Friday, January 21, 2011

BIFU LA THEA NA MONA.. KUNANI!!!!?????

Walikuwa MASWAHIBA wakubwa lakini kwasasa mambo yamebadilika na UADUI mkubwa umeingia kati yao.. CHANZO NI NINI!!!????? Hebu shuka chini uje kila mtu anaongea nini juu ya hilo....

Kwa upande wa MONALISA nilivyomuuliza kuhusiana na ugomvi wao AMESEMA kwamba HAKUNA ugomvi wowote ila alichogundua ni kwamba THEA anatafuta PROMO ya Filamu yake Mpya ambayo waliifanya wote kipindi hiko..

Monalisa hakutaka kuongea mengi zaidi ila alichosema ni kwamba ANAUMIA sana nahiyo misunderstanding iliyopo kati yao na ameishi na THEA vizuri kama ndugu yake wa damu kwa Muda mrefu hivyo kitendo cha yeye na Thea kuwa tofauti ni kama kinamuumiza..

Monalisa aliendelea kuongea kea kusema kikubwa huwa hapendi matatizo na watu na kwa mwaka huu hataki kabisa matatizo hivyo kwa yote ambayo yametokea na kwa vyote ambavyo Thea na Mike wamefanya juu yake basi AMESAMEHE, na kwa upande wa kina THEA kam kuna lolote ambalo amewafanyia basi amesema hadharani kabisa kwamba anaomba MSAMAHA na asingependa matatizo hayo yaendelee..

Nilivyomuuliza zaidi kuhusu chanzo cha ugomvi huo MONA hakuweza kuongea zaidi na kusema kuwa haelewi hayo mambo yametokea wapi kiasi kwamba anashindwa kuongea chochote....

HIVYO NDIVYO AMBAVYO NILIONGEA NA MONALISA.....
Kwa upande wa THEA anasema mambo yalianza baada ya kutangaza safari yake ya kwenda MAFIA ambayo ilikuwa kama SHEREHE iliyoandaliwa baada ya harusi yake...

Kilichotokea ni kwamba MONALISA ambae ni rafiki wa karibu wa thea kwa wakati huo alianza kusikia taarifa hizo kutoka kwa watu wengine na si kwa Thea, hivyo Thea siku alivyompigia simu kumtaarifu kuhusiana na safari hiyo inasemekana MONALISA alishusha maneno ambayo THEA hakuyaelewa ambapo kubwa alimlaumu THEA na kumwambia AMESHINDWA kumwambia mapema alihisi yeye ATAROGA hiyo sherehe haitafanyika ndiomana alimficha ama!!!! na akaendelea kusema kwamba ameona watu wengine ndio muhimu na ndiomana amewaambia wao kwanza na si yeye...

Lakini kabla ya hiyo safari walikuja kukutana tena kwenye HARUSI YA CHIKI ambapo MONALISA alivyokutana na Thea aliendelea kumlaumu lakini ghafla katika mazingira yasiyotegemewa MONA alienda KUMKALIA Mike ambae ni MUME WA THEA na kumwambia hivi UMEOA MWANAMKE WA AINA GANI, umeoa mwanamke mbaya MWEUSI, ungechelewa kidogo ningekutafutia mwanamke mzuri wa kumuoa na sio THEA...

Baada ya hapo KWA MUJIBU WA THEA kila mtu alipigwa na Butwaa kwa maneno aliyoyaongea MONALISA lakini katika hali isiyotegemewa baadae tena MONALISA alimwambia kitu Mike ambae ni MUME WA THEA ambapo sielewi ilikuaje lakini MONA akajikuta amemwambia MUME WA THEA kwamba we Mike wewe unajishaua "NTAKUNYIMA"

THEA akaendelea kusema kwamba alizidi kukwazika na neno hilo kutoka kwa rafiki yake kwamba ATAMNYIMA, akazidi kuhoji kuwa MONA ana nini cha kuweza kumnyima MUME WAKE!!!!???

Nilimuuliza THEA kama labda wana kawaida ya kutaniana lakini alichojibu ni kwamba HAWANA KAWAIDA YA UTANI na ni vitu anavyoshindwa kuelewa vimetokea wapi na MONALISA alikuwa ni mzima ambae hajanywa POMBE hivyo anachojiuliza ni NINI AMBACHO ATAMNYIMA MUME WAKE (mume wa thea). Thea akaendelea kusema kuwa baada ya hapo waliendelea na safari yao ya Mafia bila MONA kushiriki lakini walivyorudi alishangaa kupigiwa simu na watu tofauti kwa ajili ya usuluhishi, nilivyomuuliza ni nani ambae alipeleka hizo habari za KUTOKUELEWANA KWAO alisema kwamba ni mama yake mona ambae aliamua kutafuta suluhu kati yao baada ya kujua ugomvi wao ambapo MONA aliskia maneno yanayoongelewa kitu ambacho kilimkosesha raha hivyo mama MONA akaona ni uamuzi wa busara kukaa chini na kujadili kuliko kuendelea na maugomvi

Moja kati ya gazeti lililoripoti habari yao

Lakini katika hali isiyotegemewa pia siku moja THEA alipigiwa simu na polisi na kumwambia kwamba ANAHITAJIWA kituo cha POLISI CENTRAL kwa kosa la KUMTISHIA KUMUUA Monalisa ambae alifika pale Kushtaki..


Lakini Thea alikataa kuripoti na mpaka leo hajaona polisi aliefika kumkamata na anachosema kwakuwa MONA ameamua kwenda POLISI basi yeye THEA hataki kikao chochote cha usuluhishi kwakuwa MONA ameamua kupeleka mambo hayo polisi hivyo yeye THEA anasema basi bora yaishie polisi hukohuko na wayaongelee huko na si pengine popote..

Nilivyomuuliza kuhusiana na MSAMAHA ambao MONA ameomba kupitia MOVIE LEO siku ya jana THEA amesema kwamba hakubaliani na msamaha huo kwani ni wa Kinafki na kudiriki hata kusema kwamba MONA ana roho mbaya na hiyo imetokana na statement aliyoitoa MONA kwamba hakuna UGOMVI WOWOTE ila THEA ameamua kuongea hivyo ili tu KUIPROMOTE MOVIE YAO ambayo waliifanya kipindi cha nyuma.


HAYO SI MANENO YANGU ILA NI MAELEZO YA THEA KUHUSIANA NA CHANZO CHA UGOMVI

Hao walikuwa ni MARAFIKI WAZURI TU kama NDUGU.. na hali imegeuka na kwasasa HIVYO NDIVYO MAMBO YALIVYO, NI NINI KIMEINGIA KATI YAO!!!???KUNA NINI!!!????

7 comments:

Anonymous said...

Ila Huyo THEA kweli Sura yake mbaya

Anonymous said...

mara nyingi mmi migogolo ya wanawake huwa napita mbali! hasa wasanii wetu samtime wanataka promo kweli@zama

Anonymous said...

Jamani sio vizuri kugombana, Thea angekubali wasuluhishwe hata kama hawatakuwa marafiki tena lakini wamalize tofauti zao, pia angekubali msamaha toka kwa Mona ingependeza zaidi

Anonymous said...

nyie media ndo inabd muwapatanishe esp wewe zama hayo mambo yashapitwa na wakat ya kugombana

Anonymous said...

Nimekwerwa na mchangiaji wa kwanza, weka picha yako tukuone sura yako.

Hapa mimi naona mkosaji ni Monalisa, iweje akiri kuwa hana ugonvi na Thea na wakati huo huo amekimbilia polisi na mamake anataka usuruhishi, yeye angesema kilichopo tu kuwa ilitokea sintofahamu hivyo kuna usuluhishi au nilienda polisi labda kwa vitisho vya Thea kuliko anaomba msamaha wakati hana ugomvi nae.

Na atamwimbie alikuwa na maana gani anapomwambia mume wa mtu kuwa nitakunyima, amunyime nini??

Na kwa nini amwambie mume wa mtu kuwa amemuoa mwanamke mbaya, mweusi yeye mweupe, au ana uzuri gani yeye??

Ugomvi umezidi kwa wasanii sijui ni kila mtu kujiona babu kubwa au nini?? tunaomba mpatane muache ugomvi wa kitoto maana wivu haujengi unabomoa, kwa mantiki hiyo Monalisa acha wivu wa kijinga ulitaka Mike akuoe wewe???

Anonymous said...

Thea wajinga kam mona wapotezee,yeye ndoa ilimshinda asikutafutie sababu ya kutokuelewana na mmeo!

sophia said...

KAZANA MAMA WE CHA MSINGI TUNZA NDOA ASIKUALIBIE BULE YAKE YAMEMSHINDA.