Saturday, January 15, 2011

NATAFUTA MWENZA - Mzee Magali


Mzee magali ameamua kufunguka na kuweka wazi kwamba AMECHOKA KUISHI PEKE YAKE na kwasasa anatafuta MPENZI (mwenza) wa kuishi nae milele...

Hiyo ni baada ya kuishi takribani miaka SABA akiwa peke yake baada ya MKE wake kufariki mwezi wa NANE mwaka 2004 ambapo alimwachia WATOTO WANNE wavulana wakiwa wawili na wasichana wakiwa wawili ambapo wa kwanza anaitwa JOSHUA, wa pili HAPPINESS, wa tatu anaitwa ELIZABETH ambae yuko Form one kwa sasa na wa mwisho anaitwa FRANCIS ambae yuko darasa la saba
Mbali na watoto hao ambao amezaa akiwa na mkewe ambae ni marehemu kwasasa Mzee magali ANA WATOTO WENGINE WAWILI WA NJE ambapo mmoja alimzaa kabla ya Ndoa ambae ni MWANAMUZIKI anaeitwa SISTA FAY na mwingine amezaa baada ya wengine wote ambae ndie kitindamimba wake anaeitwa MAIMATHA hivyo kwa ujumla ana WATOTO SITA...

MZEE MAGALI ameongea hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha TAKE ONE kinachorushwa na CLOUDS TV kila jumanne saa TATU kamili Usiku ambapo aliongea mambo mengi sana kuhusiana na maisha yake na hayo ni machache tu kati ya yale aliyoyaongea...
kwa mengine mengi usikose JUMANNE hii saa TATU kamili USIKU Clouds TV!!!!

Haya kwa yeyote anaetamani kuwa MPENZI wa Mzee Magali basi MILANGO IKO WAZI cha kufanya TUMA MAOMBI YAKO tu na kama utakuwa na sifa anazozitaka basi Freeeeshiiiiii, tutakuita MRS MAGALI soon..

4 comments:

Anonymous said...

Kwanini asimuoe huyo mama yake maimadha? si ndo aliyezaliwa baada ya wote, inamaana mama yake yupo au mzee unaagenda ya siri? au mimi sijaelewa maelezo.

Anonymous said...

Itapendeza zaidi kama atamuo mama yake maimatha kwakuwa ndiye wa mwisho kuzaa nae au anataka kuza tena na mtu mwingine haipendezi hata kidogo, jamii haitamweleza

Anonymous said...

atoe basi email yake au namba ya simu atafutwe

Anonymous said...

Namba yake ni 111 au 100 zote zipo hewani muda wote