Wednesday, May 11, 2011

MATUMIZI YA KINGEREZA KWENYE FILAMU ZETU..!!!Si vibaya kutumia kingereza kwenye filamu lakini inategemea na sehemu gani tunatumia, mara nyingi huwa tunatumia ndivyo sivyo na hiyo imejitokeza kwenye filamu nyingi sana za kitanzania.. Hii si lugha yetu, ni lugha ambayo wengi wetu tumeikuta (lugha ya pili) hivyo haitegemewi kwamba tutakuwa Fluent katika kuongea, lakini vilevile hiyo isifanye tujiendekeze na kuchapia waziwazi hivyo inabidi tuwe makini sana wakati wa kukitumia kwasababu hizo filamu zinatazamwa na watu wa aina na mataifa tofautitofauti...

Hizo ni baadhi ya CLIPS za filamu ambazo kingereza kimetumika ndivyo sivyo... !!!!

15 comments:

Nai Us said...

Yaani ni aibu sana unajua shida inakuja wapi hao waingizaji wetu hawapendi kusoma na kuthamini kazi zao hiyo ndio sababu dear wanacho jua wao ni kupaka mikorongo na kwenda salon basi wanadhani wanakuja kuuza sura sio kazini yaani nimetamani kujificha kwa aibu kwa kweli asante sana endelea kusaidia hao labda wataelimika na kuona umuhim wao

Anonymous said...

Zama sijui kanini unachelewaga kutuletea mambo km haya blog inadooraaaa ila leo walai umenikosha mana nimcheka mie mpk basi yeuwiiiii jamani kweli NGELI utata tena sn km somo la hesabu kwa wanafunzi wengi afu sio move tu hata maisga ya kawaida wabongo tunapenda sn kujishaua ktk hilo mwisho wa siku ni aibu tena km MTUNISI yani mbavu zilitaka kunchomoka kwa kicheko. Yani wananishangaza jamani kwani lazima m2 aongee? km alivosema Hemedi sio lazima hasa km huwezi unajitia aibu.Johari,Ray Eekiel Deo Shija Shamsa ford pia nao wana matatizo ya lugha sio ngeli tu kiswaili matamshi yao sio mazuri

Anonymous said...

Ni mimi maimuna,............nimesema maimuna

grace said...

wape sana hao black n white hovyooooooooo wanajichoresha na kutuchoresha taifa zima.kama vp watuite tunaojua ngeli tuwafunze.

mimi maimunaaaa
nimesema mimi maimunaaaaa...nendeni english course!!!!!!

i love take one.nice clip Zam!!!!!

Anonymous said...

Ok let me start with you Zamaradi.. second language or L2 is any language learned after the first language or mother tongue. so sio lugha ambayo tumeikuta that's wrong. And if you want them to use proper swahili in their movies you can be a good example by presenting your program in our national Language "swahili". (withou mixing with English) Speaking English is a biggest challenge to many of us. But still we can learn instead of embarrassing ourselves. Having an accent is not a problem... but pronunciation is a big deal.It is not too late for "Bongo celebrities to learn other languages than swahili.

dada said...

Jamani hivi na hiyo subtitle hapo chini mmeiona? mbona wanatutia aibu hawa watu!!!! hili swala sio la kucheka ni lakulia kilio cha sauti kubwa (crying out loud). yaani nimeudhika kweli, msonyoo

Anonymous said...

ahahahaaha! tatizo la mastaa wetu wanajiona kila kitu wanakijua ona sasa wanavyoumbuka then wanataka wawe wa kimataifa!!mbona wenzetu wanatumia lungha zao then ndo wana translate kwa lugha ingine

Anonymous said...

Sasa wewe upo upande gani???????????? yes its not too late 4 them basi waende shule hawataki. sooooooooooooooooote tunajua ngeli sio luga yetu ni kujifunza tu na km huwezi basi tumia kiswaili simple lyk that, na ndicho anachosema zama km unaweza poa ongea huwezi jifunze umeshindwa kbs usiongee sio lazima tunajua km ni tatizo hata wizara yetu ya elimu inatambua ivo. POINT ni usingee ki2 usichokijua kitakuaibisha

Anonymous said...

Nimeipenda sana mdogo wangu Zamaradi kutuletea maada hii, ijapokuwa wewe mwenyewe una kiswa-english pia . hilo ndio tatizo letu kubwa wabongo tunadhani kuwa tukitupia maneno mawili matatu ya kiingereza basi tutaonekana muhimu kidogo. wakati wengi wetu lugha imeenda holiday au ipo MOI kitengo cha mifupa Muhimbili. kama lugha gongona si bora tungetupia vijineno vya kihaya,kichaga , kimakonde na kadhalika ?.
huo ni mtazamo tu. pls endeleza libeneke dogo Zamaradi japokuwa kutakuwa na wengi ambao itawagusa.
mdau Zee la bandari UK.

SEBO said...

as far as meaning is concerned i dont see any problem with the phrase ''be honest,go home''...alafu pili,hata kama angekuwa amekosea stil nsinge mlaum,mketema?umesahau kazi za sanaa siku zote zinareflect kile kilichopo katuka jamii husika??...siku zote ktk hollywood movies watu wenye asili ya poland huwa wanazungumza broken English eg Check ktk movie ya SALT by Angelina Jolie.wataliano,wafaransa,warusi...siku zote huwa wanakuwa presented with their broken English ktk hollywood movies na cha kusikitisha you dont find it strange...!!

By I Sebo

Anonymous said...

It pure hypocrisy criticizing people mixing Swahili and English while you are doing the same thing on your programme.

Anonymous said...

na nyie kabla ya kumshambulia zamaradi,rudieni clip tena. zama hakuwakataza kuongea english,ila alichosema ni kuiongea ndivyo sivyo..sasa hiyo to be honest,go home ndo nini? unless alitaka kusema,to be honest,Id like you to go home or to be honest,Id rather you go home! na huyo mwingine hata kusema beautiful kumemshinda. go Zama,go girl. wachane hao ma-star wanaojidai kuongea english ilhali lugha haipandi.

Anonymous said...

mmmh. haya bana. mee chimo! chichemi! chitaki! chijui!

Anonymous said...

I'm new to Bongowood whatever it is, but I find it very hard to follow the story( On most of the movies). Stories are incongruent with the environment/actors demeanor. I abhor mixing languages because it shows how unprofessional you are.

Anonymous said...

Sasa wewe ZAMARADI kama Ekzeketivu dairekta wa filamu ya " RONGU NAMBA" mbona Gardena alisema "niko huku kwenye bustani ya garden"!!!!mlikuwa mnataka kumchora!!