Friday, May 27, 2011

WATOTO KUTOKA GREENHILL SCHOOL WATEMBELEA CLOUDS ENTERTAINMENT...

Siku ya Alhamisi nilikuwa na kibarua kizito cha kuwatembeza watoto kutoka Shule ya Greenhill ambao walikuwa na ziara ya kimasomo hapa CLOUDS ENTERTAINMENT ambapo waliweza kutembelea CLOUDS FM RADIO, CLOUDS TV pamoja na CHOICE FM na kujionea jinsi vipindi vinavyotengezwa na kurushwa...

Hii ilikuwa ni picha ya pamoja na baadhi ya watoto hao ambao walikuwa zaidi ya 150 kwa siku hiyo na wote waliweza kufanikisha lengo lililowaleta na kila mtoto aliondoka akiwa ameridhika.. Hapo nyuma mwenye dreadlocks ni Graphic designer wa clouds TV Joachim Kanyopa, Mimi (Zamaradi) pamoja na mtangazaji wa kipindi cha ng'aring'ari kutoka Clouds TV Sakina Lyoka.
Nikiwa kama mwenyeji wao lilikuwa ni jukumu langu kuwatembeza kwenye kila pembe ya Jengo ambapo hapo walifanikiwa kuingia studio na kuona jinsi watu wanavyofanya kazi, aliekaa ni Dina Marios na huo ulikuwa ni muda wa leo tena ambayo huruka jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia Tatu asubuhi mpaka saba kamili za mchana..
Hiki ni chumba cha Editing Clouds TV na hapo walikuwa wakipata mawili matatu kutoka kwa Aboubakar Malipula pamoja na Ezra..
Na hapa tulikuwa Studio B ya Clouds Fm Radio ambapo walikuwa wakiangalia jinsi ambavyo interviews mbalimbali zinavyorekodiwa na kufanyika...

No comments: