Wednesday, April 6, 2011

WEWE NI MUANDISHI MZURI WA SCRIPT..!!!???? FIESTA MOVIES INAKUJA......

wewe ni muandishi mzuri wa script na uko katika mikoa ya MWANZA, ARUSHA, TANGA, MBEYA ama DODOMA!!???


Hii ni nafasi yako.. tuma script yako kupitia anuani yetu ya CLOUDS FM ambayo ni 31513 DSM na ui-address kwa ZAMARADI MKETEMA.. na hii si kwa waandishi tu bali hata kwa waigizaji kwani tutakuja mkoa mmojammoja kwa ajili ya USAILI wa kutafuta WAIGIZAJI kulingana na script ya mkoa husika na wakipatikana wanaanza Shooting haraka iwezekanavyo na mwisho wa siku filamu zote kutoka mikoa mitano tofauti zitafanyiwa promotion ya aina yake na Kuzinduliwa kwa mara moja (kwa kipindi kimoja) na MKOA ambao filamu yake itaonekana kufanya vizuri basi UTAPEWA FEDHA TASLIMU MILIONI KUMI kwa ajili ya kushoot filamu nyingine....


Kwa kuanza tutaanzia MWANZA hivyo kwa wale waandishi anza kutuma SCRIPT YAKO SASA...na kwa wale waigizaji KAENI TAYARI.. TUNAKUJA!!!

FIESTA MOVIES INAKUJA.....

3 comments:

THE DIVA LAURYN said...

Sasa Zama mimi nina Swali mi niko Dar ila soon nitahamia mwanza kabla ya tar. 20 hivi je naweza kutuma nikiwa dar?
pili, script iwe na urefu gani?

THE DIVA LAURYN said...

Na deadline itakuwa lini?

Zamaradi said...

Mwanza tutakuja wiki ijayo.. unaweza ukaileta tu hata kesho.. na script ukubwa wake unategemea na filamu yako ila hizi sio za short film ila ni SCRIPT za filamu ya kawaida ambazo hazitakiwi kuwa chini ya lisaa limoja na nusu..
ASANTE!!!