Wednesday, January 26, 2011

ORIGINAL COMEDY - MANABII WANAOKUBALIKA KWAO!!!!

ORIGINAL COMEDY kutoka kushoto JOTI (Andunje), WAKUVANGA (mama BERE au Baba Andunje), MPOKI (Rick Ross kwa sasa), MASANJA (mkandamizaji), MACREGAN KIPARA (Shemeejiii)
UMATI wa watoto ukiwafuata nyuma kwenye moja kati ya maeneo wanaotembelea huko mikoani..!!!

Kuna usemi unaosema NABII HAKUBALIKI KWAO na ni kitu ambacho kina-apply kwa watu wengi sana kwamba mara nyingi mtu huwa hathaminiki kwa watu wanaomfahamu ama waliomzoea..

Lakini kwa Original comedy hali ni tofauti kabisa, kwani ni moja kati ya KUNDI ama WATU ambao wanathaminiwa kuanzia nyumbani na hata nchi jirani, na wamefanikiwa kuteka watu wa Rika, Jinsia na hadhi tofauti kutokana na utofauti waliouleta... kuanzia VIONGOZI WA SERIKALI, WANANCHI WA KAWAIDA, WATOTO, VIJANA na watu wa AINA ZOTE.

Nakumbuka hata RAIS aliwahi kukiri kwenye siku yake ya kuzaliwa kwamba ORIGINAL COMEDY ni moja kati ya vitu anavyopenda sana kuangalia!!!!
UMATI wa watoto ukiwafuata nyuma kwenye moja kati ya sehemu wanazokwenda..
Wanaume kazini..

Mbali na hilo, Original comedy ni kundi ambalo limeleta mapinduzi makubwa sana hapa Tanzania na kubadilisha taswira nzima kwenye sanaa ya Vichekesho (Comedy), kwani zamani sanaa ya vichekesho ilikuwa inachukuliwa kama ya watu wa aina fulani na ilikuwa inadharaulika kidogo lakini kwa ORIGINAL COMEDY imekuwa tofauti na hata ile style iliyokuwa imekaa vichwani mwa watu wengi kwamba MTU AKIFANYA COMEDY LAZIMA AWE MCHAFU NA AVAE HOVYOHOVYO ilifutika kupitia watu hawa...
JOTI alileta tafrani kidogo kutokana na style yake ya KUSHTUA KIJOTI kiasi kwamba watoto majumbani huko hakukaliki na hata baadhi ya wanamuziki kama wa Dansi waliweza kuitumia kwenye Shows zao pamoja na baadhi ya wanabongoflavor kama C-pwaa..

Na kwa yote hayo nathubutu kusema kwamba ORIGINAL COMEDY ni MANABII WANAOKUBALIKA KWAO!!
BIG UP SANA KWENU.. KAZENI BUTI na MSILEWE SIFA

10 comments:

Anonymous said...

ni kwelii zama yan hao wametisha ile yenyewe

Anonymous said...

jamani mimi naomba website ya hawa orijino comedy ni hayo tu

Anonymous said...

Hawa jamaa wamejaliwa kipaji na wanijua fani yao vyema kabisa. Big up guys and keep it up. We love you!

Anonymous said...

Yap! hata mimi ni mshabiki wao namba moja. Nisipowaona au kuwasikia kwa zaid ya miezi miwili naona kuwa kuna kitu nimeki-miss. Mimi Original Comedy addict.

Anonymous said...

Wanakubalika kwao kwa ubunifu wao halisi. Ule msemo mcheza kwao hutuzwa unanikumbusha hawa OC. Tuko pamoja wazee......

Anonymous said...

Tuko wengi ambao ni mashabiki wao lakini naona pia waweke mkazo kwenye production ya dvd's ili wapenzi wao twende na wakati na kazi wanayoitoa. Big up lads. Edi.

Anonymous said...

yea ni kweli sister,lkn naona 1 wao amemiss hapo,Joseph shamba au jina la kazi vengu..yukowa pi huyo mtu?
Nawakubali sana hawa Original Comedy...Big up

Anonymous said...

Kati ya watu wachache ambao nilidhani ze commedy chali mmi kwani mwishoni mwa december kama vile nilidhani ndo wanapotea kumbe dah!!!!!!!!!!!!!!jamaa wako fire mbaya, nawahurumia sana wale wenzeo wa eastv sijui hata wanacho kifanya nni kule!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Hata mimi nawakubali 100%. Niwaulize swali moja tu : Je ideas na vichekesho wanavyoviigiza vinaandikwa/kutayarishwa na wao tu au kuna watu ambao wanawasaidia katika ubunifu (kama vile huko USA)? Nauliza hivyo kwa kuwa hawa jamaa kila siku wanatoa vunja-mbavu mpya.

Anonymous said...

Zama asante kwa kutuletea our favorite group katika blog yako hii. Tunawapenda sana the original comedy. Edson na Jenny.