Tuesday, May 17, 2011

WEMA - MIMI NA BOB JUNIOR PEACE & LOVE!!, SIJAACHANA NA DIAMOND, CHALZ ANATAFUTA SKENDO KWA NGUVU KWAMBA YUKO NA MIMI ILI AANDIKWE KWENYE MAGAZETI...

Wema sepetu
Hii ni enzi ya mapenzi yao na Chalz baba
Wema na Chalz baba
Hapa akiwa na Diamond...


SIJAACHANA NA DIAMOND na SIFIKIRII HATA KURUDIANA NA CHALZ BABA
Hapo chini ukibonyeza ni interview niliyofanya na WEMA kuhusina na Kesi yake inavyoendelea kati yake na Bob Junior, Mahusiano yake na Diamond pamoja na mahusiano yake na Chalz baba, je ni kweli wamerudiana na Chalz baba!!???? kwa yote na mengine bofya hapo chini...

WEMA by zammyt25



WEMA

Thursday, May 12, 2011

MHESHIMIWA RAIS ANANIPA TABU SANA - SIMALENGA

Kama una kumbukumbu nzuri huenda umeshaiona hii sura zamani kidogo enzi hizo kwenye tamthilia ya kaole ambapo alikuwa akitambulika kama Mr. DIMERA, lakini jina halisi ni SIMON SIMALENGA ambapo kwa sasa ameachana na mambo ya maigizo na yuko hapa CLOUDS FM RADIO kama PRODUCER wa vipindi vya NJIAPANDA pamoja na JAHAZI ingawa pia hufanya na vipindi vingine lakini pia ni Mwanafunzi wa MWL NYERERE MEMORIAL ACADEMY ambapo anachukua Bachelor in POLITICS.
Alizaliwa miaka 35 iliyopita huko Njombe mkoa wa IRINGA, na elimu yake ya msingi aliipatia Tengero priamry School huko Morogoro Vijijini wilaya ya Mgeta na hiyo ilikuwa 1987 - 1993.
Baada ya hapo alipumzika kidogo mpaka mwaka 2004 alivyokuja kujiendeleza kwa kufanya Special Programs kama Private Candidate ambapo alisoma miaka miwili kwa minne.. Na baada ya hapo alichukua ADVANCE CERTIFICATE in Journalism na kisha akachukua DIPLOMA in JOURNALISM na kisha akajikuta ameingia kwenye sanaa mpaka alipokuja kuacha na kujunga na Tasnia ya Habari...


QN: TOFAUTI YA KAZI YAKE YA ZAMANI(MAIGIZO) NA YA SASA NI NINI??
ANS: Wakati nafanya maigizo nilikuwa na malengo ya kuwafikia baadhi ya watu (kiserikali na kijamii) na kwa kipindi hiko ilikuwa ni vigumu ingawa hao watu niliotaka kuwafikia huenda wao walikuwa wakiniona kutokana na kazi yangu(maigizo) ila mimi ilikuwa ni vigumu kwa upande wangu kuwafikia, LAKINI kwasasa imekuwa rahisi kuwafikia kutokana na kazi ninayofanya ingawa vyote hivi navifanya kwa malengo fulani, kwani bado kabisa sijafika ninapotaka kufika na ili niweze kufika ninapopataka hatua nyingine niliyofanya ni kurudi shule ambapo kwasasa nasoma MWL JK NYERERE MEMORIAL kama nilivyosema awali.

QN: MALENGO YAKO NI NINI HASA!!??
ANS: Malengo yangu hasa ni kuwa MWANASIASA, na ninaposema mwanasiasa si uanasiasa tu, ila mwanasasa mwenye nia ya dhati ya kutekeleza kile ninachokiona kina upungufu kwenye jamii.
QN: WEWE NI MTU WA AINA GANI!??
ANS: Kwakweli mi ni mtu ambae kwenye Starehe SIPO KABISA, na hata ukisikia kuna wimbo umetoka mpya halafu mi naujua basi ujue huo wimbo ni Mzuri kwelikweli maana mi si mfatiliaji kabisa wa hayo mambo.. Na pia napenda kufatilia nmustakabali wa taifa letu na nini kinaendelea kitaifa hata kama ni kidogo hakiwezi kunipita, ingawa kitu kingine ambacho napenda kidogo labda MOVIES, tena aina ya movies ninazopenda ni zile za KIPELELEZI.

QN: NI NINI UNACHUKIA!!??
ANS: Nachukia sana mtu kutokua serious, sipendi mtu ambae ana mzaha mzaha mwingi, mtu ambae hayuko makini, anaamka hata hajui nini kilitokea jana kiufupi huwezi kunikuta karibu na mtu wa aina hiyo, mtu ambae hayuko Current.

QN: NI KITU GANI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO!??
ANS: Nchi yangu na watu wake.

QN: KITU GANI CHA AJABU ALICHOWAHI KUFANYA NA HUENDA ANAKIJUTIA!!??
ANS: Kupata Mtoto Nje ya Ndoa, hiko ndio kitu ninachojutia ingawa haina maana kwamba simpendi mtoto wangu, nampenda sana ila tu SIKUPLAN.

QN: Tofauti ya kazi yake ya zamani(maigizo) na sasa ni nini!??
ANS: Wakati nafanya maigizo nilikuwa na malengo ya kuwafikia baadhi ya watu (kiserikali na kijamii) na kwa kipindi hiko ilikuwa ni vigumu ingawa hao watu niliotaka kuwafikia huenda wao walikuwa wakiniona kutokana na kazi yangu(maigizo) ila mimi ilikuwa ni vigumu kwa upande wangu kuwafikia, LAKINI kwasasa imekuwa rahisi kuwafikia kutokana na kazi ninayofanya ingawa vyote hivi navifanya kwa malengo fulani, kwani bado kabisa sijafika ninapotaka kufika na ili niweze kufika ninapopataka hatua nyingine niliyofanya ni kurudi shule ambapo kwasasa nasoma MWL JK NYERERE MEMORIAL kama nilivyosema awali.

QN: MALENGO YAKO NI NINI HASA!!??
ANS: Malengo yangu hasa ni kuwa MWANASIASA, na ninaposema mwanasiasa si uanasiasa tu, ila mwanasasa mwenye nia ya dhati ya kutekeleza kile ninachokiona kina upungufu kwenye jamii.

QN: WEWE NI MTU WA AINA GANI!??
ANS: Kwakweli mi ni mtu ambae kwenye Starehe SIPO KABISA, na hata ukisikia kuna wimbo umetoka mpya halafu mi naujua basi ujue huo wimbo ni Mzuri kwelikweli maana mi si mfatiliaji kabisa wa hayo mambo.. Na pia napenda kufatilia nmustakabali wa taifa letu na nini kinaendelea kitaifa hata kama ni kidogo hakiwezi kunipita, ingawa kitu kingine ambacho napenda kidogo labda MOVIES, tena aina ya movies ninazopenda ni zile za KIPELELEZI.

QN: NI NINI UNACHUKIA!!??
ANS: Nachukia sana mtu kutokua serious, sipendi mtu ambae ana mzaha mzaha mwingi, mtu ambae hayuko makini, anaamka hata hajui nini kilitokea jana kiufupi huwezi kunikuta karibu na mtu wa aina hiyo, mtu ambae hayuko Current.

QN: NI KITU GANI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO!??
ANS: Nchi yangu na watu wake.

QN: KITU GANI CHA AJABU ALICHOWAHI KUFANYA NA HUENDA ANAKIJUTIA!!??
ANS: Kupata Mtoto Nje ya Ndoa, hiko ndio kitu ninachojutia ingawa haina maana kwamba simpendi mtoto wangu, nampenda sana ila tu SIKUPANGA kupata mtoto.

QN: NI NINI UNATAMANI KUULIZWA NA HUJAWAHI KUULIZWA POPOTE!!??
ANS: Ni kuhusu SIKU YANGU YA KUZALIWA, Sijawahi kuulizwa na mtu ninajisikiaje ikifika siku yangu ya kuzaliwa... Kiukweli kabisa SIJAWAHI KUJISIKIA VIZURI kwenye siku yangu ya kuzaliwa, sababu inaweza ikawa ya kipuuzi lakini kwangu ni ya msingi, Kwanza kabisa naona muda unakwenda hivyo najihisi nina deni na changamoto kubwa sana kwa jamii ya kitanzania kwani mimi kama kijana najihisi sijatoa mchango kwa kiasi cha kutosha hata kwa jamii inayonizunguka, hiyo ndio sababu kubwa.

QN: KITU GANI HATUJUI KUTOKA KWAKO??
ANS: Sijawahi kufanya Birthday katika maisha yangu na wala sitegemei.

QN: KINGINE TUSICHOKIJUA??
ANS: Kuna mtu ananipa Tabu sana kwenye maisha yangu, na huyu si mwingine ila ni Muheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA MRISHO KIKWETE, na kikubwa kinachonipa tabu kutoka kwa huyu mtu ni kwamba huwa natamani sana kujua kama ningekuwa na uwezo ningeweza kuingia kwenye kichwa chake ili nione tu muda wote NI NINI AMBACHO HUWA ANAFIKIRIA AMA KUWAZA, natamani sana kujua muheshimiwa rais huwa anawaza nini na pia nijue ni Mtu wa aina gani sababu huwa anabadilikabadilika sana, mara nyingine huwa charming na mara nyingine huwa tofauti kabisa, na nashkuru kwa mwaka huu nimepata bahati ya kuonana nae zaidi ya mara tatu lakini bado kuna kitu huwa kinanipa tabu sana juu yake sababu sijawahi kuongea ambacho ninacho kwenye kichwa changu (ninachotaka/tamani kumwambia).






QN: NANI ANAKU-INSPIRE??
ANS: Mh. Jakaya Mrisho Kikwete huwa anani-insipire sana, naweza nikasema hata kurudi kwangu shule kumechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na yeye, na ilikuwa nisomee sheria lakini nikaona nikisomea sheria itakuwa ngumu sana kumfikia hivyo nikaona nisomee habari na kwa kupitia hilo nashukuru nimeweza kuonana nae zaidi ya mara tatu kwa mwaka jana ingawa sijawahi kuongea ambacho ninacho kwenye kichwa changu.

QN: TOFAUTI YA ALICHOKUWA AKIKIFANYA ZAMANI NA SASA??
ANS: Zamani nilipokuwa kwenye maigizo ilikuwa tunatumia kipaji lakini ilikuwa ngumu sana kutumia akili yako kuweka ubunifu.. mambo mengi yalikuwa yanaendeshwa na kipaji zaidi na hiyo ilitokana na watu waliokuwa wakinizunguka, lakini kwasasa angalau kati ya ASILIMIA 100 angalau natumia hata 45% ya ubongo wangu katika kufanya mambo tofautitofauti, na hata sehemu ninayofanyia kazi inanipa uhuru wa mimi kufanya kazi yangu vizuri na haikulimit katika kufikiria. na kizuri zaidi kinachonifurahisha nina uhuru hata wa kujiendeleza kielimu tofauti na makampuni mengine ambayo ukisema unaenda kusoma basi ni kama umejifukuzisha kazi mwenyewe.

QN: KATIKA WATU WOTE ALIOWAHI KUWAHOJI, NI WATU GANI ALIFURAHI SANA KUHOJIANA NAO??
ANS: Mheshimiwa Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE, Profesa ANA TIBAIJUKA, pamoja na WAZIRI WA MAMBO YA NJE mh. BENARD MEMBE.

QN: MWISHO KABISA UNA CHOCHOTE CHA KUONGEA??
ANS: HUWA NAKERWA SANA na Baadhi ya MAWAZIRI, MANAIBU na MAKATIBU WAKUU WA WIZARA mbalimbali ambao hufanya baadhi ya taarifa za kiserikali kuwa SIRI.. wakati mara nyingi ninapotaka mahojiano nao huwa ni kwa nia njema na kwa maslahi ya taifa

Wednesday, May 11, 2011

LOVELY COUPLE... BABA JONII (ADAM MCHOMVU) na MAMA JONII

Anaitwa ADAM MCHOMVU (Baba Jonii) the brother from another mother akiwa na the longtime girlfriend AYSHA MCHOMVU (mama jonii)..

Hii ilikuwa ni Red Carpet ya kili Music awards this year.. Kiufupi Mama jonii anajua nini maana ya fashion huwa hakosei karibu mara zote ninazokutana nae, nafikiri hata hapo hali inajieleza!!!!

They look soooo good together kiufupi ni Nice Couple!!!!

MATUMIZI YA KINGEREZA KWENYE FILAMU ZETU..!!!



Si vibaya kutumia kingereza kwenye filamu lakini inategemea na sehemu gani tunatumia, mara nyingi huwa tunatumia ndivyo sivyo na hiyo imejitokeza kwenye filamu nyingi sana za kitanzania.. Hii si lugha yetu, ni lugha ambayo wengi wetu tumeikuta (lugha ya pili) hivyo haitegemewi kwamba tutakuwa Fluent katika kuongea, lakini vilevile hiyo isifanye tujiendekeze na kuchapia waziwazi hivyo inabidi tuwe makini sana wakati wa kukitumia kwasababu hizo filamu zinatazamwa na watu wa aina na mataifa tofautitofauti...

Hizo ni baadhi ya CLIPS za filamu ambazo kingereza kimetumika ndivyo sivyo... !!!!

NDOA YA IRENE UWOYA YAJIBU.. AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME.. KWASASA ANAITWA MAMA CHRISS!!!!!

Bongo movie star the sexiest Irene Uwoya amejifungua mtoto wa kiume siku ya Tarehe 8 mwezi huu (may) mwaka 2011 katika hospitali ya REGENCY hapa hapa DAR ES SALAAM, anasema kwamba anajisikia furaha sana kupata mtoto kiasi kwamba hawezi kuelezea..
Anasema ndoto zake siku zote ilikuwa ni kuwa na Mtoto hivyo kitendo cha kupata mtoto kimemfurahisha kupita kawaida...
Anasema pamoja na kuwa mama haina maana kwamba ameacha game (filamu) alichosema ni kwamba yeye bado yupo kwenye game ingawa kwasasa anaconcetrate kidogo kwenye swala la malezi lakini bado yupo kwenye game!!!!

Kwa habari zaidi na ukitaka kumsikia yeye mwenyewe akiongelea hilo.. Sikiliza MOVIE LEO siku ya kesho saa nne na dakika 45 asubuhi ndani ya CLOUDS FM RADIO.

HONGERA SANA IRENE KWA KUPATA MTOTO!!!!!

AUNT EZEKIEL AKIELEZEA UJIO WAKE WA DODOMA WIKI HII NDANI YA SERENGETI FIESTA FILAMU...



Hapo juu ni AUNT EZEKIEL akielezea dhumuni la safari ya DODOMA wiki hii kwenye SERENGETI FIESTA FILAMU ambapo lengo kubwa ni kutafuta vipaji vipya kabisa kwenye filamu ambapo tulianza na mikoa ya Mwanza na Arusha na wiki hii ni zamu ya DODOMA ambapo tutakuwa pale ROYAL VILLAGE siku ya JUMAPILI HII katika usaili wa kutafuta waigizaji wapya kabisa katika filamu..
Kupitia CLOUDS nitakuwepo mimi nikiongozana na MASTAR wa filamu akiwemo AUNT EZEKIEL.. hivyo kama una kipaji cha kuigiza na una ndoto za kuwa STAR mkubwa wa filamu, tukutane pale ROYAL VILLAGE siku ya JUMAPILI hii hapa.

HEMED - HAKUNA MSICHANA ANAENIVUTIA KATIKA MASTAR WA MOVIE BONGO... HII NI MOJA KATI YA INTERVIEWS ZILIZOLETA GUMZO SANA HAPA BONGO...



Hii ni moja kati ya interviews ambazo niliwahi kufanya na mastar wa movies na ikaleta gumzo sana, na hiyo yote ilitokana na majibu aliyokuwa akiyatoa HEMED kwenye maswali niliyokuwa nikimuuliza, na pia vitu alivyokuwa akiongea ambapo alizungumzia kwamba hakuna 'demu' yoyote anaemvutia yeye katika hawa wanaofanya movies.

Na pia kikubwa alichokuwa akitamani kuulizwa ni swala la wake za watu ambapo alisema wake za watu huwa wanamsumbua sana kimapenzi.. kuna mengi sana ambayo ameongea kupitia MTU KATI ambapo hii ni moja kati ya SEGMENTS zinazopatikana kwenye TAKE ONE ambapo hii ni sehemu ya kumjua mtu zaidi na vile tunavyomuona kwenye Movies..
Kwa MENGI ZAIDI.. Bofya hapo juu upate kumsikia HEMED.

Tuesday, May 10, 2011

NI KWELI KWAMBA WEMA NA DIAMOND WAMEACHANA!!!??????

Hii ni habari iliyotoka kwenye gazeti la Global publishers ambapo siku chache tu kabla ya habari hii, WEMA alitoka kuelezea how much wanapendana na DIAMOND!!!!



Juzijuzi tu hapa WEMA SEPETU alijitokeza hadharani na kuanika uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond kupitia TAKE ONE ambapo aliweza kueleza mengi sana kuhusiana na mipango yake na Diamond kimapenzi na kimaisha, lakini ghafla metoka habari kwamba WAWILI HAO hawako pamoja tena...
Je ni kweli kwamba wameachana ama ni maneno tu..!!??





kwa habari zaidi stay tuned kupitia blog hii hapa kama ambavyo uliweza kumsikia kwa mdomo wake basi atakupatia majibu yako yote kupitia yeye mwenyewe tena muda si mrefu....



Is that Love gone bad!!???

TOP TEN QUOTES za ARNOLD SCHWARZENEGGER... NI QUOTES GANI UNAZIKUMBUKA KUTOKA KWENYE MOVIES ZA KITANZANIA!!!???



Hiyo hapo juu ni misemo kumi ya Arnold kutoka movies tofautitofauti.....

Mara nyingi kwa hawa wacheza movies kuna msemo fulani ama kitu fulani ambacho mtu huwa anapenda kukitumia kwenye movies zake tofautitofauti, na hiko kitu huwa ni kitu kimoja ambacho huwa kinajirudiarudia mpaka kinakuwa kama IDENTITY ya mtu fulani...
Hapo juu ni video inayoonesha jinsi Arnold ANAVYO-SCREAM ambapo style yake ya kuscream n ileile kupita movies tofautitofauti.

Ni msanii gani wa BONGO ambae hupenda kutumia kitu kimoja ama MSEMO mmoja kwenye movies zake tofautitofauti, huenda unaufurahia huo msemo ama unakukera.. lakini swali ni MSEMO UPI ama KITU GANI kutoka kwa msanii wa BONGO ambacho unakijua huwa kinajirudiarudia kupitia MOVIES zake tofautitofauti....!!!???

Wednesday, May 4, 2011

HAPPY BIRTHDAY DJ VENTURE... 'MDAU'

Naona watu wengi sana wamezaliwa mwezi wa tano na katka hao yupo brother kutoka hapa MJENGONI anafahamika kwa jina la Boniventure Kilosa maarufu kama DJ VENTURE ambae huwa anatusabababishia mambo mazuri pale MZALENDO PUB kila jumamosi katika ile FLEVA NIGHT....

HAPPY BIRTHDAY BROTHER.. mi huwa napenda sana kukuita MDAU kutokana na mambo yetu yaleee nafkiri umeshanisoma.. wish u the best and Be good always!!!!!

VAZI LIPI LIMEKUVUTIA ZAIDI!!!???? The Knowles-Carters Celebrate Alexander McQueen’s Legacy With The Beautiful People Of NYC....

Beyonce na Jigga (jay -z) .


Pamoja na kupendeza kote lakini hili ndilo vazi llilomponza beyonce ambapo lilionekana kumbana sana kiasi cha yeye kushindwa kupanda ngazi na kutembea vizuri na kasababisha kuzomewa.. (cheki video chini)
Marc Anthony na J-lo
John Legend na Christine teigen
Jennifer hudson na Vera Wang
Jessica Alba akiwa na Cash Warren

Janelle Monae na Bruno Mars
Alicia keys na Swiss Beats
Fergie na Josh Duhamel
Marc jacobs
Lala Vazquez na Carmelo Anthony
Karl lagerfeld na blake lively
Kanye West na Lyor Cohen




Vazi la nani limekuvutia zaidi katika hayo yote hapo juu!!!????

Tuesday, May 3, 2011

BEYONCE AZOMEWA.. SABABU NI NGUO ILIYOMBANA SANA MPAKA AKASHINDWA KUTEMBEA!!

BIBI AKIKAMUA KWENYE USAILI WA KUTAFUTA WAIGIZAJI ARUSHA....


Kitu kilichonifurahisha kwa bibi huyu, alivyoingia tu hakutaka kusikia ACTION wala salamu, yeye moja kwa moja aliingia na kuanza makamuzi, hakujali kama camera iko kwake wala nini but mwisho wa siku alifanya vizuri na ni mmoja kati ya watu waliofanikiwa kupita kwenye mchujo huo!!!!
Hii ilikuwa ni SERENGETI FIESTA FILAMU jumamosi hii iliyopita ambapo tulikuwa mkoa wa ARUSHA katika kutafuta vipaji vipya kabisa kwenye swala zima la filamu kwa hisani kubwa ya SERENGETI PREMIUM LAGER!!!!!

Monday, May 2, 2011

I JUST LOVE THE PIC.. SO LOVELY!!!!

Pamoja na kwamba imeshapita.. lakini mimi nimeipenda tu hii picha.. Very very sweet!!!

Sunday, May 1, 2011

SONG OF THE DAY...

GOLDEN MOMENTS na SERENGETI FIESTA FILAMU... TIME TO SHOW LOVE...........!!!

Hapo nikiwa na wawakilishi kutoka SERENGETI.. time to show love!!!
Kama kawaaz... kushoto anaitwa Hamisi kutoka serengeti, mimi hapo kati(zamaradi mketema) na brother mwingine kutoka SERENGETI!!
Uncle hapa alinifata akaniambia mke wake ni mpenzi sana wa kipindi changu (TAKE ONE) na ananipenda sana.. hakosi kabisa kipindi!!!! Shukrani sana kwake na kwa Fans wangu wotote.. NAWAPENDA SANA!!!
Hapa nikiwa na warembo kutoka Arusha...
With Hemed.....
makini na kazi!!!! Hapa kuna mtu alikuwa ananiacha hoi sana

Uvumilivu ulitushinda, kwa vituko vya humo... huwezi kujizuia, utajikuta unacheka tu!!!
GOLDEN MOMENTS!!

Saturday, April 30, 2011

HAPPY BIRTHDAY BOSS.....!!!!


Question: What do you call people who work for you?
Answer: Very lucky

I just wanna say that I am so lucky to have you as my boss coz It's nice to work for someone who knows the secret to being a good manager... being a good person.

Happy Birthday to the world's best boss Mr. Ruge Mutahaba!


You are a wonderful person and a great boss. Wishing you success in work and life. keep up the good work.

ILIVYOKUWA LEO ARUSHA KWENYE USAILI WA KUTAFUTA WAIGIZAJI (SERENGETI FIESTA FILAMU)..

Mimi (Zamaradi Mketema) nikiwa na Hemed Suleiman tukifatilia mchakato mzima kwa umakini siku hii ya leo hapa Mawingu City centre Club Arusha!!!
Reginald Maro a.k.a P.Diddy ambae ndie cameraman wa Take One akiwa makini na kazi yake!!

Msichana kutoka Mwanza akionesha kipaji chake.. hapo alikuwa akichezeshwa na Hemed...

Jamaa katika kuigizaigiza akajikuta kampa mikono ya ukweli HEMED naona mzuka ulikuwa umempanda.. but it was all good!!!
Katika vitu vilivyonivutia leo kimojawapo ni huyu bibi ambae nae alikuja kuonesha kipaji chake....

Anaitwa HAWA SIAMI.. naweza nikasema Bibi ana kipaji sababu alikamua kwelikweli, na kingine kikubwa hakutaka kusikia neno ACTION, yeye aliingia tu na moja kwa moja makamuzi yakaanza mambo ya salamu sijui nini baadae huko.. Bibi alitisha.. soon nitakuwekea clip yake ya Video ili na wewe ufaidi nilichofaidi...
Jamaa alijipanga hadi na mabuti ya mgambo pamoja na Kirungu.. kiufupi kila mtu aliejitokeza alipata nafasi ya kuonesha kipaji chake.. Kwa picha zaidi za matukio.. endelea kusikilizia muda si mrefu nitakuletea mengine yaliyojiri!!!

SERENGETI FIESTA FILAMU ARUSHA...

Hii ilikuwa ni jana wakati tumewasili ndani ya A-City!!
Nikiwa na mmoja kati ya washiriki wa serengeti fiesta filamu
Ndani ya Studio za Clouds FM Arush, Zamaradi, Hemed katikati pamoja na DJ Ally kutoka 87.9 Arusha
Mzigoni....

VIPAJI VIPYA KWENYE MOVIE kutoka MWANZA



Hao ni baadhi ya washindi waliopatikana MWANZA kupitia Serengeti Fiesta Filamu ambapo hii ni project ya kutafuta vipaji vipya kabisa kwenye tasnia ya Filamu na tulianzia MWANZA na washiriki waliofanikiwa kupita baadhi yao ni hao hapo,hivyo tegemea mambo makubwa sana kutoka kwa vijana hao..
Katika hao kuna yeyote ambae kakuvutia!!??? Kama yupo ni yupi!?? na nini hasa ambacho kimekuvutia kwake!!?? kiufupi yupi unamtabiria makubwa zaidi!!????

Thursday, April 28, 2011

H-BABA AKIONGELEA ANACHOKIKUMBUKA KUTOKA KWENYE UHUSIANO WAKE WA KIMAPENZI WA ZAMANI NA IRENE UWOYA... pamoja na mahusiano yake ya sasa.





Hii ilikuwa ni interview iliyofanyika on TAKE ONE kupitia CLOUDS TV ambapo Wema aliongea anachokikumbuka kutoka kwa kanumba ambae ni aliekuwa mpenzi wake, na baada ya hapo niliongea na H-baba ambae kwasasa yuko kwenye mahusiano na Flora mvungi lakini hii si mara ya kwanza kwake kudate STAR wa movie hivyo na yeye nilimuuliza anachokikumbuka kutoka kwenye uhusiano wake uliopita ambapo alikuwa akitoka na Uwoya kabla ya Flora.

MAREKEBISHO ON WEMA SEPETUs INTERVIEW

kwa wale ambao walitaka kuiangalia interview ya WEMA, marekebisho yameshafanyika na sasa unaweza kuiona bila tatizo lolote
Asanteni.