Friday, July 30, 2010

TAMKO RASMI

AM VERY HAPPY sababu NIMETHUBUTU kitu ambacho watu wengi wanakihofia na hiyo ni alama na dalili nzuri sana kwangu, siku zote naamini kwamba UTHUBUTU ni ALAMA YA UJASIRI na mtu jasiri ziku zote ATASHINDA TU. huu ni mwanzo mzuri kwangu ukizingatia kwamba target yangu haikuwa kushinda ila ni kujitengenezea mazingira mazuri na njia ya kujitambulisha kwenye siasa, na kwa kiasi kikubwa sana nimefanikiwa katika hilo (kufikia targert yangu)na huo ni ushindi tosha kwangu.

NILICHOFURAHI ni kwamba UWEZO WANGU UMEONEKANA na NIMEFURAHI pia kwa KUTEULIWA kuwa MJUMBE kwenye KAMATI YA MAHUSIANO NA JAMII. Its a good starting point and am really happy ndani ya muda mfupi huu niliokuwa kwenye mchakato nimejifunza vitu vingi sana na nimepata experience kubwa mno, naweza nikasema ZAMARADI wa wiki mbili zilizopita ni TOFAUTI na ZAMARADI wa sasa kwani kuna mengi sana ambayo nimeyaona na kujifunza.

Nataka nitamke rasmi kwamba huu ni mwanzo wa safari yangu ya kisiasa, sijaishia hapa na kwasasa ndio nimetumbukia rasmi kwa miguu yote miwili.Penye nia pana njia na mimi NIA ninayo na naamini njia itapatikana. kwa wanaonisupport nashkuru sana na naomba muendelee kunisupport kwani VIJANA ndio sisi, vijana ndio taifa la leo na kesho hivyo sisi ndio wa kuleta mabadiliko na vijana TUNAWEZA, anaeamini hawezi basi HATOWEZA kamwe.

Otherwise namshukuru MUNGU,Najua NAWEZA na NITAFIKA TU MBALI kwa uwezo wake MUNGU.

HUU NI MWANZO TU.

Monday, July 19, 2010

SORRY GUYS NTAKUWA KIMYA KWA MUDA FULANI


Nimekuwa kimya kwa muda kidogo na nitaendelea kuwa kimya kwa muda fulani kutokana na sababu maalum ambayo nitaiweka wazi muda si mrefu, samahani sana kwa usumbufu ambao umejitokeza na utakaondelea kujitokeza kutokana na hilo,

Ni kweli si kwamba nakosa matukio ya kuweka yapo na yanaendelea kutokea na nina access yote ya kuwa nayo lakini niko kimya kwa maana maalum.

Asanteni sana kwa watoa comments wote (MBAYA NA NZURI) you guys u r my good fans kwa sababu mnatembelea blog yangu, nawashkuru sana na tuko pamoja.

ONE LOVE!!!

Thursday, July 8, 2010

HONGERA DA ZENA

Hongera Da Zena wa Clouds Media Group kwa kutuletea Baby Gal.. Inshaallah MUNGU akujalie na akukuzie!!!!

Tuesday, July 6, 2010

TEKNOLOJIA

Niko busy jamani
Veery Busy!!

LOGO YA CLOUDS TV YAZINDULIWA RASMI

Usiku wa jana logo ya CLOUDS TELEVISION iliweza kuzinduliwa rasmi pale club Billicanas na hivyo kuanzia leo ukiangalia Clouds TV hutaona neno 'signal test' tena ila hiko ndio kitakachoonekana.
Pichani wakurugenzi wa Clouds Media Group kutoka kushoto Joseph Kussaga pamoja na Ruge Mutahaba(kulia) wakitoa machache pamoja na shukrani kwa wageni waalikwa.
Mr. Ruge Mutahaba akitoa utambulisho kwa behind the Scene team ya clouds TV.