Monday, August 22, 2011

IRENE - NILITEGEMEA KUSHINDA, WEMA HANIPATI KABISA KISANAA na HATA SAUTI YAKE YA KITOTOTOTO

Hayo ni maneno aliyoyatoa IRENE UWOYA nilipomuhoji kupitia Movie leo ambapo swali nililomuuliza ilikuwa ni anajisikiaje baada ya kupambanishwa na wema na yeye kuibuka mshindi!!?

Jibu alilolitoa ni kwamba kwake yeye ALITEGEMEA matokeo kuwa hivyo na alitegemea kwamba atashinda kwani Wema ni mdogo sana kwake kisanaa hivyo angeshinda Wema ingekuwa kama ndoto ya alinacha..

"Mimi ninaweza kuvaa uhusika wa aina zote tofauti na wema ambae yeye ana sauti ya kitoto sana ambayo inam-limit kucheza baadhi ya sehemu, kwani sehemu anazoweza kucheza yeye ni sehemu za majonzi na mapenzi tu lakini sio zile za kufoka tofauti na mimi ambae ukinipa sehemu yoyote NAKAMUA lakini Wema hapana hivyo kwangu ni mdogo sana kisanaa" alisema irene..

Nikamuuliza pia kama ni kushindanishwa na mtu mwingine ambae kidogo angeweza kulingana nae hapa Bongo angekuwa ni nani!!?? lakini alisema mpaka sasa kwa hapa BONGO hajaona kwani yeye ni namba moja na ataendelea kuwa namba moja labda NJE lakini sio ndani ya Bongo!!

kashindano hako kaliibuka ghafla baada ya kutokea habari kwamba IRENE na WEMA wanakutana kwenye filamu moja ambapo ukaibuka utata kwamba nani atamfunika mwenzie ama nani mkali na hatimae IRENE akaibuka mshindi dhidi ya Wema..

usikose kesho kumsikiliza WEMA kupitia movie leo ndani ya leo tena ya Clouds Fm saa NNE na dk 45 asubuhi!!!

37 comments:

Anonymous said...

sasa Zama ina mana siku hizi ndo unatufanyia hivi jamani!? kwanini usituwekee hapa kwako clip tukaona wenyewe matokea yake unatutuma eti tukasikilize hauko wapi sijui! tujari kama mwanzo bwana.

Anonymous said...

she is right.wema sauti inamuangusha,ukiwa na sauti kama hiyo,kwenye sehemu ya makeke keke inakuwa ngumu,kuubeba uhalisia.maybe wema atabadili muelekeo,baada ya kusoma hizi comment atachukulia in a positive way.ila huyo irene kusema yeye ni wa juu kuliko yoyote yule,mmh hapo sina uhakika.kwani aunt ezekiel naye yupo juu.ila irene kwenye kulia anaweza, machozi yake huwa sio feki kabisa

Anonymous said...

We Irene wacha kujigamba. Ngoja nikupe siri moja ya mafanikio: Ukidhani kuwa eti wewe umekwishakamilika kisanii basi ujue hutaendelea tena. Lakini ukijua kuwa bado una kazi kubwa ya kujifunza ili uwe msanii mzuri basi utaboresha ustadi wako. Sikupondi lakini lazima nikwambie ukweli: katika acting wewe bado sana sana. Kule Hollywood, Bollywood na Nollywood watu kama wewe wanaitwa "third-rate actors". Sorry girl ukweli ni ukweli.

Anonymous said...

Miss Irene Uwoya naomba nenda shule kwanza kasomee kuigiza kabla hujaanza makidai yako. Bahati yako upo TZ, nchi nyingine zote usingeliitwa mwigizaji sinema. Ndiyo maana narudia 'in the land of the blind a one-eyed man is king'.

Anonymous said...

Ati nini? Anasema eti hapa Bongo yeye ni namba moja? What a joke! Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha + lol lol lol mara elfu. Da Irene umenivunja mbavu, laiti ungelijua kuwa wewe si mcheza sinema usingetapika uozo huo. Ha ha ha!!!!

Anonymous said...

We irene wacha kumwaga matapishi yako hapa. Ukiwa na kichwa kikubwa hivyo mwisho utakosa hata asprin au panadol ya kukutibu ukiumwa bichwa. kubali kuwa wewe nimwigizaji wa kiwango cha chini kabisa. Ukishakubali hivyo ndipo utaweza kujifunza na kujiendeleza.

Anonymous said...

tuwekee zama hapa tuone mahojiano live na huyo wema

Anonymous said...

zamaladi jamani siku izi auko poa kama zamani wengine tunaishi nje ya tanzania tulikua tunaangalia bongo movie mahojiano kupitia ww lakini siku izi umeamua kutupozea jamani na akuna mwingine alikua anaweka ila ni ww bongostarlink tunajua music ww movie tufikirie alafu unapotea sana akuna mpya kila ukifungua wep yako pleas jamani sikia kilio chetu wapenzi wa blog yako

Anonymous said...

umeona hata wewe mimi sisemii inauuuumaaaa moyo

Anonymous said...

Haya tumeona huna msanii mwingine wa kuweka, hii inatosha weka kitu kipya

Anonymous said...

Chema chajiuza kibaya chajitembeza. We ireni huna lolote waja majisifu ya kijinga hapa.

Anonymous said...

Irene, bado we ni actor uchwara umeanza majigambo, je ungelikuwa actor wa maana ungesemeja? Angalia picha yako ya ya kijinga uliyopiga umekaa mkao wa tigo na kuanika matako yako hadharani. Nyoo huna haya we!

Anonymous said...

ZAMARADI MBONA SIKU HIZI UNATUBANIA HUTUWEKEI CLIPS UNAZOFANYAGA INTERVIEW SIS WA MBALI TUNAHITAJI KUZIONA PLIZZZZZZZZZZ

Anonymous said...

Watu hodari hawajisifu dada. Wengine ndio wanaowasifu. Wewe na kanumba hamna kitu eti "ooh haniwezi" au menzako kujiita "the great". Rubbish!!! Pumbafff mkubwa.

Anonymous said...

KANUMBA MUACHENI JAMANI MTU AKIMSEMA VIBAYA NASKIA KAMA ROHOINANICHOMOKA.

Anonymous said...

Duh! Bongo hakuna star wala nn..ha ha ha ha haaaaa wote wamechoka mbaya tuu! eti irene anajisifia! nenda kasome mama uzidi kupata ujuzi zaidi acha kujisifia kuwa ww upo juu zaidi ya wema! huo ni ujinga tuu mambo ya kitotoooo! badala uongee vitu vya maana unaongea pumba kweli mtabakia hapo hapo bongo mnalalama.

Anonymous said...

ZAma jiiiiiiiiiiiiiiii Dada yangu hata eid mubaraka inakushinda hata Dina ametoa eid mubaraka sembuse wewe mtoto wa kiislam.
Wako
James

Anonymous said...

Jamani wadau vipi mbona mnamshambulia Irene wakati yeye amejibu kadiri ya alivyoulizwa! aliyeanzisha mjadala ni Zamaradi wa kutaka kupiga kura nani zaidi, na mwisho mmepiga kura sasa vipi mnamshambulia? hajasema yeye ni best duniani kote bali ni kamzidi yule aliyeshindanishwa nae basi inatosha. kelele nyingi hazimzuii yeye kujinadi, pendekezeni basi ashindanishwe na nani mwingine tupige kura ili kujua nani mkali wa BONGO.

Anonymous said...

Nakubaliani na mchangiaji aliyesema mtu ukijijua kuwa hujakamiliki basi una nafasi ya kuboresha ujuzi wako na kujiendeleza lakini ukidhani unajua lakini kumbe hujui basi umekwisha. Huyu irene hawezi kuact lakini hajajua kuwa hajui kuact...matokeo yake? Amekwama na atazidi kukwama.

Anonymous said...

Zamaradi wa Mketema. Sasa nimeamini ule usemi wa wahenga yaani "Debe tupu haliacha kutika" au "Empty tins make the loudest noise". Huyu Irene ni "debe tupu" tu katika fani ya uigizaji.

Anonymous said...

dada Irene umetuvunja mbavu kweli kweli, yaani eti wewe unajiona umefika kumbe katika sanaa ya sinema we si lolote wala chochote. Nenda shule kwanza kabla hujazidi kutuchekesha kwa utumbo wako. Ha ha ha ha

Anonymous said...

tuwekee hiza links tuone... halafu wema yupo juu Hajatulia kabisa by angetulia wema angefika mbalii sana .maana anajua kuigiza anafanya kitu kinakua REAL bt Irene anaboa kufoka sana

Anonymous said...

irene wacha makidai yako ya kipumbavu hujui kuekti wewe. kajifunze kwanza kabla hujaanza kujivika kilemba cha ukoka. mama tarimo.

Anonymous said...

Nakubliana na aliyesema debe tupu haliachi kutika ha ha ha.

Anonymous said...

Jamani naungana na mdau hapo juu Irene amejibu kama alivyoulizwa, hapa tatizo ni Zama kwakuwa hana mtu mwingine anaweza kumweka kwenye blog yake akapata comment ngingi zaidi ya wema na Irene, hebu angalia toka ameweka hiyo kitu ni muda gani umepita kama si unyunyu, kazi ya kublog imekushida funga bwana unatuzingua tu, huna habari nyingine zaidi ya wema na irene

Anonymous said...

Kwanza wote nyinyi mnafunikwa tu. Irene huna lolote zaidi ya kukaa uchi. Mwanamke anaejua kuigiza angaliu kwa viwango ni Monalisa (Yvonne Cherry)

Anonymous said...

Irene wewe si muigizaji. Nenda shule kwanza kabla hujaanza kututapikia majisifu yako.

Anonymous said...

Nyoo......muone huyo mkaa uchi akijisifu kabla ya kusifiwa.

Ines baraka said...

Kemmy yule wa kaole asemaje, tanzania hakuna celebrity hapa.Kemmy yule wa kaole asemaje, tanzania hakuna celebrity hapa.

Anonymous said...

Ines, ni kweli hakuna celebrity lakini cha kusikitisha zaidi ni kuwa hawa so-called actors ni wabovu mno katika fani ya sinema, lakini badala ya kujifunza wanaanza majigambo ya kipumbafff mara siju "eti mimi the great" na ujinga kama huo. We Irene badala ya kujipigia makofi na kujipongeza ungelitakiwa ujifunze acting kwanza kabla hujajiabisha hapa. Nakubaliana na mdau aliyesema debe tupu haliachi kutika.

Anonymous said...

Sikiza Irene bana, ngoja watu wakusifu kabla hujatapika utumbo wako hapa bana!.

Anonymous said...

SINA LA KUONGEZA ILA NAKUBALIANA NA WOTE WALIOSEMA KUWA DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA. Lack of modesty os a sign of ignorance and mediocrity. We Irene hujui ku-act hata kidogo. You are an ignorant and a mediocre third-rate so-called actor. Jifunze hiyo kazi kabla hujadhani umeshafika. Hujafika bado.

Anonymous said...

Ni kweli anaongea kama hajui kuongea!au hataki vile...nashangaa hata kny u miss alijielezea vipi?? ndio maana hakufanya vizuri miss world by then

Anonymous said...

hamna ki2 hapo,aingie class kwanza yeye na wenzie wote then 2tazungumza,otherwise utumbo mtupu

Anonymous said...

Irene...ujinga si dhambi...lakini nakuomba uufiche huo ujinga wako nyumbani badala ya 'kuuza' huo ujinga hadharani na kutupa kichefuchefu na hata kututapisha na majigambo yako ya kijinga.

Anonymous said...

irene you can't be serious, you are not an actress, wewe ni mbabaishaji tu. jifunze kuekti kwanza halafu ndio utambe.

Anonymous said...

irene nakuaminia my love we mkali. kila la heri mama