Yule mwananchi aliyechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco amefariki dunia. Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lillah alifariki dunia juzi jioni na amezikwa jana jioni katika makaburi ya mji mwema kigamboni.
Marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao Beach za Kigamboni, alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa South Beach.
Spoti na Starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika fukwe Mbalimbali za Kigamboni ikiwemo Chadibwa Beach. Marehemu Lillah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya South Beach Jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio kwenye Disco linalopigwa mwishoni kwa kila wiki fukweni hapo, Lillah hatimaye alipelekwa kwa meneja wa hoteli hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto.
Akionge kwa taabu na Muandishi wetu katika Hospitali ya Kigamboni kabla ya kuhamishiwa Muhimbili alikoagia dunia, Marehemu Lillah alisema hata Kupona mpaka pale anamshukuru Mungu kwani hakutegemea kupona kutokana na kipigo na maumivu ya moto ule. Tunaomba haki itendeke ili kukomesha unyama huu, hata kama Marehemu Lilah alikuwa mkosaji au kibaka kama walivyodai hapaswi mtu yeyote kutoa hukumu ambayo Lillah amepata.
Huu ni mfululizo wa kujichukulia sheria mikononi ambapo wezi na vibaka wamekuwa wakichomwa moto na wakati mwingine bila hatia yeyote, kwani matukio mengine yakitokea akishakamatwa anatafutwa aliyeibiwa haonekani. Mwanzoni mwa mwaka kijana mmoja alipoteza maisha maeneno ya Mwenge kwa kuitwa mwizi ilihali yeye ndio alikuwa ameibiwa Laptop yake na alipojaribu kuwakimbiza wezi walimgeuzia kibao na hatimaye wananchi walimvamia na akapoteza maisha. Marehemu Lillah ameacha mke na watoto.
Habari na picha kwa hisani ya spoti starehe
3 comments:
Wadau naomba tushinkize vyombo na habari na vya dola kuhakikisha haki inatendeka. Huwezi kumuua binadamu mwenzako kwa kuwa eti amingia disco bila kulipa!!!!! Naomba tuetote michango yetu magazetini, tuwapigie simu TV na radio stations ili kuhakikisha kesi hii haifi.
huo ni ukatil wa kupiliza huwezi kumfanyia kitu chochote chenye uhai eti kumchoma moto tena akiwa mzima anatizama . ni unyama huo yaani kmsababishia maumivu mpaka anakufa .jamani binadamu tunakwenda wapi hapo serikali ichukue hatua kwa mhusika na wananchi wapate ripoti.
DUNIA INAENDA WAPI JAMANII
Post a Comment