Wednesday, June 2, 2010

HATIMAE THEA AAMUA KUOLEWA...........

Ni wasanii wachache sana wa kike katika tasnia ya filamu ambao wameingia kwenye swala la ndoa, Wengi waliobakia bado wapowapo sana na hata ukiwauliza swala la ndoa watakujibu hawafkirii kwa sasa..

Kwa upande wa Thea huu ndio wakati wake wa kuingia rasmi kwenye ndoa kwa sasa ambapo anatarajiwa kuolewa mwanzoni mwa mwezi wa kumi na jamaa anaefahamika kwa jina la MIKE SANGU ambae aliwahi kuwa katika sanaa ya maigizo miaka ya nyuma sana.

Kikao cha kwanza cha KITCHEN PARTY kitafanyika JUMAMOSI hii ya tarehe 5 JUNE 2010 maeneo ya Kinondoni pale OASIS PUB.

HONGERA SANA MAMAA na KILA LA HERI...

6 comments:

Anonymous said...

mmmmhhh!!!! haya mama kila la heri, karibu kwenye chama, jitahidi utulie mama

Anonymous said...

hongera saaaaana Thea jamani! Nimefarijika mno kusikia hizo taarifa, na kwa jinsi ninavyokupenda unapovaa vazi la usaniiii.. Mungu awe nawe katika maandalizi, hadi kufikia siku yenyewe mahsusi
Mdau

Anonymous said...

Thea ni mmoja kati ya wasanii wanaojitahidi kufanya vizuri sana kwenye industry ya sanaa, and for doing that (getting married) u're doing a very gud thing mam'

-Ashery

Anonymous said...

Hongera sana thea kwa kuolewa.....sikujui so cnt say nothin bout u ila huyo mike wako mhmhmhhhhh.....si alikua anakaa Urafiki flats na alipanga kwa dada mmoja hivi,so namfahamu vizuriiiiiii,ninachoweza kukushauri ni kwamba ndoa haina formula ila kuwa makini sanaa na mumeo mtarajiwa maanaa...mmmmmh.

Lulu said...

Khaaa we anon wa June 7, 2010 12:01 PM una mambo kweli mbona wamtisha mwenzako namna hiyo? Siyo vizuri bwana inakuwa kama kuna baya walijua kuhusu mumewe mtarajiwa. Muache mwenzio afanye arusi yake vizuri na kama kuna tatizo mwache aljionee mwenyewe. Cha muhimu kwa sasa ni kumuombea arusi yake iende vizuri, kwani kila jambo jema linapokuja na mabaya yanasindikiza.

Anonymous said...

Jamani mm naungana na huyo mdau hapo juu,nothing personal by the way coz sikujui Thea but mdogo wangu jiulize mara 2 kwa huyo mumeo mtarajiwa,namjua vizuri sana huyu kaka nimekaa jirani nae maeneo ya Sinza kumekucha,jiulize kwanini alimwacha Umy na mwanae?baada ya hapo akawa na Sofie alozaa nae mtoto aitwae Zuwena,just to mention the few...NIWAJUAO MM.otherwise kila la kheri pengine utam-badilisha tabia yake ya ukicheche,Zamaradi usibanie hii plz