Wednesday, August 25, 2010

ILIVYOKUWA KWENYE LAUNCH YA KIPINDI CHANGU (TAKE ONE)

Jana ilikuwa ni uzinduzi wa kipindi changu kinachohusiana na mambo ya filamu cha hapa CLOUDS TV kitakachorushwa kila siku ya JUMANNE saa tatu usiku, hapo ni mimi ZAMARADI MKETEMA nikiwa na EPHRAIM KIBONDE akiniuliza machache kuhusiana na kipindi.
Nikiwa na BEN KINYAIYA
Nikiwa na YVONE CHERRYL (MONALISA)
Bosi wangu RUGE MUTAHABA kushoto akiwa na EPHRAIM KIBONDE
Kutoka kushoto SHAFII DAUDA, ZAMARADI MKETEMA pamoja na PAUL JAMES ambao wanaendesha kipindi cha michezo ndani ya CLOUDS TV.
ALI DAX mwenye mic akimhoji mmoja kati ya madirector wa filamu Tanzania WILLIAM J. MTITU
Kutoka kushoto JACKLINE WOLPER, ZAMARADI MKETEMA, ROSE NDAUKA, AUNT EZEKIEL na MAYASA MRISHO (MAYA)
BEN KINYAIYA akiwa na ABDALLAH MRISHO kutoka GLOBAL PUBLISHERS wakifatilia kwa makini kipidi cha TAKE ONE.
DAXX akihoji baadhi ya wageni hapo kuna MZEE MAGALI pamoja na HASHIM KAMBI.
Kutoka kushoto jina limenitoka kidogo, kulia ni DUDE wakiteta jambo kidogo
Nikiwa na warembo ndani ya HIJAB
Baada ya kipindi ABDALLAH MRISHO akisalimiana na wadau..
Hapa mzozo ilikuwa ni viwanja vya MKURANGA, baadhi ya wasanii wakijadili jambo hilo hapo kuna SINGLE MTAMBALIKE(RICHIE), NOVA pamoja na baadhi ya wasanii wengine
Wakijiachia na kuangalia KIPINDI KINAVYOENDELEA, it was really fun.. CLAUDE akiwa na mkewe, PAUL ISANGI pamoja na ADAM KUAMBIANA..
JACOB STEVEN (JB), SELLES MAPUNDA pamoja na wadada wakionekana kufurahia jambo fulani..
WAKUVANGA akiwa na MR. MWAULANGA!!!

kutoka kushoto FETTY kutoka CLOUDS FM, KAYANDA, MCHOMVU na DINA MARIOS...

SHUKRANI SANA KWA WOTE TULIOWEZA KUWA PAMOJA SIKU YA JANA NA HATA KWA WALE AMBAO HATUKUWA PAMOJA LAKINI TUKAWEZA KUSHIRIKIANA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, WALIOWEZA KUTAZAMA KIPINDI NA WALE WOTE WALIONISUPPORT KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE, ASANTENI SANA SANA.. MUCH LOVE & RESPECT!!
TUKO PAMOJA!!!

Tuesday, August 24, 2010

USIACHE KUANGALIA CLOUDS TV SIKU YA LEO its SUPER TUESDAY

Leo siku ya Jumanne kuanzia TATU kamili za usiku ndani ya CLOUDS TV kipindi changu kinachohusiana na mambo ya FILAMU kitaruka kwa mara ya kwanza kabisa.. hivyo kwa wale wadau na hata wasio wadau wa filamu plz dont miss kuangalia kipindi hiko kinachoitwa TAKE ONE ili tuweze kupeana maoni ya hapa na pale katika kuboresha zaidi.
Mbali na kipindi kuruka saa tatu kutakuwa na mambo mengi sana kuanzia saa mbili usiku ambayo yatarushwa LIVE KUTOKA MJENGONI ndani ya CLOUDS TV siku hii ya leo.. DONT MISS!!!
asanteni sana

Monday, August 23, 2010

Tuesday, August 17, 2010

VITU USIVYOVIJUA KUHUSIANA NA CPWAA..


1. Real name Ilunga Khalifa Born in 1982, March 2nd, mtoto wa kipekee wa Sophia Ali na Khalifa Juma.Mama Msukuma, Baba Mrangi.

2. Nilianza mziki toka mwaka 1995 nikiwa naimba kwa lugha ya kiingereza tuu! My biggest role model then were Kriss kross, N.W.A, Cypress Hill, Guru, Wu-Tang Clan, House of Pain,MC Hammer, Michael Jackson, Vanilla Ice,Shaba ranks, Sade,Salt n paper,Tribe called Quest,Nas, Jeru da maja, and Boot Camp click .

3. Nilikuwa bingwa wa Rap kanda ya kusini mwaka 1999 nikashinda zawadi ya TSH 30,000 pale ukumbi wa NBC Mbeya chini ya TBL. Balozi wa Sprite na Cowbell milk mwaka 1998-1999 Mbeya.
That's is how it all started! Mwaka 1996 Club Valentino pale Green Belt Hotel,Uhindini Mbeya ilikuwa party yao ya welcome form 1, hapo alikuwa anachana ngeli tu CD bado zilikuwa hazijasambaa mwendo wa tape, beat ni za mamtoni.

4. Nilimaliza na kufaulu Mbeya secondary School ( Mbeya day) kwa division 1. Mwaka 1999 kutoka darasa la Science 1.

5. Nilichaguliwa shule moja aliyomaliza Rais wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa, kigonsera High school, Mbinga songea.Nikasoma form 5 tuu kabla ya kuhamishwa Pugu Secondary ambako nilikataa na kuhamia Benjamin William Mkapa ( City High School) sababu ya ubushi wa mjini. I was not a boarding school kid! I loved free life!

6. Nilijiunga na kundi la NEW JACK FAMILY 2001,kariakoo na kina Dully Sykes,Abby SKillz, Marehemu Complex,Queen Doreen, Gorilla killers,A-Tu, na Zaharani kabla ya kujiunga PARK LANE na Suma Lee 2002 huko Tanga.

7. Miaka yangu yote toka form 2 nafuga nakusuka nywele, nishagombana sana na uongozi wa shule kuhusu hilo.Nilikata nywele zangu form 4 kabla ya graduation na form 5 kigonsera baada ya mkuu wa shule kusema sipati uhamisho mpaka nikate nywele. I believe in self confidence and freedom of choice.

8. Miaka yangu yote shule toka Primary school, niko ndani ya top 5 nikiporomoka top 10 na nilikuwa siiingi vipindi vingi darasani especially chuo nilipokuwa,niko busy na tours za muziki lakini matokeo yakitoka ni " A A A" uliza niliosoma nao.
Hapo ni my Caring Father ( Mr.Khalifa) me and my My Lovely God Mother ( Sophia) at IFM ( Institute of Finance Management) 2006 Hapo is when i graduated with degree in IT.

9. Nilikuwa mwanachuo/ Msanii pekee niliyegraduate na msuko IFM mwaka 2006 ( IFM Class of 2003- 2006)mwenye stashahada ya ICT.

10. Nilikuwa na bado ni mwanachama wa studio kubwa Tanzania, Bongo records.

11. Nilipata na bado nafanya kazi kwenye one of the first and still leading Tanzania High Tech Companys . www.6telecoms.co.tz and www.push.co.tz immediately after college.

12. Msanii wa kwanza kuzindua music video ( 6 in the morning), Slip Way little theatre 1996, nakualika wadau kibao wa muziki Salama Jabri, Gadner, Channel 10, Prime Times na waandishi wa habari kibao.

13. Moja ya wasanii wachanga waliowahi kuanza game kitambo na kuimba stage moja na KBC wa kwanza Unit, Balozi na Saigon wa Diplomats,Solo Thang na Wateule, Mac D, Mr. II, Soggy Doggy Anter, GWM, Adili wa Chapakazi,na Jay Moo toka miaka ya 90.

14. Msanii mwenye kipaji cha hali ya juu kwenye uchoraji wa penseli,rangi za maji na mafuta na ubunifu wa kutathmini kupitia picha za kupiga. A+ form 4 n 6 kwenye Fine Arts na uigizaji.

15. Nimeshashirikiswa kwenye album ya Wanaume family kabla hawajatengana album ya mwisho nyimbo inaitwa " Live bila Chenga" chini ya PFUNK majani, pamoja na album ya Bongo records mwaka 2006-2007.

16. Msanii aliyeanzisha na kutambulisha muziki wa CRUNK mwaka 2006 akiwa na producer lucci, Afrika ya Mashariki na mpaka leo wananiita KING of BONGO CRUNK.

17. Nishawahi kupokea kichapo kutoka kw PINA wa KIKOSI CHA MIZINGA ( sababu=Confidential) na leo ni washkaji na tunaishi sehemu moja, Block 41.

18. Msanii wa kwanza Tanzania kufanya Uzinduzi mdogo na kuvunja rekodi ya mauzo ya vinywaji kwenye FIVE STAR HOTEL Tanzania, Movenpic mwaka 2009 Desemba ( Cpwaa Pre-Launch party).

19. Msanii wa kwanza Tanzania kuanzisha blogspot kwa kutumia njia tofauti mpaka leo: simu ya mikononi: http://www.simuyangukamera.blogspot.com

20. Msanii mwenye tuzo ya Kili Music award, video bora ya mwaka 2009.



21. Msanii wa Bongo anayependwa zaidi na wanafunzi wa Primary, Secondary,International Schools, na Vyuoni, kuanzia umri wa miaka 13 mpaka 29. according to BABKUBWA MAGAZINE, EATV SKONGA na CLOUDS FM XXL SHOW.

22. Japo wananiita king of Bongo Crunk, Cpwaa ni shabiki mkubwa na mchezaji mzuri wa miziki ya DanceHall, House na Bolingo.

23. Wasanii wa muziki wa dance haswa Bolingo humfananisha na kumuona mwenzao kutokana na muonekano wake na jina lake " ILUNGA" ambalo pia ni maarufu kule na watu wa CONGO.

24. CP alipewa jina la CPWAA na Msanii mwenzake Mr. Blue akiwa chini ya Mkurugenzi wake Gadner G. Habash mwaka 2006 na mpaka leo limekuwa popular zaidi kuliko CP.Napenda sana kula Sea Food,Movies, Kusafiri, Science fictions, Animals programs, Techo updates,Cartoons and i love my drink sessions

Picha na INFO kwa hisani ya CPWAA mwenyewe kwa habari nyingi zinazohusiana na yeye pitia www.cpwaa.blogspot.com

HEMED NA YUSUPH MLELA WAZIDUNDA KIUKWELI

Hii si story ya movie ila ni ukweli kabisa imetokea wakati wa kushoot filamu ya WILLIAM MTITU ambapo vijana hao walijikuta wakizichapa.

Awali watu hawa walikuwa ndani ya BEEF zito sana na baadae wakaja kupatana na kukutanishwa katika filamu moja lakini katika hali isiyotegemewa wamejikuta wakizidunda mbele za watu (WAKIPIGANA)

Ukitaka kujua sababu iliyofanya wapigane usikose kusikiliza MOVIE LEO siku ya kesho na ZAMARADI MKETEMA saa NNE na dk 45 asubuhi ndani ya CLOUDS FM the people station.

Monday, August 16, 2010

GHOROFA YA UDONGO..

Tumezoea kuona maghorofa yaliyojengwa kwa matofali lakini hii niliikuta sehemu moja nikavutiwa nayo kidogo..
Hii inaonesha si matofali peke yake yanayoweza kujenga kitu cha namna hiyo hata udongo unajenga ghorofa kama unavyoliona hapo kwenye picha.. Saaaaafi!!!

UNAUFAHAMU UPUPU!!???

Huu ndio upupu kama umeshawahi kuuskia ambao mara nyingi watu wanatumia kumpulizia mtu ili kumkomoa ambapo kuwashwa kwake hakuelezeki.
Kiukweli kabisa sikuwahi kuuona kwa macho ndio mara ya kwanza kwahiyo kama wewe pia hukuwahi kuuona ndio huo hapo kama unavyoonekana.

MLELA na HEMED ndani ya FILAMU MOJA.. BEHIND THE SCENE!!!


NANI ZAIDI????
Hemed akiwa katika moja ya set ya filamu yao mpya ambayo wanafanya chini ya kampuni ya 5 effect kwa WILLIAM J. MTITU
HEMED na MLELA wakiwa kwenye set
Madirectors DENNISS NGAKONGWA na WILLIAM MTITU
Mwanaume kazini
Baada ya kazi.. wanakula pozi kidogo
Mlela akisoma script
Mafahari wawili ndani ya filamu moja
Mlela on set

Mwanzo vijana hawa walikuwa kwenye beef zito sana lakini kwasasa wamepatana na kutoa tofauti zao na wanafanya kazi pamoja.. tusubiri tuone filamu hiyo ambayo ni COPY ya filamu ya BESTMAN ya nje.

KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA VIWANJA WEEKEND HII

Hapa ilikuwa ILALA tayari kwa safari ya Mkuranga, kutoka kushoto IRENE PAUL, DINA MARIOS, SAKINA LIOKA, GEAH HABIB, JACKLINE WOLPER pamoja na MILLARD AYO mwenye t-shirt nyekundu.
Safari ilianzia hapo
Tukiwa tumefika,kutoka kushoto THT dancer, SHADEIYA, ADAM MCHOMVU nyuma, SOPHIA KESSY, mdadaa, JACKLINE WOLPER pamoja na ZAMARADI MKETEMA (mimi mwenye mtandio wa blue)
Tukiwa kijijini, Mwalim Twalib akitupa maelekezo ya kijiji hiko.
Millard Ayo na Zamaradi Mketema
Lazaro Matarange mwenye nyekundu pamoja na Antonio Nugaz
Tukisubiria hivyo viwanja
Mwanakijiji ADAM MCHOMVU

SHULE ZETU...

Nilikutana na hii shule maeneo ya mkuranga jina likanivutia tu...

Friday, August 13, 2010

FAMILIA YA LUIZA MBUTU (NYONI's FAMILY)

Kutoka kushoto anaitwa MODESTA NYONI, LUIZA NYONI MBUTU, MATILDA NYONI, CHRISTINA NYONI, na ANNETH NYONI kitinda mimba!!!
Happy People , Happy Family kama unavyowaona ndio familia nzima ya NYONI.. Luiza MBUTU akiwa na dada na wadogo zake.

Hapa wameongezeka watoto wao alie kushoto anaitwa JOSEPH mtoto wa Modesta Nyoni, na mtoto alie katikati anaitwa BRIAN mtoto wa LUIZA MBUTU (mama B) na kabinti huko upande wa kulia anaitwa ROSE mtoto wa MODESTA pia (aliyekaa mwenye hereni nyekundu)