Sunday, April 18, 2010

SIMBA OYEEEEEEEEEEE

Leo ilikuwa ni siku ya hekaheka na upinzani wa hali ya juu kati ya watani wa Jadi (Simba na Yanga) hatimae mtanange ukafikia mwisho na SIMBA wakaibuka kidedea dhidi ya wenzao kwa Goli 4-3.
Ilikuwa ni mechi kali sana na nilifanikiwa kuishuhudia live pale uwanja mpya wa taifa.. sikutaka kuhadithiwa leo.
Kiukweli kabisa mimi si mpenzi wa kihivyo wa mpira wa miguu na huwa sina timu, lakini cha kushangaza zaidi na hata mimi huwa najishangaa mwenyewe YANGA ikifungwa huwa ninajiskia vibaya sana though sina timu sasa sijui nijieleweje!!!!
Ila hiyo haitafanya niache kuwapa hongera zao SIMBA...
SIMBA OYEEEEEEEEEEE...!!!!!!!!!!!
kwa picha zaidi tukutane kesho.......

1 comment:

Anonymous said...

Hongera sana,wewe ni mshabiki wa yanga bila ya wewe mwenyewe kujua. Unajua hata vipaji vya watu hujificha namna hiyo bila ya mtu kujijua una kipaji.

Mdau