ya kuanza photoshoot.... hii kitu ilifanyika I-view media pale kwa Raqey!!!
Filamu inaitwa WHY DID I LOVE... COMING SOON!!!!

Monday, March 21, 2011

MASTAR WETU WA MOVIE.........

Jackline Pentzel (jacky wa chuzi) pamoja na Miriam jolwa (Jini kabula)
Guess what was going on!!!

Wednesday, March 16, 2011

NIMEIPENDA TU HII PICHA YAKE.. MSENEGAL ANAEFANYA VIZURI MAREKANI....

Kuna waafrika wengi wanaofanya vizuri marekani kupitia tasnia tofautitofauti na katika hao huyu pia ni mmojawapo..
Anafahamika kwa jina la GABOUREY "Gabby" SIDIBE alizaliwa tarehe 6 May, 1983 na ni muigizaji mwenye asili ya AFRICA kutoka SENEGAL ambae anafanya vizuri sana Marekani... na nyota yake ilionekana zaidi mwaka 2009 alipocheza filamu ya PRECIOUS na kwa hiyo filamu moja alijikuta akiingia kwenye nomination na iliweza kumpatia tuzo..
SIDIBE alizaliwa Bedford-stuyvesant, Brooklyn New York na alikulia Harlem, mama yake alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya kiafrika ambae ni muimbaji wa R&B na Gospel na aliweza ku-appear kwenye season ya TANO ya AMERICA's GOT TALENT tarehe 15 june 2010 wakati baba yake ni MSENEGALI anaeitwa IBNOU SIDIBE ambae alikuwa ni Dereva wa Tax..

Kikubwa kilichonivutia mpaka nikaweka yanayomuhusu kwa uchache ni hiyo Picha yake hapo juu.. imenivutia sana nikaona si vibaya kuitupia pamoja na machache yanayomhusu!!!

LEO TULIPATA UGENI KUTOKA DAYSTAR COLLEGE....

hawa ni vijana kutoka chuo cha uandishi wa habari cha DAYSTAR ambapo siku ya leo walifanya ziara ya kuja kutembelea hapa mjengoni na kuona jinsi vitu tofautitofauti vinavyoendelea hasahasa kupitia CLOUDS FM RADIO pamoja na CLOUDS TV.
Hapo nikiwa nao kwenye moja kati ya vyumba vya editing vya clouds TV ambapo ndio nilikuwa mwenyeji wao kwa siku ya leo..

Ziara ikiendelea katika sehemu tofautitofauti za CLOUDS TV.. hapo nilikuwa nikijibu baadhi ya vile nilivyoulizwa kuhusiana na Clouds TV na CLOUDS FM radio.
Kulikuwa na maswali tofautitofauti ambayo walikuwa wakiuliza ili kuweza kujifunza zaidi ukizingatia kwa kitu wanachosomea kinahusika zaidi na sehemu waliyotembelea leo..
Tukiwa katika moja ya vyumba vya Clouds TV ambapo huwa na watu tofautitofauti na ndio hapo walipokutana nao na mijadala ikawa inaendelea.
Joram Nyaumba ambae ni EDITOR wa Siz kitaa pamoja na 20 za town (aliekaa) akishangaa shangaa wageni..
zamaradi (mimi) akiendelea na maelekezo...
Hiyo ilikuwa ni leo majira ya saa sita mpaka saba katika ofisi za CLOUDS media group mikocheni ambapo wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari kutoka DAYSTAR COLLEGE walitutembelea kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na tasnia ya habari...

Tuesday, March 15, 2011

USIKOSE KUANGALIA TAKE ONE LEO USIKU...

kuna mengi ndani ya take one leo usiku lakini baadhi tu... unataka kujua yaliyojiri kwenye party ya kaole!!?? wasanii waliowika zamani kwa sasa wako wapi na wanafanya nini!!??? Unamfahamu AKI na UKWA wa Tanzania!!?? yaliyojiri kwenye kikao cha macomedians (wachekeshaji).. Unamfahamu vizuri SHAROBARO(kamata mwiiz men) kupitia mtu kati utapata kujua mengi kuhusiana na yeye, vitu kama JICHO LA TATU, BEHIND THE SCENE na mengineyo..

Pamoja na mengi mengine ambayo yatakuwa kama suprise USIKOSE TAKE ONE LEO SAA TATU KAMILI USIKU kupitia CLOUDS TV!!!!

UNAWAKUMBUKA HAWA..!!!!?????

Waliwahi kuwika sana kipindi fulani kupitia tamthilia kwenye kundi la kaole.. unawakumbuka hawa!!!???
nakumbuka enzi hizo niko shule mdogodogo naangalia michezo yao na ikifika tu jumamosi nilikuwa sikosi kwenye TV...

Enzi hizo tamthilia zetu zilikuwa na msisimko wa hali ya juu sijui kwakuwa vilikuwa ni vitu vigeni ama labda kwasasa hakuna wakali sielewi, lakini zamani tamthilia zilikuwa juu sana na ziliweza kuteka watu wengi sana tofauti na sasa...

alikuwa na character ya peke yake.. unamkmkumbuka!!!???

Katika watu waliokuwa wananifurahisha na kunichekesha kwa kipindi hiko, huyu pia alikuwa ni mmojawapo na kikubwa ni maneno yake ya papo kwa papo na majibu yake ya ajabu (mashushu) akiwa na mumewe ambae nae alikuwa na misemo iliyopitiliza.. Unamkumbuka huyu!!!???? Hao ni baadhi ya watu ambao ambao waliwahi kushika sana kupitia vipindi vya kwenye LUNINGA(tamthilia) na kwa enzi hizo walikuwa juu sana kupitia michezo yao.. mimi nawakumbuka.. vipi wewe unawakumbuka!!??? kama ndio Unaweza kunitajia majina yao kuanzia huyo wa kwanza mpaka wa mwisho na nini kilikuwa kinakufurahisha kwa kila mmoja...
UNAWAKUMBUKA HAO!!!???

FACE TO FACE TOUR YA KAMBI POPOTE COMING SOON!!!!

Stay tuned on CLOUDS TV...

HEBU TUJADILI HILI TAFADHALI...

Kwasasa hivi watu wengi sana wamekuwa wakifanya AUDITION (usaili) kwa ajili ya kutafuta waigizaji wapya wa filamu ambapo mara nyingi katika kutafuta waigizaji hao huwa kuna FOMU ambazo ni lazima yule anaetaka kuigiza ainunue kutoka kwa WASANII HAO WAKUBWA ambapo mara nyingi huwa zinauzwa kwa sh 5000 ama 10,000...

na ukiangalia asilimia kubwa ya watu wanaotaka kuwa waigizaji huwa hawana maisha hayo, uwezo wao huwa ni mdogo sana wa kifedha na hata nauli ya kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine huwa ni ngumu kwa upande wao (si wote ila wengi wao)...

Sasaunapomlipisha 5000 ama 10,000 ni sawa kweli!!!!???
Hivi hili swala la wasanii wachanga ambao hawajapata nafasi ya kufanya filamu kulipishwa PESA na wasanii wakubwa kwa kigezo cha kununua fomu pale ambapo wanataka kujiunga nao ni SAWA!!????

Hii imekuwa ni BIASHARA ama ndio njia ya kusaidiana!!!!?????

Naomba msaada tafadhali!!!

I DESERVE IT... ON SET!!!

Hii ilikuwa ni behind the scene ya filamu inayoitwa I DESERVE IT ambayo imedirectiwa na ADAM KUAMBIANA
Hapa Hemed akifanyiwa make-up kwa ajili ya kuingia mzigoni..
Farid uwez (Cameraman) akiwa mzigoni
Wadada ambao nao wamo kwenye hiyo filamu.. WINNIE kushoto pamoja na mdadaa mwingine hapo kulia!!!
Jacky Pentzel aliesimama, hemed pamoja na mdadaa hapo chini
RIYAMA nae anapatikana ndani ya hii filamu.. One of the actress ambao wako REAL hapa BONGO.. naona umenenepa mamii!!!
THE DIRECTOR Adam kuambiana akiwa on set nae amecheza pia kwenye hii filamu JAMAA ANAJUA SANA AISEE.. kwa mara ya kwanza nilimuona kupitia fake pastors na baadae akaonekana kwenye filamu nyingi tofauti ila kwa sasa mtizame ndani ya I DESERVE IT.

Kwenye misukosuko
Adam Kuambiana pamoja na Jack pentzel a.k.a jacky wa chuzi wakiwa on set

MAKE-UP muhimu...
Nimependa sana ADAM alivyoigiza kwenye hii filamu.. He is so real.. itafute hii filamu halafu utaniambia
mzigo unaendelea..
Huyu ndio cameraman wa hii filamu anaitwa FARID UWEZO
watu wakiwa wamepozi baada ya kumaliza kazi.. Hii ni filamu mpya ambayo imeingia sokoni inaitwa I DESERVE IT.. kikubwa nilichokipenda humu ni jinsi waigizaji walivyokuwa real, wengi wao wamecheza vizuri sana na hata director amefanya kazi yake vizuri though mapungufu madogomadogo hayakosekani.. hiyo ni kwa upande wa uigizaji tu kama una mengine nitumie maoni yako!!!

Wednesday, March 9, 2011

MARLAW KUMUOA BESTA

Uhusiano ulikuwa wa siri kwa muda mrefu karibu miaka minne sasa na kila walivyokuwa wakiulizwa walijibu hakuna chochote kati yao ni ushkaji tu uliopo.. lakini kumbe chinichini kulikuwa na mipango mizuri iliyokuwa ikiendelea ambayo matunda yake yataonekana JUMAMOSI HII ambapo ndio WATAFUNGA NDOA rasmi na kuwa MUME na MKE ambapo besta atatambulika kama Mrs Marlaw rasmi...
Kwa taarifa tu ni kwamba Kitchen party ya mwanadada tayari imeshafanyika ambapo kwasasa kinachosubiriwa ni harusi tu ili mambo yakamilike...
Nawatakia kila la Kheri kwenye harusi yao na maisha yao kwa ujumla.. MUNGU awaongoze..
HONGERENI SANA!!!

Friday, March 4, 2011

DILI LA FUNGA MWAKA: HII NI KWA WALE WENYE MADUKA YA NGUO NA VIATU NA ACCESSORIES..


Msanii Estelina sanga maarufu kama LINAH kwa mwaka huu wa 2011 amekuwa nominated kwenye TUZO TANO katika kilimanjaro Music kupitia categories mbalimbali, Mara nyingi kwenye EVENTS kubwa kubwa nje maduka/madesigner wakubwa huwa wanajitolea kuwavalisha wasanii mbalimbali wakubwa na hiyo ni moja ya njia za kujitangaza pia kwasababu huwa kunakuwa na RED CARPET na msanii anatakiwa kupendeza na mara nyingi huwa anasema amevalishwa na nani
Kwa mwaka huu ukiangalia kiwango chake na nyimbo zake na kupitia categories hizo tano zote namtabiria Ushindi mwanadada LINA na katika hilo pale anapotokea kwenye red carpet na hata wakati wa kupokea tuzo basi lazima aonekane amewaka..

Hivyo kama wewe una duka la NGUO na unaliamini kwa maana ya unaamini duka lako lina viwango vyote vya kumtoa LINA na akapendeza hasa on the EVENT basi wasiliana na mimi kupitia 0656-956726 halafu tutakutembelea hapo ulipo na Linah na kuangalia hizo pamba katika duka lako pamoja na kupiga picha ambapo katika nguo hizo zote kutoka maduka tofauti tofauti inatakiwa ipatikane MOJA ambayo ni THE BEST na itakayoshinda ndio linah atajitupia nayo on KILIMANJARO MUSIC AWARD this year 2011.... na hilo ndio litakuwa duka la ushindi..
Hii ni kutoka zamaradimketema.blogspot.com