Friday, May 27, 2011

SONG OF THE DAY.... DANCE WITH MY FATHER AGAIN - LUTHER VANDROSS!!

ALBUM YA LEO...!!!!!

Album ya leo ni mchanganyiko tu wa picha tofautitofauti ambazo huenda nimepiga siku tofautitofauti ama hata siku moja na watu tofauti tofauti kwa wakati tofauti pia.. na hizi huenda hazina maana yoyote ila ni for fun tu coz NAPENDA PICHA.. so kama unapenda picha join me na kama hupendi just skip nenda kwenye post nyingine haina mbaya....


Natamani kujua kupiga gitaa lakini tatizo hata kulishika tu ni mbinde!!!
Hapo nikiwa na Lotus kutoka Big brother..
Nikiwa na brother from another mother AD plus muite ADAM MCHOMVU a.k.a Baba jonii!!!

Kikazi zaidi sijui tulikuwa tunashangaa nini aisee.. hapo nikiwa na GEAH HABIB mamaa wa Hekaheka!!
With baba jonii katika pozi lingine...


Hiyo ndio album ya leo ambayo imejumuisha picha nilizopiga wiki hii though sio zote maana nikiziweka zote humu tutazidi kuchukiana.. LOL!!!


Wanasema HESHIMU MTU ANACHOKIPENDA, huenda kwako hakina maana lakini kwa ANAEKIPENDA kikawa na maana.. NAPENDA SANA PICHA na siwezi kuubadilisha ukweli coz that's me aisee..


na picha zenyewe ndio hizo hapo juu..FOR FUN jamani!!!


NAWAPENDA WOOTE mnaonipenda na kunichukia!!!!

WATOTO KUTOKA GREENHILL SCHOOL WATEMBELEA CLOUDS ENTERTAINMENT...

Siku ya Alhamisi nilikuwa na kibarua kizito cha kuwatembeza watoto kutoka Shule ya Greenhill ambao walikuwa na ziara ya kimasomo hapa CLOUDS ENTERTAINMENT ambapo waliweza kutembelea CLOUDS FM RADIO, CLOUDS TV pamoja na CHOICE FM na kujionea jinsi vipindi vinavyotengezwa na kurushwa...

Hii ilikuwa ni picha ya pamoja na baadhi ya watoto hao ambao walikuwa zaidi ya 150 kwa siku hiyo na wote waliweza kufanikisha lengo lililowaleta na kila mtoto aliondoka akiwa ameridhika.. Hapo nyuma mwenye dreadlocks ni Graphic designer wa clouds TV Joachim Kanyopa, Mimi (Zamaradi) pamoja na mtangazaji wa kipindi cha ng'aring'ari kutoka Clouds TV Sakina Lyoka.
Nikiwa kama mwenyeji wao lilikuwa ni jukumu langu kuwatembeza kwenye kila pembe ya Jengo ambapo hapo walifanikiwa kuingia studio na kuona jinsi watu wanavyofanya kazi, aliekaa ni Dina Marios na huo ulikuwa ni muda wa leo tena ambayo huruka jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia Tatu asubuhi mpaka saba kamili za mchana..
Hiki ni chumba cha Editing Clouds TV na hapo walikuwa wakipata mawili matatu kutoka kwa Aboubakar Malipula pamoja na Ezra..
Na hapa tulikuwa Studio B ya Clouds Fm Radio ambapo walikuwa wakiangalia jinsi ambavyo interviews mbalimbali zinavyorekodiwa na kufanyika...

PART TWO: MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI.. BAADA YA FUJO NA MBWEMBWE ZA MUDA MREFU HATIMAE HALI IKAWA HIVI...lol!!

Mwanzo wa safari watu hao unaowaona wamelala hawajielewi ndio walikuwa waongeaji kupita kiasi, wacheza show wa nyimbo zote na ndio watu waliokuwa wakionekana wana Energy.. lakini baada ya muda tu kidogo ikawa kwisha habari yao.. na hali yao ikawa mbaya kama unavyowaona hapo.. basi loote likawa KIIMYAAAAA utafikiri sio lile lililokuwa na makelele!!!!!! lol...


NAOMBA NITOE WASIFU WA KILA MMOJA KWENYE SAFARI YETU HII YA LEO...


WASIWASI MWABULAMBO: Huyu ndio alikuwa kinara wa maongezi lakini hapo ujanja wote mfukoni kama unavyomuona, mpaka nampiga picha hapo alikuwa haelewi lolote linaloendelea duniani..
SHAFII DAUDA: ha haaaa.. kazi yake kubwa ilikuwa ni kurequest nyimbo na kusema "hakuna kulala" lakini matokeo yake ndio hayo hapo yanajieleza.. kweli hakuna kulala.. lol!!

KATUNDA: Afadhali hata ya huyu.. mbwembwe hazikuwa nyingi hivyo kulala ni kama haki yake..


PETER a.k.a KABAISA: Ha ha haaaaaaa huyu bwana ndio alikuwa MAIN SPEAKER tulikutana Chalinze akiwa ametokea Morogorokwenye shughuli nyingine lakini safari nzima akaibeba yeye (kimaongezi) utafikiri tumetoka wote DAR lakini maskini hakuchukua round.. sijui alitumia nguvu nyingi kwenye kuongea!!!!!! lol


REGINALD MARO a.k.a P. DIDDY: serengeeti serengeeti.. ey ey ey ey.. ndiomana kuna ule msemo unaosema "KUNYWA KISTAARABU KWANI KUNYWA POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO" nafikiri nimeeleweka...


HAROUN: huyu hakuwa na mbwembwe sana ila wakati tuko Chalinze alipiga CHAPATI NA MAHARAGE.. sasa sijui ndio SHIBE hiyo ama kuchoka tu sielewi!!!


JIMMY JAM: Maskini Jimmy hajielewi, ye alikuwa anapiga watu picha tu na vituko vyao, naona nguvu ilikuwa ya soda tu kazi ikamshinda matokeo yake na yeye kawa Tukio.. ha haaa... pole brother!!ZAMARADI MKETEMA: Katika watu wagumu kulala wakiwa safarini basi mi mmojawapo... Ukinikuta nimelala basi ntakuwa nimechoka kwelikweli.. mi usingizi wangu huwa naulipizia nikifika nnapoenda.. Hivyo kwenye safari ya leo nafikiri tuliokuwa macho ni MIMI na DREVA tu basi.. WENGINE WOOTE kushnehi.. mpaka Sophia alilala pia Camera tu iliisha charge otherwise nae mngemuona hapa!!!!!


But all in all it was REALLY FUN... nime-enjoy sana safari ya leo, watu wote hao unaowaona hapo juu walinipa Furaha ya kutosha kila mtu akiwa na Burudani yake anayoijua yeye... NAWAPENDA WOOTE!!!
Hii ilikuwa ni kabla ya kuangusha Gari.. Utafikiri sio WAO.. Ha ha haaaaaaaa.... MBIO ZA SAKAFUNI!!!! Hiyo ndio Part TWO ya safari yetu ya leo!!!

PART ONE: SAFARI YETU ILIVYOKUWA TUNASHUKURU TUMEFIKA SALAMA TANGA..

Namshukuru sana MUNGU kwa kutufikisha salama TANGA kwani hakuna safari ndogo, waswahili wanasema safari ni safari.. na safari hii ni maalum kabisa kwa ajili ya SERENGETI FIESTA FILAMU ambapo siku ya kesho jumamosi pale LA CASA CHICA kutakuwa na Audition ya kutafuta waigizaji wapya kaisa kwenye filamu kuanzia saa NNE ASUBUHI!!!
Safari yetu ilianza saa kumi na mbili alfajiri na tulikuwa wengiwengi kidogo ambapo tulikuwa na Shafii Dauda ambae nae yuko Tanga kwa ajili ya Soka Bonanza itakayofanyika Jumapili, Wasiwasi Mwabulambo,Jimmy jam, Reginald Maro, Sophia Kessy, Mimi, Haroun, Katunda, Hellen Kazimoto na Peter a.k.a kabaisa...
Hii haikuwa tu safari but it was really FUN kuanzia kwenye gari ambapo watu wengi walicharuka kwelikweli kiufupi ilikuwa furaha tupu kama ambavyo unamuona Mr. Mwabulambo hapo akiwa na Hellen kazimoto, sikumbuki hata ni wimbo gani ulikuwa unachezwa hapo..

SASA SIKILIZIA KILICHOTOKEA BAADA YA HAPO.. HIYO NI PART ONE

NINA FURAHA KULIKO KAWAIDA KUKUTANA NA MTU HUYU LEO....

Ukiniuliza Mchekeshaji ninaempenda hapa Tanzania kiukweli kabisa jina la huyu mzee ndio litakuwa la kwanza halafu wengine ndio watafuata, anaitwa KING MAJUTO mmoja kati ya wachekeshaji wa muda mrefu sana hapa Tanzania na Asiechuja machoni mwa watu wengi.. Kuna mengi sana ambayo napenda kutoka kwa huyu mzee kiasi kwamba leo nilivyomuona tu nilishindwa kujizuia kucheka....
Nakumbuka wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikihudhuria sana maigizo yao ya jukwaani enzi hizo akiwa katika kundi la Muungano cultural troupe ambapo kila jumamosi pale Vijana social hall kinondoni ndio ilikuwa sehemu yao ya kufanyia maonesho, na baba alikuwa akipenda sana kunipeleka pale kushangaashangaa maigizo na MZEE MAJUTO ndio nilimuonea hapo kwa mara ya kwanza ambapo kwa enzi hizo alikuwa akiigiza serious na kingine alipenda sana kuigiza kama anaonewa hivi na mtu wa matatizo na sio comedy kama ambavyo anafanya sasa, lakini baadae nikaanza kumuona kwenye comedy enzi hizo kwenye television na mpaka sasa kupitia DVDs mbalimbali...
Naweza nikasema kwamba namuheshimu sana huyu mtu, na naweza kusema yeye kama yeye mbali na jina alilonalo amejijengea Heshima kubwa sana kupitia fani yake hiyo, mi naweza nikamuita LEGENDARY kwenye sanaa nzima ya Vichekesho...


Mbali na kuwa kipenzi changu Mzee Majuto alikuwa kipenzi sana cha baba yangu, enzi za uhai wa baba yangu hakuwa mtu wa kupenda kuangalia TV ama hata movies lakini ukiweka DVD ya mzee Majuto utakaa nae Mwanzo mpaka mwisho na atacheka mpaka utasikia raha, so kukutana na mzee Majuto kumenikumbusha mbali sana na nimefurahi sana kukutana nae leo...


I was not in a good mood kabisa before na nilikuwa na mambo yangu mengi sana kichwani lakini kukutana nae tu imekuwa kama dawa kwangu naomba nikiri, He made my day aisee...


MUCH RESPECT TO YOU!!!!

Tuesday, May 24, 2011

MAMA NA MWANA.. IRENE UWOYA NA MWANAE (KRISH)

A new baby anaitwa KRISH HAMAD NDIKUMANA, mtoto wa Irene Uwoya siku hii ya leo utaweza kumuona live kabisa on TAKE ONE ambapo ataongelea experience yake ya Uzazi, maana ya jina la mtoto wake na mengi kuhusiana na mtoto wake huyu wa kwanza.. USIKOSE saa TATU KAMILI USIKU on CLOUDS TV.
Kimalezi zaidi.. mama na mwana!!!
Nikiwa na mtoto krish hapo... practise makes perfect so hakuna ubaya kuanza kujifunzafunza malezi kidogokidogo mapema.. lol!!!


He looks very Cute, kwa kumuangalia tu naona kama kafananafanana na mama yake hivi, sielewi kwa upande wako unaonaje coz mi sio mzuri kihivyo katika kufananisha!!!

HONGERA SANA IRENE KWA KUPATA MTOTO.. That's a very big step in Life!!! MUNGU akukuzie!!!

HONGERA MTOTO FATNA..

Siku ya jumamosi ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ambapo alitimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa kwake na wazazi wake wakamfanyia Maulid maeneo ya Sinza pale ambapo ndugu jamaa na marafiki tuliweza kujumuika kwa pamoja na kumpongeza binti huyo... HAPPY BELATED BIRTHDAY!!!!
Huyu ndio baba wa FATNA anaitwa Athumani Shaabani maarufu kama SUKA ambae ni kaka yetu kutoka hapahapa mjengoni Clouds FM akiwa Music department.
Mmoja kati ya ma-auntie wa Fatna, sikufanikiwa kupata jina lake!!
Huyu ndio mama mzazi wa Fatna anaitwa Zena nae tuko nae hapahapa mjengoni!!!
Hapo nikijifunza malezi kidogo, nikiwa na mama mzazi wa mtoto Fatna pamoja na Fatna mwenyewe..

Vijana kutoka mjengoni.. kutoka kushoto PETER MOE, ABDUL, ARNOLD KAYANDA pamoja na HAMISI SHAABAN TALETALE a.k.a BABU TALE a.k.a LAST BORN
Kama unavyoona itifaki imezingatiwa na watu walipiga mavazi kulingana na shughuli husika...


Nilijikuta nimempenda sana huyu mtoto jamani..!!!!!!!
Kama mzazi vile.. Hapo nikiwa nimembeba mtoto fatna nae katulia utafkiri yuko na mama yake..lol!!! Njaa haina Baunsa... Mwana FA akiwa ametoka kufakamia sahani ya Biriani.. na ilikuwa ya ukweli hasa!!!
I just love this photo... ni mwaka mmoja tu lakini anaonekana mjanja ajabu!!!
Na yeye ana mawasiliano.. Hongereni sana ZENA na SUKA kwa malezi na kufanikiwa kumpata mtoto mzuri kama huyo.. MUNGU AWAKUZIE Inshaa-ALLAH!!!

OUT AND ABOUT...

Kutoka kushoto Baby Madaha, Zamaradi Mketema, Aunt Ezekiel pamoja na upcoming movie star Irene Paul (utampata kupitia handsome wa kijiji coming soon..)

Kama ilivyo hapo juu...

Nikiwa na Baby Madaha..

Kucheza pia inaruhusiwa.. hapo nilikuwa nachangamsha mwili kidogo...

Zamaradi, Rehema macho lol! pamoja na Irene..

Hapa nikiwa na Irene Paul..


Baada ya kazi ngumu ya kucheza mapumziko muhimu.. Hii ilikuwa kwa Aunt Ezekiel ambapo kulikuwa na ka-function fulani kalikotukutanisha watu tofautitofauti.. was really Fun!!!

Friday, May 20, 2011

MNAPOJIKUTA WOTE MMEVAA SARE BILA KUPANGA...

Hapo ni ADAM MCHOMVU pamoja na RAYMOND CHARLES kutoka hapa mjengoni Clouds FM ambapo walijikuta wamevaa sare bila kutegemea, ukianzia na hizo Culture hapo shingoni, style ya uvaaji pamoja na mashati waliyovaa ni kama yanawiana hivi...
Sometimes unaweza ukajikuta umeingia ofisini na bila kutegemea ukajikuta umevaa sare na mtu yoyote hapo kwa ofisi kama ambavyo imetokea kwa vijana hao hapo juu ambao style ya uvaaji ilikuwa kama inafanana hivi kwa siku hiyo!!!!

Sijui vijana ndio wanamaanisha nini hapo sielewi... but all in all PEACE & LOVE!!!


Adam mchomvu & Raymond Charles!!