Monday, June 28, 2010

UJAUZITO ULIVYOMBADILISHA ALICIA KEYS

mwanamke ukiwa na Ujauzito chochote kinaweza kikatokea, aidha ikakupenda na ukapendeza ama ikawa tofauti na vitu kama vilivyomtokea Alicia keys huko usoni na mwilini mwake vikakukumba pia.. ingawa mara nyingi reactions hizi huwa za muda mfupi.
Hapo juu alicia keys akiwa ameharibika usoni kutokana na ujauzito.

Hapa katumbo kakiwa kamechomoza kwa mbaali She looks good kwakweli (napenda kumuona msichana akiwa na mimba)

Its good unapokuwa kwenye hali hii uwe na mwenzio pembeni mkiwa free with love ina raha yake sana sio Kujifichaficha (tangulia nakuja).. hapo Alicia keys akiwa na baba watoto mtarajiwa Swiss Beats

On stage kama kawa na kitumbo.. No viatu virefu anafata rules za ujauzito.. Saafi!!

Kupendeza kama kawa.. kuwa mjamzito haina maana ya kwamba ndio uwe rafu na hovyohovyo, kuna nguo nyingi ambazo mjamzito anaweza akavaa na bado akapendeza na kuvutia, maana kuna watu wakiwa wajawazito wanajiachia mpaka wanakuwa wachafu sasa.

Thursday, June 24, 2010

HII SIO YA KUKOSA


Chill Out Session @ Cine Club by the Beach, feat Moracka, Jux, ATM, Rich Boy, Yang chiss the Dancer, 5,000/= Saturday from 8pm,Best Music Hottest Crowd, Drinks ToshaROGER THAT!!!!
JUMAMOSI HII USIKOSE!!!!

Friday, June 18, 2010

SIMU YAKO YA MKONONI NI KIELELEZO CHA WEWE


Kupitia simu yako ya mkononi unaweza ukajikuta unaexpress vitu vingi sana ambavyo watu hawavijui kuhusu wewe bila mwenyewe kujua hivyo simu ya mkononi inaweza kuwa kielelezo cha wewe na watu wakajua wewe ni mtu wa aina gani, unapenda nini, una tabia zipi na vitu vingine kama hivyo ingawa si kwa asilimia mia moja lakini kwa kiwango kikubwa mtu akakuelewa kama ni mshenzi ama mstaarabu.

Vitu vifuatavyo vinaweza kurahisisha mtu kukujua kupitia simu ya Mkononi

MLIO (RINGTONE)
Ni rahisi sana kumsoma mtu na kumjua kupitia mlio wake wa simu ya mkononi, kwa teknolojia yetu hii ya sasa ya bluetooth na mambo mengine walio wengi hutumia milio tofautitofauti kwenye simu zao kulingana na utashi na mapenzi yao.. na hapo ndipo unapokutana na nyimbo tofautitofauti kwenye simu za watu na hata sauti zilizorekodiwa ambazo zinaelezea mambo tofautitofauti. na maranyingi nyimbo tunazozichagua ni zile tunazozipenda ama zinazoelezea hisia zetu Hivyo MLIO mtu aliouchagua kwenye simu yake unaexpress vitu vingi sana kuhusu huyo mtu bila mtu mwenyewe kujua. (Mlio wako unakuelezea kwa asilimia kubwa)

MAJINA
Kila mtu ana njia yake ya kuhifadhi majina kwenye simu yake, kuna wengine huandika majina tu kawaida na kuna wengine huandika vitu tofauti tofauti kulingana na mtu aliemsave, mfano MSUMBUFU, TAKATAKA, MZUSHI, MPENDWA ama wengine husave hata kwa majina ya MATUSI.. Hivyo njia anayotumia mtu kusave majina yake kwenye simu yake inasaidia kumuelezea kinamna fulani.

GALLERY
Vitu ambavyo amevihifadhi kwenye simu yake kama nyimbo, videos na kadhalika. hii inasaidia pia kujua mtu ana tabia zipi na anapenda vitu vya aina gani. (Hii na ya hapo juu ina apply zaidi kwa mtu wako wa karibu)

Ulikuwa unalifahamu hili.. unafikiri simu yako inakuelezea???......TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Thursday, June 17, 2010

MR BLUE AIBUKIA KWENYE FILAMU

Msanii wa Bongo Flava Mr. blue ameamua kufuata nyayo za mastaa wengine wa muziki na kuamua kujiingiza kwenye Uwanja wa filamu.. BLU ameigiza katika movie yake ya kwanza kabisa akiwa chini ya Director Goodluck komba. Filamu hiyo itakwenda kwa jina la PRETTY TEACHER na ndani humo utampata Lucy komba, Mzee Chillo, idriss pamoja na wengine wengi.Mbali na BLU wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya ambao wameshafanya filamu ni pamoja na MAUNDA ZORRO, RAY C, Q- CHIEF na wengineo.

Hapa akiwa na Lucy Komba

Picha kwa hisani ya ISSA MICHUZI

NIMEAMUA KUIGIZA SHOGA - TINO

Msanii wa filamu za Kitanzania Hissan Muya maarufu kama Tino ameamua kuja kitofauti kabisa na kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa na msanii yoyote wa filamu hapa Tanzania kwa kuamua KUIGIZA KAMA SHOGA...

Huu ni ujasiri wa hali ya juu aliouonesha kwasababu nimeweza kuongea na baadhi ya wasanii wa kiume kama JB, CLAUDE, CHENI na wengineo na katika hao wote wengi wao walisema hawawezi kuigiza kama mashoga though mwisho wa siku ni sanaa tu.

Tangu kitu hiki kisemwe kupitia kipindi cha Movie leo ya clouds FM kumekuwa na MZOZO na GUMZO kubwa ambalo limeibuka baina ya watu wengi wakidai kwamba si sawa na wengine wakisema sawa..

Kwako wewe unaonaje!!???? Ni sawa mwanaume kuigiza kama Shoga??

SOPHIA KESSY ANATAKA KUJITOSA KWENYE FILAMU

Mtangazaji wa kipindi cha Bambataa hapa Clouds FM radio mwanadada Sophia Kessy anataka kujitosa kwenye filamu rasmi..

Hiyo ni baada ya kuangalia na kulisoma soko kwa muda mrefu akajikuta amevutiwa na maswala ya movie hivyo ameamua rasmi kuingia huko kwa Mamovie..

Wadau vipi .. Ataweza kupenya kwenye soko la filamu??????

ZAWADI KUTOKA KWA BIBI..Niko na zawadi yangu kutoka kwa Bibi
Leo tulienda kushoot Bibi Bomba na huyu ni mmoja kati ya mabibi tuliokwenda kuwatembelea ametupokea vizuri sana na kutuonesha ukarimu wa hali ya juu. Pia ametupa zawadi kibao yakiwemo Mahindi, Maboga, Mboga za majani na zawadi nyingine kibao kutoka shambani kwake.. hapo tukiwa nje ya nyumba yake.

Mimi hapo kushoto, Mohammed Cameraman wangu pamoja na Shagile hapo kulia

Hapo ameongezeka Wasiwasi Mwabulambo katikati na boga lake kichwani


Vijana wa kazi......
Baada ya kumaliza kazi Production team yangu.. Shukrani sana kwa BIBI tume-enjoy sana hii Trip..

I JUST LOVE MY T-SHIRT

With no good reason naipenda tu hii T-shirt yangu
Do i!!??
Ha ha haaa.. luv u my people!!!

Wednesday, June 16, 2010

MAISHA KUSAIDIANA....

We unaweza..!!!!????

KATIKA SUPRISE PARTY YA JAYDEE

Siku ya jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Lady Jaydee na mume wake GADNA G. akaamua kumfanyia suprise party ambapo akaalika wadau tofautitofauti na watu wa karibu wa jaydee bila yeye mwenyewe kujua..
Na furaha zote akiwa na mdogo wake

Mimi hapo kushoto nikiwa na Rommy Jones na my best friend Shamsa Ford..

Mbele ya Jikeki

Baadhi ya wadau waliokuwepo.. Shumileta na Zamda

Kutoka kushoto mbunge mtarajiwa shy-rose Bhanji, Mimi, Rommy Jones, Shamsa, Gadna na Khadija Mwanamboka

Jafarhai, Dabo, Jaydee, Shadee, Moracka, Mshkaji mwingine na Shaa, it was fun!!!

KIFO CHA MPAKANJIA KIMEBADILISHA MAISHA YANGU - JB


Anaitwa JACOB STEVEN ama JB, ameshafanya filamu nyingi sana nyuma kama SWAHIBA, MAHABUBA, WAKTI, MY FIANCE na yinginezo nyingi sana, ni mmoja kati ya watu wanaouvaa uhusika hasa wakiwa kwenye set, ukiniuliza binafsi filamu ninayoipenda sana zaidi kati ya zile zote alizoact nitakutajia Swahiba.

JB ni mtu mwenye Mke mmoja anaempenda sana, kwenye swala la mtoto bado hawajafanikiwa lakini mwenyewe anasema yeye ni mmoja kati ya watu wanaoishi katika ndoa zenye furaha kuliko kawaida (HAPPY MARRIAGE) na anaenjoy sana maisha yake ya ndoa.

Ukiangalia sehemu nyingi anazoigiza huwa kama mtu serious na mwenye misimamo sana lakini nje ya filamu JB ni nani??

Shuka chini ufahamu vizuri zaidi kuhusu yeye.


QN: JACOB STEVEN NI NANI NJE YA FILAMU?
ANS: Jacob Steven nje ya filamu kwanza ni MLOKOLE HUNDRED PERCENT, ni muumini wa kanisa la Mikocheni B assemblies of GOD tena muumini mzuri kwelikweli na ni mzee wa kanisa, Pili mke wangu ni Mlokole kama mimi, Tatu ni msanii NINAEPENDWA NA WASANII WENZANGU KULIKO MSANII YOYOTE am proud to say this na kama unataka kuamini fanya uchunguzi piga kura uliza wasanii ni msanii gani mnaempenda wengi watakwambia ni JB wasanii woote wakike nawachukulia upendo kama wa baba na mtoto mimi niko tofauti na wale wanaowatolea macho na kuwavua nguo, na wasanii wa kiume wote nawachukulia kama wadogo zangu na wote hao wananipenda sana sababu niko tofauti sana na wenzangu nafkiri ni Kristo Yesu aliyeko ndani yangu ndio sababu kubwa.


QN: NINI AMBACHO UNAPENDA SANA??
ANS: napenda sana kuangalia Movies siwezi kulala bila kuangalia Movies hasa movie za nje.. Napenda sana Movies.


QN: NI MSHABIKI WA TIMU GANI HAPA TANZANIA!?
ANS: Mimi ni mshabiki sana wa timu ya Ashanti united watoto wa Ilala, wakati nasoma zamani nilikuwa nacheza mpira sana nilikuwa nacheza na kina kama unamkumbuka Golikipa wa zamani Joseph fungo pamoja na Joseph Katuba nilicheza nao enzi hizo Mwananyamala kule Mtukula.. lakini Jeshini kule kwa wale waliopitiaJKT Mgambo kwa mujibu wa Sheria baada ya kumaliza Form six nilikuwa nacheze mpira sana nilichezea timu ya kikosi, na sasahivi ni kwasababu tu ya umbo lakini kama hivi tunavyokosa wafungaji wazuri natamani nipungue kidogo kidogo na nicheze kwasababu nina uwezo wa kukimbia na kupiga mashuti uwezo ambao mafoward wengi hawana.


QN: MTU GANI MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO??
ANS: Mama yangu mzazi anaitwa MARGARETH MBURA pamoja na Mke wangu QUEEN IRENE lakini hao wote hawamshindi Yesu kristo.


QN: MTU WAKO WA KARIBU NI NANI??
ANS: Zamani alikuwa ni MOHAMMED OTHMAN HERRY MPAKANJIA ambae ameshafariki lakini ukiacha huyo ambae nimemsema sasahivi watu watatu wametokea kuwa watu wangu wa karibu sana, wa kwanza ni mdogo wangu anaenifuatia anaitwa Emily steven Mbura, na wengine ni Madirector wangu wawili ambao ni Adam Kuambiana na Issa Mussa (Claude).


QN: UNAKUMBUKA NINI KWA MPAKANJIA??
ANS: nakumbuka mwaka 2000 yeye ndio alikuwa wa kwanza kuniambia JB hebu jaribu kutengeneza Movie zako mwenyewe, nakumbuka movie yangu ya kwanza ilikuwa kanisa la leo nilitengeneza enzi hizo zamani kipindi hiko gharama za utengenezaji zilikuwa chini sana nikafanya share na mjomba fujo fiamu iligharimu karibu milioni tatu, na mimi MILIONI MOJA NA LAKI TANO nilikuwa sina lakini MOHAMMED MPAKANJIA ALINIPATIA MILIONI MOJA NA LAKI TANO CASH BURE KABISA hiyo siwezi kusahau na kutoka hapo tu ndio nikaanza kufanya production zangu mwenyewe.


QN: KUONDOKA KWA MPAKANJIA KUMEATHIRI VIPI MAISHA YAKO?
ANS: Alikuwa akiwa na kitu kimembana sana mtu wa kwanza kuniambia ni mimi halikadhalika na mimi pia nilikuwa nikipatwa na kitu aidha cha furaha ama cha huzuni mtu wa kwanza kumwambia ni yeye, yeye alikuwa ni Mshauri wangu na yeye alikuwa ni Msiri wangu, MIMI NILIKUWA NIKIJUA CHOCHOTE CHA KWAKE NA HATA YEYE ALIKUWA AKIJUA CHOCHOTE CHANGU.

Kinachonifanya nimkumbuke zaidi kila baada ya kazi ilikuwa lazima tutafutane kilasiku kuachana kwetu ni mpaka kila mtu anapoenda kwake hiyo naimiss kwasababu ikifika muda kama ule namkumbuka sana sana na inaniwia vigumu kwasababu naimagine sasahivi tungekuwa sehemu fulani tunafanya hivi na vitu vingine kama hivyo. nimejaribu kupata marafiki lakini HATUJAWEZA KUWA CLOSE KAMA NILIVYOWAHI KUWA NA MPAKANJIA na hata nyuma kabla yake sikuwahi kuwa karibu na mtu kama nilivyokuwa na Mpakanjia, namkumbuka sana sana.


QN: ROLE MODEL WAKO NI NANI?
ANS: Role Models wangu ni wawili wa kwanza ni AMITAH BACHAN nampenda sana sana na mwingine ni RICHARD GERE na nimempenda sana kupitia filamu yake ya Unfaithful na Pretty woman. huwa siwezi kulala bila kuangalia filamu za hawa watu.


QN: UNAPENDA CHAKULA GANI?
ANS: Mi napenda sana SAMAKI NA KUKU zikitengenezwa na Wali na maharage. napenda mno lakini zaidi kuku.


QN: MAFANIKIO GANI AMBAYO UNAYO?
ANS: Wakati naanza Kampuni ilikuwa na Capital ya Milioni TATU tu kwenye Account lakini nimeweza kupigana kutoka Milioni tatu mpaka MILIONI HAMSINI benki.. hivyo hiko ni moja kati ya mafanikio mengi niliyoyapata kupitia filamu.

Tuesday, June 15, 2010

HABARI ZENU BANAA..................

salamu ndio jadi yetu watanzania... nawasalimu tu!!

Monday, June 14, 2010

CHANGIA DAMU...

MWANAMKE UREMBO - USIONE VYAELEA

NILIMBAMBA KEISHA SALON MOJA AKIJIWEKA SAWA
Nilimkuta Keisha salon moja hivi akijitayarisha kwa ajili ya Graduation yake ya kumaliza Form Six inayofanyika leo pale Laureate international school, hapa akiwa anatengenezwa nyusi

HAIR DO - BEFORE
hapa kabla haijamaliziwa style yake ya nywele ilikuwa ikionekana hivi

Hapa weaving likishashonewa linakatwa kistyle ili kitokee kitu kizuri

Mambo ya Sandra hayo kama unavyomuona.. Busy mwenyewe akimuweka sawa mdada

HAIR DO - AFTER

Hapa ndio mambo yamemalizika kwa nyuma inaonekana hivyo

Kwambele ndio kama unavyoiona

hapo mdada ameshapendeza.. Mwanamke Urembo

Friday, June 11, 2010

HAMMA Q ANENA BAADA YA KUTOKA JELA


Inawezekana ulikuwa hulifahamu hili lakini habari ni kwamba Mwimbaji wa PEMBE LA NG'OMBE kutoka bendi ya Dar Modern Taarab ambapo hapo awali alikuwa ni mwanamuziki wa bongo Flavour HAMA Q ameipata joto ya rumande alikokuwa under arrest katika Gereza la Keko hapa DSM kwa muda wa wiki kadhaa na ameachiwa kutoka Gereza la KEKO mwezi uliopita mwishoni kama kwenye tarehe 29 may (kama sikosei). Ambapo kesi iliyokuwa ikimkabili ni kujeruhi.

Akiwa katika studio za clouds fm leo katika leo tena

katika mahojiano leo Hamma Q ametoa hali halisi ya jinsi jela kulivyo ambapo amesema kwamba mtindo wa kulala ni ubavu ubavu na si chali wala kifudifudi ili usichukue nafasi kubwa, na ukitoka tu kwenda kujisaidia nafasi yako imechukuliwa.


Amesema alipokuwa huko amejifunza mambo mengi sana lakini kubwa ni swala zima la kubana matumizi ambapo chupa ya maji inaweza kutumiwa hata kwa siku mbili, na si kubana matumizi kwenye vyakula tu bali hata karatasi ambazo huwa wanatumia kuandika ujumbe na kuutuma kwa ndugu na jamaa zao.. kipande cha karatasi moja anaweza akakitumia hata zaidi ya mara kumi.

Na huko jela kumbe biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa ambayo ilikuwa ikitumika zama za zamani bado inaendelea ambapo ukiletewa chakula unaweza ukabadilishana na mtu kwa chupa ya maji..

hayo ndio maisha ya huko ndani ambapo yeye anasema siku moja jela ni kama mwaka hakuna uzuri kabisa ila anashukuru alivyofika huko kujulikana kwake kulimsaidia kidogo AKASALIMIKA.. masela hawakumsumbua kwa chochote mpaka anaaga jengo hilo lisilokuwa na heri.

Hii sio mara ya kwanza kwa Mastar wetu hapa Tanzania kuonja joto ya rumande ama jela, ukiachana na Wajelajela (FM Academia) ambao wao waliitungia hadi nyimbo JELA, Mtu wa kwanza katika muziki wa kizazi kipya kushtua watu kwamba jela ipo alikuwa ni Khaleed Mohammed (TID) ambae alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kabla ya kupata msamaha.. Na wengine waliokumbwa na zahma hiyo ni pamoja na Actress mwenye jina kubwa aliewahi kuwa miss Tanzania Wema sepetu, Miss tanzania 2009 Miriam Gerald, Mwimbaji wa bendi Waziri sonyo na wengineo wengi...

Kwasasa Hama Q ametoa wimbo wake mpya kabisa unaoitwa toto la kiafrika akiwa na bendi yake ya DAR MODERN TAARAB.. hatujui kama utakuwa kama Pembe la ng'ombe ama vipi!!

MAMBO YA MISS DAR INDIAN OCEAN..

Mrembo aliefanikiwa kunyakua taji la Miss Dar Indian Ocean Usiku wa jana ALICE LUSHIKO
TATU BORA ya Miss Dar Indian Ocean

Hii ndio TOP FIVE ya Miss Dar Indian Ocean (mrembo mwenye nambari 13 ndie aliechukua taji)

Kabla ya top 5 kulikuwa na NANE BORA ambayo ndio hiyo kama unavyoiona.

Meza ya Majaji kutoka kushoto BOY GEORGE, MANGE KIMAMBI, KISA na GERALD HANDO ambae ndio alitangaza washindi.


HAPA CHINI NI BAADHI YA WAHUDHURIAJI

Waandaji wa mtanange huo (Frontline management) Nancy sumari (kushoto) pamoja na Irene Kiwia
Jokate Mwegelo

Huyu ni mshiriki ambae ataiwakilisha wilaya ya Temeke

Irene kiwia (kulia) akiwa na mdadaa

Shamim zeze (8020)

Kutoka kushoto Arnold Kayanda, Rommy Jones pamoja na Ali Model (Daxx)

Vijana nao walikuwepo kushuhudia warembo.. Nas tatu

Nikiwa na Brothers.. Ze Boy (THT) kushoto kwangu, Moracka kulia pamoja na Martin anaechungulia kwa juu hapo

nikiwa na Jokate

Nancy Sumari

Martin mvuto kwanza, Ali Daxx pamoja na Rommy Jones

Nikiwa na vijana wa mjengoni (ukikaa nao hawa unacheka tu muda wote)