Friday, February 26, 2010

THIS IS IT!!.. IS IT??


Steven Kanumba 'THIS IS IT'

Kuna FILAMU mpya inakuja kuhusiana na Kanumba inaitwa THIS IS IT, hatujui kama itakuwa na chochote kuhusiana na MICHAEL JACKSON ukizingatia kwamba kuna MOVIE ya Michael Jackson inayokwenda kwa jina hilo ambayo ilizinduliwa 28th October 2009.
Lakini kwenye Cover la Kanumba tumeona kuna vitu vingi sana ambavyo vinashabihiana na Michael Jackson(Alivyopenda kuvifanya) kama vile kitendo cha kupenda watoto na kanumba anaonekana akiwa na watoto, pia Uvaaji wa kofia ni kitu alichokipenda michael Jackson na Kanumba anaonekana akiwa amevaa Kofia inayofanania na alizokuwa akipenda kuvaa Michael.

Si kitu kibaya Kujaribu kuthubutu kitu kama hiko ila since hatujajua story yenyewe inahusu nini huenda pia akawa ameamua kwenda level nyingine kwa 'KUDANCE' kama Michael.Kuna wengi waliojaribu kucheza kama Michael Jackson lakini hawakuweza kumfikia The King of pop, mfano mzuri ni watu kama Jamie Fox ambae hakuweza, Usher Raymond who was good in Dancing lakini hakuwa Michael, mwingine alieonekana Kujitahidi kidogo kuliko wengine ni Chris Brown lakini bado Michael alibaki kuwa Michael.
Ukimuangalia Kanumba hapo juu SIZE yake ni kubwa kidogo compared to Michael Jackson who was not big. sasa hatujui kama ataweza kuwapiku walioshindwa ama la kama story yenyewe itahusiana na mambo ya Dancing.ila kama ni Cover tu na jina la kuuzia Filamu tunasubiri tuone huenda story ikawa tofauti.

Dancing Movies kwa hapa Tanzania ni kitu kigeni kidogo,ila kama Kanumba atakuwa amejaribu kufanya hivyo, we will be interesting to see.
Michael Jackson 'THIS IS IT"

Baadhi ya vipande vya THIS IS IT ya Michael JacksonThursday, February 25, 2010

MCHAKATO UNAENDELEA - NANI MKALI?

Nilitoa baadhi ya picha za waigizaji wa kiume,na hawa ni wengine.. kazi kwako kuniambia kwa mwaka 2009 nani alifunika zaidi ya wenzake kwa upande wa wanaume. kwa maana ya aliefanya kazi nzuri kwa mwaka huo zaidi ya wenzake. Tuma kura yako uniambie NANI MKALI.

Mohammed Nurdin 'CHEKBUDI'Issa Musa 'CLAUDE'Deogratious shija 'SHIJA'Jacob Steven 'JB'Lumole Matovolwa 'BIGGIE'Juma Kilowoko 'SAJUKI' hapo akiwa na mkewe ambae ni mwanafilamu pia.


Endelea kutuma kura yako humu ndani uniambie nani alikamua kwa mwaka 2009 na haitakuwa vibaya ukiniambia kupitia filamu/kazi zipi pia.Wednesday, February 24, 2010

JICHO LA TATU - TUTAFIKA KWELI?

Katika Entertainment Industry hapa Tanzania kuna fani tofautitofauti, lakini zile ambazo zinaonekana ziko juu zaidi na zinachukua attention ya watu wengi ni MUZIKI, MITINDO na FILAMU.

Nikianza kuzungumzia Industry ya Filamu ni kitu ambacho kimekua juu ghafla tu miaka ya hivi karibuni, tofauti na Muziki ambayo ni Tasnia kongwe zaidi, Na Industry ya Filamu imeshatoa watu wengi sana ambao mpaka sasa ni MA-STAR WAKUBWA MNO hapa Tanzania na wanaendelea kufanya vizuri.

Kuna Usemi Usemao HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA ambapo maranyingi huwa tunatumia msemo huu kujifariji na kujipa moyo pale ambapo tunaona mambo yanaenda ‘Slow’ ama tofauti na matarajio yetu. Lakini tukumbuke vilevile kwamba NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI na DALILI YA MVUA NI MAWINGU, kwa upande wa wasanii wa Filamu wanaonesha hakuna kabisa dalili ya mabadiliko kati yao, wanaridhika haraka na kusahau walipotoka. Ili kuweza kufanikiwa katika vitu tunavyovifanya siku zote ni Vizuri kuangalia ‘NEGATIVES’ zetu zaidi kuliko ‘POSITIVES’ sababu kwa kuangalia mabaya na udhaifu wetu itatusaidia kuendelea mbele zaidi kwa kurekebisha tunapokosea kuliko mazuri yanayotufanya tubweteke na kuamini kwamba kilakitu kiko sawa wakati huenda ikawa tofauti.

Ili fani zote hizo ziweze kuendelea mbele kuna kitu kimoja kikubwa kinachohitajika sikuzote ambacho ni MEDIA kwa maana ya Vyombo vya habari kama Television, Radio, Magazeti, Mitandao n.k. Kupitia Vyombo vya habari watu ndio wanatambua uwepo wa watu ama kazi Fulani.
Business without advertising ni kama kumkonyeza mtu gizani. Hata kitu chako kiwe kizuri namna gani lakini kama watu hawakifahamu hakitakuwa na faida yoyote, It’s useless. Hivyo kazi kubwa ya Media ni kuripoti habari na mambo mbalimbali yahusuyo tasnia tofautitofauti ikiwemo na wahusika wenyewe.

Ikumbukwe kwamba si kuripotiwa kwa MAZURI TU MNAYOYAFANYA bali hata pale MNAPOKOSEA media haitakuwa nyuma kwa hilo. Na hio ni kwasababu tu unapokuwa mtu maarufu wewe ni kioo cha jamii na kama kioo cha jamii watu watataka kujua mengi sana kuhusu wewe sababu kuna wanaotamani pia siku moja wawe kama wewe. Hivyo kama umeamua kuwa Star sahau kuhusu PRIVACY.

Lakini kwa upande wa baadhi ya wasanii wa filamu ambao wao ndio wangeweza kuwa muongozo kwa wenzao hali inasikitisha kidogo, Inaonekana kabisa kwamba wanasahau walipotoka, Wanasahau kwamba VYOMBO VYA HABARI ndio vimewafikisha hapo walipo, wanasahau pia kwamba wao ni vioo vya jamii hivyo kila wanalolifanya jamii inataka kujua nini kinaendelea katika maisha yao.

Ombi langu tu kwa yeyote anaehusika msiifanye hii fani ikaonekana kama ni ya watu waliokosa muelekeo wa maisha wakaona njia pekee ni kukimbilia huku hapana. Baadhi yenu Reaction zenu zinaonesha udogo wa IQ zenu na hiyo inatukanisha moja kwa moja tasnia yetu hii nzima ya Filamu tukichukua kauli ya Samaki mmoja akioza ni wote wakati kuna wengi ambao wanajua nini wanakifanya. Kwenye hiyo ni kama inawaharibia. Filamu ni Ulimbukeni na Ujuaji mtupu uliojaa huku.

Hebu jiulizeni kuna Mastar wangapi wakubwa hapa Tanzania wame-struggle mpaka kufikia walipofika si kijina tu bali hata Kiuwezo na bado wanaheshima na kuheshimika katika jamii, hawajisahau. Mfano mzuri ni lady Jaydee ambae ni mwanamuziki, This is a real Diva na mfano mzuri wa kuigwa na watu wa tasnia zote kwa sasa, mafanikio yake yanaonekana waziwazi na hiyo ni kutokana na msingi mzuri aliojiwekea , lakini mbona hana majigambo na hizo Showing off za kienyeji!!! I RESPECT THIS WOMAN. Sidhani kama angekuwa na hizo mbwembwe mlizonazo angefika hapo alipo.
Mnachotakiwa kujua ni NO ONE IS PERFECT, kila mtu hukosea si wewe wala mimi, hata wakubwa wa nchi hukosea pia maranyingine na ndiomana kukawekwa washauri, Ubinadamu ulizingatiwa.

Sasa wewe unapokosolewa DON’T TAKE IT PERSONAL sababu hakuna mwenye Chuki na wewe, lengo ni kujenga na si kubomoa, WEWE NI NANI mpaka upambwe kila siku!? Mbona mnapenda SIFA tena zile za kijinga?? Badilikeni jamani ni aibu, nafikiri mngekuwa mnajua mastar wenzenu wa ulaya wanaishi vipi sidhani kama mngelalamika eti kwa KUKOSOLEWA FILAMU.

Lack of exposure ndio tatizo kubwa linalowakibili wengi wenu, Exposure ni kitu kizuri sana jamani, tusiishie NIGERIA tu, hebu tujaribu kuangalia mbali zaidi, siku zote siri ya mafanikio ni kuangalia wenzenu walioendelea kwenye kitu Fulani wanafanya nini juu ya jambo husika, Hakuna ubaya kuiga kitu kizuri. Tanzania ukishapita mitaa miwili mitatu watu wanakugeuzia shingo na kukuita jina basi unaona umeshamaliza kila kitu na unaridhika kabisa.

Kwa wenzetu mastar wakubwa kila wanachokifanya ni habari na wanaelewa kwamba ile ndio Price of being a superstar, sasa nyinyi kuongelewa filamu tena mara nyingine hata hujaskiliza wewe umefanya tu kuletewa tu habari “INDIRECT SPEECH” ambayo maranyingi kama sio zote haifiki kama ilivyokuwa ndio mnajipanikisha hivyo na mishipa inawasimama. Tutafika kweli?

Kiukweli mnasikitisha sana na mko kwenye hali mbaya mno bila nyinyi wenyewe kujijua. Acha wanaoendelea kuwasifia ujinga wawasifie na endeleeni kujazana ujinga ila mkikutana na WENZENU wa nchi nyingine ndio mtajiona MKO NYUMA kiasi gani, mara nyingi huwa tunapwaya.
Kibongobongo mtapeta lakini kama lengo ni kufika Hollywood kama mnavyokuwa mnajibu kwenye interview zenu kwa hali hiyo ya kutotaka mabadiliko MNAJIDANGANYA.

Mwenye masikio na asikie mwenye macho na aone, ni mawazo yangu tu si lazima ukubaliane nayo na hayahusiani na mtu yoyote.

Asante
Zamaradi Mketema.

Tuesday, February 23, 2010

NANI MKALI.....!!???

Kupitia 'Movie leo' ya Leo tena ndani ya clouds FM siku ya Jumatatu tuliweza kumpata msanii bora wa kike kwa mwaka 2009/2010 kwa maana ya aliefanya vizuri kwa mwaka jana.Na hii ilikuwa ni kupitia kura yako wewe mtazamaji wa Filamu za hapa kwetu Tanzania.
Mambo hayajaishia hapo turudi katika upande wa WANAUME, kwako wewe ni nani aliefunika kwa mwaka 2009 mpaka sasa tunavyoongea 2010. Tuma kura yako sasa humu ndani ama Sikiliza Movie leo ya leo tena kila siku Jumatatu hadi Ijumaa saa 10:45 asubuhi kwa maelezo zaidi.Tuma kwa e-mail address ya zammyt25@yahoo.com ama namba ya simu 0778 295551/0784 499547

Niambie NANI MKALI kati ya hawa wafuatao...?????Single Mtambalike 'Richie rich'Vincent kigosi 'RAY'
Yusuph Mlela 'ANGELO'Steven Kanumba 'KANUMBA'
Hemed Suleiman 'HEMED'
Mohammed Mwinkongi 'FRANK'Mahsein Awadh 'CHENI'Hajji Adam 'BABA HAJI'


Hao ni baadhi tu ya wasanii wa kiume, kuna wengi sana ,kazi kwako kuniambia mwaka jana ni nani 'ALISHINE' kuliko wengine katika Industry ya Flamu hapa tanzania.

NANI MKALI?

VIWANJANIHapo nikiwa kwa Peter Moe.

Weekend yangu was so good kiukweli, Ilikuwa saturday nikaona leo ngoja nijichanganye kwenye Viwanja mbalimbali... Siku ikaanzia kwa Brother Venture pale Mzalendo pub, i had fun sana nikaona si mbaya sababu safari moja huanzisha nyingine ngoja nijivute kwa Peter Moe na safari ikaishia pale Zonghua Garden kwenye Grooveback.. It was FUN.

Anaitwa Shamsa Ford, one of the upcoming movie star.. Nae alikuwepo.

Monday, February 22, 2010

MDADA ALIEFUNIKA 2009 KATIKA BONGO MOVIES


Aunt Ezekiel Kulia akiwa na Maimatha wa jesse


Katika MOVIE LEO kupitia kipindi cha Leo tena hapa clouds FM tulishindanisha wanadada wanaofanya filamu hapa bongo ili tuweze kumpata msichana aliefanya vizuri kwa mwaka 2009/2010. Kura ziliweza kukusanywa kupitia njia tofautitofauti kama maoni ya watu wa nje, SMS, pamoja na kuongea na Madirectors, maproducers na watu walioko kwenye tasnia hii ya Filamu. lakini njia kubwa kabisa ilikuwa ni MAONI ya watazamaji wa hizo Filamu na hatimae AUNT EZEKIEL GREYSON akaibuka kuwa Mshindi kwa kuwapiku wasichana wenzie wote wa tasnia yake.

Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta Challenge na kuangalia nani kafanya nini kwa mwaka 2009 ambao ndio tumetoka kuumaliza, hatujui mwaka 2010 nani 'atashine' .

Filamu ya kwanza kabisa iliyomtambulisha katika Tasnia hii ilikuwa ni MISS BONGO ambayo ilikuwa directed na William Mtitu..

Baada ya hapo akaja kuonekana na kushine kwenye filamu nyingine nyingi tofauti, Baadhi ya Filamu ambazo ameshawahi kuzifanya ni pamoja na TASTE OF LOVE ambayo ilielezea maisha yake halisi, WICKED LOVE, HOSTEL na nyinginezo nyingi.

Kama Mdau wa Filamu namtakia kila la Kheri mwanadada katika kazi yake ya Filamu.

Karibuni

Karibuni watu wote