Thursday, June 30, 2011

PICHA ZA MWANZA ZINAANZA..

This was meet and greet Pre fiesta party at Malaika Beach resort Mwanza.. from left mdada kutoka saut, Ally rhemtullah, Zamaradi, Vida mahimbo pamoja na a friend kutoka saut Kiamba...
Ally, Vida na mimi tukiwa na Friends kutoka St. Augustine University of Tanzania Mwanza!!


Thursday, June 23, 2011

MATAYARISHO YA FIESTA MWANZA..

Kwasasa tuko MWANZA kwa ajili ya kujipanga na FIESTA msimu wa dhahabu unaoendelea ambapo siku ya JUMAPILI pale CCM kirumba kutakuwa hapatoshi kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu mlangoni.. Hapo ni MIMI, BARBARA HASSAN mwenye handbag pamoja na HELLEN..
Hellen, Zamaradi na Barbara Hassan wa Power breakfast ya Clouds FM..

Friday, June 17, 2011

Eyooo NICHEKI.... MNAONA SWAGGA!!! ANATAFUTA MKE JAMANI...

Mnaona swagga hizo.. kitu cha yellow na Orange.. Chekzea.. maneno miguu!!! kazi ni kwako.. lol!!!
Anyone alievutiwa nae!!??? leave your contacts tafadhali!!!

PICHA YA LEO... ARNOLD KAYANDA!!!

Anaitwa Arnold Kayanda... mtangazaji wa JAHAZI na Top 20 hapa Clouds FM radio..

MAMA NA MWANA.. lol!!!

Wednesday, June 15, 2011

AMBAYO YANATUTOKEA WAKATI WA KUREKODI KIPINDI... WATCH IT!!!Hii kitu ilitokea bila kutegemea wakati narekodi kipindi cha TAKE ONE juzi ambapo wakati narekodi ghafla nikamuona Cameraman wangu amesitisha zoezi la kurekodi ikabidi nimuulize ni nini, akanijibu kwamba kuna kitu amekiona tukiache kwanza kipite, lakini katika hali ya kujiamini nikajitia sio muoga nikajipa ujasiri na kuwa ngangari na kusema kwamba turekodi nacho tu lakini kilichotokea ndio hiko hapo juu WATCH IT!!!
Kuna vitu fulani katika maisha ambavyo vinatokea bila kupanga na bila kutegemea vinakuwa vizuri na vinakuwa ni vigumu kuvipata tena sehemu nyingine yoyote.. Thats what we call Magic moments sababu haziwezi kujirudia tena hata mjipange vipi..
I love that clip!!!

Tuesday, June 14, 2011

HEBU MUANGALIENI HUYU MTOTO JAMANI.. MNAMUELEWA!!???? LOL....


anaimba take it off mwenyewe, halafu ukimuangalia vibaya unaweza kuhisi ni kajitu kazima maana hakaeleweki ni kakubwa ama katoto.. jamani!!!

I LOOVE THIS SONG.. GRENADE - BRUNO MARS.. hapo chini ni wimbo, STUDIO SESSION pamoja na THE MAKING YA VIDEO (GRENADE)HII (CHINI) NI BEHIND THE SCENE WAKATI WA KUSHOOT VIDEO YA WIMBO HUU.. WATCH IT!!


Hapo juu akielezea maana nzima ya kutumia concept aliyoitumia kwenye video ya Grenade, the use of piano na vitu vingine.. It was Behind the scene!!!


I really love the song kutoka kwa Bruno Mars!!! hiyo hapo juu ni studio session.. ENJOY!!!

PICHA YA LEO... ZAMA na CEASER!!!

Mimi nikiwa na Ceaser Daniel ambae anapatikana hapahapa CLOUDS TV kupitia kipindi cha BONGO ACCESS kila siku za jumanne baada ya Take one...
Zamaradi Mketema na Ceaser Daniel.. Usikose kuangalia TAKE ONE siku hii ya leo TATU kamili Usiku kupitia CLOUDS TV na baada ya hapo Bongo Access na Caeser.. usikose!!!

Hiyo ndio picha ya leo!!!!

Monday, June 13, 2011

ILIVYOKUWA KWENYE BIRTHDAY YA SINTAH...

Hii ilikuwa ni siku ya jumamosi pale SAVANNAH LOUNGE Quality plaza ambapo kulikuwa na birthday party ya sintah kama unavyomuona hapo akizima mishumaa kadhaa iliyowekwa kwa ajili yake..
Niliipenda hii Cake kwakweli, ilikuwa ya ukweli sana.. the colour, the decoration, and even the taste.. was soo sweet!!!
Kutoka kushoto Zamaradi, Birthday girl Sintah pamoja na Millard Ayo..
Nikiwa na Sauda Mwilima ambae ndie alikuwa MC wa shughuli nzima.,.
Mimi nikiwa na Birthday girl hapo..
Hapa hata hatujajipanga kwa picha jamani..
haya sasa camera roll.. Action.. saafi.. hapo nikiwa na Aunt Ezekiel ambapo mchana wake tulikuwa kwenye Audition pale Leaders kwenye serengeti Fiesta Filamu!!
Penny akiwa na Aunt Ezekiel
Pozi..
wadau wengi walikuwepo, hapo nikiwa na Sajent
Hii picha pamoja na baadhi ya nyingine unazoziona humu nimechukua kwenye Blog ya shamim zeze maana camera yangu siku hiyo ilifanya kazi sana kwenye serengeti fiesta filamu DAR mchana wake kiasi kwamba mpaka kufika muda huo Charge ilikuwa imeisha kabisa hivyo ikabidi nitumie simu tu kupigia picha, so kama quality ya picha nyingine sio nzuri mtanisamehe..
Belina kama unavyomuona..
Shamim akiwa na Sintah
Birthday girl Christina manongi a.k.a Sintah
Sauda Mwilima... MC wa shughuli
Jacky.. nilichogundua ni kwamba wadada wengi siku hiyo walitupia viatu na clutch za red ukianzia na huyu wa hapa juu(jacky), sauda mwilima, Belina, kuna mwingine sikufanikiwa kupata picha yake na hata mimi huko juu!!!
Mduara kama kazi... watu walienjoy sana na kila kitu kilienda sawa.. may GOD bless you sintah, live long and Happy belated birthday!!!

Friday, June 10, 2011

UNA KIPAJI CHA KUIGIZA!? UNA NDOTO ZA KUWA STAR MKUBWA WA FILAMU.. HUU NI MUDA WAKO NA KESHO NDIO SIKU YAKO..

Kwa wewe mkazi wa Dar es salaam.. Kama unajijua una kipaji cha kuigiza na ndoto zako siku zote ni kufanya vizuri kwenye Industry ya filamu basi huu ni muda wako..

Siku ya kesho pale LEADERS CLUB Kinondoni kutafanyika USAILI MKUBWA SANA wa kutafuta WAIGIZAJI kwa hapa Tanzania, na hii ni Serengeti Fiesta Filamu chini ya CLOUDS ENTERTAINMENT katika kusherehekea miaka Kumi ya Fiesta.

Naweza nikaita hii ni Golden Chance kwa yeyote mwenye ndoto za kuwa muigizaji wa Filamu hivyo sherehekea kwani huu unaweza ukawa ni msimu wa dhahabu kwako kwa kutimiza ndoto zako..

Mbali na mimi mwenyewe kuwepo ambae ndio nitaongoza zoezi zima(zamaradi) Tutakuwa na mastar wengine wengi wa Filamu kama Aunt Ezekiel, Jacky Wolper, Wema Sepetu, Jacky Pentzel, Single Mtambalike richie, Jacob Steven (JB), Yusuph Mlela pamoja na Director William Mtitu.

Hivyo Tukutane LEADERS CLUB siku ya KESHO jumamosi kuanzia saa NNE kamili ASUBUHI!!

HII NI BURE KABISA... KIKUBWA TUNACHOANGALIA NI KIPAJI CHAKO!!

NJOO UTIMIZE NDOTO ZAKO!!!

Thursday, June 9, 2011

SINA NINACHOKIJUTIA katika NILIYOYAFANYA BIG BROTHER - BHOKE!!!

Katika interview aliyofanya na JAHAZI siku hii ya LEO baada ya kutoka kwenye jumba la Big Brother, nilipata nafasi ya kumuuliza Bhoke kama kuna CHOCHOTE ambacho anajutia katika yale ambayo ameyafanya katika jumba lile la Big Brother..

Lakini Bhoke alisema kwamba hakuna na HAJUTII CHOCHOTE katika yote ambayo ameyafanya "Sijutii chochote, i really enjoyed being in the house na yote niliyoyafanya niliyafanya kama mimi so hakuna chochote ambacho naweza nikajutia..."

Na nilishawishika sana kumuuliza swali hilo kutokana na kitu ambacho kilitokea kwenye jumba lile ambapo kuna CLIP inayoonesha akifanya matendo ya kimapenzi na mshiriki wa Uganda (Ernest), hivyo kusambaa kwa clip ile kukanifanya nitamani kujua yeye kama yeye anaichukuliaje hali ile kwasasa.. Is it bothering her!? ama ni part of life na maisha inabidi yaendelee, lakini mwisho wa siku jibu lake ndio hilo kwamba kujuta hakuna nafasi kwenye maisha yake kwani chochote ambacho kimetokea, kimetokea na maisha inabidi yaendelee!!!

Kipande kilicholeta utata...

Haya kwa wale wadau mliotaka kujua jibu ndio hilo hapo!!!!! No regrets...

Wednesday, June 8, 2011

BEHIND THE SCENE.. 69 RECORDS!!!

Anaitwa ODHIAMBO.. ndio Cameraman wa 69 records.. hapa alikuwa akijipanga kabla ya kazi!!!
Mzigoni...

Hapo juu ni MIMA na NKWABI on set...

Hii ni tamthilia inayoruka CLOUDS TV kila siku za JUMATANO saa TATU kamili usiku!!!

DAR PAZURI... HILI NI ENEO MOJA HUKO MBAGALA...

Jana nilikuwa eneo moja huko mbagala (mtoni kijichi) ambako kulikuwa na shooting ya 69 records nikalipenda sana hili eneo, nafikiri nitarudi tena kwa ajili ya kufanyia kipindi..
Hii ni location kabisa ya movie, sijui kwanini huwa tunang'ang'ania sehemu zilezile kila siku wakati kuna ma-location kibao ya kufanyia filamu tena Dar hii hii....
Huyo unaemuona hapo juu tuliambiwa anaitwa Ngadu, na katika hili eneo wapo wengi mno pembezoni mwa hayo maji.. wanakuwa wanaishi kwenye vitundu vidogovidogo ambavyo wamevichimba wenyewe hapo pembezoni kama ambavyo unaona hapo chini..
Vitundu wanavyotumia kujihifadhi..
Hao ngadu ni ngumu mno kuwakamata, huyu kaka ndio alikuwa akituelezea tabia zao na jinsi walivyo, hapo alikuwa akijaribu kuwakamata ili tuwaone kwa karibu!!!


Kuna mengi sana ambayo alituelezea kuhusiana na hii sehemu, wadudu waliopo maeneo haya na tabia zao tofautitofauti... Hapo alikuwa amefanikiwa kumkamata mmoja!!!!

Nilijikuta nimependa sana hii sehemu ingawa kufika kwake huku shughuli ipo hiyo milima!!! Nilichoka vibaya mno!!

Monday, June 6, 2011

KITCHEN PARTY - HUSNA..

Jana ilikuwa ni kitchen party ya mshkaji wangu wa siku nyingi sana, anaitwa Husna Shaibu(kushoto) ambae tuliwahi kusoma wote shule moja O' level... Hongera sana mammy ukawe mke mwema huko!!!
Alisimamiwa na Best friend wake anaitwa Neema, Hapo wakikata keki!!
Wanakamati kama ambavyo unatuona.. mpango mzima ulikuwa ni kitenge na kila mtu alishona anavyojisikia kama ambavyo unaona madada walivyopendeza...
Mi niliamua nishone kama ambavyo unaona hapo juu na hivyo ndio nilivyotokea...
Raha ya kitchen Party ndio hii, Mwanamke Nyonga babu mengine haihuuuu... Go ADA, Go ADA, Go Go Go ADA.. Chezea mama MALCOM WEWE.. umetishaaaaaa!!!


Huyu ndio dada wa Bi Harusi anaitwa Jamila!!!
Bi harusi.. hapa sijui ilikuwa nini.. nshasahau.. lol!!!
Mh jamani mpiga picha hata sijajipanga, kashafotoa.. hapo nilipata bahati ya kukutana na school mate wa Enzi hizo.. anaitwa Rukia Haruna Meza mwanafunzi wa UDOM kwasasa!!!
Kutoka kushoto anaitwa TINA (mcharuko), BONITA (ndio ambae ananing'arisha kwenye ma-lace wig), MIMI hapo kati, Na Warembo wengine kama unavyowaona...
Chezea JOHARI wewe.. nae alikuwepo kama DADA wa Bi harusi!!
Ada (mama Malcom), Zamaradi na Jacky Pentzel.. tulikutana huko pia!!!
Zamaradi Mketema na Jacky Pentzel..
Ada, Jacky Pentzel, Zamaradi na Blandina Chagula (johari)
Wadada katika Pozi!!!!
Shughuli ni watu na watu wenyewe ndio sie.. kote kote nipo... hapo na mi nikicheza taarab mwanamke ujue vyote sio uzungu mwanzo mwisho mkataa kwao mtumwa.. chezea.. lol!!!!
Husna alitukutanisha wengi jana.. was really happy to meet you mammy baada ya muda mrefu sana...
Haya sasa mpenda picha.. Swagga is on.. ha haaa..
Nikiwa na Bi harusi hapo.. ma-school mate tulikutana.. It was a good thing sana and and i had alot of fun kukutana tena na watu hawa katika style hii.. maana hii ni baada ya miaka mingi ya kupotezana na kukutana juu kwa juu!!!
baada ya long time kitambo
Hapo ni baada ya kucheza SANA, kiukweli jana nilifurahi sana na kucheza vya kutosha kwenye sherehe hii, bi harusi mwenyewe nae alikuwa Mcharuko, alicheza hatari lol!! hapo tulikuwa tumeshacheza sana tumechoka na kitchen party ndio ilikuwa imeishia hapo.. from left.. Jacky, Zamaradi, Johari na Husna mwenyewe!!!
Hongera mama na kila la kheri kwenye harusi yako.. Ukatulie na mumeo huko!!!