kwa kuziangalia tu hizo sura hapo juu unahisi zinaletaleta na nani!!???hao watoto unaowaona hapo juu ni mapacha, na mmoja kati yao kwasasahv ni mmoja kati ya mastar wakubwa sana wa filamu hapa tanzania..
hebu niambie ni nani!????
This Blog is all about Social and Entertainment issues... Karibu kwenye Dunia yangu!!! kwa mawasiliano tumia zamaradi.takeone@gmail.com
niliweka hii picha hapo juu na kuomba watu waguess huyo ni nani.. na wengi wameonekana wako makini sana na kutaja jina la hemed, na hilo ndio jibu sahihi.. huyo ni hemed suleimaan akiwa na mama yake mzazi na hapo aalikuwa na umri wa miaka 5, na ilikuwa ni mwaka 1991!!
hii ni picha inayoonesha walivyo sasa.. hemed na mama yake
na hapa ni hemed mwenyewe ama phd kama anavyopenda kujiita.. nakuletea mwingine soon ili uchemshe bongo kdg

hako katoto unakokaona hapo juu ni mmoja kati ya mastar wakubwa sana wa filamu kwa sasa.. hapo akiwa na mama yake.. hebu hisi huyo ni nani!??? halafu nipe jibu..
hapa ni baba yake mzazi na mama yake enzi hizo.. hii ni kukupa clue tu ili upate urahisi wa kutambua.. kwa kuwaangalia unahisi wamefanana na msanii gani wa filamu kwa sasa!??










Msanii Star wa filamu ambae alianza kuigiza akiwa na umri mdogo ameamua kufunguka na kuweka wazi kwamba ana mpango wa kwenda EUROPE kwa sababu moja tu ya kumtafuta JUSTIN BIEBER....
Nilipata nafasi ya kumtembelea kama mara mbili hivi kwenye wiki hizo zilizopita na kiukweli kabisa ukiangalia hali yake kiafya kwasasa naweza kusema ni kama hairidhishi.. Hii ilikuwa mara ya kwanza nilivyokwenda kumuona ambapo alikuwa akiweza hata kuinuka na kutembea kidogo
Lakini nilivyorudi mara ya pili hali ilikuwa kama tete hivi sababu hata uwezo wa kutembea mwenyewe vizuri kwasasa hana, akitaka kusimama lazima ashikilie ukuta na hata akitaka kutembea anakuwa anatambalia ukuta ambao nao naweza kusema si kwamba unamsaidia, haumsaidii chochote sababu hujikuta anaanguka pia..
Hivyo muda mwingi kwasasa huutumia kulala tu, na amekuwa hajiwezi kwa chochote kwasasa, na hata kujisaidia pia saa nyingine hujikuta anamalizia sehemu aliyokuwa saabu nguvu za kuinuka hana...
Kwasasa mzee Kipara anakaa Kigogo kwenye nyumba ya Kaole chini ya Uangalizi wa kaole ambapo kuna kijana waliemuweka ambae ndio anamsaidia bega kwa bega katika kumuuguza na kumtunza, hivyo kwa mtu yoyote ambae atatamani kwenda kumuona anaweza akafika kigogo pale na kwenda kumuona...
Kikubwa tumuombee tu aweze kurudi katika hali yake ya zamani, ambapo nakumbuka zamani ulikuwa ukienda kumtembelea alikuwa akipata hadi nguvu za kukusindikiza tofauti na sasa ambapo hata kutoka nje ya chumba chake tu ni tabu na kikubwa anacholalamikia ni miguu pamoja na kwamba kuna maradhi mengine yanayomsumbua pia...
Kwa leo sina mengi sana ya kuongea ila zaidi ni kukushukuru kwa kuweza kutambua siku yangu hii muhimu na kufanya kitu cha kuweza kunipa na kuongeza furaha katika siku yangu... Thats what friends are for!!!..
Nakupenda sana... Together Forever!!!
Katika tarehe ambazo nazipenda basi nafikiri tarehe 4 ya mwezi wa KUMI itakuwa inaongoza sababu ndio siku niliyozaliwa..

Hakuna zaidi yako mama
LOVE YOU MAMA, VERY PROUD OF YOU!!!!!
Anaitwa MLOPELO, kwa wale ambao ni wafUatiliaji wa maigizo ya kaole kipindi hiko hatakuwa mgeni kwenu, alikuwa akiigiza kama mchawimchawi hivi akishirikiana na bi mwenda enzi hizo, ila kwasasa ni kama amesimamisha shughuli za sanaa kwa muda kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda wa miaka miwili..
Nimekuwa kimya kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja sasa, kuna wengi wametuma comments negatives and positives kulalamikia hali ya ukimya wangu.. lakini kiukweli kabisa kwa wote waliotuma comments ziwe mbaya ama nzuri nathamini sana kwakuwa mnanithamini pia na ndiomana mnapoingia na kukuta hamna kitu,kidogo mnakuwa mnakwazika na kuongea vile ambavyo mnaongea..
Hongera sana Venture kwa kufanikiwa kuivuka hatua hii muhimu sana kwenye maisha!!!! kila la kheri kwenye ndoa yako!!