Inawezekana ulikuwa hulifahamu hili lakini habari ni kwamba Mwimbaji wa PEMBE LA NG'OMBE kutoka bendi ya Dar Modern Taarab ambapo hapo awali alikuwa ni mwanamuziki wa bongo Flavour HAMA Q ameipata joto ya rumande alikokuwa under arrest katika Gereza la Keko hapa DSM kwa muda wa wiki kadhaa na ameachiwa kutoka Gereza la KEKO mwezi uliopita mwishoni kama kwenye tarehe 29 may (kama sikosei). Ambapo kesi iliyokuwa ikimkabili ni kujeruhi.
Akiwa katika studio za clouds fm leo katika leo tena
katika mahojiano leo Hamma Q ametoa hali halisi ya jinsi jela kulivyo ambapo amesema kwamba mtindo wa kulala ni ubavu ubavu na si chali wala kifudifudi ili usichukue nafasi kubwa, na ukitoka tu kwenda kujisaidia nafasi yako imechukuliwa.
Amesema alipokuwa huko amejifunza mambo mengi sana lakini kubwa ni swala zima la kubana matumizi ambapo chupa ya maji inaweza kutumiwa hata kwa siku mbili, na si kubana matumizi kwenye vyakula tu bali hata karatasi ambazo huwa wanatumia kuandika ujumbe na kuutuma kwa ndugu na jamaa zao.. kipande cha karatasi moja anaweza akakitumia hata zaidi ya mara kumi.
Na huko jela kumbe biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa ambayo ilikuwa ikitumika zama za zamani bado inaendelea ambapo ukiletewa chakula unaweza ukabadilishana na mtu kwa chupa ya maji..
hayo ndio maisha ya huko ndani ambapo yeye anasema siku moja jela ni kama mwaka hakuna uzuri kabisa ila anashukuru alivyofika huko kujulikana kwake kulimsaidia kidogo AKASALIMIKA.. masela hawakumsumbua kwa chochote mpaka anaaga jengo hilo lisilokuwa na heri.
Kwasasa Hama Q ametoa wimbo wake mpya kabisa unaoitwa toto la kiafrika akiwa na bendi yake ya DAR MODERN TAARAB.. hatujui kama utakuwa kama Pembe la ng'ombe ama vipi!!
No comments:
Post a Comment