Thursday, January 13, 2011

KILA LA KHERI RUGE MUTAHABA.. KILA LA KHERI THT!!!

RUGE MUTAHABA

Hapa akiwa na muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Usiku wa jumanne ilikuwa ni Siku kubwa sana kwa Tanzania House of Talents THT ambapo waliweza kuadhimisha miaka mitano tangu ianzishwe pamoja na utambulisho wa ALBUMS za wanamuziki wake...

Ni kazi kubwa sana imefanyika mpaka THT kufika hapo walipo na hatimae kujivunia mafanikio waliyonayo mpaka kufikisha miaka mitano kwani matunda yake yameonekana na yanaonekana dhahiri..

Na kinapofanyika kitu kizuri ni lazima mtu apongezwe na kwa kazi iliyofanyika sina budi kumpongeza Mr. Ruge Mutahaba pamoja na wanamuziki na wafanyakazi wote wa THT kwani mpaka hapo ilipofika si kazi ndogo.. kinachotakiwa ni kusonga mbele na kutokukata tamaa kwa maneno yoyote yanayotaka kuwarudisha nyuma kwani kazi yenu inaonekana...
Siku ya event.. Kemi pamoja na Ruge Mutahaba wakiongoza msafara wa wageni rasmi kuingia ukumbini
Products za THT siku ya utambulisho wa Album zao kutoka kushoto ni AMINI, MWASITI, DITTO, MATALUMA, BARNABA pamoja na LINA...

Naamini kwa kuanzisha THT haujasaidia tu kwenye nyanja ya Burudani bali hata katika UCHUMI WA NCHI kupitia Ajira ambazo vijana wanapata kupitia vipaji vyao unavyoviinua..

I believe SO many people are PROUD OF YOU... and Am among them!!!
Kila la kheri THT, Kila la kheri Ruge Mutahaba...

No comments: