Tuesday, March 16, 2010

'SHAMSA' NYOTA INAYOCHIPUKIA KWA KASI KWENYE FILAMU BONGO


Amezaliwa miaka 23 iliyopita kwa jina la Shamsa Wassy 'Ford' , ni mmoja kati ya waigizaji wanaokuja juu sana kwenye tasnia ya filamu akiwa ameshafanya filamu kadhaa lakini hasa iliyomfanya atambulike ni filamu ya Saturday Morning aliyofanya na kampuni ya Game first quality.


Ili kumjua zaidi shuka nae kwenye mahojiano hapo chiniQN: NI SWALI GANI AMBALO UNATAMANI KUULIZWA NA HUKUWAHI KUULIZWA POPOTE PALE?
ANS: kitu ambacho sipendi kutoka kwa mwanaume


QN: NI KITU GANI AMBACHO HUPENDI KUTOKA KWA MWANAUME?
ANS: Sipendi mwanaume anaetumia mgongo wa wanawake kuendesha maisha yake, mwanaume tegemezi ambae hana msaada wowote.


QN: KITU GANI KILIKUSUKUMA KUINGIA KWENYE SANAA?
ANS: Sanaa ni kitu ambacho nimekuwa nakipenda siku zote na ninaamini nina kipaji na pia napenda kuitumia sanaa ili kuelimisha jamii yangu.


QN: MSANII GANI WA KIKE ANAEKUVUTIA HAPA TANZANIA?
ANS: Namkubali sana Riyama, ni mtu anaeweza kuigiza sehemu yoyote, anavaa uhusika inavyotakiwa na anabadilika kutokana na mazingira, kiufupi namkubali sana huyu dada.


QN: UNAICHUKULIAJE TASNIA YETU YA FILAMU KWA UJUMLA?
ANS: Ukiangalia zamani na sasa kwakweli tunajitahidi sana, ingawa bado kuna machachemachache ya kurekebisha lakini tasnia yetu imekua mno tofauti na zamani.


QN: SANAA INALIPA?
ANS: Kimtindo inalipa hivyohivyo kibongobongo hatupati kikubwa lakini kidogo cha kujikimu kimaisha tunapata ingawa huwezi kufananisha na wenzetu kama Nigeria ama nchi nyingine, wenzetu wanafaidika zaidi lakini kwa Tanzania kipato chetu ni tofauti na kazi tunayofanya, wanaofaidika zaidi ni watengenezaji filamu na si sisi waigizaji.


QN: MATARAJIO YAKO NI NINI?
ANS: kuwa msanii mkubwa sana na kutambulika kimataifa.


QN: KATIKA FILAMU ZOTE ULIZOFANYA NI IPI AMBAYO UNAHISI UMEKAMUA ZAIDI?
ANS: Nimeshafanya filamu kama tano hivi ikiwemo hard time ambayo haijatoka, saturday Morning na nyinginezo lakini ambayo nahisi nimekamua zaidi ni CRAZY LOVE ambayo bado haijatoka.


QN: UNAPATA USUMBUFU WOWOTE KWA WANAUME?
ANS: Nikiwa kama mtoto wa kike na msichana mrembo napata usumbufu lakini najua jinsi ya kukabiliana nao hivyo hainisumbui sana.


QN: UMEOLEWA?
ANS: Sijaolewa, sina mchumba, sina Boyfriend na wala sihitaji kwa muda huu.


QN: MH! HAYA UNAPENDA NA KUCHUKIA NINI?
ANS: Napenda kuona wenzangu wakifanikiwa na nachukia sana Unafki.


QN: UNAMSHUKURU NANI NA NANI MPAKA HAPA ULIPOFIKA?
ANS: Kwanza kabisa MUNGU, pili wazazi wangu, Zamaradi Mketema, Familia ya Ford, Ray Kigosi, na Kampuni ya Game first Quality.


QN: UNAJIONAJE NDANI YA MIAKA MITANO IJAYO?
ANS: Kimaendeleo nitakuwa mbali sana na nitakuwa nimeshatambulika sana kupitia kazi yangu ya sanaa.


QN: SHUKRANI
ANS: Asante sana nashkuru pia.

9 comments:

Anonymous said...

Weh unakubalika ile mbaya dada.
Kama unamkubali Riyama, basi fuata nyayo zake, yule dada ni fireeeee

Kila la kheri.

disminder.

Anonymous said...

mdadiva we komaa na game never give up but kikubwa usilewe masifa tu wangu aminia kwa saaaana

Anonymous said...

mdadiva we komaa na game never give up but kikubwa usilewe masifa tu wangu aminia kwa saaaana

Anonymous said...

amependeza sana dada huyu japo sijamuona kwenye movie ila yaelekea yupo makini katika kazi yake na anajua anachofanya.

Anonymous said...

uko poa but pungua coz,hata mastaa wa mbele hawan unene wako,hofu yangu unaweza kukosa casting ya maana ttz unene,kuna jamaaa wa hollywood wanakuja kuatafuta casting kwa ajiri ya movie watakayo tengeneza bongo

Anonymous said...

zama vipi mambo uwe una wai kutuweke habari mpya mapema.

Anonymous said...

zama vipi mambo uwe una wai kutuweke habari mpya mapema.

Anonymous said...

kwa nini huitaji mwanaume, au na wewe tukuweke kwenye kunbdi la akina CHESHIJE @ MAUREEN? ( WASAGAJI)

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.