Saturday, April 30, 2011

ILIVYOKUWA LEO ARUSHA KWENYE USAILI WA KUTAFUTA WAIGIZAJI (SERENGETI FIESTA FILAMU)..

Mimi (Zamaradi Mketema) nikiwa na Hemed Suleiman tukifatilia mchakato mzima kwa umakini siku hii ya leo hapa Mawingu City centre Club Arusha!!!
Reginald Maro a.k.a P.Diddy ambae ndie cameraman wa Take One akiwa makini na kazi yake!!

Msichana kutoka Mwanza akionesha kipaji chake.. hapo alikuwa akichezeshwa na Hemed...

Jamaa katika kuigizaigiza akajikuta kampa mikono ya ukweli HEMED naona mzuka ulikuwa umempanda.. but it was all good!!!
Katika vitu vilivyonivutia leo kimojawapo ni huyu bibi ambae nae alikuja kuonesha kipaji chake....

Anaitwa HAWA SIAMI.. naweza nikasema Bibi ana kipaji sababu alikamua kwelikweli, na kingine kikubwa hakutaka kusikia neno ACTION, yeye aliingia tu na moja kwa moja makamuzi yakaanza mambo ya salamu sijui nini baadae huko.. Bibi alitisha.. soon nitakuwekea clip yake ya Video ili na wewe ufaidi nilichofaidi...
Jamaa alijipanga hadi na mabuti ya mgambo pamoja na Kirungu.. kiufupi kila mtu aliejitokeza alipata nafasi ya kuonesha kipaji chake.. Kwa picha zaidi za matukio.. endelea kusikilizia muda si mrefu nitakuletea mengine yaliyojiri!!!

No comments: