Tuesday, April 13, 2010

NILIPATA MTOTO NIKIWA FORM FIVE - HEMED

Wiki hii nniliweza kufanya mahojiano kidogo na HEMED na nilitaka kujua machache kuhusiana na yeye si kifilamu ila maisha yake nyuma ya pazia.. Anafahamika kwa jina la HEMED SULEIMAN kijana aliezaliwa mwaka 1986 31st August na elimu yake ya Msingi alianzia pale OYESTERBAY primary School na kumalizia katika Shule ya Msingi BUNGE na baada ya hapo akajiunga na masomo ya sekondari pale ANNUUR ISLAMIC SECONDARY mkoani Tanga na baadae akaendelea na kidato cha tano na sita katika Shule za ECKENFORDE na COASTAL high school zote za huko Tanga ambako ndiko alikomalizia Elimu yake ya High School.
Majibu yake hayakuwa mabaya ila hakuweza kuendelea na chuo badala yake akajiunga kwenye TUSKER PROJECT FAME na mwaka uliofatia pia alishindwa kuingia chuo ila kwasasa ana mpango wa kujiunga na chuo kwa mwaka huu akienda kusomea MARKETING.

Kwa kujua mengi zaidi kuhusu yeye cheki na interview yake hapo chini

QN: NI KITU GANI AMBACHO UNAPENDA SANA KATIKA MAISHA YAKO?
ANS:Kiukweli kabisa napenda sana kula na kwa siku nakula mara NANE, mpaka ikifika saa sita usiku kila siku nakuwa nimeshamaliza kuku WAWILI NA NUSU ama WATATU na kitu kingine napenda sana kuwa na BABY(mpenzi) na sio kuwa na mpenzi wangu labda tutoke twende Club hapana ila napenda sana kuwa na mpenzi wangu tujifungie ndani faragha tupeane vitu.. Hivyo ndio vitu viwili ninavyovifeel zaidi.

QN: INASEMEKANA WEWE NI MTU WA WATOTO SANA KWA MAANA YA KUPENDA WASICHANA, HIYO NI KWELI?
ANS: hiyo ilikuwa zamani kiukweli kwasababu wanasema ujana maji yamoto kwasababu nakumbuka wakati naanza resi za kuwa star nilikuwa nataka kila mtu anijue kila mtu anione kwahiyo nilikuwa mtu fulani sijatulia lakini nimekuja kugundua kwamba ukiwa serious sana na kazi na uki-concetrate katika ku-build future yako upumbavu unatakiwa uache pembeni kwasababu ukiendekeza sana inaweza ikakuharibia mbele kwahiyo nina imani sasahivi nimekua na NIMEBADILIKA na niko na mchumba mmoja.

QN: KATIKA HIZO PITAPITA ZAKO HUKUFANIKIWA KUPATA MTOTO?
ANS: Niko na MTOTO MMOJA wa kiume ana miaka miwili na miezi saba anaitwa TRINIDAD huyu mtoto nilimpata nikiwa Form five nakumbuka kwenye kuingia form six wakati nasoma na nimezaa na msichana mmoja anaitwa ...... ah!! acha nimpotezee jina ntampa promo kwasababu alinimwaga ni msichana fulani hivi so.. yeah yupo nina mtoto mmoja nashkuru nimemkubali kwasababu amefanana na mimi.. Handsome boy!

QN: ANACHUKIA NINI?
ANS: Sipendi dharau na sipendi mtu ambae anasema uongo ndiomana huwa mimi najaribu sana kuwa mkweli kwa kila kitu ambacho nakifanya ama kitu ambacho niko nacho kwahiyo mtu akiwa muwazi kwangu nakuwa namuelewa zaidi.
pia sili chakula ukiweka vitunguu na ukitaka kuninyima msosi weka vitunguu mi sili na mama yangu anajua, kwahiyo hata nyumbani kwetu msosi ukipikwa unakuwa hauna vitunguu kwasababu sipendi, pia sili mboga ya majani yoyote unayoijua wewe na hata matunda pia nachagua nakula maembe, ndizi na mananasi mengine yote sili.


QN: UNAPENDA MSICHANA WA AINA GANI?
ANS: Kitu cha kwanza kabisa ninachokiangalia kwa msichana ni RANGI, ila kitu cha ajabu ni kwamba SIPENDI MSICHANA MWENYE RANGI YA AINA YANGU, napenda msichana MWEUSI.. aanzie kwenye U-brown fulani mpaka kwenye weusi ila asiwe mweusi sana na kingine awe MKALI, ila WADADA WENYE RANGI YANGU MTANISAMEHE.

QN: UNAJIVUNIA NINI MPAKA SASA KUTOKANA NA FILAMU?
ANS: mafanikio ni makubwa sana kwanza kujulikanam, nimetokea ni mtu fulani najulikana sana hasa mikoani, filamu zimenifanya mpaka huko vijijini ndanindani watu wanitambue hivyo imenifanya umaarufu umeongezeka na kunipa heshima kwa watu wazima hilo la kwanza
La pili ni MAENDELEO YANGU BINAFSI, sikufichi sasahivi NAPIGA PAMBA KALI, GHETTO KWANGU PAKO FRESH na hata kula sasahivi nakula fresh kama hivyo kuku wawili watatu kwasiku nakula wakati zamani ZEGE(chips mayai) nilikuwa nalifkiria yani.. hivyo nashkuru MUNGU niko fresh.


QN: Asante sana
ANS: Karibu.

Huyo ndio HEMED.. Natumaini utakuwa umejua machache kuhusiana na yeye kama alivyojielezea kwenye majibu yake ambayo sijapunguza wala kuongeza neno langu lolote..
UNATAKA NIKULETEE NANI MWINGINE na nini unataka kujua kutoka kwake???

15 comments:

Anonymous said...

masupastaa acheni nyodo...
dogo umesoma kipawa primary school...tena class A....hayo maisha tu kila mtu anaapitaaaaa.....
ustaa wa maigizo na ushaanza kupakacha ulipotoka.....usipakane na karakata basi!!!!

Anonymous said...

masupastaa acheni nyodo...
dogo umesoma kipawa primary school...tena class A....hayo maisha tu kila mtu anaapitaaaaa.....
ustaa wa maigizo na ushaanza kupakacha ulipotoka.....usipakane na karakata basi!!!!

Anonymous said...

hey,zama please please baby mi naomba umuoji presenter mwenzako unayefanya kazi nae hapo mjengoni who is ma best male presenter ever,guess who....???B12 a.k.a BDozen yani zama this guy i really really love him bt funs wake wengi hatujui undani wa maisha yake like kitu gani anapenda kitu gani hapendi u know...!ye anawahoji wenzake tu bt 2 me cjawahi kuona akihojiwa so zama do that for me cwty pleaaaaase...!!thn after huyo we need adam mchomvu hope itakuwa pouwa coz wengi hatuwajui kiundani

Anonymous said...

sound so childish

tweety said...

Nimempenda sana, yuko wazi, siyo wale wanaoficha halafu wanaumbuka. duh angekuwa mweusi basi ningetuma application hahahahahahah lakini bahati mbaya naye mweupe halafu kwa siku itabidi tupike kuku watano ndani ya nyumba, duh na maisha haya!! nimekusamehe bure.
kwikwikwikwikwi
all the best kaka, utapata penzi la roho yako tulia mtoto

Anonymous said...

Hi Zamaradi! kwa sasa nihitaji an interview wid Yusuph Mlela...
PLIZZ DO IT 4ME,AYT?

Anonymous said...

Kama sanaa yenyewe inalipa kwa ajili ya kula kuku na kupiga pamba ni bora mrudi shule mkasomee fani zingine kuliko kuendelea kupoteza muda.

Anonymous said...

kibongobongo dogo anafunika ana star look kila ukimwona ni kama unamwona for the first time halafu ana heshima.kaza buti dogo we wa ukweli level zako kimataifa

Anonymous said...

sio vizuri kuwa na chuki lakini huyu jamaa ananikera...ana nyodo kweli inabidi akue...kwanza masuper star wa bongo wengi mnazidi kunenepeana hamna star quality inabidi mkeep fit....hemed unacheza roles nzuri sana kwenye movie zako...ni mpole na mstaarabu mwenye hekima..kwanini usiingize hizo quality kwenye maisha yako? just free advice

Anonymous said...

nimempenda amekua mwazi sana . ila sasa jamani huli vitunguu hotelini inakuaje au wewe huli hoyeini inaonyesha uko choosy sana wewe madem weupe hupendi, matunda nayo ya kuchagua ! anyway all the best

Anonymous said...

i ril lav thic man!!anafanya vizuri ktk game though life yake ya nje watu wanaponda bt for ma side he rock!!!kip it up man!haya jamani brown colour...

Anonymous said...

yupo juu anga za filam kaza buti kaka life iko like road full of bums,cornerz, inshallah Allah atakufikisha da plc u wana!!

Anonymous said...

kwakweli sio siri nakubaliana na mwenzangu hapo it sounds childish nafikiri wasnii inabidi wajifunze kuongea kwenye umma wengi wanakuwa kama wanakurupuka. mwnaume asifiwi kwa kla babu

Anonymous said...

dah hemed ndugu yngu nmependa sana short intro yko...imetulia sana tu mzazi...ila umenibore ulivosema kuhusu siku hizi unakula vizuri na hata pamba sahivi mzuka tofaut na zamani...hayo sio ya kujisifu kaka...jisifie manedeleo yko kiujumla na watu wanakupokea vp ktk sanaa yko ya uigizaji...mwisho kabisa napenda kukupa hongera kwa kujaaliwa kua na mtoto kaka!!!pamoja sana tuuuu...nakutakia kila la kher na mafanikio ktk shughuli zako za kila siku...



haya zamaradi tunataka utuletee b dozen aka b12...pamoja na mully b...na adam mchomvu!!!plzzzzzzzzzzz zamaradi usiache!!!


hongera sana kwa kazi nzuri dada zamaradi..pamoja sana tuuu

Anonymous said...

kweli maendeleo ni kula kuku wawili kwa cku bado hujakua kaka pole sana rudi shule tu ukasome halafu ukijiacha natural unapendeza sana mambo ya kujiweka madawa kuvaa hereni ubishoo tu hata hupendez