Thursday, April 22, 2010

WOLPER - NAPENDA MWANAUME ANAENUKIA

Akiwa katika pozi

On the interview with clouds TV


Alizaliwa miaka 21 iliyopita huko MOSHI Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa kwanza na msichana peke yake kati ya watoto wanne wa mzee Wolper.
Elimu yake ya msingi aliipatia katika shule ya msingi Mawenzi huko Kilimanjaro wakati Sekondari alipitia katika shule za St. Magreth, Ikenye Arusha na akaja kumalizia Masai huko Kenya.. na baadae akajishughulisha na biashara zake binafsi hatimae mtu ambae anaitwa Lucy Komba akagundua kipaji chake na ndio ikawa mwanzo wa kuingia kwenye filamu.

Mbali na mwanaume anaenukia pia kuna vingi kama vigezo vya aina ya mwanaume anaependa.. ukitaka kujua mengi kuhusiana na yeye shuka nae kwenye interview hapo chini...

QN: Kama Ingetokea nafasi ya kuzaliwa upya, ungependa kuwa nani?
ANS: Ingetokea nafasi ya kuzaliwa upya kwanza nisingeingia kwenye filamu, unajua kwanini napenda sana kazi yangu na naiheshimu lakini magazeti yanatuharibia, nachukia sana magazeti, naona kabisa kwamba usupastaa ni mzigo wa mwiba, unaweza ukawa unafanya tu kitu kwa mapenzi yako kwa ajili ya kuenjoy lakini kikakurudia tofauti, labda uko tu club unacheza ama umevaa unavyojiskia basi mtu atakupiga picha inakufanya ukose uhuru, hivyo mimi ningezaliwa upya SIDHANI KAMA NINGEINGIA KWENYE FILAMU.

QN:Kwako Furaha ya kweli ni nini?
ANS: Asikwambie mtu pesa ndio kilakitu Zamaradi, NAPENDA SANA PESA aisee, nikiwa sina hela huwa nakuwa kama naumwa yani, hivyo kwangu pesa ndio kila kitu na ndio furaha yangu.. Ujue mi mchaga eeh!! lakini ninavyosema pesa simaanishi kwamba pesa ya kupewa ama nikae tu naisubiri hapana ila napenda kila ninachokifanya kiniingizie hela, napenda kuitafuta pia na ndiomana najishughulisha na biashara zangu nyingine mbali na filamu.

QN:Unapenda mwanaume wa aina gani??/ vigezo vyako ni vipi kwa mwanaume?
ANS: Kwanza mchapakazi, awe ananielewa na aelewe nini nachokifanya, asiwe na wivu, anijali, aniamini lakini kubwa awe smart yani hapo ndio uuh.. napenda mwanaume SMART na ANUKIE.

QN: Kitu gani ambacho watu huwa wanakusifia nacho sana??
ANS: Mara nyingi kitu ambacho watu naskia wananisifia nacho sana ni MACHO.. wanasema nina macho mazuri lakini mi sijui chochote mi naona kawaida tu.. na vingine vingi under carpet.

QN: Unapendelea nguo/mavazi ya aina gani?
ANS: Zamani kabisa nilikuwa napenda sana kuvaa ki-tom boy (kiume) hata mavazi yangu mengi yalikuwa hivyo lakini watu wengi walikuwa hawapendi miniwe hivyo so baada ya watu kunisema ikabidi tu niache hivyo sasahivi navaa kike nimebadilika navaa kike ingawa siku mojamoja sana huwa navaa kitom boy kama naenda kwenye michezo ama kitu kinachofanania, napenda kuvaa mavazi yoyote yanayonipendeza,napenda kupendeza in short.

QN: Nani ni mtu muhimu sana katika maisha yako??
ANS: Mtu muhimu katika maisha yangu ni MAMA YANGU kwakweli, yani huyu ndio kila kitu kwangu.. nampenda sana mama yangu.

Huyo ndio Jaqueline Wolper mtoto wa kichaga ambae kwasasa anafanya vizuri sana kwenye sanaa ya filamu hapa BONGO na ni mmoja kati ya wale waigizaji wa kike wakali.. Hope utakuwa umejua japo kwa uchache kuhusu yeye.

8 comments:

maria said...

Habari yako Zama, natumai uko poa. napenda kukuuliza swali moja hivi CLOUDS TV imeshaanza kurusha vipindi vyake? nitafurahi kama utanijibu maana nina shauku ya kujua.

Anonymous said...

mmmmmmmmh tuanze kunukia sasa!

Good interview hasahasa nimelipenda jibu lake la kusema hela. Kuna watu waajabu sana wengine husema hela si kitu....ngoja uzikose ndipo uone dunia haizunguki.....

Safi sana J- Wolper

Zamaradi said...

Kwa sasa ni signal test tu.. Vipindi kama vipindi bado ila vitaanza muda si mrefu.. so stay tuned.
Asante.

Anonymous said...

Zamaradi mbona huwaulizi, Vipi kuhusu elimu ni wasichana wadogo sana wanatakiwa kuwa shule kwa miaka yao. najaribu kukumbuka mimi nilipokuwa na miaka 21 nilikuwa form six, mbona hawa wasanii wa filamu wanaonekana wameanza maisha mapema na wameridika nayo, hawana mipango kujiendeleza kielimu wanachowaza wao ni pesa. na pesa zenyewe wanazopata ni za kujikimu na sio za maendeleo.

Anonymous said...

Ohhh mdau wa hapo juu na (Wolper) mwenyewe ngoja niwafungue kidogo macho pesa si kila kitu, furaha nzuri duniani ni kumjua Mungu I mean Jesus or Mtume wako then pesa zinafuata . usiringie uhai wako huo wa kutafuta pesa aliyekupa ni mungu si pesa zako. so furaha kubwa ni kuwa mzima maana kupitia uzima ndio unatafuta pesa hizo unazotaka na uzima hutoka kwa mungu mwenyewe akitaka anakuchua muda wowote.


Critics

Benny

Anonymous said...

Nimefurahi kweli mahojiano ya wolper, wee ni mzuri jamani mungu kakubariki.

Hersi said...

he he hee...Zama itabidi umpe Wolper namba yangu tuwasiliane kama anataka wa kunukia!

Anonymous said...

Mmmmhhh huyu ana macho gani yanayotishia uhai wa mtu??acha kujifagilia wewe binti macho yako c mazuri ki hivyo.