Monday, August 22, 2011

IRENE - NILITEGEMEA KUSHINDA, WEMA HANIPATI KABISA KISANAA na HATA SAUTI YAKE YA KITOTOTOTO

Hayo ni maneno aliyoyatoa IRENE UWOYA nilipomuhoji kupitia Movie leo ambapo swali nililomuuliza ilikuwa ni anajisikiaje baada ya kupambanishwa na wema na yeye kuibuka mshindi!!?

Jibu alilolitoa ni kwamba kwake yeye ALITEGEMEA matokeo kuwa hivyo na alitegemea kwamba atashinda kwani Wema ni mdogo sana kwake kisanaa hivyo angeshinda Wema ingekuwa kama ndoto ya alinacha..

"Mimi ninaweza kuvaa uhusika wa aina zote tofauti na wema ambae yeye ana sauti ya kitoto sana ambayo inam-limit kucheza baadhi ya sehemu, kwani sehemu anazoweza kucheza yeye ni sehemu za majonzi na mapenzi tu lakini sio zile za kufoka tofauti na mimi ambae ukinipa sehemu yoyote NAKAMUA lakini Wema hapana hivyo kwangu ni mdogo sana kisanaa" alisema irene..

Nikamuuliza pia kama ni kushindanishwa na mtu mwingine ambae kidogo angeweza kulingana nae hapa Bongo angekuwa ni nani!!?? lakini alisema mpaka sasa kwa hapa BONGO hajaona kwani yeye ni namba moja na ataendelea kuwa namba moja labda NJE lakini sio ndani ya Bongo!!

kashindano hako kaliibuka ghafla baada ya kutokea habari kwamba IRENE na WEMA wanakutana kwenye filamu moja ambapo ukaibuka utata kwamba nani atamfunika mwenzie ama nani mkali na hatimae IRENE akaibuka mshindi dhidi ya Wema..

usikose kesho kumsikiliza WEMA kupitia movie leo ndani ya leo tena ya Clouds Fm saa NNE na dk 45 asubuhi!!!

Friday, August 19, 2011

Msanii SHAMSA FORD anawatakia IJUMAA KAREEM!!!

Msanii wa Filamu Shamsa Ford anawatakia wasomaji woote wa blog hii ijumaa karim..
Ameshafanya filamu nyingi kama Saturday Morning, End of the day, Zawadi ya Birthday na nyinginezo nyingi sana!!!!

NI MZEE GANI ANAEKUVUTIA KWENYE FILAMU kati ya MZEE CHILO, MZEE KAMBI na MZEE MAGALI!!??? NANI MKALI!!!????

HASHIM KAMBI a.k.a MZEE KAMBI!!!
CHARLES MAGALI a.k.a MZEE MAGALI!!!
AHMED ULOTU a.k.a MZEE CHILO
Kati ya hao wote hapo juu kwa upande wako nani anakuvutia zaidi kiuigizaji!!??? na kitu gani kinakuvutia kwake katika uigizaji wake!!??
Ama kwa kifupi NANI MKALI!!?????

Tuesday, August 16, 2011

KUTOKA MJENGONI LEO HII...

Da Maryam na mimi... hapo sakina alitupiga picha ya kushtukiza tukaona si vibaya tukaendelea na zoezi matokeo yake ndio picha zote hizo...
Nikiwa na Sakina wa Lyoka, mamaa wa ng'aring'ari!!!
Da maryama na Da sakina!!

Utamu wa picha unaendelea na mapozi tukaweka na swaum zetu..

nikaona nitie ufundi wa Black and white.. mwanamke kujistiri!!!


Mfungo unaendelea ya 16 leo.. Ramadhan Kareem!!!

Zoezi likaishia hapa kwa siku ya leo.... tungoje ya kesho tena!!!!
Shukrani Sakina kwa kuwa mpiga picha wetu leo.. lol!!!!!


Thursday, August 11, 2011

WEMA SEPETU v/s IRENE UWOYA.. NANI ZAIDI!!!!??????

Kwa maoni yako kati ya IRENE UWOYA pamoja na WEMA SEPETU nani mkali kiuigizaji!!??? na kwanini?? wote ni wasichana warembo na waigizaji wakubwa hapa Tanzania, kwa upande wa Irene tayari ameshacheza filamu kama Diversion of Love ambayo ndio ya kwanza, kisha Oprah ambayo ndio ilimtoa kabisa baada ya hapo akfanya nyingi nyingine kama my dreams,pretty girl, senior bachelor ambayo ni ya mwaka huu na nyinginezo nyingi...
Kwa upande wa WEMA, a point of no return ndio ilimtambulisha, kisha Family tears, baada ya hapo akafanya nyingi kama,red valentine, lerato, basilisa na nyinginezo nyingi sana
KWA UPANDE WAKO WEWE UNAESOMA HAPA na kwa maoni yako, KATI YA IRENE UWOYA na WEMA SEPETU..


NANI MKALI!!!??????

Tuesday, August 9, 2011

RAMADHAN KAREEM...

Nilikuwa kimya lakini tuko pamoja, nawatakia RAMADHAN NJEMA wapenzi woote wa blog hii.. Tuko pamoja..
RAMADHAN KARIM

UNAIONAJE COVER!!!????.... COMING SOON!!!

Hebu nipe maoni yako kuhusiana na cover hiyo unayoiona hapo juu....
Ni filamu mpya kabisa inaitwa NZOWA ambapo ndani kuna Mzee MASHAKA wa kaole, NATASHA, WASTARA, SAJUKI, TINO, MUHOGO MCHUNGU, DUDE pamoja na wengineo na ni filamu inayozungumzia maisha...

UNAIONAJE COVER!!!???