Saturday, April 30, 2011

HAPPY BIRTHDAY BOSS.....!!!!


Question: What do you call people who work for you?
Answer: Very lucky

I just wanna say that I am so lucky to have you as my boss coz It's nice to work for someone who knows the secret to being a good manager... being a good person.

Happy Birthday to the world's best boss Mr. Ruge Mutahaba!


You are a wonderful person and a great boss. Wishing you success in work and life. keep up the good work.

ILIVYOKUWA LEO ARUSHA KWENYE USAILI WA KUTAFUTA WAIGIZAJI (SERENGETI FIESTA FILAMU)..

Mimi (Zamaradi Mketema) nikiwa na Hemed Suleiman tukifatilia mchakato mzima kwa umakini siku hii ya leo hapa Mawingu City centre Club Arusha!!!
Reginald Maro a.k.a P.Diddy ambae ndie cameraman wa Take One akiwa makini na kazi yake!!

Msichana kutoka Mwanza akionesha kipaji chake.. hapo alikuwa akichezeshwa na Hemed...

Jamaa katika kuigizaigiza akajikuta kampa mikono ya ukweli HEMED naona mzuka ulikuwa umempanda.. but it was all good!!!
Katika vitu vilivyonivutia leo kimojawapo ni huyu bibi ambae nae alikuja kuonesha kipaji chake....

Anaitwa HAWA SIAMI.. naweza nikasema Bibi ana kipaji sababu alikamua kwelikweli, na kingine kikubwa hakutaka kusikia neno ACTION, yeye aliingia tu na moja kwa moja makamuzi yakaanza mambo ya salamu sijui nini baadae huko.. Bibi alitisha.. soon nitakuwekea clip yake ya Video ili na wewe ufaidi nilichofaidi...
Jamaa alijipanga hadi na mabuti ya mgambo pamoja na Kirungu.. kiufupi kila mtu aliejitokeza alipata nafasi ya kuonesha kipaji chake.. Kwa picha zaidi za matukio.. endelea kusikilizia muda si mrefu nitakuletea mengine yaliyojiri!!!

SERENGETI FIESTA FILAMU ARUSHA...

Hii ilikuwa ni jana wakati tumewasili ndani ya A-City!!
Nikiwa na mmoja kati ya washiriki wa serengeti fiesta filamu
Ndani ya Studio za Clouds FM Arush, Zamaradi, Hemed katikati pamoja na DJ Ally kutoka 87.9 Arusha
Mzigoni....

VIPAJI VIPYA KWENYE MOVIE kutoka MWANZAHao ni baadhi ya washindi waliopatikana MWANZA kupitia Serengeti Fiesta Filamu ambapo hii ni project ya kutafuta vipaji vipya kabisa kwenye tasnia ya Filamu na tulianzia MWANZA na washiriki waliofanikiwa kupita baadhi yao ni hao hapo,hivyo tegemea mambo makubwa sana kutoka kwa vijana hao..
Katika hao kuna yeyote ambae kakuvutia!!??? Kama yupo ni yupi!?? na nini hasa ambacho kimekuvutia kwake!!?? kiufupi yupi unamtabiria makubwa zaidi!!????

Thursday, April 28, 2011

H-BABA AKIONGELEA ANACHOKIKUMBUKA KUTOKA KWENYE UHUSIANO WAKE WA KIMAPENZI WA ZAMANI NA IRENE UWOYA... pamoja na mahusiano yake ya sasa.

Hii ilikuwa ni interview iliyofanyika on TAKE ONE kupitia CLOUDS TV ambapo Wema aliongea anachokikumbuka kutoka kwa kanumba ambae ni aliekuwa mpenzi wake, na baada ya hapo niliongea na H-baba ambae kwasasa yuko kwenye mahusiano na Flora mvungi lakini hii si mara ya kwanza kwake kudate STAR wa movie hivyo na yeye nilimuuliza anachokikumbuka kutoka kwenye uhusiano wake uliopita ambapo alikuwa akitoka na Uwoya kabla ya Flora.

MAREKEBISHO ON WEMA SEPETUs INTERVIEW

kwa wale ambao walitaka kuiangalia interview ya WEMA, marekebisho yameshafanyika na sasa unaweza kuiona bila tatizo lolote
Asanteni.

Tuesday, April 26, 2011

UPCOMING MOVIE STAR....!!!!

Anaitwa Myrosh Kaida, amezaliwa 23rd October 1985, ni mwanafunzi kutoka St Augustine university of Tanzania ambapo yuko mwaka wa pili akichukua Bachelor of Education..


Ni mmoja kati ya watu ambao watashiriki filamu za Fiesta na hiki ni kipaji kipya kabisa kutoka MWANZA ambapo kuna wenzake wengine wengi ambao nitawaletea picha zao mmoja baada ya mwingine.. kwa kuanza nimeanza na huyu.


Ana malengo mengi sana lakini kubwa ni kuwa muigizaji mkubwa sana kwenye filamu na kufanikiwa katika kila atakachokifanya....


HIKO NI KIPAJI KIPYA KABISA kutoka MWANZA, TANZANIA..KWA KUMUANGALIA TU UNAMUONAJE.. ATAFAA KWENYE FILAMU!!????


NAHITAJI MAONI YAKO!!!!?????
SERENGETI FIESTA FILAMU

Kutokana na ubize na majukumu yaliyokuwa mbele yangu pamoja na safari za hapa na pale nilishindwa kuweka picha za Tour yetu nzima ya Mwanza ambapo tuliongozana na Hemed pamoja na Jackline Wolper lakini soon nitawaletea picha hizo ambapo tulikuwa mwanza kwa ajili ya kusaka vipaji kwenye swala zima la filamu!!!


Wiki ijayo tutakuwa ARUSHA hivyo wakazi wa Arusha wenye vipaji kaeni mkao wa kula tunakuja


Tuko pamoja!!!!

UNAMJUA HUYU!!???... PICHA YA LEO....

Anaitwa Hassan Kundamayi a.k.a HK kutoka HK Vision ambapo ni Video Producer na ameshatengeneza videos mbalimbali kama Tatizo umasikini ya vumilia, Njiapanda ya Barnaba na Pipi, Dar es salaam stand up ya chidi benzi na nyinginezo nyingi sana.


Lakini mbali na kuwa producer wa video HK pia ameshawahi kuwa mwanamuziki ambapo zamani kama unakumbuka alishawahi kuimba na alishirikiana na RENEE LAMIRA kwenye wimbo unaoitwa TATIZO OUT na mwingine aliwahi kuimba na Esther Wassira wimbo unaitwa UMERUDIA TENA na alikuwa na style yake ya peke yake katika uimbaji ila sielewi kwasasa kwanini aliamua kuachana na swala la mziki...


Huyo ndio HK na hiyo ndio picha yetu ya leo!!!

Wednesday, April 20, 2011

STAY TUNED...

Kuanzia wiki ijayo kwa kuwajali wale ambao wako mbali na hawashiki CLOUDS TV.. nitakuwa naweka vipande tofautitofauti ama vitu tofautitofauti kutoka kwenye kipindi changu cha TAKE ONE ili tuweze kwenda sawa..
ASANTENI SANA
TUKO PAMOJA SANA
NAWAPENDA WOTE !!!

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH WEMA SEPETU KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIAMOND....


Hiyo ilikuwa ni interview ambayo niliifanya kupitia TAKE ONE ya CLOUDS TV ambayo huwa kila JUMANNE saa TATU kamili Usiku na MARUDIO ni Jumatano saa NNE na dakika tano usiku

Tuesday, April 19, 2011

FILAMU MPYA KUTOKA JAROWE.. THE DIARY!!!!! UNAIONAJE COVER!!????

Kutoka kushoto ni JACKLINE PENTZEL, WEMA SEPETU pamoja na ROSE NDAUKA kwa pamoja wanaunda kundi linaloitwa JAROWE ambapo wana malengo mengi sana kwenye Industry ya Filamu BONGO.. kwasasa hivi wamekuja na filamu yao mpya kabisa inayoitwa THE DIARY kama cover yake inavyoonekana hapo juu.. UNAIONAJE COVER...!!???
COVER ya PART 1 kama inavyoonekana kwa mbele na nyuma
Huu ni muonekano wa Cover ya PART TWO... THE DIARY coming soon kutoka JAROWE ambapo ni kifupi cha JACKY,WEMA na ROSE..


STAY TUNED!!!!

Monday, April 18, 2011

ALIYECHOMWA MOTO SOUTH BEACH AFARIKI DUNIA.

Yule mwananchi aliyechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco amefariki dunia. Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lillah alifariki dunia juzi jioni na amezikwa jana jioni katika makaburi ya mji mwema kigamboni.Marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao Beach za Kigamboni, alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa South Beach.

Spoti na Starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika fukwe Mbalimbali za Kigamboni ikiwemo Chadibwa Beach. Marehemu Lillah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya South Beach Jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio kwenye Disco linalopigwa mwishoni kwa kila wiki fukweni hapo, Lillah hatimaye alipelekwa kwa meneja wa hoteli hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto.

Akionge kwa taabu na Muandishi wetu katika Hospitali ya Kigamboni kabla ya kuhamishiwa Muhimbili alikoagia dunia, Marehemu Lillah alisema hata Kupona mpaka pale anamshukuru Mungu kwani hakutegemea kupona kutokana na kipigo na maumivu ya moto ule. Tunaomba haki itendeke ili kukomesha unyama huu, hata kama Marehemu Lilah alikuwa mkosaji au kibaka kama walivyodai hapaswi mtu yeyote kutoa hukumu ambayo Lillah amepata.

Huu ni mfululizo wa kujichukulia sheria mikononi ambapo wezi na vibaka wamekuwa wakichomwa moto na wakati mwingine bila hatia yeyote, kwani matukio mengine yakitokea akishakamatwa anatafutwa aliyeibiwa haonekani. Mwanzoni mwa mwaka kijana mmoja alipoteza maisha maeneno ya Mwenge kwa kuitwa mwizi ilihali yeye ndio alikuwa ameibiwa Laptop yake na alipojaribu kuwakimbiza wezi walimgeuzia kibao na hatimaye wananchi walimvamia na akapoteza maisha. Marehemu Lillah ameacha mke na watoto.


Habari na picha kwa hisani ya spoti starehe

Friday, April 15, 2011

KUTANA na KIMORA wa TANZANIA kupitia filamu mpya iliyofanyiwa UINGEREZA inaitwa FACEBOOK

Utampata kupitia filamu mpya kabisa ambayo imechezwa na watanzania waishio uingereza inaitwa FACEBOOK.. humo ndani amecheza kama KIMORA (jina alilotumia kwenye filamu) na tegemea mengi kutoka kwake katika film industry ya Tanzania!!
Kutoka kushoto Kimora, Geofrey ambae ndie Ex. producer wa hiyo filamu, Zamaradi Mketema (mimi) pamoja na Thecla ama Suzzy kama alivyocheza kwenye filamu ya Facebook..


Wadada wa kwenye filamu ya FACEBOOK
hapa ni katika Interview na TAKE ONE pembeni hapo ni Raymond Charles.. Cameraman wa Take One. Kimora kama anavyoonekana.. The NEW actress in Tanzania.. isubirie Filamu ya FACEBOOK ili kuweza kuona kama yaliyomo yamo ama la!!!

Monday, April 11, 2011

ACHOMWA MOTO KWA KUZAMIA SOUTH BEACH..

Pichani ni Bwana Lilah Hussen alieungua vibaya mwili mzima akiwa ndani ya Ambulance ya hospitali ya Kigamboni tayari kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuchomwa moto na walinzi pamoja na meneja wa hoteli ya South Beach iliopo kigamboni alipobainika kuwa aliingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
Na Mdau Pius Micky wa Spoti na Starehe

Kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Lilah Hussen,amechomwa na moto mwili mzima na walinzi wa Hotel ya South Beach wakishirikiana na Meneja mmiliki wa Hotel hiyo aliejulikana kwa jina moja la Shipata.

Tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana,limetokea jana mchana katika hoteli hiyo. Wakiongea na mwahabari wetu, ndugu wa majeruhi huyo wamesema kuwa ndugu yao alifika ufukweni hapo ambapo kila mwisho wa wiki panakuwa na muziki kwa ajili ya kujiburudisha na alipoingia ndipo alipokamatwa na walinzi kwa kutokuwa na alama maalumu ambayo huvaliwa mkononi kwa waliolipa kiingilio cha hotelini hapo (kiingilio ni Tsh. 7,000/- kwa mtu) ndipo walinzi hao walipochukua jukumu la kumpeleka kwa Meneja wa Hoteli hiyo na ndipo meneja huyo alipoamrisha kijana huyo avishwe mipira na kuchomwa moto.

Bwana Lila ambaye kwa sasa kahamishiwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili amesema yeye ni mfanyabiashara ndogo ndogo na mkazi wa Kigamboni na kuwa alikwenda hapo baada ya kuvutiwa na muziki pasi kujua kama hayo yaliyofanyika hapo yangemkuta.

Ndugu wa majeruhi huyu wamefungua kesi katika kituo cha Polisi Kigamboni lakini hadi hivi sasa na kwa masikitiko wanasema bado hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wa tukio hilo kitu ambacho kinazidi kuwasikitisha ndugu hao wa majeruhi. Ufukwe wa hoteli ya South Beach umekuwa ukijizolea umaarufu kwa michezo ya ufukweni lakini wananchi wa kawaida ambao wanaishi eneo hili wamekuwa wakilalamikia ada kubwa ya kiingilio ufukweni hapo ikiwa ni Tsh. 7,000/- ada ya kuingia tu bila kinywaji.
Hivyo inafanya wakazi wa maeneo hayo watamani kufika mahala hapo lakini kutokana na gharama za kiingilio kuwa kubwa inawabidi waishie kusikia sifa tu toka kwa watu waendao mahala hapo.

Kijana Lilah kwa sasa yuko Hospitali ya Muhimbili akiendelea kupata matibabu kwani hali yake ilikuwa ni mbaya sana. Jeshi la Polisi mnaombwa kuliangalia swala hili kwa kina na ikiwezekana hatua za haraka za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika waliofanya jambo hili ambalo ni la kinyama kabisa kwani hili si jambo la kulifumbia macho hata kidogo.
Habari na picha kwa hisani ya Othmani Michuzi.

Friday, April 8, 2011

ILIVYOKUWA JANA PALE LEADERS.....

Dina, mimi hapo katikati (zamaradi) pamoja na Shadee.. Jacky wolper, Zamaradi Mketema na Dina Marios... Clouds TV team wakiwa na CASTO pale kati (mwananchi wa kawaida)

Rehema kutoka THT akiwa na SIMPLE (ze boy) kutoka 69records.
Reuben Ndege (ncha kali)
Mashujaa band wakifanya vitu vyao...
Joan Matovolwa akiwa na watoto wakiwa wamevalia jezi zao..
B12 (dozen) nae alikuwepo.. shabiki nambari moja wa Arsenal...
hali ya uwanja ilivyokuwa..
Kutoka kushoto DINA MARIOS, ZAMARADI MKETEMA, SHADEE, BARBARA HASSAN pamoja na MARTIN KADINDA huko nyuma..
Mh hakuna mashabiki waliokuwa na fujo kama MAN UNITED.. hapo nilipishana nao wakiwa wanashangilia... naweza nikawaita mabingwa wa kushangilia hata wakifungwa wao wanashangilia tuuu...
Hao bwana... Mbwembwe nyingi mwisho wa siku CHALI.. hamna kitu!!!


Dina, Zamaradi, shadee pamoja na Barbara Hassan...

NILIKUMBUKA ENZI KIDOOGO....

Jana pale leaders wenzangu wakiwa wako busy na mpira mimi nilikuwa busy kidogo na baiskeli nikikukumbukia enzi hizo ambapo jana ndio niliendesha tena baiskeli kwa mara ya kwanza baada ya kama miaka kumi na tano hivi ambapo nilikuwa mpenzi sana wa baiskeli.. Enzi hizo nikitoka tu shule ninachojua ni hiko.... Ninachokumbuka wakati wa kujifunza baiskeli nilikuwa nikianguka anguka sana, kila siku mavidonda na makovu kwa ajili ya baiskeli... lakini baadae nikawa master though sasahv utu-uzima kidogo unanifanya nisiwe sana kiviile.. jana wakati naendesha nikawatia hamu na kina Asma Makau pamoja na Shadee ikabidi nao watafute baskeli waendeshe... Ingekuwa sio msongamano wa magari DAR nahisi huu ndio ungekuwa usafiri wangu coz huwa na-feel comfortable sana na naenjoy sana ku-ride a bicycle.. lakini kwa DAR hii sitaki hata kujaribu kuendesha baiskeli barabarani coz nitaishia pabaya... Barbara ndio alikuwa anafanya kazi ya kunipiga picha na simu yake, asante sana kwa kuwa mpiga picha wangu kwa muda na asante kwa kaka alieniazima baiskeli pale leaders jana.. u made my day sana coz hiko ni kitu ninachokipenda mnoo... huyoo naondoka!!!!!!

JUMATANO HII NILIKUWA CONTINENTAL KWENYE KANGA MOJA....

Jumatano hii niliamua kutoka kidogo kwenda kusafisha macho pale continental club maeneo ya Town ambapo kulikuwa na kanga moja (laki si pesa) (KANGA MOKO). . na si jumatano hii tu ila kila jumatano usikose kwenda kushangaa shangaa kidogo!!!
Hii picha ilikuwa ya kushtukiza kidogo, Dina ndio alikuwa anatupiga halafu akatufotoa kabla hatujajipanga ikabidi barbara kama aikwepe hivi mwisho wa siku ikampata.. Geah habib.. mratibu wa kanga moja huyo.. ukitaka kuwapata kwa ajili ya show inabidi uzungumze na Geah vizuri maana ndio meneja wao..
Barbara Hassan wa Power Breakfast Clouds FM.
Dina Marios wa Leo Tena ya Clouds FM.
Anaitwa Sheila.. rafiki yake Barbara nae alikuwepo tukajumuika wote... Zamaradi mketema na Barbara Hassan..
Ada na Zamaradi...
Dina Marios.. Ukiwa Continental huwezi kuacha kushangaa.. hapo sijui nilikuwa nashangaa nini.. Sielewi.. but mwisho wa siku was good coz we had fun na kila kitu kilikwenda sawa....