Monday, January 31, 2011

MAMA BISHANGA AONGEA LEO DAR...Mama Christina Innocent , jina la Usanii ni Mama Bishanga (kushoto) na kulia ni mwanae Hendrick Nambira, jina la Usanii Kenny akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye picha na kutoa ushauri kwa Wasanii wa Tanzania jinsi Filamu zinavyoendeshwa nchi nyingine,na kuwapongeza jinsi Watanzania walivyoendelea kwenye majukwa ya usanii, kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anna Itenda -Maelezo.

Mama Bishanga ameongelea
mambo makuu matatu:

1. Umuhimu wa wasanii wa filamu na watendaji (wapiga picha, waongozaji, watu wa taa nk.) wafanye juu chini wasomee fani hiyo badala ya kutegemea uzoefu tu kwani bila weledi fani hio itadoda. Ameitaka serikali itoe kipaumbele mafunzo ya sanaa ya filamu kama zilivyo fani zinginezo.

2. Amesisitiza umuhimu wa uhalisia ambao unakosekana sana katika filamu za Tanzania kiasi nyingi zionaonekena kama maigizo yasiyo na mvuto. Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maadili ya nchi na kukataza kabisa waigizaji kucheza michezo ya ngono nje nje kwani hio si utamaduni wa mtanzania. Kuhusu filamu ya 'Shoga' inayozi9nduliwa wiki hii amesema ushoga si desturi ya Kitanzania na bila shaka filamu itapendwa kwani inatoa tahadhari ya tabia hio chafu. Ila amesema si vyema watu wakambeza mchezaji mkuu wa filamu hio kwa kudhani yeye ni shoga kweli, na kwamba huo sio ustaarabu kwani hata yeye aliwahi kusemwa mitaani na wenye uelewa mdogo kuwa ni mama mkatili baada ya kucheza kama mama mkwe mkatili.

3. Amewataka wasanii na wadau wa tasnia ya filamu kuendeleza libeneke kwani kazi zao zinaonekana na kuheshimika sana na kwamba wakiongezea weledi wa kwenda shule hakuna wa kuwagusa. Alimfagilia sana JK kwa kujituma kuendeleza michezo na sanaa, na kusema wasanii na wanamichezo wamuenzi Rais wetu kwa kujituma na kufanya vyema

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MICHUZI.

No comments: