Monday, April 4, 2011

ILIKUWA NI SIKU, SAA, MWEZI na HATIMAE umetimia MWAKA TANGU UTUTOKE.. NIMEKUKUMBUKA SANA BABA..

Nakumbuka ilikuwa siku ya pasaka tarehe 4 mwezi wa 4, 2010 ambapo ndio ULIFUMBA MACHO mojakwamoja na SIJAKUONA TENA, ilikuwa ni SIKU NGUMU SANA KWANGU na LEO ni tarehe inayonikumbusha mambo mengi sana kuhusu wewe.. umetimiza MWAKA MMOJA tangu ututoke BABA, KWANGU haukuwa baba tu ila ulikuwa babu, ulikuwa rafiki na mshauri pia,nakumbuka mengi sana kutoka kwako lakini kubwa mapenzi yako kwangu, ucheshi na utani wako na yote ambayo hakuna mtu mwingine anaeweza kuziba pengo lako.. nakumbuka usiku mmoja kabla hujafariki nilikwambia "NAKUPENDA BABA" pamoja na kwamba ulikuwa umekata kauli lkn naamini ULINISIKIA, na hiko ndio kinachonifariji mpaka leo, nitaendelea kukupenda na kukukumbuka daima.. you were the BEST DAD ever..

Kukosekana kwako kwenye maisha yangu kumeacha pengo kubwa sana kwani kuna MENGI ambayo yametokea nyuma yako lakini naamini yote ni MIPANGO ya MUNGU.. Katika maongezi yetu ya kila siku na mama haukosi kuingia hata mara moja kwani naamini ulikuwa ni wa kipekee baba.. kikubwa ambacho nakumbuka kila nikitoka ama kwenda kwenye jambo lolote ulikuwa ukiniombea kwanza na kuniambia nenda kilakitu kitakuwa sawa kwa uwezo wake MUNGU.. lakini leo haupo tena!!

Kuna muda huwa nakukumbuka najifungia ndani mwenyewe nalia sana mwisho wa siku nainua mikono juu na kumshukuru MUNGU kwani yeye aliekuchukua ndio anajua kilakitu na hajakosea.. Nakumbuka neno lako moja ulilokuwa unapenda sana kuniambia kwa utani huku unacheka "NIKIONDOKA UTAPATA TABU SANA WEWE" sikuwa naelewa maana yake kabla ama labda nilikuwa nalichukulia kirahisi lakini nafikiri sasa ndio naelewa.. ni kama bado naiona sura yako katika hali tofautitofauti...

Natamani sana ungekuwepo ili angalau uone matunda ya ulichokipanda lakini naamini MUNGU ana maana yake zaidi katika kila analolifanya na hakuna analolikosea...

M/MUNGU akuondolee adhabu na ailaze roho yako mahali pema peponi..

AMIN!!!

19 comments:

Anonymous said...

RIP BABA.

zuwena said...

pole sn zama, ni ngumu kusahau, kikubwa tunatakiwa kumwombea dua mzee wetu, pole sn mpz... mwenyezi mungu amweke mahala pema

rukia meza said...

POLE MWAYA NDIO MAISHA, YN MZEE MKETEMA ALIKUWA MCHESHI SANA, NAKUMBUKA ALIPOKUA AKIJA PALE SHULENI KUNDUCHI, ALIKUA HABAGUI YULE MZEE ENZI ZILE MAJI YA PAKTI YA UHAI ALIKUA AKIJA NA FUKO TELE, MUNGU AMPUMZISHE SALAMA

Mwanaid Rajab said...

pole sana Zama yote ni mipango ya Mungu ni ngumu sana pale tunapowapoteza watu wa karibu yetu,tena haswaa wale tuwapendao.
Mie mwenyewe nilimpoteza Baba yangu kipenzi miaka mitano iliyopita so i knw exactly wat ur going through.
Kilichobaki ni kuwaombea Dua,M/Mungu awaepushe na adhabu ya kabri inshaallah.
Sisi ni wake na Hakika kwake tutarejea.
Kila nafsi itaonja Umauti,wao mbele sisi nyuma yao.

middy said...

Zama honest nimesoma hiyo text machozi yamenitoka coz nimempoteza baba yangu pia miaka kadhaa iliyopita,so kilichobaki tuwaombee dua mungu awaepushe na adhabu ya kabri.

Anonymous said...

Pole zama we all belong there,Tuswali na tumwomea dua,na ww pia fanya starehe zote lakini tenga muda wako uswali kabla hujaswaliwa.
Kweli Baba yako Alikuwa anakupenda coz nakumbuka tulipokuwa Kunduchi Girls Alikuwa anakuja kukutembelea mara kwa mara alafu masikni umri kidogo ulikuwa umeenda lkn he was alwayz there na kunduchi kulivyokuwa mbali lakini bado alikuwa anakutembelea.

Anonymous said...

pole sana zamaradi maneno uliyoandika hakika yanachoma moyo nakutia uchungu lakini yoote nikazi ya mungu haina makosa sote ndiyo njia yetu nikujipa moyo tu nakuzidi kumwombea baba yako kwani hauko naye kimwili lakini kiroho uko naye pole sana dada mungu akutie nguvu maana ni vigumu kusahau.

Anonymous said...

Kufiwa na baba au mama hakuna hata siku mija uamke pasipo kukumbuka hivo nakupa pole nna miaka 7 toka nipoteze baba na miezi 5 toka nipoteze mama na kila siku nawakumbika as if ilitokea jana.
Kusema unaomba Mungu apunguze azabu ya kaburi shoga utasugua mswala mpk kiama haiwezekani hata kdg kila mmoja atavuna alichokipanda cha msingi ni kumshukuru Mungu tu.Ni vile watu hawajua maombi na sala haziwezifuta zambi za m2 kamwe if they are kungekuwa hakuna jehanam mana kila m2 angeenda kwa mungu

Anonymous said...

its so touching n u reminded me wen i lost my father in 1997,til today i cnt believe that h is gone but u know i be;live where yo father is,h is so proud of u zamaradi n always make him proud n pray for him

Anonymous said...

POLE DADA 'ANGU ITAFIKIA UTAZOEA KILA KITU.NAMI ILINISUMBUA SANA MWANZONI LKN NAMSHUKURU MUNGU SASA IMENIONDOLEA KHALI HIYO.

Anonymous said...

Tumuombe mungu amemfisha hali akiwa muislam na amfufue hali akiwa muislam,na Inshaalah ampeleke kwenye Pepo yake ya firdaus.
AMEEN YA RABBIL ALAMIN

Anonymous said...

ZAMA POLE SANA MPENZI MUNGU NA AKUWEZESHE KUFANYA KAMA AMBAVYO BABA ALIKUELEA HIVYO USIMWANGUSHE HATA KIDOGO MAANA KWA KUFANYA HIVYO UTAMUENZI BABA YAKO. NI VIGUMU KUSAHAU LAKINI MUNGU SIKU ZOTE NDIYE MFARIJI WETU NA NDIYE BABA YETU WA KARIBU. MUNGU NA AKUWEZESHE NA KUKUTIA NGUVU.

Anonymous said...

REST IN PEACE DAD

mwantum kipwassa said...

hakika inauma saaana. sms yako imenigusa kwa upande wa maisha yangu umeniacha nalia peke yangu kwa kumkumbuka baba yangu pia. all in all
MUNGU AWAREHEMU MILELE AMINA.

Anonymous said...

Dah!!!!!! pole sana dada, message yako imenkumbusha mbali sana, nimemkumbuka baba yangu mzazi, machozi yamenitoka, i think alikuwa as ur dad, am still proud of him and am praying always.
REST IN PEACE, AMEN

msaki said...

pole sana zamaradi.....mungu amlaze mahali pema peponi

Zamaradi said...

ASANTENI SANA WOTE KWA CONCERN YENU.. NAWSHUKURU SANA SANA NA TUKO PAMOJA SANA.. naamini bila nyinyi hakuna mimi.. SHUKRANI SANA KWA WOTE.. nimefarijika sana..
Tuko pamoja!!!

MAJOY said...

POLE ZAMARADI MWENYEZI MUNGU HUFANYA KILA JAMBO KWA MAKUSUDI YAKE HIVYO TUNAPASWA KUSHUKURU KWA KILA JAMBO.
POST HII INASIKITISHA SANA UMENIFANYA NITOE MACHOZI KWANI NAMI BABA YANGU ALIKUFA MWAKA JANA MWEZI WA SITA NA ALIKUA NI ZAIDI YA BABA KWANGU.TUWAOMBEE TU MPZ.
REST IN PEACE MR. MKETEMA

annette said...

hey zamaradi...pole sana kipenzi kazi ya MUNGU haina makosa..