Monday, November 12, 2012

STAY TUNED... BACK sooon...

Its been a year now since my last post on this blog.... nimepata comments nyingi sana watu wakinisema kuhusiana na ukimya wangu tena wengi wakinichamba hasa.. sitaki kutoa sababu yoyote on why nilikuwa kimya kwa muda wote huo sababu mwisho wa siku haitasaidia chochote kile..

kikubwa nawapenda woooote sana sana mliotuma comments mbaya na nzuri sababu mmeniamsha na kunifanya nione how this blog of mine ina mafans... am happy'

Muda si mrefu nitarudi rasmi kabisa kwa nguvu ileile ili tuweze kwenda sawa.... got so many things for you guys so just stay tuned sweethearts'

 Ntaanza tu kuwawekea vipindi ambavyo hii ni maombi ya baadhi ya watu ambao wako nje na hawakufanikiwa kuviona lakini kwa updates ya vitu tofauti vinavyoendelea soooooon tutakwenda sawa..

NAWAPENDA WOOOOOOTE SANA SANA!!!!!!

Thursday, November 10, 2011

MWINGINE HUYO.. GUESS WHO!!

kwa kuziangalia tu hizo sura hapo juu unahisi zinaletaleta na nani!!???

hao watoto unaowaona hapo juu ni mapacha, na mmoja kati yao kwasasahv ni mmoja kati ya mastar wakubwa sana wa filamu hapa tanzania..
hebu niambie ni nani!????

MMEPATIA.. lol

!niliweka hii picha hapo juu na kuomba watu waguess huyo ni nani.. na wengi wameonekana wako makini sana na kutaja jina la hemed, na hilo ndio jibu sahihi.. huyo ni hemed suleimaan akiwa na mama yake mzazi na hapo aalikuwa na umri wa miaka 5, na ilikuwa ni mwaka 1991!!
hii ni picha inayoonesha walivyo sasa.. hemed na mama yake
na hapa ni hemed mwenyewe ama phd kama anavyopenda kujiita.. nakuletea mwingine soon ili uchemshe bongo kdg

G5 click wanakuletea.. BODA KWA BODA beach concert!!


BODA KWA BODA BEACH CONCERT ON 12th Nov.....,here comes what you have been waiting for tz BODA KWA BODA BEACH CONCERT..Stage will be covered by Jaguar from Kenya ,Sumalee,Country boy & Stamina,GodZilla,Aslay,Beka,Reycho,Young D and many more.Dj Zero will be on the mix to make the crowd going crazzieeee with the hottest hitz.

ENTRANCE : 10,000tshs
VENUE: MBALAMWEZI BEACH "the finest beach"
TIME: 7pm

Monday, November 7, 2011

GUESS WHO...!

hako katoto unakokaona hapo juu ni mmoja kati ya mastar wakubwa sana wa filamu kwa sasa.. hapo akiwa na mama yake.. hebu hisi huyo ni nani!??? halafu nipe jibu..hapa ni baba yake mzazi na mama yake enzi hizo.. hii ni kukupa clue tu ili upate urahisi wa kutambua.. kwa kuwaangalia unahisi wamefanana na msanii gani wa filamu kwa sasa!??

HONGERA SANA VENTURE kwa kutuletea BABY GIRL...

hhatimae ndoa imejibu, hapo juu a new baby girl akiwa na auntie.. kako soo chwit jamani.. na kanaonekana kajanja.. lol
nhapo juu ni new parents berna na venture.. hongereni sana sana,

Friday, October 28, 2011

MOJA YA SCENE ZILIZOWAHI KUNIFURAHISHA ZA FILAMU...


Haimaanishi kwamba hiyo filamu ndio the best film hapana, ila ninachozungumzia ni kipande nilichokipenda ambacho kinapatikana kwenye filamu inayofahamika kwa jina la MTAANI KWETU..
Kizuri lazima kisifiwe na hata pale tunapoenda tofauti lazima tuongee pia lengo ni kusonga mbele zaidi na hakuna chuki binafsi..

Hiko ni kipande kinachomuonesha Richie kama mtu aliepoteza mtoto wake sasa anakwenda polisi kuripoti akiwa na jirani yake kufika huko kuna madhila yanayomkuta pamoja na kwamba amepotelewa mtoto wake...

Nikikiangalia hiki kipande mara nyingine kinanichekesha kutokana na Transformaton ya uso wa Richie ambae mwanzo aliingia na mbwembwe zote polisi huku akionekana mjuaji na mjanja mwingi lakini anapopewa kibano na anapobadilika hata uso wake unabadilika na anaonekana mdogoo tofauti na alivyokuwa mwanzo..

Kikubwa ni uhusika aliouvaa Richie na wote wengine, lakini kwa richie zaidi ni ule uhusika wa uso wake ulivyokuwa na ile transformation ya hatari iliyotokea kwenye uso wake..

Zaidi angalia hapo juu...

MJUE MSANII SHAMSA FORD...

Wednesday, October 26, 2011

THE LOST ADAM - moja kati ya filamu nilizozipenda kwa mwaka huu...



Nimeangalia filamu nyingi sana kwa mwaka huu na hiyo ni kutokana na kazi yangu pia.. Kiukweli kuna improvements nyingi sana kwenye filamu zetu kwasasa lakini mara nyingi kitu ambacho huwa kinatuangusha ni STORY za filamu zetu.. nyingi ziko too shallow, na haya mambo ya part one na two ndio kabisa yanazidisha u-shallow kwenye filamu

Lakini pamoja na kwamba story nyingi ziko Shallow, bado kuna watu ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye filamu, ambapo hata kama story ni ya kawaida utakutaSCRIPT yake imesimama na hata DIRECTOR anakuwa ameitendea haki kiasi kwamba unaangalia filamu na unaona kabisa kwamba hii filamu imedirectiwa..

Moja kati ya filamu nilizoziona na zikanifurahisha kwa mwaka huu.. ni filamu ambayo imedirectiwa na Mtitu Game ambayo inaitwa THE LOST ADAM..

Kikubwa ni Uchezaji wa baadhi ya watu humo ndani.. ni kwamba wamefanya vizuri sana nikianzia na ROSE NDAUKA ambae amevaa uhusika vilivyo kabisa, JACOB STEVEN(JB) pia amefanya vizuri sana na naweza kusema huyu ni mtu ambae kwa movies zake nilizowahi kuangalia naweza kusema Hajawahi kuniangusha.. pia kuna Patcho Mwamba, Hemed Suleiman na wengine wengi ambao kila mtu amekamua kwa nafasi yake..

Kikubwa nampongeza sana Director wa hii filamu kwa kazi aliyoifanya kwani ukiangalia filamu yenyewe unaona kabisa kwamba imekuwa directed na mtu ambae yuko serious na anaijali kazi yake, ila zaidi angalia hiko kipande hapo juu ambacho ni MOJA kati ya SCENES nilizozipenda sana kwenye hii Filamu..

Tuesday, October 25, 2011

USIKOSE TAKE ONE LEO USIKU on CLOUDS TV


Usikose TAKE ONE siku ya LEO saa TATU KAMILI USIKU on CLOUDS TV na Zamaradi Mketema!!

Thursday, October 20, 2011

DAD and SON.. soo lovely!!


Allen Mushi na mtoto wake jayden!

PICHA YA LEO.. warembo wa bongo movie!!


Wema kajala na lulu!!

KWA KUMSIKILIZA LULU AKIONGELEA MWENYEWE KUHUSIANA NA JUSTIN BIEBER.. BONYEZA HAPO CHINI!!!

LULU na JUSTIN BIEBER by nelly@g5click.com

LULU na JUSTIN BIEBER by nelly@g5click.com
Hiyo ni Interview niliyofanya nae kwenye redio ambapo amejielezea mwenyewe kiurefu zaidi kwamba, NI kweli?? na kama kweli ni kimapenzi ama kishabiki?? na pia Bieber akitaka mapenzi klwake itakuwaje??
Kwa majibu yote msikilize LULU hapo juu!!!

Wednesday, October 19, 2011

HEMED na MLELA kuja kivingine..

tegemea kuwaona katika filamu mpya kabisa itakayotoka hivi karibuni ambapo wameigiza character tofauti kabisa wakiwa mererani kwenye machimbo
ukiangalia juu juu hapo unaweza usiwatambue harakaharaka kwa jinsi walivyojiweka na muonekano wao ulivyo
hapa akipewa dozi na wamasai wa mererani
coming soon!!

HII NI KWELI..!!?? lol





























Hebu angalia hizo picha hapo kwa umakini sana halafu uniambie kuna ukweli wowote katika maana zilizotolewa kwenye hizo aina za ulalaji wa mtu na mpenzi wake!??

Niambie WEWE na YEYE mnahusika kwenye ipi zaidi kati ya hizo hapo juu!!?? na ukiangalia aina yenu ya ulalaji inaendana na jinsi mahusiano yenu yalivyo!!???

LET'S SHARE

Tuesday, October 18, 2011

USIKOSE TAKE ONE LEO na kila JUMANNE kupitia CLOUDS TV saa TATU KAMILI USIKU!!

MLOPELO AILALAMIKIA CLOUDS KWA KUTOPIGA WIMBO WAKE


Msanii wa siku nyingi wa maigizo MLOPELO ambae alikuwa akiigiza kama jini mara nyingi kwa enzi hizo kupitia kaole ameibuka na kuilalamikia CLOUDS kwa kutopiga wimbo wake ambao kwa mujibu wa yeye anasema uko kwenye mahadhi ya R n B..
Kwa kuusikiliza wimbo huo na malalamiko yake bonyeza hapo juu ili uweze kuuusikiliza vizuri wimbo huo na kusema yaliyomo yamo!!!

Monday, October 17, 2011

LULU ANATARAJIA KWENDA EUROPE KUMTAFUTA JUSTIN BIEBER.. ANASEMA ATACHANGISHA HATA KADI KWASABABU HIYO...

Msanii Star wa filamu ambae alianza kuigiza akiwa na umri mdogo ameamua kufunguka na kuweka wazi kwamba ana mpango wa kwenda EUROPE kwa sababu moja tu ya kumtafuta JUSTIN BIEBER....

Nilipomuuliza sababu ya kumtafuta kama ni ya kishabiki ama ya kimapenzi alijibu kwamba ni kishabiki lakini lolote pia linaweza kutokea,Lakini hapohapo nikataka kujua kama amesahafanya juhudi zozote za kuwasiliana nae akasema kwasasa bado hapana ila anachotaka kufanya ni hiko kumuendea hukohuko kumsaka..

Kuhusiana na NAULI nilipotaka kujua amejipangaje LULU akasema atachangisha kadi kwasababu anaamini kitendo anachotaka kukifanya ni cha kimaendeleo na ni UJASIRI mkubwa kwasababu amejitosa kwenda kumtafuta mtu ambae hapatikani kirahisi hivyo ni USHUJAA..

kabla sijamaliza interview nae nilimuuliza lulu ikitokea bahati akakutana nae na mara itokee JUSTIN BIEBER nae amevutiwa na yeye KIMAPENZI, je atakuwa Tayari!!??? alichonijibu ni kwamba YANI BILA KUULIZA YUKO TAYARI KABISA na hilo sio swali la kuuliza kwani bila wasiwasi atafanya hivyo..

Soon nitakuletea CLIP ya sauti ya interview ambayo nilifanya nae!!

Monday, October 10, 2011

HALI YA KIAFYA YA MZEE KIPARA SI YA KURIDHISHA SANA...

Nilipata nafasi ya kumtembelea kama mara mbili hivi kwenye wiki hizo zilizopita na kiukweli kabisa ukiangalia hali yake kiafya kwasasa naweza kusema ni kama hairidhishi.. Hii ilikuwa mara ya kwanza nilivyokwenda kumuona ambapo alikuwa akiweza hata kuinuka na kutembea kidogo
Lakini nilivyorudi mara ya pili hali ilikuwa kama tete hivi sababu hata uwezo wa kutembea mwenyewe vizuri kwasasa hana, akitaka kusimama lazima ashikilie ukuta na hata akitaka kutembea anakuwa anatambalia ukuta ambao nao naweza kusema si kwamba unamsaidia, haumsaidii chochote sababu hujikuta anaanguka pia..
Hivyo muda mwingi kwasasa huutumia kulala tu, na amekuwa hajiwezi kwa chochote kwasasa, na hata kujisaidia pia saa nyingine hujikuta anamalizia sehemu aliyokuwa saabu nguvu za kuinuka hana...
Kwasasa mzee Kipara anakaa Kigogo kwenye nyumba ya Kaole chini ya Uangalizi wa kaole ambapo kuna kijana waliemuweka ambae ndio anamsaidia bega kwa bega katika kumuuguza na kumtunza, hivyo kwa mtu yoyote ambae atatamani kwenda kumuona anaweza akafika kigogo pale na kwenda kumuona...
Kikubwa tumuombee tu aweze kurudi katika hali yake ya zamani, ambapo nakumbuka zamani ulikuwa ukienda kumtembelea alikuwa akipata hadi nguvu za kukusindikiza tofauti na sasa ambapo hata kutoka nje ya chumba chake tu ni tabu na kikubwa anacholalamikia ni miguu pamoja na kwamba kuna maradhi mengine yanayomsumbua pia...

KAJALA - MTOTO WANGU NDIO KILA KITU KWANGU


Hii ilikuwa kupitia kipindi cha TAKE ONE ya Clouds TV ambapo Kajala aliweza kufunguka vitu vingi sana kuhusiana na maisha yake ikiwemo mahusiano yake yaliyopita na P.funk jinsi walivyokuwa wakiishi, siku ambayo hataisahau ambapo aliwahi kupelekwa segerea,kitu kilichosababisha na vitu vingi kuhusiana na maisha yake..

Kwa hayo na mengine mengi bonyeza hapo juu (kwenye video yake) ili uweze kumsikia na kumuona mwenyewe akiongelea kuhusiana na maisha yake!!!!