Monday, January 31, 2011

BONGO ACCESS.. LEO USIKU!!!

Mara ya kwanza kabisa alionekana kupitia Bongo Star Search mwaka 2009 ambapo alikuwa akihost kabla ya Godwin Gondwe kuingia, lakini baadae akawa kimya kidogo for a reason... na sababu ya ukimya wake utaijua leo kupitia CLOUDS TV baada tu ya TAKE ONE saa tatu na nusu usiku CLOUDS TV kupitia BONGO ACCESS ambacho ni kipindi kipya kabisa... hii ni sehemu pekee ambayo utapata kuona EVENTS zote zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika hapa BONGO...

Anaitwa CAESAR DANIEL.. Usikose Bongo Access jumanne hii na kila jumanne saa tatu na nusu usiku!!


BONGO ACCESS... YOU BETTER BE THERE OR NOWHERE!!!!

MAMA BISHANGA AONGEA LEO DAR...Mama Christina Innocent , jina la Usanii ni Mama Bishanga (kushoto) na kulia ni mwanae Hendrick Nambira, jina la Usanii Kenny akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye picha na kutoa ushauri kwa Wasanii wa Tanzania jinsi Filamu zinavyoendeshwa nchi nyingine,na kuwapongeza jinsi Watanzania walivyoendelea kwenye majukwa ya usanii, kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anna Itenda -Maelezo.

Mama Bishanga ameongelea
mambo makuu matatu:

1. Umuhimu wa wasanii wa filamu na watendaji (wapiga picha, waongozaji, watu wa taa nk.) wafanye juu chini wasomee fani hiyo badala ya kutegemea uzoefu tu kwani bila weledi fani hio itadoda. Ameitaka serikali itoe kipaumbele mafunzo ya sanaa ya filamu kama zilivyo fani zinginezo.

2. Amesisitiza umuhimu wa uhalisia ambao unakosekana sana katika filamu za Tanzania kiasi nyingi zionaonekena kama maigizo yasiyo na mvuto. Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maadili ya nchi na kukataza kabisa waigizaji kucheza michezo ya ngono nje nje kwani hio si utamaduni wa mtanzania. Kuhusu filamu ya 'Shoga' inayozi9nduliwa wiki hii amesema ushoga si desturi ya Kitanzania na bila shaka filamu itapendwa kwani inatoa tahadhari ya tabia hio chafu. Ila amesema si vyema watu wakambeza mchezaji mkuu wa filamu hio kwa kudhani yeye ni shoga kweli, na kwamba huo sio ustaarabu kwani hata yeye aliwahi kusemwa mitaani na wenye uelewa mdogo kuwa ni mama mkatili baada ya kucheza kama mama mkwe mkatili.

3. Amewataka wasanii na wadau wa tasnia ya filamu kuendeleza libeneke kwani kazi zao zinaonekana na kuheshimika sana na kwamba wakiongezea weledi wa kwenda shule hakuna wa kuwagusa. Alimfagilia sana JK kwa kujituma kuendeleza michezo na sanaa, na kusema wasanii na wanamichezo wamuenzi Rais wetu kwa kujituma na kufanya vyema

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MICHUZI.

BIFU LINA FAIDA AMA HASARA!!??? LINAMPANDISHA MSANII AMA LINAMSHUSHA!!!????

Kwasasa kwenye Entertainment industry tofauti na zamani kumeibuka system ya wasanii kugombana wenyewe kwa wenyewe na hii imekuwa kama kitu cha kawaida HASAHASA kwenye industry ya FILAMU tofauti kabisa na muziki..

Ukiangalia kwasasa kila kukicha utaskia huyu amegombana na huyu, mara huyu kamtukana huyu mpaka wengine kufikia KUPIGANA KABISA na vitu vingine kama hivyo.... ninachojiuliza MABIFU YANAMPANDISHA MSANII ama YANAMSHUSHA!!!!??????

Mifano hai ya mabifu yaliyowahi kutokea
1. AUNT EZEKIEL Vs WEMA SEPETU ambapo sababu ilikuwa Hartman ambae alisemekana kutembea na wema sepetu baada ya aunt.

2. WEMA SEPETU vs KANUMBA huu ulikuwa ni ugomvi mkubwa kabisa mpaka ilifikia kupelekana polisi baada ya Wema kuvunja kioo cha gari cha kanumba.. hili lilikuwa bifu la kimapenzi zaidi.

3. AUNT EZEKIEL Vs SHUMILETA sababu haikueleweka vizuri lakini nafkiri mpaka leo hawana maelewano mazuri

4. RAY Vs KANUMBA kabla hawajawa maswahiba waliwahi kuwa mafahari wawili wasiopikika chungu kimoja enzi hizo.

5. MAYA Vs SHAMSA FORD hawa walidundana kabisa kwenye sherehe moja (ilikuwa kwenye Baby Shower ya Emelda) kabla ya kugombana walikuwa mtu na dada yake lakini mambo yakabadilika.

6. JACKY CHUZI Vs JINI KABULA sababu ilikuwa MR. CHUZI ambae alikuwa mwanaume wao

7. JACKY CHUZI Vs WEMA SEPETU Urafiki uligeuka uadui kwasasa sielewi wako vipi

8. HEMED vs MLELA Hili ni bifu ambalo lilizungumziwa sana na nafkiri ni moja kati ya mabifu maarufu hapa Tanzania.

9. HEMED Vs RICHIE limejitokeza juzi na hili ndio limenifanya nijiulize bifu lina faida ama Hasara

10. JACKY WOLPER Vs SHILOLE ambao walidundana kabisa Leaders Club lakini naskia kwasasa ni mashosti tena.

11. THEA Vs MONALISA ambao walikuwa maswahiba hasa wa kufa na kuzikana lakini kwasasa mambo sio mambo tena

Hayo ni baadhi tu ya mabifu ambayo yaliowahi kutokea kwenye Industry ya Filamu, lakini ninachojiuliza ni kwamba MABIFU YANA FAIDA ama HASARA???? na BIFU KAMA BIFU LINAMPANDISHA MSANII AMA LINAMSHUSHA!!!???? msaada tafadhali..

Saturday, January 29, 2011

BEHIND THE SCENE...

ISSA MUSA (claude) katika harakati za kurekodi filamu kutoka kampuni ya 5effect chini ya William Mtitu...
Single Mtambalike (Richie rich)

Tukiwa hoi, Zamaradi na Mwasiti..


Dennis Ngakongwa (cameraman) akiwa makini na kazi yake..
Waigizaji wakiwa na Director wao William Mtitu!!!
Wasanii kutoka 5 effects wakiwa ON SET...

Friday, January 28, 2011

USIKU HUU KIKAZI ZAIDI...

kazi zetu hizi hazina usiku wala mchana, hapa nikiwa nasubiria kushoot take one kwenye moja ya Location ya movie ambapo wasanii walikuwa wakishoot filamu yao... hapo nikiwa na mwasiti ambae alinipa escort
Hoi tumejichokea... kilichofata nilimuacha mwasiti akalale mimi nikaendelea kupiga mzigo
kazi ni kazi


Thursday, January 27, 2011

MIMI SIRINGI ILA HII NDIO STYLE YA MAISHA YANGU (NINA SWAGGA)- HEMED

watu wengi sana wamekuwa wakimlalamika HEMED kama mtu anaeringa, kujiskia na majivuno na hiyo ikasababisha kwenye interview niliyofanya nae nimtupie hilo swali anieleze ni kweli kwamba anaringa, na kama ni kweli kwanini ana tabia hiyo ya kujiskia, hivyo nikamuomba aliongelee hilo kama ni kweli ana tabia hiyo ama vipi..

HEMED Alisema..
"Kila mtu ana maisha yake na kila mtu anaishi vile apendavyo mimi hii ndio style ya maisha yangu, kwamba nimeamua kuishi hivi basi nitaishi vile ninavyopenda mimi, lakini ukizungumzia swaala la kuringa kiukweli hata mama yangu mzazi alishawahi kukiri kwamba mimi siringi ila watu wananichukulia vibaya"

Akaendelea...
"Unajua kuna TOFAUTI KATI YA KURINGA NA SWAGGA, kuringa ni zile habari za kike za kujiona wakati binaadamu wote tuko sawa, SWAGGA ni kile kitu ambacho lazima uwe nacho wewe kama style yako sasa kama utakuwa huna SWAGGA lazima utapea ndiomana NDUGU YANGU MLELA ANAPEA, kwahiyo MIMI SWAGGA TU LAKINI SIO KAMA NARINGA MI NIKO PEACE,mi shabiki yangu akiniambia HEMED naomba nikushike mkono basi niko radhi nimkumbatie hiyo yote kuonesha Love."

Nikamuuliza kwahiyo MLELA hana Swagga alichojibu ni kwamba yeah MLELA hana SWAGGA...

Hemed akishow love kwa watoto
UNA LOLOTE!!!!????

Wednesday, January 26, 2011

ORIGINAL COMEDY - MANABII WANAOKUBALIKA KWAO!!!!

ORIGINAL COMEDY kutoka kushoto JOTI (Andunje), WAKUVANGA (mama BERE au Baba Andunje), MPOKI (Rick Ross kwa sasa), MASANJA (mkandamizaji), MACREGAN KIPARA (Shemeejiii)
UMATI wa watoto ukiwafuata nyuma kwenye moja kati ya maeneo wanaotembelea huko mikoani..!!!

Kuna usemi unaosema NABII HAKUBALIKI KWAO na ni kitu ambacho kina-apply kwa watu wengi sana kwamba mara nyingi mtu huwa hathaminiki kwa watu wanaomfahamu ama waliomzoea..

Lakini kwa Original comedy hali ni tofauti kabisa, kwani ni moja kati ya KUNDI ama WATU ambao wanathaminiwa kuanzia nyumbani na hata nchi jirani, na wamefanikiwa kuteka watu wa Rika, Jinsia na hadhi tofauti kutokana na utofauti waliouleta... kuanzia VIONGOZI WA SERIKALI, WANANCHI WA KAWAIDA, WATOTO, VIJANA na watu wa AINA ZOTE.

Nakumbuka hata RAIS aliwahi kukiri kwenye siku yake ya kuzaliwa kwamba ORIGINAL COMEDY ni moja kati ya vitu anavyopenda sana kuangalia!!!!
UMATI wa watoto ukiwafuata nyuma kwenye moja kati ya sehemu wanazokwenda..
Wanaume kazini..

Mbali na hilo, Original comedy ni kundi ambalo limeleta mapinduzi makubwa sana hapa Tanzania na kubadilisha taswira nzima kwenye sanaa ya Vichekesho (Comedy), kwani zamani sanaa ya vichekesho ilikuwa inachukuliwa kama ya watu wa aina fulani na ilikuwa inadharaulika kidogo lakini kwa ORIGINAL COMEDY imekuwa tofauti na hata ile style iliyokuwa imekaa vichwani mwa watu wengi kwamba MTU AKIFANYA COMEDY LAZIMA AWE MCHAFU NA AVAE HOVYOHOVYO ilifutika kupitia watu hawa...
JOTI alileta tafrani kidogo kutokana na style yake ya KUSHTUA KIJOTI kiasi kwamba watoto majumbani huko hakukaliki na hata baadhi ya wanamuziki kama wa Dansi waliweza kuitumia kwenye Shows zao pamoja na baadhi ya wanabongoflavor kama C-pwaa..

Na kwa yote hayo nathubutu kusema kwamba ORIGINAL COMEDY ni MANABII WANAOKUBALIKA KWAO!!
BIG UP SANA KWENU.. KAZENI BUTI na MSILEWE SIFA

HAPPY BIRTHDAY MILLARD....!!!

Nakumbuka mara ya kwanza kabisa kukuona ilikuwa Habari Maelezo sikumbuki kulikuwa na press conference gani lakini tulikutana pale kama wanahabari kipindi hiko ukiwa WAPO RADIO na mimi nikiwa C2C Television, hapo ndipo tulipojuana..

Baada ya muda kidogo nikawa namuona mtu anasoma taarifa ya Habari and i used to like usomaji wake wa habari nakumbuka nilikuwa nasema napenda huyu mtu anavyosoma taarifa ya habari bila kugundua kwamba ni yuleyule ambae nilikutana nae habari maelezo... siku moja baada ya muda mrefu simu yangu ikaita namba ikaandika MILLARD wakati napokea ndio nikakumbuka kwamba this is the SAME Millard ambae anatangaza Habari na ndio yule ambae nilikutana nae Habari maelezo and he became a good brother and friend...

Na baada ya muda fulani HATIMAE wote tukakutana katika SAME RADIO STATION CLOUDS FM ambapo ndio tunapiga mzigo yeye akiwa anafanya AMPLIFAYA saa MOJA mpaka TATU usiku na mimi nikiwa CLOUDS TV kwenye TAKE ONE pamoja na MOVIE LEO ndani ya Leo tena ya Clouds FM..

WISH U LUCK IN EVERYTHING U DO.. KEEP IT REAL.. YOU ARE THE BEST

HAPPY BIRTHDAY BROTHER!!!!

Monday, January 24, 2011

B12 AFUNGUA DUKA LA NGUO.. BORN TO SHINE!!!!

Kwa wale wote ambao wanapenda kupendeza THIS IS YOUR TIME, Hamisi Mandi a.k.a B12, Twangala tweezy, The Navigator ama King of the afternoon Shows amefungua rasmi duka lake la nguo ambalo linapatikana maeneo ya MWENGE barabara ya AFRIKA SANA karibu na Ofisi za TRA mkabala kabisa na DUKA la wadada la MIMI'S...

Duka linaitwa BORN 2 SHINE ambapo lina bango jeusi hivi na maandishi kama ya Silver... Fanya kama unapitia hivi kwa RABA kali, VIATU vya aina zote, MASHATI, JEANS, T-shirts pamoja na vitu vyote ambavyo unahitaji...

CONGRATULATION BROTHER.. Thats a good step.. BORN TO SHINE always!!!

HAPPY FAMILY...

Mmoja kati ya waigizaji wa kike wanaofanya vizuri sana hapa BONGO, The SEXIEST movie star IRENE UWOYA akiwa na husband wake HAMAD NDIKUMANA with their CUTE son..

I just love this pic coz it shows how happy the family is..!!

Sunday, January 23, 2011

KUTANA NA MISS XXL 2010

Anaitwa Hamisa Hassan Miss XXL 2010, alipatikana kupitia XXL BACK TO SCHOOL BASH inayoandaliwa na Kipindi cha XXL kutoka CLOUDS FM ambapo alikuwa ni mmoja kati ya washiriki ambapo jicho langu lilimuona kutoka mbali na nikamuomba ashiriki akakubali na hatimae aliweza kuibuka mshindi..

Amezaliwa DECEMBER 10 mwaka 1994 mkoani MWANZA akiwa ni Mnyamwezi kwa kabila... Shule ya msingi amesomea MABATINI primary School na kwasasa bado anaendelea na Masomo ambapo yuko FORM FOUR kwenye moja ya shule za sekondari hapa DSM.

ROLE MODEL wake kwa hapa Tanzania ni LISA JENSEN na anasema anampenda sana Lisa kwasababu ni muigizaji na mwanamitindo at the same time na kikubwa anapenda anavyoact, na mtu mwingine anaemuangalia (role model) ni sheria ngowi coz ni big designer hapa Tanzania na anafanya kazi zake kimataifa,Wakati kwa NJE anampenda sana BEYONCE.

Plans zake ni kuwa mwanamitindo na muigizaji mkubwa hapa BONGO.. I think maproducers wa filamu CAST mmeiona...

Nikimuangalia HAMISA kwa mbali naona kama anafananiafanania na WEMA SEPETU vile KIMUONEKANO... She is SO BEAUTIFUL and PHOTOGENIC too!!!

I just like her kiukweli...

Huyo ndio MISS XXL 2010...

MEET RIO PAUL THE FASHIONISTA.. EVEN MEN HAVE THEIR STYLE!!!

Style sio kwa wasichana tu, hata wavulana nao wana styles zao as you can see hapo juu, Rio the fashionista na style yake ya nywele..hiyo kitu ya Blue hapo kichwani ndio imenivutia mpaka nikaamua kutumia hii picha...sikuwahi kuiona popote, that can be ur identity brother!!!Hapa akiwa katika style nyingine ya nywele...
RIO akiwa na ALLY KIBA
Swagga is ON....


Sio nywele tu hata likija swala la mavazi utamshikia mbali...
Kitu cha Supra pale kati...
Hapa akiwa na Jokate Mwegelo
Mafashionista wamekutana.. kutoka kushoto RIO PAUL, ALLY RHEMTULLAH one of the best designers hapa Bongo, the top model FIDELINE IRANGA pamoja na mkaka hapo pembeni..
Rio paul pamoja na Jokate Mwegelo.. They look Georgeus!!!

Fashion sio kwa wasichana tu hata wavulana nao wamo na unaweza ukawa na style yako ya kuvaa kutegemea na mapenzi yako!!!

Friday, January 21, 2011

BIFU LA THEA NA MONA.. KUNANI!!!!?????

Walikuwa MASWAHIBA wakubwa lakini kwasasa mambo yamebadilika na UADUI mkubwa umeingia kati yao.. CHANZO NI NINI!!!????? Hebu shuka chini uje kila mtu anaongea nini juu ya hilo....

Kwa upande wa MONALISA nilivyomuuliza kuhusiana na ugomvi wao AMESEMA kwamba HAKUNA ugomvi wowote ila alichogundua ni kwamba THEA anatafuta PROMO ya Filamu yake Mpya ambayo waliifanya wote kipindi hiko..

Monalisa hakutaka kuongea mengi zaidi ila alichosema ni kwamba ANAUMIA sana nahiyo misunderstanding iliyopo kati yao na ameishi na THEA vizuri kama ndugu yake wa damu kwa Muda mrefu hivyo kitendo cha yeye na Thea kuwa tofauti ni kama kinamuumiza..

Monalisa aliendelea kuongea kea kusema kikubwa huwa hapendi matatizo na watu na kwa mwaka huu hataki kabisa matatizo hivyo kwa yote ambayo yametokea na kwa vyote ambavyo Thea na Mike wamefanya juu yake basi AMESAMEHE, na kwa upande wa kina THEA kam kuna lolote ambalo amewafanyia basi amesema hadharani kabisa kwamba anaomba MSAMAHA na asingependa matatizo hayo yaendelee..

Nilivyomuuliza zaidi kuhusu chanzo cha ugomvi huo MONA hakuweza kuongea zaidi na kusema kuwa haelewi hayo mambo yametokea wapi kiasi kwamba anashindwa kuongea chochote....

HIVYO NDIVYO AMBAVYO NILIONGEA NA MONALISA.....
Kwa upande wa THEA anasema mambo yalianza baada ya kutangaza safari yake ya kwenda MAFIA ambayo ilikuwa kama SHEREHE iliyoandaliwa baada ya harusi yake...

Kilichotokea ni kwamba MONALISA ambae ni rafiki wa karibu wa thea kwa wakati huo alianza kusikia taarifa hizo kutoka kwa watu wengine na si kwa Thea, hivyo Thea siku alivyompigia simu kumtaarifu kuhusiana na safari hiyo inasemekana MONALISA alishusha maneno ambayo THEA hakuyaelewa ambapo kubwa alimlaumu THEA na kumwambia AMESHINDWA kumwambia mapema alihisi yeye ATAROGA hiyo sherehe haitafanyika ndiomana alimficha ama!!!! na akaendelea kusema kwamba ameona watu wengine ndio muhimu na ndiomana amewaambia wao kwanza na si yeye...

Lakini kabla ya hiyo safari walikuja kukutana tena kwenye HARUSI YA CHIKI ambapo MONALISA alivyokutana na Thea aliendelea kumlaumu lakini ghafla katika mazingira yasiyotegemewa MONA alienda KUMKALIA Mike ambae ni MUME WA THEA na kumwambia hivi UMEOA MWANAMKE WA AINA GANI, umeoa mwanamke mbaya MWEUSI, ungechelewa kidogo ningekutafutia mwanamke mzuri wa kumuoa na sio THEA...

Baada ya hapo KWA MUJIBU WA THEA kila mtu alipigwa na Butwaa kwa maneno aliyoyaongea MONALISA lakini katika hali isiyotegemewa baadae tena MONALISA alimwambia kitu Mike ambae ni MUME WA THEA ambapo sielewi ilikuaje lakini MONA akajikuta amemwambia MUME WA THEA kwamba we Mike wewe unajishaua "NTAKUNYIMA"

THEA akaendelea kusema kwamba alizidi kukwazika na neno hilo kutoka kwa rafiki yake kwamba ATAMNYIMA, akazidi kuhoji kuwa MONA ana nini cha kuweza kumnyima MUME WAKE!!!!???

Nilimuuliza THEA kama labda wana kawaida ya kutaniana lakini alichojibu ni kwamba HAWANA KAWAIDA YA UTANI na ni vitu anavyoshindwa kuelewa vimetokea wapi na MONALISA alikuwa ni mzima ambae hajanywa POMBE hivyo anachojiuliza ni NINI AMBACHO ATAMNYIMA MUME WAKE (mume wa thea). Thea akaendelea kusema kuwa baada ya hapo waliendelea na safari yao ya Mafia bila MONA kushiriki lakini walivyorudi alishangaa kupigiwa simu na watu tofauti kwa ajili ya usuluhishi, nilivyomuuliza ni nani ambae alipeleka hizo habari za KUTOKUELEWANA KWAO alisema kwamba ni mama yake mona ambae aliamua kutafuta suluhu kati yao baada ya kujua ugomvi wao ambapo MONA aliskia maneno yanayoongelewa kitu ambacho kilimkosesha raha hivyo mama MONA akaona ni uamuzi wa busara kukaa chini na kujadili kuliko kuendelea na maugomvi

Moja kati ya gazeti lililoripoti habari yao

Lakini katika hali isiyotegemewa pia siku moja THEA alipigiwa simu na polisi na kumwambia kwamba ANAHITAJIWA kituo cha POLISI CENTRAL kwa kosa la KUMTISHIA KUMUUA Monalisa ambae alifika pale Kushtaki..


Lakini Thea alikataa kuripoti na mpaka leo hajaona polisi aliefika kumkamata na anachosema kwakuwa MONA ameamua kwenda POLISI basi yeye THEA hataki kikao chochote cha usuluhishi kwakuwa MONA ameamua kupeleka mambo hayo polisi hivyo yeye THEA anasema basi bora yaishie polisi hukohuko na wayaongelee huko na si pengine popote..

Nilivyomuuliza kuhusiana na MSAMAHA ambao MONA ameomba kupitia MOVIE LEO siku ya jana THEA amesema kwamba hakubaliani na msamaha huo kwani ni wa Kinafki na kudiriki hata kusema kwamba MONA ana roho mbaya na hiyo imetokana na statement aliyoitoa MONA kwamba hakuna UGOMVI WOWOTE ila THEA ameamua kuongea hivyo ili tu KUIPROMOTE MOVIE YAO ambayo waliifanya kipindi cha nyuma.


HAYO SI MANENO YANGU ILA NI MAELEZO YA THEA KUHUSIANA NA CHANZO CHA UGOMVI

Hao walikuwa ni MARAFIKI WAZURI TU kama NDUGU.. na hali imegeuka na kwasasa HIVYO NDIVYO MAMBO YALIVYO, NI NINI KIMEINGIA KATI YAO!!!???KUNA NINI!!!????

MLEMAVU WA MACHO ANAEFANYA VIZURI KWENYE MUZIKI WA KIZAZI KIPYA...

Anafahamika kwa jina la MR. Hi na Mlemavu wa macho anaefanya vizuri sana kwenye muziki wa kizazi kipya anaetamba na wimbo wake wa NATAMANI...

amesema kwamba laiti angepata hata DAKIKA MOJA TU ya kuona basi kitu anachotamani sana kukiona ni DUNIA.. anatamani akipewa nafasi ya kufumbua macho japo kwa dakika moja basi aone hali ya dunia ilivyo kwani amekuwa akiisikia tu na kuimagine vitu..

Mbali na kuiona dunia MR. HI anasema ikiwa anapewa nafasi ya kumuona mtu mmoja tu basi ataomba aoneshwe MPENZI WAKE yukoje...

kwa hayo na mengine mengi usiache kusikiliza CLUB 10 siku ya JUMAMOSI katika redio yako CLOUDS FM ambapo hapo utakutana na PG KWEKA maarufu kama BAGHDAD saa tatu mpaka sita asubuhi ambapo humo utapata kumsikia kiurefu na kujua mengi kuhusiana na MR. HI!!!!

FILAMU YA USHOGA YA TINO IKO TAYARI...

Hiyo ndio COVER ya filamu ya TINO inayoitwa SHOGA ambayo ameigiza kama SHOGA, kama unavyoiona hapo juu, ameonesha kama sura mbili ambapo upande mmoja ni taswira ya msichana na upande mwingine ni sura ya kiume ambayo ni yake mwenyewe TINO.. Na filamu hii itazinduliwa rasmi siku ya tarehe 4 mwezi FEBRUARI pale TRAVERTINE HOTEL na baada ya hapo wakazi wa MWANZA kaeni mkao wa kula....
Hissan Muya (TINO) akiwa katika sura yake ya kawaida..
Kwa wale wote waliokuwa na maswali juu ya filamu hiyo , majibu yote yatapatikana siku ya Uzinduzi wa FILAMU hiyo na kwa habari zaidi kuhusu TINO, nini anafanya na kuhusu Filamu yake hiyo.. USIKOSE kuangalia TAKE ONE siku ya JUMANNE saa TATU kamili USIKU palepale CLOUDS TV!!!

NIPE MAONI YAKO.. UNAIONAJE COVER YAKE (ya kwanza kabisa)!!!!?????

Thursday, January 20, 2011

TATTOO ZINA MAANA KUBWA SANA KWENYE MWILI WANGU- JACKY WA CHUZI

Kama anavyoonekana hapo kwenye picha Jacky ameweka wazi kwamba ana jumla ya TATTOO SITA kwenye mwili wake, NNE zikiwa sehemu zinazoonekana na MBILI zikiwa sehemu ambazo ni NGUMU kuonekana.. zinazoonekana ni kama hizo moja ni ya alama ya LIPS ambayo iko kwenye ziwa, na nyingine TATU ni za alama ya NYOTA ambazo mbili ziko kwenye viganja vya mikono na moja ikiwa mguuni.. Wakati MBILI nyingine zilipo ni SIRI YAKE...
Hii ni moja katika zile zinazoonekana ambayo ipo kwenye mguu wake wa kushoto..
Mambo ya LIPS kwenye Boobs... Chekzea!!!
Hii ni moja kati ya zile zinazopatikana kwenye mikono yake....

SINA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA JUMA NATURE
Katika interview aliyofanya na mimi kupitia TAKE ONE Jacky AMEKANA kabisa mahusiano yake na JUMANATURE kama ambavyo iliwahi kusemwa na kuandikwa kwenye gazeti moja ila alichosema ni kwamba mahusiano yao ni ya kikazi zaidi na hakuna zaidi ya hapo
Anaitwa Jackline Pentzel maarufu kama JACKY CHUZI jina lililotokana na yeye kuwa na uhusiano aw kimapenzi na Tuesday kihangala maarufu kama Mr. Chuzi ambae kwasasa mahusiano yao yamebaki historia..

Pamoja na yote anamzungumzia chuzi kama mtu mzuri ambae pamoja na kuachana hawana tatizo lolote na wanaendelea na kazi kama kawaida..

Uhusiano wake na Chuzi ulileta mambo mengi sana kubwa likiwa ni BIFU zito aliloingia na KABULA maarufu kama JINI KABULA ambae ni mzazi mwenzie na Chuzi lakini kwasasa wameona ni upuuzi na wameamua kuweka tofauti zao pembeni ukizingatia kwamba wote hawako na CHUZI hivyo kwasasa ni MARAFIKI WAKUBWA...

Kuhusiana na Tattoo zinazoonekana kwenye mwili wake JACKY amekiri kwamba anapenda sana Tattoo na zana maana kubwa sana kwenye mwili wake ingawa hakutaka kuweka wazi maana hiyo lakini kubwa alilosema ni kwamba BOYFRIEND WAKE anapenda sana Tattoo zilizo kwenye mwili wake...

Huyo ndio JACKY maarufu kama JACKY WA CHUZI ambae utampata kupitia filamu kama WRONG NUMBER, BRANCH OF LOVE, MAPITO na nyinginezo nyingi sana....

Kwa haya na mengine mengi kuhusu jacky USIKOSE kuangalia TAKE ONE jumanne hii SAA TATU kamili USIKU ndani ya CLOUDS TV!!!!

Una Lolote!!!????

Wednesday, January 19, 2011

THE BEAUTIFUL WOLPER.....

Ukizungumzia wasichana wazuri kwenye Movie Industry huwezi kumuacha Jackline Wolper..
Akiwa kwenye pozi tofauti
Ndani ya Crazy color..
Black haiongopi..
So cute.. pendeza sana mamii
Fashionista pia...
Huyo ndio Jackline Wolper katika pozi tofautitofauti....
Nini unapenda kutoka kwake!!!!????