Nakumbuka ilikuwa siku ya pasaka tarehe 4 mwezi wa 4, 2010 ambapo ndio ULIFUMBA MACHO mojakwamoja na SIJAKUONA TENA, ilikuwa ni SIKU NGUMU SANA KWANGU na LEO ni tarehe inayonikumbusha mambo mengi sana kuhusu wewe.. umetimiza MWAKA MMOJA tangu ututoke BABA, KWANGU haukuwa baba tu ila ulikuwa babu, ulikuwa rafiki na mshauri pia,nakumbuka mengi sana kutoka kwako lakini kubwa mapenzi yako kwangu, ucheshi na utani wako na yote ambayo hakuna mtu mwingine anaeweza kuziba pengo lako.. nakumbuka usiku mmoja kabla hujafariki nilikwambia "NAKUPENDA BABA" pamoja na kwamba ulikuwa umekata kauli lkn naamini ULINISIKIA, na hiko ndio kinachonifariji mpaka leo, nitaendelea kukupenda na kukukumbuka daima.. you were the BEST DAD ever..
Kukosekana kwako kwenye maisha yangu kumeacha pengo kubwa sana kwani kuna MENGI ambayo yametokea nyuma yako lakini naamini yote ni MIPANGO ya MUNGU.. Katika maongezi yetu ya kila siku na mama haukosi kuingia hata mara moja kwani naamini ulikuwa ni wa kipekee baba.. kikubwa ambacho nakumbuka kila nikitoka ama kwenda kwenye jambo lolote ulikuwa ukiniombea kwanza na kuniambia nenda kilakitu kitakuwa sawa kwa uwezo wake MUNGU.. lakini leo haupo tena!!
Kuna muda huwa nakukumbuka najifungia ndani mwenyewe nalia sana mwisho wa siku nainua mikono juu na kumshukuru MUNGU kwani yeye aliekuchukua ndio anajua kilakitu na hajakosea.. Nakumbuka neno lako moja ulilokuwa unapenda sana kuniambia kwa utani huku unacheka "NIKIONDOKA UTAPATA TABU SANA WEWE" sikuwa naelewa maana yake kabla ama labda nilikuwa nalichukulia kirahisi lakini nafikiri sasa ndio naelewa.. ni kama bado naiona sura yako katika hali tofautitofauti...
Natamani sana ungekuwepo ili angalau uone matunda ya ulichokipanda lakini naamini MUNGU ana maana yake zaidi katika kila analolifanya na hakuna analolikosea...
M/MUNGU akuondolee adhabu na ailaze roho yako mahali pema peponi..
AMIN!!!