Wednesday, May 5, 2010

MZEE ANAENG'ARA KWENYE FILAMU - MZEE CHILO

Ni mmoja kati ya wazee wachache sana wa Tanzania wanaofanya vizuri sana kwenye maigizo na filamu kwa ujumla ambapo alianza kujulikana kupitia tamthilia ya JUMBA LA DHAHABU.

Jina lake halisi ni AHMED ULOTU.. amezaliwa huko Moshi Kilimanjaro siku ya tarehe 9 December 1950 akiwa ni mtoto wa pili kati ya saba, watano wakiwa wa kike na wa kiume wawili.

Elimu yake ya sekondari alianzia pale AZANIA secondary school mwaka 1966 na kumalizia hapo wakati elimu ya chuo kikuu aliipatia ISLAMIC UNIVERSITY OF MADINA huko SAUDI ARABIA ambapo alisomea Theology...

Mbali na Uigizaji Mzee Chilo ni mfanyabiashara na mwalimu by proffesional ambapo alishawahi kufundisha shule za sekondari WERUWERU, KIBOSHO, UMBWE na OLDMOSHI huko Kilimanjaro..

Kabla ya kuingia kwenye fani alikuwa anatamani sana kuwa muigizaji na siku moja alisikia tangazo la kutafuta waigizaji na ndio hapo kipaji chake kikaanza kuonekana na kiligunduliwa na mtu anaitwa Aunt Chaiba, na baada ya hapo alijiunga na DUNIA INC kama promoter kisha akajikuta ameingia kwenye fani rasmi.

Mzee Chilo ana mke na MTOTO MMOJA anaeitwa Fatma(24), na mbali na muonekano wake wa filamu kiuhalisia ni mtu wa swala tano na anamjua MUNGU vizuri sana. ila ikija kwenye kazi anafanya vizuri sana kwenye filamu.


Anamzungumzia mkewe kama mtu muelewa na anajua kwamba lengo lake ni Kuelimisha jamii hivyo hawezi kuchagua sehemu ya kucheza kwasababu pale inakuwa si yeye (tabia yake) ila ni filamu, hivyo maranyingi anapoigiza tofauti humpa taarifa mkewe kabla hata hajafanya hiko kitu.

Kitu ambacho kiliwahi kumpa ugumu katika filamu zote alizofanya ni ile sehemu aliyotakiwa kuigiza kama MZEE ANAELAWITI WATOTO WADOGO ambapo ilikuwa ni filamu ya MARIA SARUNGI inayoitwa DOGODOGO ila mwisho wa siku alifanikiwa kuifanya na ni filamu ambayo ilipata tuzo kutoka UNICEF.

Kwasasa yuko pale pilipili entertainment akiendeleza fani yake lakini Lengo lake kubwa ni kuwa Director by proffesional na si uzoefu kama madirector wengi wanavyofanya hapa Tanzania, na zaidi anataka kufika aidha Hollywood ama Bollywood hapo ndipo atakuwa amekamilisha ndoto yake ya mda mrefu.


Binafsi nampa Big up sana kwa kazi zake nzuri kwani mara zote ambazo namuona kwenye filamu anauvaa uhusika inavyotakiwa.

5 comments:

Anonymous said...

Mimi pia uwa namkubali sana huyu baba. Lakini katika dini ya kiislamu sijui!! siwezi kutoa hukumu hiyo ni kazi yake muumba, ila kukumbatia wanawake vile na kuwa-kiss, kulala nao katika kitanda hata kama ni second, haikubaliki.
sijui ni kazi tunamuombea, maana sote tunafanya lakini hukumu anaijua Muumba.

Ila mzee uko juu nakukubali sana tu.

Jacob said...

I really like that Mzee chilo page. Kweli imetulia na mimi nampa bigup kwa sn na akaze buti zaidi. its me Dr J Lusekelo frm MUHAS

Jacob said...

Hiyo page ya Mzee chilo imetulia sana sista Zamaradi hata mimi nampa bigup kwa sn na akaze buti zaidi-ni mimi Dr. J Lusekelo kutoka MUHAS MTC

mkibosho said...

nakukubali mkibosho wetu uko juu kama moto wa kifuu huna mpizani kutokana na umri wako.

Muadilifu said...

Mbona mnatuharibia lugha jamani. Sio HIKO KITU, ni HICHO KITU. Asante kwa kunielewa.