Friday, June 10, 2011

UNA KIPAJI CHA KUIGIZA!? UNA NDOTO ZA KUWA STAR MKUBWA WA FILAMU.. HUU NI MUDA WAKO NA KESHO NDIO SIKU YAKO..

Kwa wewe mkazi wa Dar es salaam.. Kama unajijua una kipaji cha kuigiza na ndoto zako siku zote ni kufanya vizuri kwenye Industry ya filamu basi huu ni muda wako..

Siku ya kesho pale LEADERS CLUB Kinondoni kutafanyika USAILI MKUBWA SANA wa kutafuta WAIGIZAJI kwa hapa Tanzania, na hii ni Serengeti Fiesta Filamu chini ya CLOUDS ENTERTAINMENT katika kusherehekea miaka Kumi ya Fiesta.

Naweza nikaita hii ni Golden Chance kwa yeyote mwenye ndoto za kuwa muigizaji wa Filamu hivyo sherehekea kwani huu unaweza ukawa ni msimu wa dhahabu kwako kwa kutimiza ndoto zako..

Mbali na mimi mwenyewe kuwepo ambae ndio nitaongoza zoezi zima(zamaradi) Tutakuwa na mastar wengine wengi wa Filamu kama Aunt Ezekiel, Jacky Wolper, Wema Sepetu, Jacky Pentzel, Single Mtambalike richie, Jacob Steven (JB), Yusuph Mlela pamoja na Director William Mtitu.

Hivyo Tukutane LEADERS CLUB siku ya KESHO jumamosi kuanzia saa NNE kamili ASUBUHI!!

HII NI BURE KABISA... KIKUBWA TUNACHOANGALIA NI KIPAJI CHAKO!!

NJOO UTIMIZE NDOTO ZAKO!!!

13 comments:

Anonymous said...

asante dada kwa hili tangazo nina swali je kuna vigezo vya umri na jinsia?

Anonymous said...

hongera zama,ila sioni sababu ya kuwaleta hao the so called mastaa wa bongo,kwani wao ndo wanaharibu tasnia hii y filamu,m2 anaigiza siku 2 halfu anageuka director,kasomea wapi hakuna,wakowengi2 wachakachuaji,so if you wanna take this industry to the next level please,give us a break,wakeep left,2tafutie new and real talents,ni hayo2....lucy

Anonymous said...

hongera zama,ila sioni sababu ya kuwaleta hao the so called mastaa wa bongo,kwani wao ndo wanaharibu tasnia hii y filamu,m2 anaigiza siku 2 halfu anageuka director,kasomea wapi hakuna,wakowengi2 wachakachuaji,so if you wanna take this industry to the next level please,give us a break,wakeep left,2tafutie new and real talents,ni hayo2....lucy

Anonymous said...

Nakubaliana na Lucy. 1. Hao ma-star wa sinema za bongo ni mabomu matupu. 2. Kinachohitajika siyo interviews/usaili; kinachohitajika ni mafunzo ya uigizaji/acting. Uigizaji ni fani zinazosomewa iwe huko Hollywood au Bollywood. Tuacheni ubabaishaji; watu waanze kusomea acting kama fani nyingine zozote za sanaa. UDSM na chuo cha sanaa bagamoyo zina waigizaji wazuri lakini hawapewi fursa ya kuonyesha ustadi wao kwa kuwa hapa Bongo mambo ni ma-connection tu na ubabaishaji. Ukiijua fani yako wababaishaji wanakuogopa. Huo ndio ukweli.

Anonymous said...

lucy umesema kweli. ukiwatizama maactor wa tz katika sinema utawapa alama 1 kwa kumi yaani 10%. waingereza wanasema in the land of the blind a one-eyed man is king. yeah, let's take tz acting to th next level badala ya watu kujipachika majina kama the greatest (lol)...

Anonymous said...

Nakubaliana na anon wa 11:46 AM. Tuache kuchakachua fani ya sinema. Kuanzia plot, directing na acting majority ya sinema za Tanzania ziko duni na ovyo sana. Nadhani sababu ni hiyo ya kutokuwa na mafunzo. Ismailson.

Anonymous said...

Nafurahi kuwa wadau mumesema ukweli: mimi naona 90% ya mastaa wa filamu TZ ni mabomu wasiojua kuigiza. Mafunzo yanahitajika, si ubabaishaji wa kujuana.

Anonymous said...

hongera sana sintah. lakini MC vipodozi vimezidi sijuwi anapiti pitia kwa mkongo. lakini dada Belina kapendeza ile mbaya l love yuo mdada Belina.

Anonymous said...

Nimefurahi kuona kuwa watz wenye kujua sinema wameng'amua kuwa mastaa wetu karibu wote ni feki na mabomu tu. Kisa? Hawataki kujifunza wanajiona wao tayari wanajua.

Anonymous said...

Mimi naona makosa yako kwenye casting, yaani kuwachagua maactors. Minavyoelewa mimi, kutokana na kusoma, huko Hollywood, Ulaya na Mumbai kuna watu ambao wanaitwa casting directors. Hawa wanashirikiana na directors/waongozaji kaika kuona kama actor anaoana na role atakayopewa na kama anaweza kuigiza kiasi cha kuwa personality yake inatoweka na anaichukua personality ya yule mhusika/character anayomuiga 100%. Hapa TZ castring inafanywa kwa kujuana tu basi! Kama hao waandalizi wangelikuwa serious wangeliwaalika watu kama kina Dr Martin Mhando kwenye shughuli hiyo ili awaige msasa na awafundishe ABC ya uigizaji wa sinema. Dr Mhano ni mwenyekiti wa ZIFF na hadi juzi nilimuona Zanzibar. Yeye ni professor wa sinema Australia na amewahi kuigiza na kuongoza filamu nyingi Afrika, Japan na Australia. Hao ndio watu wa kutunufaisha...sio hao mastar uchwara wasiojua kichwa wala miguu ya fani ya sinema.

Anonymous said...

Zama, mbona katika hao ma-stars uliowataja sioni hata mmoja aliyesomea kwa karibu au kwa mbali fani hii ya sinema? Kama uko karibu nao nakuomba chonde chonde washauri wakasomee fani hii au angalau waende chuo kikuu kufanya Theatre Arts. Asante.

Anonymous said...

Zamaradi, kama kweli wewe unajali sinema za TZ, basi naomba uwatolee uvivu hao waigizaji wetu wenye kujidanganya kuwa wao ni mastaa kumbe hawajui kitu. Usiogope kuwaambia kuwa uigizaji pia unasomewa kama vile fani zingine zote.

Anonymous said...

Nimefarijika kuona kuwa wabongo wengi tumetambua ubabaishaji wa maactors wetu. Mimi ningependa kutazama na kununua dvd za TZ au za Kiswahili, lakini badala yake nanunua devd's za Ulaya, USA na India ambamo waigizaji wanazama katika character wanayoiga kiasi cha kuwa unasahau kuwa wanaact tu. As long as maactors wetu hawajajua misiingi ya uigizaji tutaendelea kutoa filamu ambazo ni third rate.