Kupitia simu yako ya mkononi unaweza ukajikuta unaexpress vitu vingi sana ambavyo watu hawavijui kuhusu wewe bila mwenyewe kujua hivyo simu ya mkononi inaweza kuwa kielelezo cha wewe na watu wakajua wewe ni mtu wa aina gani, unapenda nini, una tabia zipi na vitu vingine kama hivyo ingawa si kwa asilimia mia moja lakini kwa kiwango kikubwa mtu akakuelewa kama ni mshenzi ama mstaarabu.
Vitu vifuatavyo vinaweza kurahisisha mtu kukujua kupitia simu ya Mkononi
MLIO (RINGTONE)
Ni rahisi sana kumsoma mtu na kumjua kupitia mlio wake wa simu ya mkononi, kwa teknolojia yetu hii ya sasa ya bluetooth na mambo mengine walio wengi hutumia milio tofautitofauti kwenye simu zao kulingana na utashi na mapenzi yao.. na hapo ndipo unapokutana na nyimbo tofautitofauti kwenye simu za watu na hata sauti zilizorekodiwa ambazo zinaelezea mambo tofautitofauti. na maranyingi nyimbo tunazozichagua ni zile tunazozipenda ama zinazoelezea hisia zetu Hivyo MLIO mtu aliouchagua kwenye simu yake unaexpress vitu vingi sana kuhusu huyo mtu bila mtu mwenyewe kujua. (Mlio wako unakuelezea kwa asilimia kubwa)
MAJINA
Kila mtu ana njia yake ya kuhifadhi majina kwenye simu yake, kuna wengine huandika majina tu kawaida na kuna wengine huandika vitu tofauti tofauti kulingana na mtu aliemsave, mfano MSUMBUFU, TAKATAKA, MZUSHI, MPENDWA ama wengine husave hata kwa majina ya MATUSI.. Hivyo njia anayotumia mtu kusave majina yake kwenye simu yake inasaidia kumuelezea kinamna fulani.
GALLERY
Vitu ambavyo amevihifadhi kwenye simu yake kama nyimbo, videos na kadhalika. hii inasaidia pia kujua mtu ana tabia zipi na anapenda vitu vya aina gani. (Hii na ya hapo juu ina apply zaidi kwa mtu wako wa karibu)
Ulikuwa unalifahamu hili.. unafikiri simu yako inakuelezea???......TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
8 comments:
Yah kuhusu ulichikisema uko sawa kwa kiasi fulani coz kama njia ya mawasiliano inayotumika kwenye dunia ya leo simu yako inajieleza vya kutosha kuhusu wewe na hakuna kitu muimu katika hii dunia kama mawasiliano.
Yah kuhusu ulichikisema uko sawa kwa kiasi fulani coz kama njia ya mawasiliano inayotumika kwenye dunia ya leo simu yako inajieleza vya kutosha kuhusu wewe na hakuna kitu muimu katika hii dunia kama mawasiliano.
Duuuuuhhh!!!! nilikuwa sifahamu hili, nimekubaliana nawe ni kweli kabisa ulichokisema
Chukua hatua.........HAKI ELIMUUUUUUUUU MBAAAAAAAAH
screena saver haina picha yeyote zaidi yaile samsang, hakuna ya mwanangu, yangu au ya mume wangu, pili haina mlio kabisa mimi hupendelea viberation. sina music wala picha hata moja zaidi ya mtoto wangu juzi alipotimiza miaka 5 hiyo 1 tu, how do you describe me?????????
Asante sana mdau, hili ni wazi kwa wanapsycholojia wengi wanafahamu jinsi ya kuwasoma watu kupitia vitu walivyo navyo, sio simu tu, hata jinsi mtiu anavyoongea, anavyovaa, na hata marafiki wa mtu wanatosha sana kuwa kilelelezo cha mtu mhusika. Huwezi kuwa mcharuko halafu upende nyimbo za dini, sio rahisi mara nyingi mtu wa aina fulani hupoenda vitu vinavyoendana na tabia yake aliyonayo. Nawasilisha asante.
I dnt think so,kuna watu wanaweza weka ringtone ya gosple lkn hawajaokoka wala c wakristu,mtu anaweza kupretend aonekane kivingine wakati yeye ni mtu mwingine kabisa,kuhusu majina aliyosave c mpaka mtu ascrow simu yako ndio ayakute,na huyo mtu km akipata huo wasaa baci ni mtu anaekujua already,anyway to me hii haijaniingia kiviile,mtu anijue through my cell phone naah
nadhani ni ngumu sana mtu kukujua kupita simu yako kama tujuavyo simu ya ni kitu private sana, mimi yangu na mumewangu kila mtu na yake kivyake sasa huyo mwingine tena atakaepekua simu yangu zaidi ya hubby wangu atakuwa anatka nini kama sio udaku. somehow hii haijakaa sawa.
Post a Comment