Wednesday, June 8, 2011

DAR PAZURI... HILI NI ENEO MOJA HUKO MBAGALA...

Jana nilikuwa eneo moja huko mbagala (mtoni kijichi) ambako kulikuwa na shooting ya 69 records nikalipenda sana hili eneo, nafikiri nitarudi tena kwa ajili ya kufanyia kipindi..
Hii ni location kabisa ya movie, sijui kwanini huwa tunang'ang'ania sehemu zilezile kila siku wakati kuna ma-location kibao ya kufanyia filamu tena Dar hii hii....
Huyo unaemuona hapo juu tuliambiwa anaitwa Ngadu, na katika hili eneo wapo wengi mno pembezoni mwa hayo maji.. wanakuwa wanaishi kwenye vitundu vidogovidogo ambavyo wamevichimba wenyewe hapo pembezoni kama ambavyo unaona hapo chini..
Vitundu wanavyotumia kujihifadhi..
Hao ngadu ni ngumu mno kuwakamata, huyu kaka ndio alikuwa akituelezea tabia zao na jinsi walivyo, hapo alikuwa akijaribu kuwakamata ili tuwaone kwa karibu!!!


Kuna mengi sana ambayo alituelezea kuhusiana na hii sehemu, wadudu waliopo maeneo haya na tabia zao tofautitofauti... Hapo alikuwa amefanikiwa kumkamata mmoja!!!!

Nilijikuta nimependa sana hii sehemu ingawa kufika kwake huku shughuli ipo hiyo milima!!! Nilichoka vibaya mno!!

1 comment:

Anonymous said...

dah! zama hayo mazingira bomba kweli yan,ila tatizo la malocation manager wa bongo michosho,hawatembei, halafu wanapenda vi2 vya kuiga mno ndo mana picha movies zao zinachosha,na ndo sababu kubwa huwa siziangalii hata kidogo,...lucy