Thursday, January 20, 2011

TATTOO ZINA MAANA KUBWA SANA KWENYE MWILI WANGU- JACKY WA CHUZI

Kama anavyoonekana hapo kwenye picha Jacky ameweka wazi kwamba ana jumla ya TATTOO SITA kwenye mwili wake, NNE zikiwa sehemu zinazoonekana na MBILI zikiwa sehemu ambazo ni NGUMU kuonekana.. zinazoonekana ni kama hizo moja ni ya alama ya LIPS ambayo iko kwenye ziwa, na nyingine TATU ni za alama ya NYOTA ambazo mbili ziko kwenye viganja vya mikono na moja ikiwa mguuni.. Wakati MBILI nyingine zilipo ni SIRI YAKE...
Hii ni moja katika zile zinazoonekana ambayo ipo kwenye mguu wake wa kushoto..
Mambo ya LIPS kwenye Boobs... Chekzea!!!
Hii ni moja kati ya zile zinazopatikana kwenye mikono yake....

SINA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA JUMA NATURE
Katika interview aliyofanya na mimi kupitia TAKE ONE Jacky AMEKANA kabisa mahusiano yake na JUMANATURE kama ambavyo iliwahi kusemwa na kuandikwa kwenye gazeti moja ila alichosema ni kwamba mahusiano yao ni ya kikazi zaidi na hakuna zaidi ya hapo
Anaitwa Jackline Pentzel maarufu kama JACKY CHUZI jina lililotokana na yeye kuwa na uhusiano aw kimapenzi na Tuesday kihangala maarufu kama Mr. Chuzi ambae kwasasa mahusiano yao yamebaki historia..

Pamoja na yote anamzungumzia chuzi kama mtu mzuri ambae pamoja na kuachana hawana tatizo lolote na wanaendelea na kazi kama kawaida..

Uhusiano wake na Chuzi ulileta mambo mengi sana kubwa likiwa ni BIFU zito aliloingia na KABULA maarufu kama JINI KABULA ambae ni mzazi mwenzie na Chuzi lakini kwasasa wameona ni upuuzi na wameamua kuweka tofauti zao pembeni ukizingatia kwamba wote hawako na CHUZI hivyo kwasasa ni MARAFIKI WAKUBWA...

Kuhusiana na Tattoo zinazoonekana kwenye mwili wake JACKY amekiri kwamba anapenda sana Tattoo na zana maana kubwa sana kwenye mwili wake ingawa hakutaka kuweka wazi maana hiyo lakini kubwa alilosema ni kwamba BOYFRIEND WAKE anapenda sana Tattoo zilizo kwenye mwili wake...

Huyo ndio JACKY maarufu kama JACKY WA CHUZI ambae utampata kupitia filamu kama WRONG NUMBER, BRANCH OF LOVE, MAPITO na nyinginezo nyingi sana....

Kwa haya na mengine mengi kuhusu jacky USIKOSE kuangalia TAKE ONE jumanne hii SAA TATU kamili USIKU ndani ya CLOUDS TV!!!!

Una Lolote!!!????

6 comments:

Anonymous said...

Swali kwangu kwenda kwake siku akiachana na huyo jamaa ambaye anapenda Tatoo na akakutana na mwingine asiyependa tatoo je haita mletea shida!? ktk mahusiano?

Anonymous said...

mi sijapenda alivoachia hizo nyonyo zake,kama picha za uchi bana.

Anonymous said...

Minyoyo mibaya kama ya ki....... aibu. Wewe zamaradi umeanza kuwa mji.... hebu tuwekeemambo ya maana humu ndani na yenye akili kama ulivyo wewe banaaaa

Anonymous said...

WATZ kwa kuiga bwana...hovyooo!!!! Kuna jamaa wengi ambao wanajuta kuwa na tatoo za kudumu, kwani kusiondoa kwa laser ni ghali sana. Bora tu upake hina itatoka yenyewe.

Anonymous said...

Zama acha kutoa picha za nusu uchi. Huyo dada amejidhalilisha yeye mwenyewe. Tuyapime maadili yetu kwa kujiuliza : je, mama au baba yangu au wakwe zangu [na watoto] wanastahili kuona jinsi ninavyoanika matiti yangu hadharani au ni aibu tupu???

Anonymous said...

85% YA WASANII WA BONGO WANAJIUZA HUYO AKIWA M1 WAPO HAHAHAAAAA WATAUZA SANA LAZIMA WAAMBULIE UKIMWI aibu yote hyo ya nn?
ustar bila uchi inawezekana!!!!