Habari Zamaradi,
Nimefurahishwa na uchambuzi wako na kuonesha ni jinsi gani hujafurahishwa na suala la matumizi ya lugha ya kiingereza katika filamu zetu.Mimi naomba niliongelee suala hili kwa mtazamo wangu.
Nimewahi kukaa na hawa jamaa zangu na kuongea nao juu ya matumizi ya kiingereza lakini kama ulivyo sema, ueledi umekuwa mkubwa sana kwao kiasi kwamba, kuwashauri ni kama kutwanga maji kwenye kinu.Kwanza kabisa, sielewi hii ya kuzipa filamu majina ya kiingereza imetoka wapi, mimi sioni kama kuna maana ya jina liwe la kiingereza alafu filamu inachezwa kwa kiswahili.
Umeongelea wasiwasi wako kwamba hadhira kubwa ya filamu hizi ni kina mama wa nyumbani, watoto n.k, nakubaliana na wewe ila hata kama wangekuwa na ufahamu mkubwa wa lugha hiyo, bado nisingeona maana ya matumizi ya "kiing-kiswa" kwenye hizi filamu zetu. Tuamue moja kama ni kiingereza ama kiswahili.
Umeongelea tafsiri (sub-tittle)ni kitu kizuri, ila nazo zina makosa mno ya lugha ya kiingereza hasa kwenye sarufi (grammar) kiasi kwamba wala auhitaji uelewa mkubwa wa kiingereza kutambua makosa. Mimi nashindwa kuelewa, Tanzania kuna wataalam kibao wa lugha ambao wanaweza kutafsiri kwa kiingereza fasaha. Hii ni moja ya mambo ambayo yanasababisha tasnia ya filamu ionekane kuwa haina watu makini. Ukija kwenye matamshi ndo usiseme si kiingereza tu hata kiswahili chenyewe wakati mwengine unashindwa kuelewa hapa inakuwaje? Lugha ni kitu muhimu mno katika filamu na cha kufanya ni kuonesha kwamba uko makini na kile ukifanyacho.
Kama tunataka filamu zetu zifikie katika kiwango cha kimataifa lazima tuwe makini, unapompelekea mgeni filamu na kukuta makosa kama hayo sidhani kama kazi yako ataichukulia kwa uzito.Kwenye suala la hadithi naona tunacheza hadithi za kufikirika saana. Unajua katika mazingira yetu kuna story ambazo mtu akika chini na kuzipangilia kwa kuweka matukio yenye mvuto, hakika filamu zetu zitakuwa nzuri zaidi ya hapo.
Ukiangalia nyingi ya ya filamu zetu utaona, kikubwa kioneshwacho ni maisha ya hali ya juu mno, kunavitu hapo nyumbani ukivifanyia utafiti utapata hadithi nzuri sana. Nakupa mfano, utakuta mtu akimfumania mpenzi wake anatoa bastola, kitu ambacho kwa kwetu hapo bastola ni kitu adimu kwa sisi wananchi wa kawaida kuona, mara nyingi silaha tusionazo labda upite benki, polisi n.k na kumkuta skari na SMG.
Mwisho jamaa zangu life style wanayo ishi si nzuri kwa mustakabali wa tasnia ya filamu. Haiwezekani haipiti wiki bila kuona skendo kwenye udaku inayo muhusu msanii wa filamu. Unajua kuna maarufu wengi tu Tanzania, lakini wa filamu wamekuwa warahisi mno kiasi kwamba hawana hesma tena.
Angalia jinsi wasanii wa bongo flava wanavyo shirikishwa katika masuala muhimu ya kitaifa, mfano mabalozi wa Malaria, why kusiwe na wengi wa filamu. Hata mimi siwezi kukufanya uwe balozi wangu kama jamii inakuona ni zimbukuku, bongo-lala,fisadi wa mapenzi,na hayawani!
Shule muhimu ndugu zangu, wenzenu tumepitia huo umaarufu vidole hauna maana hata kidogo.
Shukrani.
PICHA ZA DADA DINA CARE'S FOUNDATION WAKITEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA
VETERANI
-
Mwisho wa wiki hii kikundi cha Dina Care's tulitembelea kituo cha watoto
yatima cha Veterani kilichopo Temeke na kushinda pia kupata nao chakula cha
mchan...
10 years ago
9 comments:
Na kwa kuongezea tu,hakuna Msanii wa Filamu anayeijua hiyo lugha angalau robo tu ya kiufasaha,wengi ni wale wa "Yes,yes Mzungu kala mafenesi"
Kwahiyo hata hicho "Kiswa-Kinge" kinakuwaga broken tupu,past tense,present tense humohumo yaani gramar hakuna kabisa.
Ushauri wangu wangeacha kabisa kutumia hiyo lugha
ameeeen we mdau.manake kuna wadada kila cku kwenye udaku wachafu mno kiasi mtu unashindwa hata kuvutiwa na kazi yake,mimi siku zote nitamheshimu monalisa coz anajitunza hata kama ana mambo yake huyaoni hadharani lakini wengine kichefuchefu mpaka unajiuliza huyu ana ndugu kweli?inabidi kulinda status zao kama vioo vya jamii.kamwe hawataupata ubalozi kwa hali hiyo watausikia tuuuuuuuuuuu
mh hapa pana mengi yamejificha ndani yake. wiki iliyopita nilipita salon moja ya kike nikakuta binti mdooogo sana ambaye ni mwanafilamu wa hapa nchini, matendo anayofanya pale, hayasemeki, mtoto anaongea na mabwana watatu tofauti na kila mmjoa anapewa muda wake, mbaya zaidi anasema eti huyu lazima nikaonane naye kwani anataka kunipa kazi katika filamu yake mpya, bora huku nitapata kutoka zaidi. kivazi sasa!! nadhani mtu hakatazwi kuvaa vile anapenda lakini kuna maeneo na muda. mtoto kavaa nguo haina mikono iko kifuani, fupi iko chini ya makalio tu, halafu imechanua, nguo ya ndani yote inaonekana, VIPI AKIBAKWA? msanii kioo cha jamii lazima uwe mfano wa kuigwa.
Tatizo la mavazi kwa wasanii wetu ndio usiseme kwani hawajui mavazi yapi yanavaliwa wapi ni hovyo hovyo tu tena kote kote kwenye filam na kwenye maisha yao ya kawaida
Jamani lazima kuambizana. Wasanii wetu wa filamu mnatia aibu, kuweni vioo vya jamii kweli, huyo binti nadhani ni LULU. mtoto kadata ile mbaya sijui hata shule kama kamaliza, nini future ya mtoto huyo? fine; ni maisha yake lakini anafundisha nini jamii inayomzunguka kutokana na kazi yake kama yeye binafsi hafanyi vitendo vizuri.
me nadhani tukitumia lugha yetu ya taifa itakuwa nzuri zaidi au kama ni kingereza kiwe kingereza ijulikane moja, lakini humo katika filamu zetu; asante mdau wa mwanzo, ni uozo mtupu. kusema kweli uzuri wa picha, sauti na kuvaa usanii mmefuzu lakini wapi maisha halisi ya Mtanzania katika filamu tunazofanya? kuiga si mbaya kwani ulimwengu unabadilika kila siku, lakini tupeni ladha halisi pia. maisha ya filamu za kitanzania ni yale maisha ya watu wachache sana katika nchi hii.
Thanx Zam.
tatizo lingine tumezidi sana ku copy sana, kuna movie flan hivi inaitwa REGINA, yan wamefanya copy n peste kwenye movie flan hivi inaitwa deliver us us from eve yan ni kila kitu, n
jamani mimi sijawai kucoment humu ila hii topic nimeipenda nimekua nikimtumia coment nyingi ray kwenye blog yake but anazibania hazitoi .kwakweli mimi niko nje ya nchi kwa muda mrefu sana na nimekua nikiagizishia hizi filamu ili zinikumbushe kwetu Tanzania lakini unakuta movie jina la kizungu ndani movie watu wanachanganya lugha ya kizungu na kiswahili KWANINI HATUTUMII LUGHA YETU YA TAIFA?KWANINI HATUJIVUNII LUGHA YETU?? iyo lugha yenyewe broken wanayoongea kwenye filamu..subtitle zinawekwa with direct translation wangapi tanzania wana elimu na kuijua lugha ya kizungu kwa ufasaha kabisa kwanini hawaajiri kufanya iyo kazi?watanzania tunapenda kuiga NIGERIA lugha yao ni kiingereza jamani msiwaigeee..halafu hao directors wa izo movie mnaweka high class life wakati 70percent of the population wako katika hali ya chini?what are they trying to insinuate? namsupport alieandika hii article kwenye movies usage of guns jamani sio kitu common kwetuu tanzania movie directors especially ray if ur reading this comment TRY TO BE REALISTIC AND STOP FAKING IN YOUR MOVIES..ACT WHAT RELATES TO OUR SOCIETY AND NOT SHOWING LEAVING LARGE WHILE TANZANIA IS NOT THAT WAY SAWA U CAN SHOW THAT BUT NOT EVERY MOVIE NI UTAJIRI TUU ONYESHENI WITH OTHER PART OF THE PEOPLE'S CLASS..ni mawazo yangu tuu
Ukijaribu kusoma na mambo mengi yaliyopita utakubaliana nami muda mchache ujao hizi movie za humu ndani zitaachwa kutizamwa na wengi. Nitakupa mfano mpira wa miguu, watu siku hizi asilimia kubwa wanaangalia ligi za nje na sio ligi ya ndani kama wapo namba imepungua sana tofauti na miaka ya nyumba. Hii ilitokana na vilabu vya nchini kutokuwa na mwelekeo.Angalia Bongo Flava ilivyoshika chat ni baada muziki wa Kikongo kupigwa chini na wabongo kupenda cha kwao na ndo maana hata sasa unaona kuna mabalozi kutoka wanamziki wa huko, na ndicho kitakachotokea katika filamu hizi za kibongo watu wanasema wee kwa kuwashauri sio hapa tu hata ukienda kwenye blog zingine lakini hawasikii na kingine kazi zipo nyingi sio wote tuwe kwenye filamu tu au umiss, Bongo bwana kaaazi kweli kweli.
Inaboa.
Mdau
Hi Zamaradi naandika kuhusu filamu ya My wedding kwani nimeapa sintakaa niangalie movie za kibongo tena mana nimeona nimeitupa hela yangu tu labda nilichofaidi ni kuangalia fashioni siwezi kuandika mengi nimeandika kwa Dinnah ukweli ni kwamba naomba muwaambie wasnii sisi ndio tunanunua kazi zao sasa kama wanatoa kazi ambazo sio nzuri wasitegemee watapata wateja naungana na rafiki yangu mmoja ananiambiaga kua movie za kibongo zinaangaliwa na watu ambao awana kazi ni kweli sasa sitakaa ninunue tena movie imetangazwa kama nini kumbe hakuna lolote mtu avai uhalisia ni mwanasheria anajiita kasuka nywele za gold na anavaa skin gins ofc jamani wasanii wa kibongo alafu mnategemea kutoka kweli kwa stail hiyo mi nimekasirika nagombana na Tv yangu karibu ningeivunja
Post a Comment