Tuesday, June 8, 2010

YALIKUWA NI MAPENZI TU....

Katika maisha inaweza ikatokea ukampenda mtu mpaka ukawa na uwezo wa kufanya chochote kwa ajili yake.. When it comes to Celebrities inaweza ikatokea ukampenda Celebrity fulani aidha mwanamuziki, muigizaji, mtangazaji, mcheza mpira ama yoyote tu kiasi kwamba kwako kushikana mkono tu na yeye inakuwa ni KITU KIKUBWA kuliko chochote.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja wa TANZANIA aliruka Fence na kwenda kumkumbatia mchezaji wa Brazil KAKA na kisha kuondoka akiwa na furaha ya ajabu.

lakini baadae mapolisi walimtia nguvuni na kuanza kumpa kichapo kitu ambacho naona kama sio sawa.. nafkiri wangemkamata tu na kumuweka chini ya ulinzi kisha kufata sheria jinsi ilivyotaka na si kichapo kile alichopewa.
THAT WAS LOVE kwa mchezaji huyo wa Brazil na kwake yeye jana ilikuwa ni kama kutimiza moja ya NDOTO ZAKE za muda mrefu..

Inasemekana kwamba kijana huyo ni Mtanzania anaeishi south Africa na alitoka South Africa kuja Tanzania maalum kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ya BRAZIL na TAIFA STARS

No comments: