Monday, April 11, 2011

ACHOMWA MOTO KWA KUZAMIA SOUTH BEACH..

Pichani ni Bwana Lilah Hussen alieungua vibaya mwili mzima akiwa ndani ya Ambulance ya hospitali ya Kigamboni tayari kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuchomwa moto na walinzi pamoja na meneja wa hoteli ya South Beach iliopo kigamboni alipobainika kuwa aliingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
Na Mdau Pius Micky wa Spoti na Starehe

Kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Lilah Hussen,amechomwa na moto mwili mzima na walinzi wa Hotel ya South Beach wakishirikiana na Meneja mmiliki wa Hotel hiyo aliejulikana kwa jina moja la Shipata.

Tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana,limetokea jana mchana katika hoteli hiyo. Wakiongea na mwahabari wetu, ndugu wa majeruhi huyo wamesema kuwa ndugu yao alifika ufukweni hapo ambapo kila mwisho wa wiki panakuwa na muziki kwa ajili ya kujiburudisha na alipoingia ndipo alipokamatwa na walinzi kwa kutokuwa na alama maalumu ambayo huvaliwa mkononi kwa waliolipa kiingilio cha hotelini hapo (kiingilio ni Tsh. 7,000/- kwa mtu) ndipo walinzi hao walipochukua jukumu la kumpeleka kwa Meneja wa Hoteli hiyo na ndipo meneja huyo alipoamrisha kijana huyo avishwe mipira na kuchomwa moto.

Bwana Lila ambaye kwa sasa kahamishiwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili amesema yeye ni mfanyabiashara ndogo ndogo na mkazi wa Kigamboni na kuwa alikwenda hapo baada ya kuvutiwa na muziki pasi kujua kama hayo yaliyofanyika hapo yangemkuta.

Ndugu wa majeruhi huyu wamefungua kesi katika kituo cha Polisi Kigamboni lakini hadi hivi sasa na kwa masikitiko wanasema bado hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wa tukio hilo kitu ambacho kinazidi kuwasikitisha ndugu hao wa majeruhi. Ufukwe wa hoteli ya South Beach umekuwa ukijizolea umaarufu kwa michezo ya ufukweni lakini wananchi wa kawaida ambao wanaishi eneo hili wamekuwa wakilalamikia ada kubwa ya kiingilio ufukweni hapo ikiwa ni Tsh. 7,000/- ada ya kuingia tu bila kinywaji.
Hivyo inafanya wakazi wa maeneo hayo watamani kufika mahala hapo lakini kutokana na gharama za kiingilio kuwa kubwa inawabidi waishie kusikia sifa tu toka kwa watu waendao mahala hapo.

Kijana Lilah kwa sasa yuko Hospitali ya Muhimbili akiendelea kupata matibabu kwani hali yake ilikuwa ni mbaya sana. Jeshi la Polisi mnaombwa kuliangalia swala hili kwa kina na ikiwezekana hatua za haraka za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika waliofanya jambo hili ambalo ni la kinyama kabisa kwani hili si jambo la kulifumbia macho hata kidogo.
Habari na picha kwa hisani ya Othmani Michuzi.

14 comments:

Anonymous said...

Dah jamani kweli tupo Tanzania ama?c'mon no way out huu ni zaid ya unyama lol,,plz plz yan kwa waamdishi hili swala mlishikilie kidedea mpaka hatima ya waliofanya unyama huu itambulike ,,to be honest zama hope so hata viongozi wa nchi wameliona hili na kiukweli this is to much,,hapa ninawastua na watu waone unyama huu then tuungane katika kuupiga vita jama dah,buku 7 si kitu cha kutaka kumtoa roho mtu ,,waliohusika wachukuliwe hatua bana lol,,pole kaka.

Anonymous said...

MMMH HII NI HATARI SASA MLIANZA CHOMA MOTO WEZI SASA MMEAMIA HUKU HAWA WATU WANABIDI WASHITAKIWE MANAGER MZIMA AKILI MAJI

Kev West said...

Yani beach kama ile elfu 7 inawatoa roho mpaka wanaona ishu kumchoma mchizi. Labda Sheria haita fanya kazi yake lakini kwa jina la Mwenyezi Mungu hamtupi mja wake atanyoosha mkono wake. Inauma.. Si angemtoa nje tu? What a shame!

middy said...

DAAAH AM SPEACHLESS

Anonymous said...

hadi leo picha ni hiyo hiyo tu ya aliyechomwa moto? changamka mama na blog yako imezubaa sana.

Anonymous said...

we nawe km kawaida tupe habari nyingine lol hata mgonjwa kashapona sasa we bado umemuweka tu

mwanaid said...

Jamani nackia huyo kaka ameshafariki dunia jana,daah inauma sana yaani kumuua mtu kwa Tshs. 7000/= kweli huu ni unyama,ukiwaona machoni kama watu kumbe hawana hata utu lool.

zay said...

Haya mambo ya kuchukuwa sheria mkononi sio ishu wala nn??yaani unamuua mtu kwa sh. elf 7,Jman tunaomba sheria ichukue mkondo wake.Mackini kaka wa watu kaacha mke na watoto,daah kaita mgima mgima...

Anonymous said...

The guy is dead Zama.

Anonymous said...

zama huyo mkaka ame kufa leo.. tears drop jaman.. it realy hurts.

Anonymous said...

Mgonjwa hajapona jamani kashaiyaga dunia tangu juzi,so sorry

Anonymous said...

Mgonjwa hajapona jamani kashaiyaga dunia tangu juzi,so sorry

Anonymous said...

Jamani huyo mgonjwa amefariki.........
Wachukuliwe hatua kwanini nchi yetu inakuwa ya kuchezewa tusikubali kwa hili........
Eeehe Mungu mpunguzie madhambi yake umpokee

Anonymous said...

anon wa April 11, 2011 4:42 PM
unalitumiaje neno lol? unaonyesha kukasirishwa na ishu hii lakini pia unaliweka hili neno katika sentensi zako, unalitumia vibaya manake hili neno "lol" linamaanisha "loughing out loud". sasa unawezaje kucheka kwa sauti huku unasikitika? ni sawa na kupiga mluzi huku unatafuna njugu lol!!!