Friday, March 26, 2010

ANAITWA HAMIS MANDI a.k.a B dozen

Nilitoa hii picha na kuomba watu waniambie wanahisi HUYI NI NANI... Kwa wale wote waliokuwa wakiuliza huyu ni nani ama ambao walijaribu ku-guess wameshapata jibu, anaitwa HAMIS MANDI ama B-dozen mtangazaji wa CLOUDS FM RADIO kwenye kipindi cha XXL.
Hapa akiwa anaonekana kwa vizuri huku style yake ya nywele ikiwa inaonekana.

B-12 akiwa mzigoni........ Wooooooote waliosema huyu ni DOZEN wamepatia Congratulation guys.. Kwa wengine waliojaribu asanteni sana.. Tuko pamoja!!
Tusubiri nini kitafuata kwenye Guess WHO!!HIZI MAKE-UP ZETU KWENYE FILAMU NI SAWA KWELI??

Ukizungumzia Make-Ups watu wengi akili huenda moja kwa moja kwenye kupendeza, But when you talk about Make-up in film ni kitu tofauti kabisa.

Katika filamu huwa kunakuwa na uhusika tofautitofauti, watu huweza kucheza kama Mke wa mtu, Sugar mummy, changudoa, House girl, chizi, Jini, Mchawi n.k.

Na kama unavyojua kwamba Filamu ni Kuchukua maisha halisi na kuyaweka katika maigizo hivyo ni muhimu kumfanya mtu anaecheza sehemu fulani afananie na sehemu anayocheza ili aweze kuleta UHALISIA kwa maana ya kuvaa uhusika kamili si wa maneno tu bali hata KIMUONEKANO, kama ni Chizi inabidi aonekane chizi kweli,kama ni Changudoa muonekano wake inabidi uwe hivyo kulingana na sehemu anayocheza na SI KWA KUPENDEZA peke yake kama ambavyo wengi tunafikiria.

Hivyo maana halisi ya Make-ups katika Filamu ni kitu chochote ama ile hali ya kumbadilisha mtu ili aweze kuwa na muonekano na A-fit kwenye uhusika anaotakiwa kuucheza (kwenye sehemu husika) inaweza ikawa wa kupendeza ama kuchukiza. Let say mfano mtu anaweza akacheza kama MZIMU ama JINI anaweza akapakwa masizi, kwenye Filamu hata kama mtu amepakwa MASIZI ili atishe, hiyo kwenye filamu hatutaita masizi bali ni MAKE-UP.

So that’s HOW make-up inafanya kazi kwenye Filamu.

Lakini tukirudi kwenye filamu zetu za hapa nyumbani, maranyingi ma-MAKE-UP artist wetu wanafeli kwenye hili na sielewi tatizo linakuwa wapi, mtu anaweza akacheza yuko nyumbani tu kawaida AMETOKA KUAMKA lakini ATAREMBWA kupitiliza kiasi kwamba hata ule uhalisia huupati. Ama yuko kijijini hajawahi kufika hata mjini na maisha yake ni ya hali ya chini kabisa lakini kawekwa DAWA ama WAVE, haonekani kabisa kama ni wa kijijini kiasi kwamba anapoteza lengo zima la sehemu husika.

Kwa wewe mdau wa filamu uliefanikiwa kuangalia FILAMU kadhaa za hapa nyumbani hivi hizi make-up zetu ni sawa kweli?? zinaendana na mazingira halisi??

MATUMIZI YA MAKE-UP ZETU YANAENDANA NA MAANA HALISI?? AMA TUNACHOJALI NI MAUZO (KUPENDEZA) TU BILA KUANGALIA SEHEMU HUSIKA ANAYOCHEZA MTU?

Zamaradi Mketema.

Wednesday, March 24, 2010

I LOVE MY TATTOOS - UWOYA

Moja kati ya vitu anavyovipenda Irene Uwoya katika mwili wake ni tattoo zilizochorwa kwenye maziwa kifuani mwake ambazo zina alama ya nyayo za kitu kama paka ama chui.


Hapa zikiwa zinaonekana kwa karibu zaidi.


Kila mtu ana kitu anachokipenda katika mwili wake, je wewe unapenda nini kwenye mwili wako??


MASTAR WANAVYOJIACHIA BONGO.. FASHION POLICE: NANI KAFUNIKA.....???

Anafahamika kwa jina la SYLVIA SHALLY mmoja kati ya warembo waliofanikiwa kuingia tano bora ya Miss Tanzania 2009/2010


Akiwa ndani ya Boot nyeupe

Hapa akiwa katika pozi tofauti

IRENE UWOYA 'Mama ndikumana'


Uwoya akiwa ndani ya kiatu cha Draft.

ELIZABETH GUPTA

Ndani ya Simple gladiator

Elizabeth katika pozi jingine tofauti


Hii ni miguu ya wanadadiva wawili kutoka kushoto SHADEIYA ndani ya Brown boots and the one one with purple heels ni LOVENESS LOVE wa Clouds FM radio 'DIVA'


Hapa wakiwa wanaonekana kwa vizuri zaidi (SHADEIYA na LOVENESS LOVE)


King of the afternoon shows Hamis Mandi a.k.a B 12, B dozen, B twangala, B whatever men.B12 Akionekana full

The Top model FIDELINE IRANGA
Akiwa ndani ya Pozi tofauti
Kwenye swala la viatu FIDE alitokea kama hivi

Handsome Boy MWINYI MACHOZI, mwimbaji wa machozi band.

Na chini alitokea hivyo
Kazi kwako kuniambia katika hao nani alikukuna zaidi kimavazi.

Tuesday, March 23, 2010

one eye

always ponder why all who take snaps close one eye and say cheeez.
anyone got an answer???

busy as a bee and chilling out

cornering ZAIN's Tunu Kavishe with brother-in-arms Ephraim Kibonde
Chilling out with the Clouds FM and Clouds TV fellas


with Kate de Luna

This is after my first interview with a real Diva...
USA's Kat de luna when she visited Dar es salaam, Tanzania, lately.
You should hear her purring voice that behind the mike floats like a flute on high note

interviewing busta ryhmes in Dar es salaam, Tanzania

At Clouds TV I get to interview most of the visiting international celebrities. this time around Busta Ryhmes is starring. Man the guy is huge but as humble as hulk. He responded to all my questions with intergrity and respect. He is one professional dude, I can say
the dude is big...
Busta shows lots of care and respect to me
I love Tanzania, he says
Busta and Spliff Star just cant believe they have a huge following in Tanzania
Spliff Star with the Clouds TV crew and I

NI MCHEKESHAJI GANI ANAKUVUTIA KWA HAPA BONGO?

Kuna wachekeshaji wengi sana hapa Tanzania na wanafanya kazi nzuri sana ingawa ni wachache wanaotambulika zaidi. wapo wakongwe na wanaochipukia, na kwasasa ushindani umekuwa mkubwa kidogo baina yao..
Ukiwa kama mmoja kati ya watazamaji wa kawaida ni MCHEKESHAJI GANI ambae huwa anakuvunja mbavu zaidi hapa TANZANIA na kwanini??

Tuesday, March 16, 2010

'SHAMSA' NYOTA INAYOCHIPUKIA KWA KASI KWENYE FILAMU BONGO


Amezaliwa miaka 23 iliyopita kwa jina la Shamsa Wassy 'Ford' , ni mmoja kati ya waigizaji wanaokuja juu sana kwenye tasnia ya filamu akiwa ameshafanya filamu kadhaa lakini hasa iliyomfanya atambulike ni filamu ya Saturday Morning aliyofanya na kampuni ya Game first quality.


Ili kumjua zaidi shuka nae kwenye mahojiano hapo chiniQN: NI SWALI GANI AMBALO UNATAMANI KUULIZWA NA HUKUWAHI KUULIZWA POPOTE PALE?
ANS: kitu ambacho sipendi kutoka kwa mwanaume


QN: NI KITU GANI AMBACHO HUPENDI KUTOKA KWA MWANAUME?
ANS: Sipendi mwanaume anaetumia mgongo wa wanawake kuendesha maisha yake, mwanaume tegemezi ambae hana msaada wowote.


QN: KITU GANI KILIKUSUKUMA KUINGIA KWENYE SANAA?
ANS: Sanaa ni kitu ambacho nimekuwa nakipenda siku zote na ninaamini nina kipaji na pia napenda kuitumia sanaa ili kuelimisha jamii yangu.


QN: MSANII GANI WA KIKE ANAEKUVUTIA HAPA TANZANIA?
ANS: Namkubali sana Riyama, ni mtu anaeweza kuigiza sehemu yoyote, anavaa uhusika inavyotakiwa na anabadilika kutokana na mazingira, kiufupi namkubali sana huyu dada.


QN: UNAICHUKULIAJE TASNIA YETU YA FILAMU KWA UJUMLA?
ANS: Ukiangalia zamani na sasa kwakweli tunajitahidi sana, ingawa bado kuna machachemachache ya kurekebisha lakini tasnia yetu imekua mno tofauti na zamani.


QN: SANAA INALIPA?
ANS: Kimtindo inalipa hivyohivyo kibongobongo hatupati kikubwa lakini kidogo cha kujikimu kimaisha tunapata ingawa huwezi kufananisha na wenzetu kama Nigeria ama nchi nyingine, wenzetu wanafaidika zaidi lakini kwa Tanzania kipato chetu ni tofauti na kazi tunayofanya, wanaofaidika zaidi ni watengenezaji filamu na si sisi waigizaji.


QN: MATARAJIO YAKO NI NINI?
ANS: kuwa msanii mkubwa sana na kutambulika kimataifa.


QN: KATIKA FILAMU ZOTE ULIZOFANYA NI IPI AMBAYO UNAHISI UMEKAMUA ZAIDI?
ANS: Nimeshafanya filamu kama tano hivi ikiwemo hard time ambayo haijatoka, saturday Morning na nyinginezo lakini ambayo nahisi nimekamua zaidi ni CRAZY LOVE ambayo bado haijatoka.


QN: UNAPATA USUMBUFU WOWOTE KWA WANAUME?
ANS: Nikiwa kama mtoto wa kike na msichana mrembo napata usumbufu lakini najua jinsi ya kukabiliana nao hivyo hainisumbui sana.


QN: UMEOLEWA?
ANS: Sijaolewa, sina mchumba, sina Boyfriend na wala sihitaji kwa muda huu.


QN: MH! HAYA UNAPENDA NA KUCHUKIA NINI?
ANS: Napenda kuona wenzangu wakifanikiwa na nachukia sana Unafki.


QN: UNAMSHUKURU NANI NA NANI MPAKA HAPA ULIPOFIKA?
ANS: Kwanza kabisa MUNGU, pili wazazi wangu, Zamaradi Mketema, Familia ya Ford, Ray Kigosi, na Kampuni ya Game first Quality.


QN: UNAJIONAJE NDANI YA MIAKA MITANO IJAYO?
ANS: Kimaendeleo nitakuwa mbali sana na nitakuwa nimeshatambulika sana kupitia kazi yangu ya sanaa.


QN: SHUKRANI
ANS: Asante sana nashkuru pia.

Monday, March 15, 2010

EYO NICHEKI

Elizabeth Michael 'LULU'
Elizabeth akiwa katika pozi tofautitofauti

Anafahamika kwa jina la ELIZABETH MICHAEL ama LULU, ni mmoja kati ya watoto walioleta changamoto kubwa katika fani ya maigizo na filamu kwa ujumla akiwa ameanza fani hiyo katika umri mdogo wa miaka minne mwaka 2000. Kikundi chake cha kwanza kilikuwa Mbalamwezi sanaa Group na mwaka 2003 akajiunga rasmi na KAOLE sanaa Group na hapo ndipo kipaji chake kilipotambulika zaidi.
Mpaka sasa ameshacheza filamu nyingi tu zikiwemo Dangerous Girl, Family tears na nyinginezo nyingi na pia ni bado mwanafunzi wa KIDATO CHA TATU katika shule moja hapa jijini DSM akiwa anachukua mchepuo wa ARTS.
Pamoja na kwamba anafanya fiamu Malengo yake ya baadae ni kuwa MANAGING DIRECTOR wa kampuni fulani ama BUSINESS WOMAN.
Big up sana na tunategemea mazuri zaidi kutoka kwako.
KATIKA BONANZA LA WASANII LEADERS

Jackueline Wolper
Baadhi ya warembo waliohudhuria bonanza linalofanyika kila jumamosi pale leaders club

Miriam Jolwa ama JINI KABULA kama anavyotambulika na wengi


Toka kushoto Shamsa Ford, Hassan miundombinu na Jacqueline Wolper ndani ya Bonanza la wasanii


Tuesday Kihangala a.k.a MR. CHUZI nae alikuwepo

Warembo wakijiachia

Jackueline Wolper na Jini Kabula wakibadilishana mawazo


Bi Mwenda nae alikuwepo katika kuweka jumamosi yake safi


Hapa akilirudi sebene kimyakimya juu ya kiti.. lilimkolea kwelikweli!!

Thursday, March 11, 2010

UWOYA NDANI YA BONGO

Kwasasa yuko ndani ya Bongo akiendelea na swala zima la kufanya filamu na SI kwamba ndoa yake iko matatizoni kama watu wanavyosema.

Hapa niliwakuta Double tree akiwa na upcoming artist katika movie industry ya Bongo Shamsa Ford.

FILAMU GANI ILIKUSISIMUA KWA MWAKA 2009

Tumetoka kumaliza mchakato wa kumtafuta msanii wa kike na wa kiume aliefanya vizuri kwa mwaka 2009/2010 na sasa mchakato umehamia kwenye FILAMU gani ni nzuri kwako na
ilikusisimua kwa mwaka 2009 kulingana na vigezo vyako wewe..
Unaweza kupiga kura yako humu kwa kuniambia filamu hiyo ama sikiliza movie leo ya leo tena
jumatatu hadi ijumaa saa 10:45 asubuhi ndani ya CLOUDS FM kwa maelezo zaidi.
Kumbuka kwamba majibu yanatokana na maoni ya watazamaji na si msimamo wangu/wetu.

Monday, March 8, 2010

GUESS WHO!!???

Mara nyingi tumezoea kuona style za nywele kwa wakina dada lakini hata wakaka sikuhizi wana style zao za nywele mojawapo ikiwa ni hiyo unayoiona hapo juu, jaribu kuhisi HUYO NI NANI na ukipatia kuna zawadi kwa ajili yako, na hiki kitakuwa ni kitu cha kuendelea kwa kila wiki ambapo nitaweka picha mbalimbali za watu ambazo si rahisi kuzitambua kisha wewe ujaribu kutambua na kuniambia ni nani.. !!!
Haya kwa kuanza niambie HUYO NI NANI??