Saturday, January 8, 2011

HAPPY BIRTHDAY to you DITTO..


Leo ni siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki kutoka THT Lameck Dotto Benard maarufu kama DITTO, kiukweli kabisa mi ni mmoja kati ya washabiki wa ukweli wa Ditto na ni wimbo mmoja tu ulionivuta kwake unaofahamika kwa jina la WAPO... mbali na wimbo naweza nikamzungumzia Ditto kama mmoja kati ya vijana wenye Discipline na heshima kwa watu wote kitu ambacho kitamfanya afike mbali zaidi....

mbali na wimbo wa WAPO kuna nyimbo nyingi ambazo ameshafanya na JUMANNE ni siku nzuri ya kujua ngoma zake zote ambazo ziko ndani ya ALBUM yake pale MLIMANI CITY kwa kiingilio cha shilingi 30,000 tu ambapo ALBUM za wanamuziki SITA kutoka Tanzania House of Talent (THT) zatazinduliwa siku hiyo... Mbali na Ditto utaweza kusikia album ya wanamuziki wanaong'ara kwa sasa kama LINA, BARNABA, AMINI, MWASITI, MATALUMA pamoja na DITTO mwenyewe.. Hii si ya kukosa!!!

Hapa Ditto akiwa na muheshimiwa Rais

Kama hufahamu kijana huyu leo hasherehekei peke yake ila ni siku ya kuzaliwa ya pacha wake pia ambapo kwa pamoja wanatimiza miaka 24...

MUNGU akubariki sana kwenye kazi ya mikono yako na kila la heri ufike mbali zaidi na zaidi.

HAPPY BIRTHDAY TO YOU BROTHER!!!!

1 comment:

Anonymous said...

Anaonekana ni mpole halafu ana heshima sana.
Hongera kwa siku yenu ya kuzaliwa Doto na kulwa.