Thursday, May 20, 2010

KUMECHISHA SIO NGUO PEKE YAKE

Unaweza ukaangalia jinsi mpangilio ulivyo kuanzia Hereni, bangles, nguo, na kucha... so tusikariri kumatch si nguo peke yake.

HAWA WAMECHANGIA CCM.. WEWE JE???

Belle 9 na Diamond
C - pwaa

Chege

Proffesor JAY
Dully Sykes
Joh Makini

Barnaba na Amini (THT)

Mwasiti na Chidi
Mwana FA


Wednesday, May 19, 2010

UNAKUMBUKA ENZI HIZO - PICHA BLACK N WHITE...

Enzi hizo picha zilikuwa kama hivi...... hakukuwa na option nyingine lakini sasahivi black & white utake mwenyewe tu.. ingawa zina utamu wake kidogo.. hapo nikiwa kama mtu wa zamani.
Kwasasa improvement unaonekana kama ulivyo sio zamani nyekundu inaonekana nyeusi...
Hapo ni BUGGY MASTER kushoto, MWASITI akiwa kati na MIMI hapo pembeni kulia...

Mwasiti akiwa na blue na mimi pembeni.. ONE LOVE!!!!


Tuesday, May 18, 2010

SHUKRANI KWA WOOTE TULIOKUWA PAMOJA KATIKA 40 YA MZEE WANGU

baadhi ya watu tuliokuwa pamoja ....... Asanteni wooote kwa kujumuika nasi.
Hifla kushoto akiwa na Aunt Ezekiel... Asanteni sana wapendwa kwa kufika

Aunt akiwa na Amanda
Brothers.. Venture kushoto akiwa anatabasamu pamoja na Gerald Hando.. i really appreciate thanks alot guys
Kutoka kushoto Dj Venture, gerald hando, Jackueline Wolper, Wakuvanga(Mama Bere) pamoja na Bazo Komu.... Nawashukuru sana sana.. MUNGU awabariki sana!!!

Mwasitii... mummie love u soooo much
From left Neema Chande,Hifla, Aunt Ezekiel pamoja na Amanda Posh
Hilda, Mwasiti pamoja na Shamsa Ford (she is always there for me.. luv u ma')
Hilda Lema, Mwasiti pamoja na Shamsa ... thank u guys!!
Aunt Ezekiel na Jackueline Wolper
Muda muafaka

Nas tatu kushoto mwenye kanzu nyeupe akiwa na mshkaji wake katikati pamoja na the best Dancer wa pale THT 'the boy' ... vijana wamebadilika kabisa swagga ilikuwa ni kanzu tu.. thank u guys
the boy kutoka THT akiwa na JUX pamoja na Mo-racka... I really appreciate ujio wenu
Muda muafaka

Thanks to all of you guys ambao tulikuwa pamoja.. bila kuwasahau GEA HABIB, CHENI, TINO, SAJUKI, MZEE CHILO, ANTONIO NUGAZ, MUSA GEORGE, BAGA na wooooooooooote tuliokuwa pamoja na hata ambao hatukuwa pamoja shukrani ziwajie wote.
Tuko pamoja!!!!Friday, May 14, 2010

NAWASALIMU TU.........

Si vibaya ijumaa ya leo nikitoa japo salamu tu kwa wadau wa blog hii.....

Nikiwa na REUBEN NDEGE (Ncha kali) mzee wa 255 ndani ya XXL ya Clouds FM the people station

IJUMAA KAREEM

Katoto haka kanawatakia IJUMAA NJEMA wooooooooooote...


Kakiwa kametoa macho

Hapa naona mcharuko umeanza.. IJUMAA NJEMA kwenu wote.. nice weekend!!!

Wednesday, May 12, 2010

UNATAKA KUJUA KUHUSU NANI????

Tell me...
Nakupa hiyo nafasi unataka kujua kuhusu STAR gani hapa Bongo...
Na si vibaya ukiniambia unataka kujua nini kuhusu yeye ili nikupe kitu roho inapenda...
I will do that for you ili tuweze kwenda sawa...
Hope tuko pamoja!!!

Tuesday, May 11, 2010

VIPI HAMNA STORY...!!???

Vijana wakiwa busy na simu zao.. sijui waliishiwa vya kuongea??
maana wako pamoja lakini hakuna ushirikiano, kila mmoja busy na simu yake...
kutoka kushoto ni DJ MULLY B kutoka Clouds FM, MARTIN (mvuto kwanza) pamoja na Mchezaji wa timu ya YANGA.. JERRY TEGETE.

PICHA YA LEO.... NIKIWA NA KEISHA!!

Nikiwa na KEISHA... Kagiza kwa mbaaaali

Hapa mwanga kidoogo

Hapa Mwanga sana...
ipi umeipenda!?

Thursday, May 6, 2010

KANUMBA AIBUKA NA WEMA TENA

Si mara ya kwanza wao kuwa kwenye filamu pamoja..

Tumeshawaona kwenye A POINT OF NO RETURN, FAMILY TEARS na RED VALENTINES ambazo zote zilikuwa gumzo kubwa na ziliweza kufanya vizuri sana lakini baadae ikawa kimya kidogo kwa wao kuonekana pamoja...

Hatimae kimya kimevunjika na kwa 2010 huu ni ujio mpya kabisa wakiwa pamoja... WHITE MARIA!!!
Kaa mkao wa kula.

Picha kwa hisani ya ABDALLAH MRISHO.

WANTED.....!!! WANATAFUTWA...

GRACE MWAKABUNGU(20)
Huyo anaeonekana hapo ndio mtoto mkubwa na ametoroka na mdogo wake.

Awali alionekana na mtu aliekuwa akimtambulisha kama MJOMBA WAKE lakini wazazi hawamtambui kabisa mjomba huyo.

Hatimae siku ya siku alitoroka alfajiri ya saa kumi na moja, na alipofika huko akampigia simu mzazi wake na kumwambia asimtafute yuko salama na hawezi kurudi lakini mbaya zaidi katoroka na MDOGO WAKE ambae yuko kidato cha pili (FORM TWO)
Huyo ndio MDOGO wa huyo hapa juu yeye yuko FORM TWO amekatisha masomo na kutoroka na dada yake.

Mbaya zaidi inasemekana wanaonekana mtaani wakirandaranda usiku bila muelekeo wowote.

TAFADHALI KWA YEYOTE ATAKAEWAONA WATOTO HAWA ATOE TAARIFA KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA POLISI.
Wednesday, May 5, 2010

MZEE ANAENG'ARA KWENYE FILAMU - MZEE CHILO

Ni mmoja kati ya wazee wachache sana wa Tanzania wanaofanya vizuri sana kwenye maigizo na filamu kwa ujumla ambapo alianza kujulikana kupitia tamthilia ya JUMBA LA DHAHABU.

Jina lake halisi ni AHMED ULOTU.. amezaliwa huko Moshi Kilimanjaro siku ya tarehe 9 December 1950 akiwa ni mtoto wa pili kati ya saba, watano wakiwa wa kike na wa kiume wawili.

Elimu yake ya sekondari alianzia pale AZANIA secondary school mwaka 1966 na kumalizia hapo wakati elimu ya chuo kikuu aliipatia ISLAMIC UNIVERSITY OF MADINA huko SAUDI ARABIA ambapo alisomea Theology...

Mbali na Uigizaji Mzee Chilo ni mfanyabiashara na mwalimu by proffesional ambapo alishawahi kufundisha shule za sekondari WERUWERU, KIBOSHO, UMBWE na OLDMOSHI huko Kilimanjaro..

Kabla ya kuingia kwenye fani alikuwa anatamani sana kuwa muigizaji na siku moja alisikia tangazo la kutafuta waigizaji na ndio hapo kipaji chake kikaanza kuonekana na kiligunduliwa na mtu anaitwa Aunt Chaiba, na baada ya hapo alijiunga na DUNIA INC kama promoter kisha akajikuta ameingia kwenye fani rasmi.

Mzee Chilo ana mke na MTOTO MMOJA anaeitwa Fatma(24), na mbali na muonekano wake wa filamu kiuhalisia ni mtu wa swala tano na anamjua MUNGU vizuri sana. ila ikija kwenye kazi anafanya vizuri sana kwenye filamu.


Anamzungumzia mkewe kama mtu muelewa na anajua kwamba lengo lake ni Kuelimisha jamii hivyo hawezi kuchagua sehemu ya kucheza kwasababu pale inakuwa si yeye (tabia yake) ila ni filamu, hivyo maranyingi anapoigiza tofauti humpa taarifa mkewe kabla hata hajafanya hiko kitu.

Kitu ambacho kiliwahi kumpa ugumu katika filamu zote alizofanya ni ile sehemu aliyotakiwa kuigiza kama MZEE ANAELAWITI WATOTO WADOGO ambapo ilikuwa ni filamu ya MARIA SARUNGI inayoitwa DOGODOGO ila mwisho wa siku alifanikiwa kuifanya na ni filamu ambayo ilipata tuzo kutoka UNICEF.

Kwasasa yuko pale pilipili entertainment akiendeleza fani yake lakini Lengo lake kubwa ni kuwa Director by proffesional na si uzoefu kama madirector wengi wanavyofanya hapa Tanzania, na zaidi anataka kufika aidha Hollywood ama Bollywood hapo ndipo atakuwa amekamilisha ndoto yake ya mda mrefu.


Binafsi nampa Big up sana kwa kazi zake nzuri kwani mara zote ambazo namuona kwenye filamu anauvaa uhusika inavyotakiwa.

UNAWAJUA HAWA??? UPCOMING MOVIE STARS.. BONGOWOOD

Kutoka kushoto Zamda Salim na Monica Malaki.. Nyota mpya kabisa katika filamu Bongo. Utawapata kupitia filamu kama Hot friday na nyinginezo nyingi hasa za RJ company. ni kitu kizuri sana kuwa na watu wapya kwenye industry kwani wanaleta changamoto kwa wakongwe na kufanya watu wafanye kazi nzuri zaidi.
Jina lake halisi ni MONICA MALAKI utampata kupitia filamu ya HOT FRIDAY kama main character(mhusika mkuu) na pia kwenye MY DREAMS ambapo amecheza scene chache.
Anaitwa Zamda Salim, filamu alizofanya kama main character mpaka sasa ni UNFORTUNATE LOVE, BORN AGAIN na HOT FRIDAY na mbali na hizo kuna nyingine nyingi alizocheza scene kadhaa kama THE IMAGE, MY DREAMS(3), WAKTI na nyinginezo nyingi ambazo hazijatoka.
Wakiwa kwenye pozi la pamoja...

Tuesday, May 4, 2010

HAPPY BIRTHDAY DJ VENTURE

Siku ya leo mmoja kati ya Brothers ambao tuko wote hapa Clouds ametimiza miaka yake kadhaa ya kuzaliwa...

Kila jumamosi huwa anatusababishia pale Mzalendo Pub Millenium tower unaweza ukapitia jumamosi hii uone pana happen kiasi gani.

Wish you luck in everything you do na MUNGU akubariki sana.

HAPPY BIRTHDAY BROTHER.....